Thursday, December 31, 2015

JESHI LA POLISI LATOA KAULI KUINGIA MWAKA MPYA

Saa chache kabla ya kufunga mwaka kuna hii taarifa kutoka Jeshi la Polisi..


Tukiwa tumebakiza masaa machache kabla ya kuuaga mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka 2016, Jeshi la Polisi limetoa tahadhari kuelekea mkesha wa mwaka mpya.
Katika taarifa ya Jeshi hilo iliyotolewa na msemaji Advera Bulimba imesema wamejipanga vyema kukabiliana na vitendo vya uhalifu vitakavyojitokeza na kuimarisha ulinzi katika fukwe za bahari na maeneo mbalimbali ya starehe.
Taarifa hiyo pia imewataka watumia barabara kuwa makini na wananchi waache tabia ya kuchoma matairi barabarani pamoja na kupiga fataki kwani hatua hali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Taarifa hiyo ilisomeka hivi..
JES 1 JES 2

Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

BARCELONA NAYO YAUANZA MWAKA IKIJIKITA KILELENI


Spanish La Liga | LOGS

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Barcelona16122240152538
2Atletico de Madrid1712232481638
3Real Madrid17113345162936
4Celta de Vigo179442823531
5Villarreal169342115630
6Deportivo de La Coruna176922516927
7Athletic Club178362518727
8Sevilla177552319426
9Eibar176652119224
10Valencia CF165742114722
11Malaga175571114-320
12Real Betis175571323-1020
13Espanyol176291628-1220
14Getafe174581826-817
15Real Sociedad174491825-716
16Las Palmas174491624-816
17Sporting de Gijon164391525-1015
18Granada CF173591831-1314
19Rayo Vallecano1742111839-2114
20Levante1725101230-1811

ARSENAL YAUANZA MWAKA KWA KUJIKITA KILELENI


English Barclays Premier League | LOGS

PosTeamPWDLGFGAGDPts
1Arsenal19123433181539
2Leicester City19116237251239
3Manchester City19113537201736
4Tottenham Hotspur1998233151835
5Crystal Palace199462316731
6Manchester United198652216630
7Liverpool198652222030
8West Ham United197842823529
9Watford198562420429
10Stoke City198562019129
11Everton196853528726
12Southampton196672623324
13West Bromwich Albion196581824-623
14Chelsea195592329-620
15Norwich City195592232-1020
16Bournemouth195592234-1220
17Swansea City194781624-819
18Newcastle United1945101934-1517
19Sunderland1933131938-1912
20Aston Villa1915131534-198

NDEGE YAKATIZA SAFARI ANGANI KISA PANYA

Ndege ya abiria ilivyokatiza safari yake angani kisa Panya..

Matukio yameendelea kuchukua headlines India.. ukiachia lile tukio la joto kali lililofanya watu kushindwa kuvumilia  na kukaa ndani ya maji wakihofia maisha yao huku wengine wakipoteza maisha kutokana na joto kali kuna hii nyingine imetokea huko.
Ndege ya Air India ambayo ilikua ikitoka Mumbai kuelekea London, Uingereza ililazimika kugeuza safari  ikiwa na abiria wake 171 na kurudi ilipotoka baada ya abiria kubaini kuwepo kwa panya ndani ya ndege hiyo.
Ingawa juhudi za kumpata panya huyo ziligonga mwamba  lakini  rubani  alilazimika kurudi Mumbai ili kuwatoa wasiwasi abiria zaidi ya 170 waliokuwa wakisafiri kwa kutumia ndege hiyo ya shirika la ndege la India.
Baada ya kutua abiria walilazimika kubadilishiwa ndege na kuanza safari upya ya kuelea London.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

Tuesday, December 29, 2015

ASAJILIWA PAPO HAPO MKATABA WAVUNJWA

FC Barcelona yavunja mkataba na mchezaji saa chache baada ya kumsajili, kisa Real Madrid …

Mapenzi ya wachezaji katika vilabu fulani barani Ulaya, imekuwa kawaida hata kama hawavichezei. December 28 klabu ya FC Barcelona imeingia kwenye headlines baada ya kumsainisha mchezaji na kisha kufuta mkataba wake masaa machache baada ya kugundua kuwa ametweet vitu ambavyo vinaihusu timu ya Real Madrid.
Baada ya kufuzu majaribio na Barcelona B Sergi Guardiola alisaini mkataba lakini ulifutwa mapema, baada ya mashabiki wa klabu hiyo kufanya jitihada za kufuatilia mtandao wake wa twitter na kuona posts ambazo zinaonesha mapenzi na Real Madrid

KOMBE LA MAPINDUZI CUP KUTIMUA VUMBI ZANZIBAR

Burudani inahamia Zanzibar, Kombe la Mapinduzi 2016 Yanga, Azam FC na Simba ndani, ratiba kamili ipo hapa …


Ni kawaida kila mwaka kufanyika kwa mashindano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar, kwa mwaka 2016 michuano hiyo inafanyika kama kawaida. Kombe la Mapinduzi kwa sasa Bingwa mtetezi wa Kombe hilo ni klabu ya Simba. Jumapili ya January 3 2016. Hii ndio ratiba kamili mtu wangu ya michuano ya Kombe la Mapinduzi.
OFFICIAL FIXTURE
CHANZO CHA HII STORI: BIN ZUBEIRY ONLINE SPORTS
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

WAZIRI MKUU MIKOANI

ZIARA YA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA MKOANI KIGOMA

zit1
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akizindua soko na Mwaro wa samaki wa Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28 , 2015.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa huo Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit2
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akikagua dagaa wanaokaushwa kitalaam kwa kutumia jua  wakati  alipozindua soko na mwaro wa kisasa wa samaki wa Kibirizi  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
zit5
Mkazi wa Kigoma mjini akionyesha bango katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kwenye soko la samaki la Kibirizi mjini Kigoma Desemba 28, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit6
Waziri Mkuu, Kassim  Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa mkuu wa mkoa wa Kigoma, Issa Machibya kuhusu bunduki iliyokatwa ili kupunguzwa urefu ambayo ilikamatwa na polisi mkoani Kigoma wakati ilipotumika katika uhalifu. Mheshimiwa Majaliwa alikwenda kwenye Ofisi ya  Kamanda  wa polisi wa Mkoa wa Kigoma kukagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  Desemba 28, 2015.. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit7
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akitazama kifaa kinachotumiwa na wahalifu kutengeneza  risasi za bunduki aina ya goboli wakati alipokagua silaha mbalimbali zilizokamatwa na polisi  mkoani Kigoma na kuhifadhiwa kwenye Ofisi ya Kamanda wa polisi wa mkoa huo, Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit8
 Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit9
 Watumishi wa Serikali Kuu na Serikali za Mitaa  wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  wakati alipowahutubia  mjini Kigoma Desemba 28, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
zit10
Waziri Mkuu, Kassim Majliwa  akizungumza na watumishi wa  serikari Kuu na Serikali za Mitaa mjini Kigoma Desema 28, 2015. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Issa Machibya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MNIGERIA AHUKUMIWA KUNYONGWA MALAYSIA KWA KOSA LA KUKUTWA NA UNGA

Hii ndio hukumu kwa Mnigeria aliyenaswa na ‘unga’ Malaysia..


Kumekuwa na nchi nyingi zikijitahidi kupambana na ishu ya dawa za kulevya Duniani, nchi nyingine imefikia mpaka hatua ya kuweka sheria kali ili kudhibiti kabisa kuingizwa na matumizi ya dawa hizo.
Kwenye list ya nchi ambazo zinatajwa watu wake wengi kukamatwa kwa dawa za kulevya, Nigeria nayo imo !! stori za Wanigeria wengi kutajwa na kukamatwa na dawa za kulevya zimesikika na kugusa pia vichwa vya habari.
Kilichonifikia kutoka Malaysia ni ishu ya Mnigeria mmoja,  Ekene Collins Isaac ambaye amehukumiwa kunyongwa hadi kufa baada ya kukutwa na hatia ya kusafirisha dawa za kulevya miaka mitatu iliyopita nchini humo.
Ekene Collins Isaac
Ekene Collins Isaac
Ekene Collins Isaac alikamatwa akiwa amemeza kusafirisha dawa hizo aina ya methamphetamine zenye uzito unaokaribia kilogram moja.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

Monday, December 28, 2015

MAN U , CHALSEA HAKUNA MBABE

Kilichojiri Old Trafford kati ya Man United Vs Chelsea, kutana na matokeo ya mechi za EPL

Michezo 8 ya Ligi Kuu Uingereza imechezwa jana  Jumatatu ya December 28, ikiwa ni muendelezo wa mechi za Ligi Kuu Uingereza, mechi ambayo ilikuwa inapewa nafasi kubwa na hisia za mashabiki wengi wa soka, ni mchezo kati ya Man United dhidi ya klabu ya Chelsea iliyomtimua Jose Mourinho hivi karibuni na kumpa kibarua cha muda Guus Hiddink.
2520
Mvuto wa mchezo huu unakuja kufuatia vilabu hivyo viwili kutofanya vizuri kiasi hata, Chelsea kufikia maamuzi ya kumfuta kazi Jose Mourinho, wakati Man United wakiwa wanahusishwa kuwa katika mpango kama huo wa kutaka kumfukuza kocha wake wa kiholanzi Louis van Gaal.
3704
Mchezo huo ambao ulikuwa umeteka hisia za watu wengi umemamlizika kwa sare ya kutofunga, kwa matokeo hayo Man United wanakuwa nafasi ya 6 ikiwa na point 30, wakati klabu ya Chelsea itakuwa nafasi ya 14 baada ya sare hiyo na kufanya itimize jumla ya point 20.
3321
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu Uingereza zilizochezwa December 28
  • Crystal Palace 0-0 Swansea
  • Everton 3-4 Stoke
  • Norwich 2-0 Aston Villa
  • Watford 1-2 Tottenham
  • West Brom 1-0 Newcastle
  • Arsenal 2-0 Bournemouth
  • Man Utd 0-0 Chelsea
  • West Ham 2-1 Southampton

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, kituo kiko na huduma ya Hosteli na kutoa kozi mbalimbali zikiwemo Computer na lugha za kigeni, Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

MAWAZIRI WENGINE WAAP[ISHWA LEO IKULU

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI IKULU LEO

2
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mh. Profesa Makame Mbarawa Ikulu, ambapo amewapisha mawaziri watano kujaza nafasi za mawaziri zilizokuwa wazi katika wizara kadhaa za serikali ya awamu ya tano, Hafla ya kuwaapisha mawaziri hao imefanyika leo asubuhi.(PICHA NA JOHN BUKUKU – FULLSHANGWE-IKULU)
3
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mh. Gerson Lwenge kuongoza wizara hiyo ikulu leo asubuhi.
4
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango kuongoza wizara ya fedha.
5
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Waziri wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Dk. Joyce Nderichako.
6
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akimuapisha Naibu Waziri wa Wizara ya Ndani Hamad Yussuf Masauni.
7
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa katika picha wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. Goerge Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
8
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akipiga picha ya pamoja na mawaziri walioapishwa pamoja na manaibu Waziri katika  wa pili kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mh. Samia Suluhu Hassan, wa pili kutoka kulia ni Mh. Majaliwa, Kassim Majaliwa Waziri Mkuu, Kulia ni Mh. Goerge Masaju Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Ombeni Sefue.
9
Baadhi ya Mawaziri wakiwa wamekaa katika hafla hiyo kutoka kushoto ni Mh. Dk. Agustino Mahiga waziri wa mambo ya nje , Ushirikiano wa Kimataifa , Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kimataifa na Kikanda,  Mh. Dk. Harrison Mwakyembe Waziri wa Sheria na Katiba, Mh. Charles Kitwanga Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi na Mawasiliano Mh. Injinia Edwin Mgonyani.
10
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mh. Waziri Mkuu Majaliwa, Kassim Majaliwa na Mwanasheria Mkuu wa serikali Mh. George Masaju katika hafla hiyo.
11
Mawaziri walioteuliwa wakisubiri kuapishwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli Ikulu leo jijini Dar es salaam. 
12
Baadhi ya waandishi wa habari waksubiri kushuhudia tukio hilo.

MAAJABU NA KWELI

mzee aliyesafiri kwa miezi saba pekeyake baharini kutoka Marekani..

Kwenye vitu ama stori ambazo zimeonekana kukamata vichwa vya habari vya kimataifa kwa saa kadhaa mfululizo pamoja na mitandao mikubwa, iko pia stori ya mzee mwenye umri wa miaka 53, jina lake ni John Beeden.
Mzee Joe alianza safari yake San Francisco Marekani siku ya June 1 2015 akiwa na boti yake ndogondogo na kufanikiwa kufika Jiji la Cairns Australia, siku ya jana December 27 2015… safari yake imekamilika kwa kusafiri jumla ya siku 209 ambazo kwa hesabu nyingine ni miezi saba kamili !!
Kwa umbali ambao mzee huyo amesafiri, hesabu zinaonesha kuwa amekuwa akisafiri kwa jumla ya saa 15 kila siku ambapo ina maana kwa siku alikuwa na saa kama tisa tu za kupumzika.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

Sunday, December 27, 2015

LIST YA WASHINDI WA TUZO ZA GLOB SOCCER 2015

List ya washindi wa tuzo za Globe Soccer Awards 2015, Lionel Messi kashinda, hii ndio list kamili …

Ikiwa ni siku kadhaa zimepita toka gazeti la Hispania la Marca litangaze list ya wachezaji kumi bora kwa mwaka 2015 ikiongozwa na Lionel Messi ikifuatiwana Neymar na Cristiano Ronaldo kutajwa kuwa nafasi ya nane. December 27 Lionel Messi ametajwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka 2015 (Globe Soccer Awards) inayotolewa kila mwaka.
winners_home-1
List ya washindi wa tuzo za Gloge Soccer Awards 2015
Globe Soccer Awards 2015 zilizotolewa Dubai ni tuzo maalum kwa ajili ya wanasoka, viongozi bora wa klabu, wakala bora, kocha bora. Hizi ni tuzo ambazo zinatolewa kwa uandaaji au ushirikiano wa chama cha mawakala wa wachezaji soka barani Ulaya EFAA (European Association of Player’s Agents) na umoja wa vilabu vya soka barani Ulaya  ECA (European Club Association). Hii ndio list ya washindi wa tuzo hizo kwa mwaka 2015.
  • Lionel Messi (Mchezaji bora wa mwaka)
  • FC Barcelona (Klabu bora kwa mwaka)
  • Jorges Mendes (Wakala bora wa mwaka)
  • Marc Wilmots (Kocha bora wa mwaka)
  • S.L BENFICA (Acadeny bora ya mwaka)
  • Ravshan Irmatov (Refa bora wa mwaka)
  • Josep Maria Bartomeu (Rais bora wa klabu)
  • Andrea Pirlo (Life time Archivement)
  • Frank Lampard (Life time Archivement)


Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA CANDLE EDUCATION CENTRE TANGA

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu, Candle wako na huduma ya Hostel pamoja na kutoa kozi mbalimbali za kielimu na ufundi, Candle wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746