Thursday, June 4, 2015

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO JUNE 04 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
upda
MWANANCHI
Waziri Mkuu Mizengo Pinda atakipa wakati mgumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Bunda, baada ya baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo kutishia kuwa hawatakipigia kura kutokana na kiongozi huyo kutoa ahadi hewa ya upatikanaji wa maji safi na salama.
Wakazi hao wameapa kuwa labda ahadi hiyo iliyotolewa na Waziri Pinda Machi mwaka jana, itekelezwe kabla ya Uchaguzi Mkuu, kinyume cha hivyo hawataipigia kura CCM ili kuonyesha kuwa hawaridhiki na namna wanavyodanganywa.
Wakazi hao walitoa tishio hilo juzi katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa CCM akiwamo, Katibu wa CCM mkoa wa Mara Adam Ngalawa na Naibu Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mfaume Kizigo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo, walisema, wameazimia kutoipigia kura CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba kwa kuwa viongozi wa CCM na Serikali yake wanatoa ahadi za uongo na zisizotekelezeka.
Michael Kweka alitaja ahadi iliyotolewa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda Machi mwaka jana kwamba tatizo la maji lingekoma Juni, kuwa ni moja ya ahadi hewa za viongozi wa Serikali ya CCM zinazowachefua wananchi.
“Hatutawapigia kura za urais, ubunge wala udiwani wagombea wote watakaoletwa na CCM mwaka huu kwa kuwa wanakuwa wakitudanganya kwa ahadi hewa,”Kweka.
Kweka alisema akiwa ziarani wilayani Bunda Machi mwaka huu, Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa ahadi kwamba tatizo la maji lingekwisha ifikapo Juni mwaka huu, lakini hadi sasa hakuna dalili zozote za kumaliza kero hiyo.
Alisema hali hiyo inawafanya wakazi wa mji huo ambao wamekuwa wakidamka nyakati za usiku kutafuta huduma ya maji safi na salama kuichukia Serikali ya CCM, wakiamini kuwa haiwajali. “Mimi kero yangu ni maji. Hiki kimekuwa kilio chetu kwa muda mrefu.
Lakini kinachotuumiza ni ahadi hewa za viongozi wa Serikali ya chama chetu cha Mapinduzi kuhusu mradi unaotekelezwa hapa. Mnaonaje tukiwanyima kura sababu mmezidi ubabaishaji,” alisema mkazi mwingine wa eneo hilo akiwahoji viongozi wa CCM waliokuwapo meza kuu.
Nyerere Lucas aliilalamikia Serikali ya CCM kwa kile alichoeleza kuwa imeshindwa kutimiza ahadi zake za kuboresha miundombinu ya barabara wilayani humo kama ilivyoahidi katika Uchaguzi Mkuu uliopita na kuwafanya wakazi wa maeneo hayo kusafiri kwa tabu kutafuta maji mbali na maeneo yao. Kero nyingine walizolalamikia wakazi wa wilaya hiyo ni mikopo kwa vijana na akinamama.
Walisema mikopo kwa makundi hayo imekuwa ikitolewa kwa watu maaalum hasa vikundi vinavyomilikiwa na watumishi wa serikali, jambo ambalo limeonekana kwamba kuna nia ya dhati ya kuwasahau wananchi.
Hata hivyo, Katibu wa CCM mkoa wa Mara, Adam Ngalawa katika majibu yake ameshindwa kueleza lini mradi huo wa maji utakamilika badala yake akasema umepangwa kutekelezwa katika bajeti ya mwaka
MWANANCHI 
Wanasiasa wanaojiandaa kuingia katika Uchaguzi Mkuu, wametakiwa kumuomba Mungu ili awape nafasi hizo kwa njia sahihi kuliko kutumia ‘sangoma’.
Wito huo ulitolewa jana na Mchungaji Samuel Mshana kwa niaba ya Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Dodoma katika ibada ya kuuaga mwili wa marehemu Eugen Mwaiposa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ukonga (CCM).
Mwaiposa alifariki dunia juzi akiwa usingizini kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa shinikizo la damu, mwili wake ulisafirishwa jana kwa ndege ya kukodi kupelekwa Dar es Salaam ambako utazikwa keshokutwa nyumbani kwake Kipunguni, Dar es Salaam.
Ilikuwa ni siku ya huzuni jana, wakati wa ibada iliyofanyika kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, iliyohudhuriwa na umati wa waobelezaji wakiwamo wabunge, wafanyakazi, viongozi wa mkoa na Taifa akiwamo Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Katika Bunge la kumi, huyu ni mbunge wa saba kufariki dunia.
Akihutubia kwenye ibada hiyo, Mchungaji Mshana alisema ni wakati wa kuangalia namna watu wanavyopaswa kutafuta madaraka kupitia njia zisizofaa.
Serikali katika ibada hiyo iliwakilishwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera na Bunge, Jenister Mhagama, ambaye alisema hadi Mwaiposa kabla ya kukutwa na umauti alionekana mwenye afya njema na aliomba kuchangia katika hotuba ya Wizara ya Afya. Mhagama alisema, Serikali na Chama cha Mapinduzi vimepoteza mtu mahiri ambaye pengo lake halitazibika na kutoa rambirambi ya Sh5 milioni.
MWANANCHI
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM, akieleza kuwa anataka kulifanyia Taifa mambo matano, ikiwa ni pamoja na kutenganisha biashara na siasa na kusimamia maadili ya viongozi wa umma.
Alitaja mambo mengine kuwa ni kusimamia Muungano, kukamilisha mchakato wa kuandika Katiba Mpya, kuweka mfumo wenye motisha kwa wote ili kuchochea uchumi endelevu na wa viwanda, vita dhidi ya rushwa na kukiimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM) kiuchumi.
Sitta alitangaza nia hiyo jana kwenye Ikulu ya Wanyanyembe iliyopo Itetemia, takriban kilomita saba kutoka mjini Tabora.
“Ili kukomesha tatizo hilo (la rushwa), hatuna budi kutunga sheria itakayotenganisha biashara na uongozi,” Sitta alisema akiungana na Rais Jakaya Kikwete ambaye pia aliwahi kuahidi kutenganisha siasa na biashara lakini hadi sasa bado hajatunga sheria hiyo.
“Mtu achague moja, biashara au uongozi wa siasa. Ikiwa mfanyabiashara atataka kuingia katika uongozi wa siasa itabidi akabidhi mali na biashara zake kwa mdhamini atakayeziendesha wakati mhusika anatumikia umma,” alisema Spika huyo wa Bunge la Tisa.
Alisema mikataba mibovu ya huduma na mauzo, ununuzi hewa, ununuzi uliojaa unyonyaji, uteuzi wa wazabuni kwa rushwa na hasa rushwa katika ajira, imelisababisha Taifa hasara kubwa.
Alisema hatua ya pili ya kupambana na rushwa ni kutunga sheria mpya zilizo kali na ambazo zitakuwa na matokeo ya kumzuia mtu asitamani kusaka rushwa.
“Katika hilo tutahakikisha mali za viongozi zinatajwa kwa uwazi. Mali isiyolingana na kipato na kukosa maelezo ya kutosheleza itaifishwe, kesi za rushwa ziwe na utaratibu wenye uwazi,” alisema mbunge huyo wa Urambo Mashariki.
“Tume inayoshughulikia maadili ya viongozi ipewe nguvu kubwa za uchunguzi na ufuatiliaji wa mali za viongozi bila kuzuiliwa na mamlaka yoyote. Pia Tume ifanye kazi zake kwa kuyaweka mambo wazi kuhusu watuhumiwa, tuhuma zao, majibu yao na hatua zinazofuatia. Vikao vya tume vya kusikiliza mashauri ya maadili viwe vya wazi kwa wananchi.”
Alisema adhabu ya utoaji na wapokeaji rushwa itakuwa kali na iambatane na mali zitakazothibitika kupatikana kwa rushwa, zitataifishwa.
NIPASHE
Mji wa Dodoma na viunga vyake, leo unatarajiwa kuwaka moto baada ya vigogo sita wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) watakapokuwa wanachukua fomu ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Vigogo wanaochukua fomu leo ni pamoja na Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, Mawaziri Wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Frederick Sumaye, Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta na Balozi Ali Abeid Karume.
Mbali ya vigogo hao sita, pia yupo kada mwingine wa chama hicho, Amosi Siyatemi, anayelezwa kuwa ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu Mzumbe.
Idadi hiyo ya wanaochukua fomu za kuomba kuwania urais itafikisha jumla ya makada 11 wa CCM ambao tayari wamekwisha kuchukua fomu za kuomba ridhaa kwa chama chao kuwania nafasi ya juu ya uongozi nchini.
Wengine waliochukua fomu jana ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere na Balozi Amina Salum Ali.
Lowassa alitakiwa kuchukua fomu jana, lakini aliahirisha kutokana na msiba wa Mbunge wa Ukonga, marehemu  Eugen Mwaiposa, aliyefariki dunia usiku wa kuamkia juzi mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, wa kwanza kuchukua fomu atakuwa Siyatemi, akifuatiwa na Sumaye, Dk. Bilal, Balozi Karume, Lowassa na atakayefunga dimba ni Dk. Magufuli.
NIPASHE
Zaidi ya tembo 10,000 katika Hifadhi ya Ruaha-Rungwa wamepotea ama hawajulikani walipo.
Akitangaza matokeo ya sensa ya tembo ya mwaka 2014 mjini hapa jana, Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, alisema wataalam wa hifadhi wameshindwa kubaini waliko au nini kimewatokea tembo hao na kulinganisha kupotea huko sawa na ilivyotokea kwa ndege ya Malasia Machi mwaka huu ambayo haijaonekana hadi leo.
Sensa hiyo ilifanywa na Shirika la Taifa la Utafiti Wanyamapori (TAWIRI), Frankfurt Zoological Society na Vulcan Inc katika eneo la kilomita za mraba 268,692 ambazo ni sawa na asilimia 28.3 ya eneo lote la nchi, kuanzia Mei hadi Novemba 2014.
Maeneo ilikofanyika sensa hiyo ni Serengeti, Tarangire-Manyara, Katavi-Rukwa, Burigi-Biharamulo, Malagarasi-Muyovosi, Soulus-Mikumi na Ruaha-Ruangwa, Mkomazi na Saadani.
“Wizara yangu inajipanga kikamilifu kujua sababu za kupotea kwa tembo hao…je?, waliuawa au waliondoka katika eneo la hifadhi?. Kwa kawaida kama kuna idadi kubwa ya vifo vya wanyama kama hiyo kunakuwa na mabaki ya mizoga au mifupa kitu ambacho hakijaonekana tangu kupotea tembo hao,” alisema.
Idadi ya tembo katika Hifadhi ya Ruaha-Rungwa imepungua kutoka 20,000 mwaka 2013 hadi kufikia 8,272 mwaka 2014.
“Tembo 10,000 katika Hifadhi ya Ruaha-Rungwa hawajulikani walipo na wala mizoga yao haijaonekana, wamepotea kama ile ndege ya Malasia. Hali hii inatufanya kuendesha sensa nyingine majira ya kiangazi kuanzia Agosti hadi Novemba, wataalam wanajiuliza kila siku tembo hao wamepotelea wapi, hizi ni habari zinazosumbua,” alisema.
Aidha, alisema matokeo ya sensa hiyo pia yamebaini kuwapo kwa upungufu mkubwa katika mfumo wa ekolojia ya Ruaha-Rungwa.
Akitangaza matokeo ya ujumla ya sensa hiyo, Nyalandu alisema imeonyesha kupungua kwa tembo kutoka 110,000 mwaka 2009 hadi 43,330 mwaka 2014.
Hata hivyo, waziri huyo  alisema idadi ya tembo imeongezeka kutoka 13,000 mwaka 2013 hadi 15,217 mwaka jana, ongezeko ambalo ni zaidi ya tembo 2,000.
MTANZANIA
Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Harrison Mwakyembe, ameibuka na kusema hajawahi kumshambulia kwenye mitandao Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kuhusu sakata la Richmond.
Kauli hiyo ya Dk. Mwakyembe imekuja siku chache baada ya kusambazwa kwa waraka unaodaiwa kuandikwa naye, ukimuhusisha na tuhuma za kumshambulia Lowassa, jambo ambalo amelifananisha kuwa ni sawa na siasa za kitoto.
Alisema kutokana na kusambazwa kwa waraka ambao umeandikwa nyadhifa zake za ubunge na uwaziri, hivi sasa ameshaanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya watu waliokuwa wakiusambaza.
Waziri Mwakyembe ambaye kitaaluma ni mwanasheria na mwanahabari, alisema anapata shaka hata na baadhi ya vyombo vya habari pamoja na mitandao hiyo na kudai kuwa anamshambulia Lowassa.
“Ninashangazwa sana na hii mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari (magazeti), vimekuwa vikiandika vitu vibaya ikiwa ni pamoja na kumshambulia Lowassa wakati hata siku moja sijazungumza nao.
“Kitendo cha baadhi ya watu wa aina hii kuwaandika vibaya wanasiasa katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya watu wengine ni ishara ya woga wa kisiasa na kushindwa kujiamini katika misimamo yao.
“…Kinachonikera kupindukia ni kuwa taarifa hizo sijawai kuziandika ila kuna mtu ama kundi maalumu la watu limeziandika na kuweka jina langu na nafasi zangu za uongozi kama mbunge na waziri, huu si uungwana na wala si siasa kwa kuchezea majina ya watu. Kama siasa zimefika huku basi ni za hatari,” alisema.
Dk. Mwakyembe ambaye pia ni Mbunge wa Kyela mkoani Mbeya, alisema katika kipindi hiki cha kuelekea Uchaguzi Mkuu, watu wanapaswa kuacha woga na kutojiamini.
“Kitendo cha kutumia majina ya watu na kuelezea hisia zao ni kukosa ujasiri na hata yanayosambazwa kwenye mitandao hayaendani na hadhi yangu kiongozi, sina tabia ya woga na uongo,” alisema.
Alisema baada ya kupata taarifa zilizopo mitandaoni alilazimika kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi Kitengo cha Makosa ya Mtandaoni pamoja na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), ili kulalalimikia mchezo huo mchafu.
Dk. Mwakyembe alisema vyombo hivyo vimeshaanza uchunguzi mkali ili kuwabaini watu walioandika na kutuma taarifa hizo.
Alisema kutokana na hali hiyo, amedhamiria na kuhakikisha kesi ya kwanza ya matumizi mabaya ya mitandao inaanzia kwake kwa kuwa hana utamaduni wa woga, na watu wanapaswa kuwa wazi endapo wanakuwa na vitu na si kutumia majina ya watu.
Dk. Mwakyembe alisema anashangazwa na watu kutumia jina lake kumchafua kwa kuwa hana tatizo na mtu yeyote na kama chanzo ni suala la Richmond, ilikuwa ni kazi aliyopewa na Bunge.
MTANZANIA
Baadhi ya wagonjwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), wamelalamikia hatua ya uongozi wa hospitali hiyo kushindwa kuchukua hatua za dharura za kutoa huduma za CT-Scan, ambayo imeharibika kwa kipindi cha miezi miwili sasa.
Wagonjwa hao walisema wamekuwa wakiteseka kwa kipindi cha miezi miwili sasa bila kupata huduma hiyo.
Mmoja wa wagonjwa hao aliyejitambulisha kwa jina la Rashid Omari, alisema ni mwezi wa pili sasa amekuwa akienda na kurudi hospitalini hapo bila ya kupata huduma.
“Kila nikifika bado nakutana na bango la ujumbe unaosomeka mashine ni mbovu mafundi wanafanya matengenezo, nimekuwa nikienda na kurudi huku tatizo likizidi kukuwa, mpaka sasa sijui hatima yangu itakuwaje,” Omari.
Ofisa Uhusiano wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha, alikiri kuharibika kwa mashine hiyo na kusisitiza kuwa tayari uongozi umeshaagiza kifaa cha mashine hiyo kutoka nchini Afrika Kusini.
“Tunatarajia kifaa hicho kitafika haraka iwezekanavyo ili kuweza kuwapatia huduma ya kipimo cha CT-Scan wagonjwa wetu wanaokuja kwa ajili ya kufanyiwa kipimo hicho,” ligaesha.
MTANZANIA
Baraza Kuu la Uongozi la Chama cha Wananchi (CUF), limemvua uanachama mjumbe wake kutoka Mkoa wa Shinyanga, Chifu Lutayosa Yemba.
Chifu Yemba ambaye pia alikuwa ni mpinzani wa Prof. Ibrahim Lipumba katika kuwania uenyekiti wa CUF kwenye uchaguzi uliofanyika mwaka jana, alivuliwa uanachama kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha za chama pamoja na kutumia vibaya jina la mwenyekiti wa chama hicho.
Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya kikao hicho cha Baraza Kuu kilichoanza vikao vyake jana jijini Dar es Salaam, kilisema kuwa tuhuma za mjumbe huyo zilifikishwa mbele ya kikao hicho na kufikiwa uamuzi huo.
“Kikao cha Baraza Kuu bado kinaendelea hapa na ajenda kubwa ilikuwa ni tuhuma dhidi ya Chifu Yemba ambaye anadaiwa kutumia jina la Mwenyekiti wa chama kuanzisha Saccos na hata kusababisha chama kudaiwa shilingi milioni 12.
“Lakini pia amekuwa akitumia jina la Mwenyekiti wa chama, Profesa Lipumba katika mradi wake huo binafsi ambao anauendesha na hata kusababisha chama kuingia katika mgogoro hasa katika Mkoa wa Shinyanga,” kilisema chanzo hicho.
Chifu Yemba alipambana na Profesa Lipumba katika uchaguzi wa kuwania nafasi ya uenyekiti ambapo alipata kura 30 huku Lipumba akishinda kwa kura 659 na kufanikiwa kukiongoza tena chama hicho.
Chanzo hicho kilisema baada ya kufikiwa kwa uamuzi wa kuvuliwa uanachama kwa Mjumbe huyo wa Baraza Kuu, alitolewa nje ya ukumbi kwa ulinzi maalumu hadi nje ya geti na kuondoka.
Yemba kwa muda amekuwa haelewani na hata kushambuliana katika mitandao ya kijamii na Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Abdul Kambaya ambaye hivi karibuni alishindwa kura za maoni za kuwania ubunge wa Jimbo la Kinondoni.
Kutokana na kushindwa huko kwa Kambaya, kuliibua hisia mbalimbali miongoni mwa wana CUF hali iliyosababisha baadhi ya kikundi cha watu kuandamana na kwenda Makao Makuu ya CUF kufikisha malalamiko yao kuhusu mwenendo wa uchaguzi Kinondoni.
Alipotafutwa Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Uenezi wa CUF, Abdul Kambaya, alithibitisha kuvuliwa uanachama kwa Chifu Yemba na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la CUF.
Kwa habari na matukio mbalimbali ni hapa hapa tangakumekuchablog

Wednesday, June 3, 2015

KITRISHO CHA EBOLA CHATOWEKA SERALEON

Kenya Airways yarudisha safari za S.Leone

Shirika la ndege la Kenya limeanza tena kusafirisha wateja wake baina ya miji ya Nairobi na Freetown nchini Sierra Leone.
Ni shirika la kwanza kurejea nchini humo baada ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola kuzuka mwaka uliopita.
Idadi ya maambukizi inapungua na kumekuwa na watu 12 tu waliopata maradhi hayo katika wiki moja iliyopita.
Shirika la ndege la Ufaransa pia linatarajiwa kurejea nchini humo baadaye mwezi huu.

JEURI YA PESA

Hii gari ilikuwa story kubwa sana mitandaoni TZ ikahusishwa na pesa za ESCROW, ni kweli iko TZ?

B7k1IiDIQAA0pUg
Story zilikuwa nyingi mitandaoni kuhusu picha ya hii gari.. nakumbuka wakati ule ishu ya ESCROW ilikuwa bado mjadala mkubwa Bungeni na mtaani pia hapa TZ.. Watu wakasema kuna kigogo mmoja wa ESCROW ndio aliyeagizia hii Rolls Royce Phantom.
Hii iko kwenye mitandao tena, hii gari ni story kubwa Nairobi kila inakopita yani.. Kumbe haikutua TZ kama ambavyo watu walidhani, ilitua Kenya na iko tayari mtaani mtu anatembelea.
Rolls Dude
 Hapa tayari iko barabarani na namba za usajili wa Kenya.
rolls_r
rolls2
Rollls
Hii ndio headline ya story ya leo kutoka , Jiji la Nairobi.
Kwa habari matukio na mambo kedekede , ni hapa hapa tangakumekuchablog

KITISHO CHA NDOVU KUTOWEKA TZ YATANDA

Idadi kubwa ya ndovu yatoweka Tanzania


Wanaharakati wa wanyamapori wameelezea hali ya kutoweka kwa idadi ya ndovu kwa asilimia sitini nchini Tanzania katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kama janga.
Kwa mujubu wa kikundi  kinachofuatilia maisha ya wanyamapori, TRAFFIC, linasema idadi hiyo inaashiria kiwango halisi cha uwindaji haramu.
Waziri wa Maliasili na Utalii   Tanzania Lazaro Nyalandu, amesema kuwa tatizo hilo lipo kwa kiwango tofauti nchini humo, akitoa mfano kuwa eneo la Serengeti idadi yao inaongezeka .
Amesema mamia ya walinzi wa wanyamapori wamekodiwa kukabiliana na uwindaji haramu

FIFA , NI MOTO KWENDA MBELE

FIFA:Interpol yataka maafisa 6 kukamatwa

Shirika la maafisa wa polisi wa kimataifa Interpol limetoa ilani ya kukamatwa kwa watu sita wanaohusishwa na FIFA kufuatia madai ya kuhusika na ufisadi.
Agizo hilo linawalenga maafisa wanne wa mashirika makuu pamoja na maafisa wawili wakuu wa zamani wa shirikisho la soka duniani FIFA akiwemo aliyekuwa makamu wa rais wa shirikisho hilo Jack Warner.
Sita hao tayari walikuwa wametajwa katika mashtaka yaliofunguliwa dhidi yao na mamlaka ya mahakama za Marekani wiki iliopita.
Ilani hiyo inawalenga watu wanaotafutwa kwa lengo la kuwakamata ili wasafirishwe hadi mataifa waliohusika na ufisadi huo ili washtakiwe ,lakini mataifa hayawezi kulazimishwa kumzuilia mtu yeyote aliyetajwa.

RAFAEL NADAL HAVUMI LAKINI NAE YUMO

Bei ya saa ya staa wa Tennis Rafael Nadal nayo kwenye headlines..

nadaa
Ukiwazungumzia wanamichezo ambao wana utajiri mkubwa zaidi duniani jina la Cristiano Ronaldo, Floyd Mayweather au Messi huenda ndio wanaoongoza kwa kuwa na utajiri mkubwa zaidi.
Kuna wanamichezo wengine ambao ni nadra kuwasikia wakijitangaza au kutajwa kuwa na utajiri mkubwa lakini mmoja wao ni mcheza tenis Rafael Nadal ambaye naye ameamua kuonyesha jeuri ya fedha.
nadal2
Wakati wa michuano ya French Open alipokuwa akipambana na Jack Sock, Nadal alivaa saa yenye thamani ya pauni 510,000 ambazo ni sawa na fedha za kitanzania zaidi ya bilioni 1.7.
Saa hiyo aina ya  RM27-02 imetengenezwa na kampuni ya Luxury Swiss na unaambiwa kampuni hiyo ilitengeneza saa 50 tu za aina hiyo ambayo moja imevaliwa na mchezaji huyo.
huyu
Rafael Nadal ni bingwa wa michuano ya French Open mara tisa.
Kwa habari na michezo pamoja na matukio mbalimbali ni hapa hapa tangakumekuchablog

BENITES AINGIA MADRID KIMKWARA

Rafa Benitez aanza usajili Real Madrid.

Rafa-Benitez

Zikiwa zimepita dakika chache tangu kocha Rafa Benitez alipothibitishwa kuwa kocha mpya wa Real Madrid , taarifa mpya juu ya wachezaji watakaosajiliwa chini yake imeibuka .
Kocha huyo mpya alikutana na Rais wa Real Madrid Florentino Perez hapo jana usiku wakati wa chakula usiku na agenda kuu ya mkutano wao ilikuwa usajili wa wachezaji akiwemo kipa wa Manchester United David De Gea.
Kwa mujibu wa habari za ndani , Benitez ameidhinisha usajili wa De Gea na kinachosubiriwa ni mazungumzo rasmi baina ya Real pamoja na Manchester United ili kukamilisha usajili wa kipa huyo .
Real Madrid wamekuwa wakimfuatilia David De Gea kwa muda mrefu na inaonekana kuwa ni kiasi cha muda tu kabla ya usajili wa mchezaji huyo kukamilika japo Manchester United kwa upande mwingine wamekuwa wakihaha kumsainisha mkataba mpya .
wachezaji wa Man United wanafikiri kuwa David De Gea hatarudi kwenye timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao .
wachezaji wa Man United wanafikiri kuwa David De Gea hatarudi kwenye timu hiyo kwa ajili ya msimu ujao .
Hivi karibuni United imeweka ofay a mshahara wa paundi 200,000 kwa kipa huyo oa ambayo hata hivyo bado hajaikubali na inaaminika kuwa moyo wake umeamua kuwa atajiunga na Real .
Kwa upande mwingine wachezaji wengi ndani ya Old Trafford wanaamini kuwa kipa huyo hatarejea klabuni hapo kwa msimu ujao na viongozi wa United akiwemo kocha Louis Van Gaal wameanza kufanya mipango ya kusajili kipa mwingine .

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Kila mmoja hutamani harusi yake iwe ya kitofauti…lakini huyu alitamani yake iwe hivi!!(Pichaz)

aruc
Maharusi wengi hutamani siku ya harusi kuwa siku ya kitofauti zaidi katika maisha yao wakiamini ndio siku pekee ambayo ni ya furaha zaidi huku wengine wakitumia kila aina ya njia kuhakikisha sherehe yao inapendeza.
bride
Utakuta wengine wanatumia usafiri wa farasi au magari ya kifahari kuhakikisha tu sherehe inakuwa ya kipekee zaidi kwao lakini kwa Jenny Buckleff ilikua tofauti kwani yeye alitumia jeneza kama usafiri wake.
aruc2
Jenny alitaka kuwashangaza wageni waliofika kwenye sherehe yake hata kwa mumewe pia kwani hakumwambia mtu yoyote kuhusu uamuzi wake huo.
nne
Siku ya sherehe aliingia ukumbini akiwa ndani ya jeneza lililokuwa likisikumwa kwa pikipiki huku kila mmoja akishikwa na butwaa kutokana na kitendo hicho ambacho si rahisi kutokea.
akitoka
Kwa habari , matukio na michezo ya papo hapo ni hapa hapa tangakumekuchablog

WALAJI WA NYAMA YA MBWA UJUMBE HUU HAPA

Kumbe nyama ya mbwa inaweza kukusababishia kifo? kuna hawa watu imewatokea..

mee
Kuna baadhi ya nchi kama China wana desturi ya kula nyama ya mbwa hata baadhi ya makabila ya hapa Tanzania inadaiwa hutumia nyama ya mbwa kama kitoweo.
Pamoja na ulaji huo ambao wengi wao wanaamini hauna madhara, kuna taarifa kutoka Nigeria zinazohusisha watu watano kupoteza maisha baada ya kudaiwa kula nyama hiyo wakiwa katika hoteli moja ambayo ni maarufu kwa ulaji wa nyama ya mbwa.
Brain Ogbondah ambaye ni mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo alisema watu hao waliripotiwa kufa ikiwa ni muda mchache baada ya kula nyama hiyo iliyoandaliwa na Friday Dickson.
Uchunguzi wa tukio hilo bado unaendelea na viongozi wa familia wamewataka watu kuacha kula nyama hiyo.
Kwa habari matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO JUNE 03 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

late
MTANZANIA
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU), imetakiwa kukunjua kucha zake kwa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Prof. Ibrahim Lipumba, alisema sasa umefika wakati kwa Takukuru kuhakikisha wanadhibiti matumizi ya fedha kwa wagombea wanaotangaza nia katika vyama mbalimbali.
Profesa Lipumba ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), alisema ni lazima Mkurugenzi wa Takukuru, Dk. Edward Hosea, aeleze mikakati yake ya namna atakavyopambana na rushwa, hasa kwa wagombea ambao si waadilifu na ambao wamekuwa wakitumia fedha.
“Ni muhimu katika kipindi hiki kuelekea Uchaguzi Mkuu, Dk. Hosea akaelezea mikakati yake ya kupambana na wanaowania uongozi ambao wanakiuka maadili ili waeleze fedha wanazotumia wanazitoa wapi. Na jambo hili liwe kwa vyama vyote,”Prof. Lipumba.
Akizungumzia uteuzi wa wagombea ubunge na urais kupitia Ukawa, alisema hivi sasa kila chama kipo katika mchakato wa ndani kwa ajili ya kukamilisha taratibu zake.
“Ukawa unaendelea vizuri, nami nimetangaza nia ndani ya chama changu kwa nafasi ya urais, nasubiri mkutano mkuu wa chama chetu ndiyo utatoa uamuzi wa mwisho.
“Tukishakamilisha kazi hii kwa kila chama sasa ndiyo kamati maalumu ya viongozi itaketi kwa mujibu wa utaratibu uliowekwa na Ukawa na kisha utatoa na jina la mgombea mmoja wa urais ambaye atapambana na vyama vingine,”  Lipumba.
Alizungumzia pia utendaji kazi na weledi wa taasisi za Serikali ikiwamo Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB), ambao walichunguza tukio la kupigwa kwa viongozi na wafuasi wa CUF Januari 27, mwaka huu wakati walipokuwa wanakwenda kuahirisha mkutano wa hadhara.
Ripoti iliyotolewa na tume hiyo, ilieleza kwa kina namna Jeshi la Polisi lilivyotumia nguvu kupita kiasi na hata kusababisha majeruhi kadhaa kinyume cha sheria.
MTANZANIA
Mbunge wa Ukonga jijini Dar es Salaam, Eugen Mwaiposa, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana mjini Dodoma akiwa usingizini.
Akitangaza msiba huo bungeni jana, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai, alisema Mwaiposa alifariki dunia akiwa nyumbani kwake eneo la Chadulu mjini hapa.
Alisema kwa muda mrefu mbunge huyo aliyeingia bungeni kwa mara ya kwanza mwaka 2010, alikuwa na tatizo la shinikizo la damu.
Wabunge walikuwa wakiendelea kuchangia bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bunge, Lediana Mng’ong’o ambaye ghafla alimkatiza mchangiaji kuzungumza na kumpisha kwenye kiti Naibu Spika Ndugai, ambaye alitoa taarifa za kifo cha mbunge huyo.
Ndugai, alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa uchunguzi zaidi wa wataalamu.
Alisema mwili wa marehemu utaagwa kesho mjini hapa baada ya ndugu wa marehemu kuwasili.
Kutokana na msiba huo, Ndugai alitangaza kuahirishwa kwa Bunge hadi keshokutwa na kuagiza Kamati ya Uongozi kukutana na wabunge watapatiwa taarifa kwa njia ya mtandao wa simu.
“Natumia kifungu cha 152 kuahirisha Bunge hadi Alhamisi saa 3:00 asubuhi,” Ndugai.
Mwaiposa ni mbunge wa pili kufariki dunia kwa mwaka huu, akimfuatia Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba, aliyefariki dunia Februari 28.
NIPASHE
Makada watano wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo watafungua pazia kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa na chama hicho kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Leo ndiyo siku ya kwanza ya uchukuaji fomu ndani ya CCM kwa ajili ya kurithi nafasi ya Rais Jakaya Kikwete ambaye anang’atuka kwa mujibu wa katiba ya nchi.
Makada watakaochukua fomu hizo leo baada ya kutangaza nia kuwania nafasi hiyo ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya; Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Stephen Wasira; Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa; Balozi wa Umoja wa Afrika (AU) katika Umoja wa Mataifa (UN), Balozi Amina Salum Ali na Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Charles  Makongoro Nyerere.
Makada hao watatangulia kuchukua fomu hizo huku chama hicho kikitoa masharti makali yanayotakiwa kufuatwa na wagombea.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM wa Idara ya Oganizesheni, Dk. Mohamed Seif Khatibu, alisema makada watano wataanza kufungua pazia la uchukuaji fomu leo katika makao makuu CCM mjini Dodoma.
Alisema katika utaratibu huo, Prof. Mwandosya ndiye atakayekuwa wa kwanza kuchukua fomu saa 4:00 asubuhi akifuatiwa na Wasira.
Dk. Khatibu alisema Lowassa atakuwa wa tatu kuchukua fomu hiyo saa 7:00 mchana, akifuatiwa na Balozi Amina saa 8:30 na Nyerere atafunga dimba kwa leo.
Alisema ratiba ya uchukuaji fomu hiyo haikupangwa kwa kufuata umaarufu au cheo cha mtu ndani ya chama na serikali bali umezingatia mgombea kuwahi kutoa taarifa katika chama kwamba anataka kuchukua fomu.
Kwa upande wa Zanzibar, alisema wagombea wanaowania urais wa Zanzibar watachukulia fomu katika ofisi za CCM na wale wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watachukulia mjini Dodoma.
NIPASHE
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani ya  Nchi, Pereira Ame Silima, amesema moja ya mambo ambayo hayakufanyika vizuri mwanzoni wakati wa uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa ni kutovifanya vitumike kupiga kura katika uchaguzi mkuu.
Amesema kama kitambulisho hicho kingeboreshwa kingeweza kutumika kwa ajili ya kupiga kura, hivyo kusingekuwapo uandikishaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Waziri huyo aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam,  wakati wa ufunguzi wa kongamano la kimataifa la uandikishaji wa vitambulisho vya Taifa lijulikanalo kama ‘Govetnment Forum on Electronic Identity in Africa’, unaofanyika Afrika kwa mara ya kwanza na kujumuisha wataalam zaidi ya 300 wa ndani na nje ya Afrika.
“Kama tungejipanga mwanzo vizuri ni wazi kusingekuwapo haja ya mchakato unaoendelea wa kuandikisha kwa kutumia BVR, ni nafasi kwetu kujifunza na kujirekebisha na pia watajifunza kutoka Tanzania,”.
Silima alisema siku zijazo vitambulisho hivyo vitaboresha zaidi ili kutumika kwenye maeneo mbalimbali, na kwamba kwa siku za usoni vitatumika kwenye malipo mbalimbali.
Aliwataka Watanzania wanaoshiriki katika kongamano hilo kupokea na kutumia teknolojia inayotoka kwenye makampuni mbalimbali duniani.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Dickson Maimu, alisema watu milioni 6.1 wameandikishwa katika maeneo ya Zanzibar, Dar es Salaam, Pwani, Lindi, Mtwara, Morogoro na Tanga na kwamba watu milioni 2.5 wamepatiwa vitambulisho.
Alisema kongamano hilo linalojulikana ‘Govetnment Forum on Electronic Identity in Africa’, limeleta pamoja nchi 24 ambazo zitajadili kwa kina changamoto zilizopo kwenye uandikishaji, uandaaji wa vitambulisho vya Taifa na jinsi gani vitatumika kwa maendeleo ya Taifa.
NIPASHE
Waziri wa Uchukuzi Samuel Sitta, amevunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari (TPA) iliyoundwa na mtangulizi wake, Dk. Harrison Mwakyembe, na kuunda bodi mpya yenye wajumbe wanane kuanzia Juni 2, mwaka huu.
Uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa kifungu Namba 6 Kifungu kidogo cha 2 (b) cha Sheria ya Bandari namba 17 ya mwaka 2004 kinachompa mamlaka ya kuvunja na kuteua wajumbe wa bodi.
Sitta alitangaza uteuzi huo jana jijini Tanga wakati wa ziara ya kikazi katika Bandari ya Tanga na baadaye kuzungumza na wafanyakazi waliokusanyika katika uwanja wa Baraka na kusisitiza kuwa mabadiliko hayo yametokana na vitendo vya uonevu alivyokuta vikiendelea kufanywa ndani ya TPA.
“Uteuzi huu unatengua uteuzi wa wajumbe wa sasa wa bodi hiyo kuanzia leo Juni 2, mwaka huu na lengo la uteuzi wa wajumbe hawa ni kuleta tija na ufanisi wa utendaji kazi ndani ya wa Mamlaka na kwa nafasi ya Mwenyekiti mpya wa Bodi nasubiri uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete kwani ndiye mwenye mamlaka hiyo kisheria,” alisema.
Dk. Mwakyembe aliteua bodi ya TPA  Novemba 6, 2012.
NIPASHE
Taasisi za serikali zinadaiwa Sh. bilioni 20 na mamlaka za maji nchini.
Hayo yalisemwa jana bungeni na Naibu Waziri wa Maji, Amos Makalla, alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Leticia Nyerere.
Mbunge huyo alisema ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara inadaiwa Sh. milioni 102 na Jeshi la Wananchi wa Tanzania linadaiwa Sh. milioni nane na kuhoji kwa nini serikali haiingilii kati ili kuhakikisha kwamba madeni hayo yanalipwa ili kuiwezesha Mamlaka ya Maji ya Musoma (MUWASA) kufanyakazi yao kikamilifu na kwa mafanikio.
Akijibu, Makalla alikiri serikali kutambua kuwapo kwa madeni hayo.
Alisema Jeshi la Wananchi linadaiwa Sh. milioni 2.4, hospitali zinadaiwa Sh. milioni 113 na madeni mengine hivyo mamlaka hiyo inaidai serikali jumla ya Sh. milioni 390 na kwamba mamlaka zote za maji nchini zinaidai taasisi za  serikali Sh. bilioni 20.
“Sisi (Wizara ya Maji) tutashirikiana na Wizara ya Fedha kuona kwamba madeni haya yanalipwa ili mamlaka hizi ziweze kufanyakazi kwa ufanisi,” alisema.
Awali katika swali la msingi, Mbunge wa Musoma Mjini, Vicent Nyerere, alitaka kujua kama serikali ipo tayari kutoa ruzuku kwa mamlaka za maji ikiwamo Muwasa ili ziweze kujiendesha na kupunguza mzigo kwa wananchi.
Pia alihoji kama ni sawa wizara na idara za serikali kama JWTZ, Polisi, Ikulu kukatiwa maji kwa kushindwa kulipia huduma hiyo.
Akijibu, Makalla alisema serikali ilianzisha mamlaka za majisafi na usafi wa mazingira nchini ambazo ziko katika madaraja matatu, ‘A’, ‘B’ na ‘C’.
Alifafanua kuwa mamlaka za daraja ‘B’ ni zile ambazo zinapata ruzuku ya kulipia sehemu ya gharama za umeme wa kuendesha mitambo.
HABARILEO
Watanzania milioni 25.4 wamejitokeza kupima Ukimwi kwa hiari, ikiashiria kwamba nusu ya Watanzania wamepima kujua hali yao kuhusu maambukizi ya Ukimwi.
Idadi hiyo ni ongezeko la watu milioni 4.9 waliopima kufikia Desemba 2013.
Takwimu hizo zimetolewa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Seif Rashid wakati akiwasilisha bajeti ya wizara yake katika kikao cha 19 cha mkutano wa 20 wa Bunge.
Alisema hadi kufikia Desemba 2014, idadi ya watu waliopima virusi vya Ukimwi (VVU), walikuwa 25,468,564 na kufanya ongezeko la watu 4,999,323.
Kwa mujibu wa Waziri wanaopima VVU kwa hiyari imeongezeka kutoka watu 11,640 mwaka 2009 na kufikia 20,469,241 kwa mwaka 2013.
Alisema mafanikio hayo yametokana na kutekelezwa mpango mkakati wa lll wa sekta ya afya katika kupunguza maambukizi ya Ukimwi.
Alisema takwimu zilizopo zinaonesha kuwa kampeni imefanikiwa kuhamasisha wananchi na pia kupunguza kiwango cha maambukizi ya VVU kutoka asilimia 5.8 mwaka 2008 hadi 5.3 mwaka 2012 .
Alisema pamoja na kuendelea kutekeleza mpango mkakati huo wa tatu wa sekta ya afya wa kupambana na Ukimwi (2013-2017) kwa kutoa ushauri nasaha na upimaji wa VVU kwa hiari, wizara itaendelea kupanua huduma na upimaji kufikia ongezeko la watu 7,411,619 na kutoa dawa za ARV kwa waviu 880,681.
Aidha, alisema kwamba wizara yake imewezesha kliniki 109 zinazotoa ARV kwa wanawake wajawazito wenye VVU (Option B+) ziweze pia kutoa huduma za kupambana na Ukimwi kwa watoto wanaosihi na VVU.
MWANANCHI
Waziri Mkuu  wa zamani, Frederick Sumaye ametangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, huku akibainisha kuwa amejipima, ametafakari na kujiridhisha kuwa anatosha kushika wadhifa huo wa juu nchini.
“Kama kuna mtu mwingine amekamilika kuliko mimi niambieni na nitampisha (katika mbio za urais),” alisema Sumaye wakati akitatangaza nia hiyo jana jijini Dar es Salaam mbele ya wanahabari, akitumia takriban saa moja na nusu kueleza sifa za Rais ajaye na vipaumbele vyake.
Sumaye, mmoja wa makada sita waliokuwa wamefungiwa na CCM kwa kukiuka taratibu za kampeni, alikuwa Waziri Mkuu kwenye Serikali ya Awamu ya Tatu kwa kipindi chote cha miaka kumi na pia alikuwa mbunge wa Hanang hadi alipoamua kutogombea nafasi hiyo mwaka 2010.
Waziri huyo mkuu wa zamani amekuja na kauli mbiu ya Uongozi Bora: Komesha Rushwa, Jenga Uchumi, huku akibainisha vipaumbele vyake kuwa ni pamoja na kujenga na kuimarisha uchumi.
Vipaumbele vingine ni kulinda Muungano, mshikamano, amani na utulivu na kuboresha huduma za kijamii na maisha ya Watanzania, kupambana na maovu ya rushwa, ufisadi, dawa za kulevya, mauaji ya kishirikina, uhusiano wa kimataifa na masuala muhimu ya uhifadhi wa mazingira, kilimo, ajira, ulinzi wa rasilimani na michezo na utamaduni.
Sumaye alisema Watanzania wanataka Rais anayetambua uzito wa kazi iliyopo mbele yake na wananchi wote na awe tayari kuwa Jemedari wa Jeshi hilo ili kupata ufumbuzi wa matatizo yao yanayowakabili.
Alisema wananchi wengi wanamfahamu kwa utendaji wake naye anajua wanachokihitaji na sifa za Rais wanayemhitaji, hivyo yeye ndiye anayefaa kwa nafasi hiyo.
“Mtu anayetaka kuwa Rais ni lazima awe tayari kujipima, kutafakari, ajiridhishe, kuwa anatosha kiafya, kiakili, kimaadili na kidhamira kuwaongoza Watanzania.
“Kama kuna mtu anapungukiwa kimojawapo, hana sifa za kuwaongoza Watanzania,” alisema Sumaye huku akishangiliwa na baadhi ya wafuasi waliomsindikiza katika mkutano huo uliofanyika Hoteli ya Hyatt Regency.
Alisema kiongozi huyo awe tayari kupimwa na umma vigezo hivyo na siyo ajipime na kwamba yeye yupo tayari kupimwa na umma.
Katika hotuba yake hiyo iliyokuwa ikirushwa na baadhi ya televisheni na redio nchini, alisema Watanzania wanahitaji Rais atakayekuwa mtumishi wa kuwaongoza na siyo bosi, na pia awe mtu atakayewaongoza kwa uadilifu.
Sifa nyingine za kiongozi huyo ni kuwa mzalendo wa dhati anayejua Watanzania walipotoka, wanapopitia na wanakoelekea; mwaminifu, mjasiri, mtiifu wa sheria na katiba na anayeheshimu mipaka ya cheo chake.
MWANANCHI
Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), Sepp Blatter ametangaza kuwa atajiuzulu nafasi yake hiyo kutokana na kashfa ya rushwa iliyolikumba shirikisho hilo.
Akitangaza uamuzi huo, Blatter mwenye miaka 79 alisema baada ya kuitisha mkutano wa dharula wa Fifa: ”Muda mfupi ujao kunatakiwa kuchaguliwe rais mpya.”
Blatter alichaguliwa wiki iliyopita kuliongoza shirikisho hilo, licha ya wajumbe saba wa juu wa Fifa kukamatwa na maafisa usalama wa Marekani siku mbili kabla ya uchaguzi huo.
Blatter alisema: “Uamuzi huu hauungwi mkono na kila mtu.”
Awali Fifa ilikanusha madai kwamba katibu wao mkuu, Jerome Valcke alihusika katika kashfa ya ufisadi ambapo hongo ya mamilioni ya dola ilitolewa.
Fifa inasema hamna afisa wake yeyote wa ngazi ya juu aliyehusika kwa njia yoyote katika kashfa hiyo.
Inasemekana malipo hayo ya rushwa yalitolewa na serikali ya Afrika Kusini kwa maafisa wa soka wa huko Marekani ili waunge mkono wenzao Waafrika waliong’ambo katika nchi za visiwa vya Caribbean.
Waendesha mashtaka wa Marekani wanasema hongo hiyo ilinuiwa kusaidia kununua kura kuiwezesha Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia lililofanyika mwaka 2010.
Kwa habari matukio na michezo kutoka pembe mbalimbali, ni hapa hapa tangakumekuchablog

Tuesday, June 2, 2015

MAFURIKO TANGA PICHAz

 Wanafunzi wa shule ya msingi ya Donge  kata ya Mabawa  Tanga, wakiangalia nyumba zilizozingirwa na maji kufuatia mvua kubwa zilizoanza kunyesha toka juzi mfululizo.





BASHRI KUAPISHWA BAADA YA KUSHINDA UCHAGUZI BILA KUWA NA MPINZANI

Rais Bashir aapishwa kwa muhula mwengine

Rais Omar al-Bashir, ameapishwa kwa muhula mwengine wa miaka mitano baada ya kupata ushindi mwengine kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika April.
Al- Bashir,angali na kesi Mahakama ya Kimataifa, The Haghe (ICC)  inayomtuhumu kwa mauaji yaliyofanywa dhidi ya baadhi ya wakaazi wa Darfur, nchini humo.
Uchaguzi huo  ilisusiwa na vyama vya upinzani lakini ikaendelea licha ya wapiga kura wachache kujitokeza..
Viongozi wa Kenya , Misri na Zimbabwe ni baadhi ya waliohudhuria sherehe hiyo ya kuapishwa kwa Al Bashir ambaye amekuwa madarakani tangu alipochukua hatamu za uongozi kupitia mapinduzi ya mwaka 1989.
Kwa habari na matukio ya papo hapo , ni hapa hapa tangakumekuchablog

VIERA KUIKOCHI NEWCASTLE UNITED

Viera awania umeneja Newcastle United

Mchezaji kiungo wa zamani wa Arsenal na Manchester City Patrick Vieira yuko katika orodha ya watu wanne waliohusishwa kushika nafasi ya kocha wa timu ya Newcastle United.
Steve McClaren, ambaye alitupiwa virago na timu ya Derby County wiki iliyopita, naye yumo katika orodha hiyo.
Mchakato wa mahojiano utaanza wiki hii kwa Vierra mwenye umri wa miaka 38 kuhojiwa. Kocha huyo wa timu ya Manchester City kwa wachezaji chini ya umri wa miaka 21 amejiandaa kukabiliana na mikimiki ya ligi kuu.
Vieira, ambaye alikuwa katika kikosi cha timu ya Ufaransa iliyotwaa Kombe la Dunia mwaka 1998, aliwahi kushinda pia mataji matatu ya ligi na makombe manne ya FA katika miaka yake tisa akiwa na timu ya Arsenal.
Alihamia Juventus ya Italia mwaka 2005 lakini alirejea katika ligi kuu ya England mwaka 2010 alipojiunga na Manchester City na kuisaidia kushinda kombe la FA mwaka 2011 kabla ya kustaafu soka miezi miwili baadaye.
Iwapo atafanikiwa atakuwa miongoni mwa makocha wanne vijana kuliko wote katika orodha ya makocha wa sasa wanaofundisha katika ligi kuu ya England.
Newcastle imekuwa haina kocha mkuu wa kudumu tangu Alan Pardew ajiunge na Crystal Palace mwishoni mwa mwaka jana.
Newcastle, ambayo ilimaliza nafasi ya 15 katika msimu wa 2014-15 wa Ligi Kuu, inatumaini kumteua meneja wake katika kipindi cha wiki mbili zijazo.

STEP BLATTER AJIUZULU

Rais wa FIFA Sepp Blatter kujiuzulu


Rais wa Shirikisho la Soka Duniani FIFA Sepp Blatter amesema kuwa atajiuzulu kama Rais wa Shirikisho hilo kufuatia kashfa ya ufisadi.
Akitangaza kujiuzulu,kwake Sepp Blatter mwenye umri wa miaka 79 ameitisha kikao cha dharura mara moja ili kumchagua rais mpya.
Blatter alichaguliwa tena wiki iliopita licha ya maafisa wake saba wakuu kukamatwa siku mbili kabla ya uchaguzi .
Lakini alisema kuwa mamlaka yake hayaungwi mkono na kila mtu.
Kwa habari na mtukio ya ukweli na uhakika usiache kuwa mbali nami, na niko tayari kukupatia kinachonifikia hapa hapa tangakumekuchablog

AJUZA WA MIAKA 85 AOKOLEWA BOTI ILIYOZAMA

Ajuza aokolewa katika boti iliozama China

Waokozi nchini Uchina wanaowasaka manusura kutoka kwenye meli ya abiria iliyozama katika mto Yangtze wameweza kumvuta kutoka kwenye meli hiyo mwanamke mwenye umri wa miaka 85.
Mwanamke huyo ni mmoja wa watu wapatao 12 wanaofahamika kunusurika katika ajali hiyo iliyotokea baada ya meli hiyo kuzama jana usiku .
Miili ya watu imekuwa ikivutwa kutoka kwenye meli hiyo.
Watu zaidi ya 450 walikuwa ndani ya  meli hiyo ilipopata ajali kutokana na hali mbaya ya hewa.
Kwa habari na matukio pamoja na burudani ni hapa hapa tangakumekuchablog

MAZITO YAIBUKA KOMBE LA DUNIA AFRIKA KUSINI

Ushahidi wa rushwa waliyotoa South Afrika ili kupewa uenyeji wa kombe la dunia huu hapa

  Kwa takribani wiki mbili sasa neno ‘rushwa’ limekuwa likiliandama sana shirikisho la soka duniani FIFA.
Wiki iliyopita maafisa 10 wa shirikisho hilo walikamatwa na serikali ya Marekani kwa kujihusisha na skendo ya ubadhirifu wa £100m, jambo ambalo lilipelekea wadau mbalimbali kumuomba Rais wa shirikisho hilo Sepp Blatter kujiuzulu.
Jerome Valcke
 Hata hivyo Blatter amegoma kufanya hivyo, lakini ikiwa suala la ubadhirifu wa £100m likiwa bado la moto, leo hii umetolewa ushahidi kwamba katibu mkuu wa FiFA Jerome Valcke alihusika na rushwa ya $10m kutoka kwa shirikisho la soka la Afrika ya kusini. Kwa mujibu wa mkuu wa shirikisho la soka la SA, Danny Jordaan, amethibitisha kwamb ni kweli nchi hiyo ililipa kiasi hicho kwenda Raisi wa shirikisho la soka la CONCACAF wa wakati huo,  Jack Warner mnamo mwaka 2008, kwa jili ya kusaidia maendeleo ya soka barani humo na sio rushwa iliyosaidia nchi hiyo kupata uenyeji wa kombe la dunia mwaka 2010.

 Kwa upande wa FIFA wamemtaja, muargentina Julio Grondona ndio alikuwa mhusika mkuu ktika kuidhinisha malipo hayo ya $10 million.
Grondona alikuwa na cheo cha umakamu wa raisi na pia mwenyekiti wa kamati ya masuala ya fedha ya shirikisho hilo, hata hivyo Grondona alifariki dunia mwaka 2014.
Kauli ya FIFA kwamba Grondona ndio alitoa ruhusa ya kufanyika kwa malipo hayo ya rushwa inaonekana kumsafisha Jerome Valcke, baada ya gazeti la New York Times kutoa taarifa kwamba Valcke ndio aliyeidhinisha malipo hayo ya rushwa.
Lakini leo hii umetolewa ushahidi wa barua unaonyesha Valcke ndio aliyeidhinisha malipo hayo ikiwa ni rushwa kutoka nchi ya South Africa ambayo ilipewa uenyeji wa mashindano ya kombe la dunia mwaka 2010.

 Mwendesha mashtaka wa Marekani amesema kwamba South African ililipa fedha hizo kwa Mr. Warner – ambaye wakati huo alikuwa makamu wa raisi wa FIFA ili kutimiza ahadi yao baada ya kupewa haki ya kuandaa kombe la dunia 2010.
Fifa iliichagua South Africa kuandaa fainali hizo mbele ya Morocco.

KWA WASHABIKI WA MAN UNITED (UZI MPYA HUU HAPA)

Uzi Mpya wa Manchester United huu hapa.

united new kit


Imekuwa utamaduni wa klabu mbalimbali barani ulaya kuzindua jezi mpya kila msimu ambapo jezi hizi huingia sokoni na kuuzwa kwa mashabiki wa klabu husika huku klabu hiyo ikijiingizia kipato ambacho husaidia kwenye uendeshaji wa shughuli zake .
Manchester United inatarajiwa kuzindua jezi mpya siku za hivi karibuni ambapo zitakuwa jezi ambazo zimetengenezwa na mdhamini mpya wa klabu hii ambaye ni Adidas . Adidas wameingia mkataba na United baada ya klabu hiyo kumaliza mkataba wake wa muda mrefu na kampuni ya Nike  

Jezi mpya za United zitakazotumika msimu ujao zimevuja kwenye mtandao wa Internet ambapo picha ya mchezaji Ashley Young imeonekana ambapo mchezaji huyo ni kama amepozi akiwa anapigwa picha maalum kwa ajili ya matangazo ya jezi hizo . Hata hivyo United haijatoa taarifa rasmi kuhusu uzinduzi wa jezi mpya na kilichoonekana ni picha ambayo wengi wameihusisha na jezi ambazo United itazindua siku za karibuni .
 Kwa habari, matukio na michezo motomoto na uhakika ni hapa hapa tangakumekuchablog

USHETWANI MWENGINE HUU HAPA

Uamuzi wa baba wa kambo wa Kim Kardashian umefikia hapa…

caity
Moja ya familia zisizoishiwa vituko na kila mara kuingia kwenye headlines ni pamoja na familia ya Kriss Jenner ambaye ni mama mzazi wa staa maarufu duniani Kim Kardashian.
Baada ya kusambaa kwa muda mrefu habari kuhusu kujibadilisha jinsia kwa baba wa kambo wa Kim Kardashian, aitwaye Bruce Jenner, sasa ni rasmi kuwa baba huyo amejibadilisha jinsia yake na sasa anajulikana kama Caitlyn Jenner.
bruc2
Uamuzi huo umevuta hisia za watu wengi kwenye mitandao ya kijamii, lakini pia umeonekana kupokelewa  tofauti na familia nzima ya Kardashian kwani mkewe wa zamani Kriss Jenner na familia yake wameonekana kutopendezwa na maamuzi hayo ingawe mwenyewe amefikia uamuzi huo alioutangaza rasmi kwenye jarida la Vanity Fair.
bruc
Katika Ukurasa wake mpya wa Twitter alioufungua muda mchache baada ya kujitangaza na kupata follewers wengi, Bruce Jenner ameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo na kuandika hivi maneno mengi ya kujisifia.

BABA AWAFUNGIA MKE NA MTOTO , KISA MKE AMEMZALIA MTOTO WA KIKE

Baba amfungia mkewe bafuni kwa miaka mitatu kisa mtoto wa kike…unajua alikua anampa nini?…

man
Suala la kuchagua jinsia ya watoto ni makubaliano kati ya wazazi na pia huwahusisha wote wawili, lakini pia ujio wa mtoto mwenye jinsia yoyote ndani ya familia ni mapenzi na baraka za Mungu
Mwanaume huyu raia wa India hakupishana na baadhi ya wanaume wengi ndani ya jamii zetu ambao wamekua na chaguo lao wenyewe pindi linapokuja suala la kupata mtoto.
Rameshwar Rao aliamua kumfungia mkewe na mtoto wake wa kike bafuni kwa muda wa miaka mitatu kisa tu amemzalia mtoto wa kike kinyume na matarajio yake ya kupata mtoto wa kiume.
Baada ya mkewe Priyanka kugundua ni mjamzito wa mtoto wa kike alimwambia mumewe ambaye alimtaka aitoe mimba kwa kuwa alitaka mtoto wa kiume, lakini mkewe alikataa kuitoa na kuamua kurudi kwa wazazi wake akajifungue.
Alikaa kwa wazazi wake takribani miaka mitano na kuamua kurudi wakati mtoto akiwa tayari mkubwa baada ya wote kusameheana, lakini cha kushangaza mwanaume aliamua kuwafungia bafuni yeye na mtoto wake huku akiwapa maji na wali kwa muda wote.
Kwa sasa mwanaume huyo anashikiliwa na polisi baada ya marafiki wa familia yake kugundua kitendo alichokifanya kwa mkewe lakini mke wake amewaomba polisi hao kumwachia huru ili waendelee kuishi pamoja.
Kwa habari matukio na michezo ya uhakika na ukweli usiache kuwa karibu nami hapa hapa tangakumekuchablog

UGUMBA WAMPELEKA KUIBA MTOTO HOSPITALI YA MWANANYAMALA

Mwanamke kakamatwa akitaka kuiba mtoto Mwananyamala..

A picture shows the feet of a new-born at the maternity of the Argenteuil hospital, in a Paris suburb, on July 22, 2013.  AFP PHOTO / FRED DUFOUR        (Photo credit should read FRED DUFOUR/AFP/Getty Images)
Mwanamke mmoja ambaye amesema kwamba mume wake alikuwa anamdai kila siku mtoto.. akaamua aingie Hospitali ya Mwananyamala kwenye wodi ya Wajawazito, akajifanya na yeye ni mjamzito.
Baada ya kukaa kwa muda wanawake wenzake walimshtukia alikuwa kwenye pilika pilika za kutaka kuiba mtoto, walipopeleleza wakajua kwamba hakuwa mjamzito na alikuwa na mpango wa kuiba mtoto.. ishu ikafika Polisi na kwa sasa bado kesi iko mikononi mwao.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika ni hapa hapa tangakumekuchablog

ANUSURIKA KULIWA NA SIMBA , LAKINI AFARIKI KUTOKANA NA MAJEREHA

Simba kapitia dirishani na kuvamia watalii kwenye gari Afrika Kusini, hili sio tukio la kwanza !

animalplIX-15
Vyombo vikubwa vya habari vimeripoti sana hii ishu leo June 02 2015, unaweza ukaamua kufungua kioo ili uone vizuri wanyama wakati uko mbugani unatalii, hii sio salama sana kwa vile kwenye hifadhi kuna wanyama wengine wakali kama simba ambao wanaweza kufanya chochote kibaya wakipata nafasi.
Mwanamke alikuwa ndani ya gari akiendelea kutalii ndani ya Lion Park, akatokea simba jike mmoja, akavamia kwenye gari kupitia kwenye dirisha la gari na kumshambulia mwanamke ambaye alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata.
Askari wa hifadhi waliwahi na kuwafukuza simba lakini mwanamke alifariki kutokana na majeraha makubwa aliyoyapata huku mwanaume aliyekuwa akiendesha gari hiyo akiendelea kupata matibabu baada ya kujeruhiwa pia.. tukio la mtu kufariki kutokana na kujeruhiwa na simba hii ni mara ya tatu ndani ya kipindi cha miezi minne ndani ya hifadhi hiyo.

WAKAZI WA KIVULENI KATA YA KIOMONI TANGA WAONYESHA NJIA


Tangakumekuchablog

Tanga,WAKAZI wa kijiji cha Kivuleni kata ya Kiomoni halmashauri ya jiji la Tanga, wamechangia zaidi ya shilingi milioni ishirini kwa ujenzi wa  kituo cha afya ili kuondokana na kero ya kufuata matibabu masafa ya umbali zaidi ya kilometa 15.

Wakizungumza  na waandishi wa habari mapema leo, wakati wa hatua za awali za ujenzi wa kituo hicho, walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakipata shida ya kufuata matibabu ambapo baadhi ya wakati wanawake wajawaziti hujifungua njiani.

Walisema kituo hicho mara baada ya kukamilika kwake itakuwa msaada kwa wakazi wengi wakiwemo wa vijiji vya jirani ambapo mbali ya masafa hayo wamekuwa wakikumbana na adha ya miundombinu mibovu ya barabara .

“Kwanza tunamshukuru diwani wetu kwa kujitolea eneo lake kujengwa kituo cha afya na ndio sisi tukashawishika kuchanga pesa tuanze ujenzi----tunaimani ndani ya mwaka mmoja huduma itaanza” alisema Rehema Hassan

“Wahanga wakubwa wa mambo ya afya ni wanawake wajawazito na wazee na mara nyingi wanawake wakati wanapotaka kujifungua hupata shida baada ya miundombinu ya barabara mibovu na wengine hujifungulia njiani” alisema

Kwa upande wake Diwani wa kata hiyo, Kauli Makame, amewataka wananchi kuendeleza na moyo wao wa kuchangia na wa kujitolea hadi kituo hicho kitakaposimama na kutoa ahadi ya kuwa nao bega kwa bega.

Alisema wakati wa vikao vya mabaraza ya Udiwani amekuwa akilipigia kelele kero ya wananchi wa kata hiyo kwa kukosa huduma ya matibabu jambo ambalo hufuata matibabu masafa marefu.

“Kwa kuona kero ya wananchi wangu na mimi mwenyewe kama diwani nimetoa eneo langu ili kujengwa kituo----nimelitoa kabla ya kuwa diwani hii ni kuonyesha kuwa nimeguswa na kero za wananchi wenzangu” alisema  Makame

“Kwa jitihada zangu na za viongozi wenzangu leo tumeanza kwa kulisafisha eneo ambalo tutajenga kituo na kesho tutaanza kulipima ili kuanza ujenzi mara moja kwa pesa za wananchi ambazo wamechanga wao wenyewe” alisema

Aliwataka wananchi hao kuendeleza moyo wao wa kujitolea hadi ambapo kituo hicho kitakaposimama na kuahidi kuwa nao bega kwa bega hadi kitakapokamilika na kuahidi kusaidia kila ambapo kutahitajika msaada.

                                           Mwisho

 Katapila likisafisha eneo ambalo kitajengwa kituo cha afya kijiji cha Kivuleni kata ya Kiomoni halmashauri ya jiji la Tanga  baada ya kukusanya zaidi ya shilingi milioni 21 kwa nguvu zao. Eneo hilo limetolewa na Diwani kaya ya Kiomoni , Kauli Makame ikiwa ni jitihada za kuondosha kero ya kufuata huduma za matibabu zaidi ya kilometa 15 kutoka kijijini hapo.




SOMA MAKUBWA YALIYOJIRI MAGAZETI YA LEO, JUNE 02 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisni kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

HAYAA

MWANANCHI
Hamasa ya wanaCCM kutangaza nia ya kuwania urais imemwibua mwanafunzi Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Umma katika Chuo Kikuu cha Mzumbe, Maliki Malupu (34).
Malupu alitangaza nia ya kugombea urais kupitia CCM akiahidi kushughulikia suala la elimu, afya, kilimo na michezo huku akijua kuwa umri wake haujatimia miaka 40 inayotakiwa kikatiba.
Akitangaza nia hiyo mjini Morogoro jana, Malupu alisema kutokana na uaminifu na uadilifu wake, ameamua kuwania nafasi hiyo pamoja na mambo mengine kwa kuwa ni haki yake kikatiba.
Alipoulizwa atatimizaje nia yake hiyo bila kuwa na sifa kikatiba, alisema vifungu vya katiba vinavyotaja umri vina utata, hivyo ameamua kuingia kuvitafutia suluhisho.
“Unajua ibara ya 39 (1) (b) inasema lazima utimize miaka 40, lakini ibara (d) inasema mtu mwenye sifa za kuwa mbunge au mjumbe wa baraza la wawakilishi anaweza kuwania urais,” alisema akifafanua kuwa yeye ana sifa hizo.
Akieleza sababu nyingine zilizomsukuma kuwania urais, Malupu alisema kuwa ni kuhakikisha sekta ya elimu inaboreshwa kikamilifu kwa kuwa muda mrefu imekuwa ikichezewa na baadhi ya viongozi.
Alisema muundo wa sekta hiyo unapaswa kurekebishwa kwa ama kufutwa au kuondoshwa utaratibu wa kupanga viwango vya ufaulu wa GPA kwa wanafunzi wa elimu ya sekondari katika mitihani ya kidato cha sita na cha nne.
Alisema utaratibu huo haufai kwa kuwa hautoi matokeo ya kuboresha maarifa kwa wanafunzi, pia unawaathiri wanafunzi kisaikolojia katika kujitofautisha wao na wanafunzi wa elimu ya juu.
“Nitahakikisha naboresha mitalaa kwa masomo ya kidato cha nne na cha sita ili kuleta weledi wa kina na wa kutosha, nitaboresha mazingira ya watumishi sekta ya elimu ikiwa ni pamoja na kuboresha mishahara na stahiki za walimu wa msingi hadi vyuo,” alisema.
Katika mkutano wake wa saa 1.30, Malupu alisema atahakikisha anadhibiti suala la maprofesa kuacha kazi yao ya weledi na kukimbilia katika siasa na ataboresha stahiki zao na mishahara kwa kuwalipa vizuri wanaofundisha vyuo vya Serikali na binafsi bila ubaguzi wowote ili kuimarisha sekta ya elimu ngazi vyuo vikuu.
Malupu alisema ataitazama sekta ya kilimo kwa kuongeza vyuo vikuu vya kilimo ili kuleta tija ya kilimo katika sekta hiyo na Serikali yake itakuwa na mkakati mahsusi wa kutoa elimu na mitaji kwa wakulima wanaofanya kilimo chenye tija na kilimo cha kujikimu. Katika afya, Malupu alisema kuwa atahakikisha suala la afya linasimamiwa kikamilifu ikiwa ni pamoja kuwapatia wazee huduma bure na kwamba zahanati, vituo vya afya na hospitali zinapatiwa vifaatiba vya kutosha ili kuondoa malalamiko kutoka kwa wananchi.
Malupu pia alizungumzia wananchi wanaoishi katika visiwa vya Ukerewe mkoani Mwanza na Mafia mkoani Pwani kuwa wamesahaulika, hivyo akiteuliwa na baadaye kuchaguliwa atahakikisha anakifanya kisiwa cha Ukerewe kuwa mkoa unaojitegemea ili kuwapunguzia wananchi umbali wa kufuata huduma Mwanza.
MWANANCHI
 Katibu Mkuu wa Chadema, Dk  Willibrod Slaa amesema Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), mwaka huu, unaingia kwenye uchaguzi ukiwa na safari ya uhakika na siyo ya matumaini kama ilivyotolewa na mmoja wa watangaza nia ya kugombea urais katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Dk Slaa alisema, kauli hiyo ni moja kati ya nyingi zinazotolewa na viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambazo Watanzania wamechoka kuzisikia na badala yake wanahitaji vitendo.
Alitoa kauli hiyo juzi mjini Tunduma wilayani Momba mkoani Mbeya, alipokuwa akihutubia wakazi wa mji huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Shule ya Msingi Tunduma.
Dk Slaa alisema Watanzania wanahitaji safari yenye uhakika wa maendeleo ambayo watayapata Oktoba, mwaka huu, kupitia upinzani lakini siyo  kutoka kwa kiongozi yeyote wa CCM.
“Eti safari ya matumaini, hivi kweli Tanzania iliyojaa kila aina ya madini na utajiri wa kutisha halafu tunasema safari ya matumaini badala ya vitendo? Watanzania tumechoka na kauli za matumaini, tumechoka kuishi kwa matumaini katika nchi yetu,” alisema Dk Slaa.
Mbali na hilo, Dk Slaa  aliwashangaa baadhi ya watangaza nia wa CCM walioiponda Serikali yao kwamba imeshindwa wakati wao ndio walitakiwa kuwa mstari wa mbele kuondoa kero hizo.
Ukawa wajipanga
Akizungumza kuhusu Ukawa walivyojipanga kuingia Ikulu Oktoba mwaka huu, Dk Slaa alisema wana akiba ya kutosha ya viongozi makini wa kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi.
Alisema wakishika dola hawatakuwa na sababu yoyote ya kukopa viongozi kutoka kwa CCM.
“Hatuna njaa ya viongozi ndani ya upinzani, tunao wa kutosha. Hatuna haja ya kwenda CCM kuwakopa viongozi, Oktoba tupeni ridhaa upinzani tubadili sura ya nchi,” alisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Mbozi Magharibi (Chadema), David Silinde alisema, licha ya Serikali ya CCM kuamua kugawa majimbo katika maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kujiokoa, hawataambulia kitu kwani wamejipanga kukabiliana na hali yoyote itakayojitokeza.
“CCM tumewagundua na janja yao, baada ya kuona wabunge wao wamekabwa koo, ndio wanatafuta njia mbadala ya kujiokoa kwa kugawa majimbo, lakini tunasema majimbo yote yaliyopendekezwa kugawanywa Mbeya kama yatapitishwa tunachukua yote,” alisema Silinde.
MTANZANIA
MBIO za kusaka urais kwa makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zimezidi kushika kasi baada ya mtoto wa tano wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, Charles Makongoro Nyerere kujitosa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Wakati Makongoro akichukua uamuzi huo kwa mara ya kwanza katika historia ya familia ya Mwalimu Nyerere, mkoani Mbeya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Kazi Maalumu, Profesa Mark Mwandosya naye ameingia kwenye mbio hizo.
MAKONGORO
Akitangaza nia yake katika eneo la Mwitongo kijijini Butiama jana, Makongoro aliwashambulia makada wenzake ndani ya CCM ambao wanaongoza makundi ya kuwania urais kwa kuwaita ni ‘vibaka’ wanaokivuruga chama hicho kwa maslahi yao binafsi.
Akitoa mfano kwa baadhi ya makada wanaoongoza makundi ndani ya chama hicho, Makongoro aliwataja kwa majina kuwa ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, Naibu Waziri wa Fedha,Mwigulu Nchemba na Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wasira.
Alisema makada hao kwa muda mrefu wamekuwa wakitumia fedha nyingi kuendesha makundi ya urais na akahoji sababu za kutafuta cheo hicho cha juu kwa fedha.
CCM irudishwe kwa wazalendo kwa sababu vibaka wamekuwa na mlengo mbaya wa kukiendeleza chama hicho, alisema.
Alisema ndani ya chama hicho kumekuwa maradhi ya rushwa ambayo yameiambukiza nchi nzima.
Makongoro alisema yeye ni mzalendo wa kweli na anataka kuirudisha nchi katika misingi ya uadilifu endapo CCM itampa ridhaa ya kupeperusha bendera katika uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu.
Alisema ndani ya chama hicho kumekuibuka genge la watu wachache ambao utajiri wao ni wa shaka na umejijenga kwa fedha chafu.
“Ndani ya chama tawala wamekuwapo ‘vibaka’ wachache… unajua kibaka ni kibaka tu hata kama kapewa gari la Serikali lina bendera ya taifa mbele atabaki kuwa kibaka tu.
“Wananijua vizuri huwa siwaonei haya kuwaambia ukweli, hawa ndiyo wanaotuvurugia chama na hawamheshimu Mwenyekiti wa chama, Rais Jakaya Kikwete,” alisema Makongoro.
Katika hotuba yake ambayo alitumia saa mbili, Makongoro alijikita kuzungumzia madhara yanayotokana na rushwa ndani ya CCM.
Alisema baadhi ya makada wanaotumia rushwa wamezalisha makundi na mipasuko isiyo ya lazima huku akisisitiza kuwa anachukia kuwapo makundi ndani ya chama hicho.
Kwa mujibu wa Makongoro, hali hiyo imechochea badhi ya viongozi wa CCM katika ngazi mbalimbali wakiwamo wenyeviti wa mikoa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama hicho kuishi kama mifugo.
Alisema hali hiyo imesababisha baadhi ya viongozi hao kuishi maisha ya kusukumwa kwa upepo wa makundi yanayomilikiwa na watoa fedha.
“Vibaka waturudishie CCM yetu, watambue wao ni wachache na sisi wazalendo ni wengi, hawatushindi na fedha zao na kitaeleweka tu.
“Leo hii viongozi wetu wa CCM wamekuwa ni watu wa kuendeshwa na vibaka hawa wanahongwa fedha ovyo…wao wana mifugo yao ndani ya NEC basi mimi sijafuga hata kuku, nasema kitaweleweka,” alisema Makongoro.
Alisema yeye hawezi kufanya hivyo kwa sababu rasimu ya ilani ya chama hicho bado haijapitishwa na chama, hofu yake ni kwamba anaweza kutoa ahadi na zikawa kinyuume na ilani ya chama chake.
“Nimewasikia wanajinadi,nawashangaa sana, najiuliza kwani wao ni akina nani watoe ahadi kabla ya ilani ya chama? Ikitokea ahadi yako ikaenda kinyume na ilani si ndiyo mwanzo wa kuwa na rais muongo…sitaki kuwa rais muongo nitaheshimu chama changu kwa kila mchakato na maelekezo,” alisema Makongoro.
Aliwaasa Watanzania wawaogope watu wanaoonekana kuwa na haraka ya kukimbilia kutawala nchi.
“Ukiona watu kazi inatangazwa ifanywe kwa utaratibu wake na mtu aliyeiomba kazi hiyo anakiuka taratibu, muogopeni sana huyo hafai kukukuongoza maana hata akikuongoza ataendelea kukiuka taratibu ili ajinufaishe,” alisema Makongoro.
Wanawake wananipenda
Makongoro alisema anakerwa na siasa chafu dhidi yake zinazoenezwa na baadhi ya wanasiasa wenzake ndani ya CCM.
Alizitaja siasa hizo kuwa ni tuhuma za kulaaniwa na baba yake, ulevi na mtu anayependa wanawake.
Akijibu tuhuma hizo, Makongoro alihoji umati uliomiminika kumsikiliza kwamba, “jamani naonekana nimelaaniwa? Naelekea kuokota makopo? Jamani mnanionaje, naonekana mlevi? na umati ulikataa kwa kusema, “hapana”.
“Eti wanasema Makongoro anapenda wanawake sasa wanataka nipende wanaume? Wanawake wananipenda na mimi nawapenda, hizi siasa chafu wanazonituhumu hazinisumbuilangu ni moja tu vibaka rudisheni nchi yetu,” alisema.
MTANZANIA
WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi, ametegua kitendawili kuhusu hatima ya madai ya wananchi katika mradi wa ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni.
Lukuvi amesema kutokana na hali hiyo kuanzia sasa kila mwananchi mwenye kiwanja au nyumba yake atalazimika kuuza kiwanja chake kwa bei anayoitaka au kujenga nyumba kwa mujibu wa ramani ya mji mpya
Akizungumza na wananchi hao juzi katika mkutano uliofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni Dar es Salaam, Lukuvi, alisema sintofahamu iliyokuwapo ilitokana na hapo awali wananchi kutowekwa wazi kuhusu mchakato wa uuzaji wa maeneo yao.
“Wananchi wamekuwa katika sintofahamu juu ya uuzaji wa maeneo yao, wengine mnafikiri Serikali ndiyo itakayonunua ardhi yenu na wengine mnafikiri ardhi inadalaliwa na Wakala wa Kusimamia Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni (KDA),” alisema Lukuvi na kuongeza;
“Hakuna Serikali itakayouza ardhi wala KDA kudalalia ardhi yenu…wananchi wa Kigamboni ndiyo mtakaoamua juu ya uuzaji wa ardhi yenu na serikali itakuwa mwangalizi ili wananchi wasiibiwe kwa kuuza bei ya chini sana,” alisema Lukuvi huku umati huo ukimshangilia.
Alisema wananchi wanachotakiwa ni kuchagua mambo matatu katika mpango huo ambayo ni kuuza ardhi yao wenyewe moja kwa moja kwa wawekezaji, kuingia ubia na wawekezaji na kutafuta fedha za kujenga wenyewe.
Alisema kama mwananchi ataamua kujenga mwenyewe atatakiwa kufuata ramani na mpango wa mji mpya unavyoonyesha.
“Mtu anaweza kuamua kujenga mwenyewe lakini si kwamba unaamua kujenga unachotaka bali utajenga kilichopo kwenye mpango, haiwezekani eneo la kujenga majengo makubwa ya biashara wewe ujenge choo,” alisema Lukuvi.
Alisema ili kuhakikisha wananchi wanatekeleza mambo hayo matatu ni lazima wapatiwe hatimiliki za maeneo yao suala ambalo awali halikuwapo kwa madai kuwa hakuna haja ya kutoa hati kwa eneo ambalo tayari lipo kwenye mpango.
“Katika suala la kutoa hati nilipingana na watu wa Mipango Miji na nikawaambia lazima wananchi wapewe hati zao ili wakati wa kufanya makubaliano na wawekezaji wawe na ushahidi wa kumiliki ardhi hiyo,” alisema Lukuvi.
MTANZANIA
KAMBI Rasmi ya Upinzani bungeni imesema Serikali inayoongozwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) imeiba sera yake ya elimu inayozungumzia elimu bure kuanzia shule za msingi hadi chuo kikuu.
Mbali na hilo, wapinzani wameonya makada wa chama hicho wanaotangaza nia ya kuwania urais kuacha kutumia sera hiyo ya upinzani kwa sababu walikuwa Serikalini tangu uhuru na wameshindwa kufanya hivyo.
Akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo bungeni jana kwa mwaka wa fedha 2015/2016, Msemaji Mkuu kwa kambi hiyo katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Susan Lyimo, alisema elimu haijawahi kuwa kipaumbele katika sera za CCM kwa awamu zote za utawala wake na ndiyo maana imeshindwa kutekeleza hata Ilani yake ya uchaguzi.
“Sera ambayo CCM imepigia upatu kwa miaka yote 53 ya uhuru na ambayo pia imeshindwa kutekeleza ni kilimo, ndiyo maana tangu enzi za uongozi wa Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere sera zilizosikika ni Siasa ni Kilimo, Kilimo cha Kufa na Kupona, Kilimo ni Uti wa Mgongo wa Taifa na sasa Kilimo Kwanza. Hatujawahi kusikia elimu kwanza kwa utawala wa CCM kwa miaka yote 53 ya Uhuru,” alisema.
Suzan ambaye ni Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema) alisema sera ya elimu kwanza ni ya upinzani na kwamba ipo katika ilani ya uchaguzi ya Chadema ya mwaka 2005 na 2010 na imepewa kipaumbele cha kwanza, cha pili na cha tatu.
“Itakumbukwa kwamba Chadema iliposema elimu bure kama ingechaguliwa kuunda serikali mwaka 2005 na 2010, CCM iliendesha propaganda chafu ya kuwapotosha wananchi kwamba haiwezekani kutoa elimu bure.
“Lakini ili kuthibitisha ile methali isamayo kwamba njia ya muongo ni fupi, CCM hivi sasa imekubali kula matapishi yake na kusema katika kipengele cha 3.1.5 cha sera mpya ya elimu ya mwaka 2014 kwamba elimu itakuwa bure,” alisema na kuongeza:
“Huu ni uthibitisho kuwa CCM imebobea katika wizi hadi kufikia hatua ya kuiba sera ya upinzani waziwazi bila aibu. Ukawa ikitwaa madaraka ya dola katika uchaguzi wa Oktoba mwaka huu, elimu ya msingi hadi Chuo Kikuu itakuwa bure.”
Sera mpya ya elimu
Kuhusu sera mpya ya elimu, alisema imekuwa hazitekelezeki kwa kuwa ni sera bainishi na imekuwa ikibainisha upungufu pekee na kuacha sehemu ya utekezaji.
Alisema ili sera hiyo iweze kutekelezeka ni lazima kuwapo na walimu bora, zana bora za kufundishia na walimu wenye motisha.
“Tanzania imekuwa ikisifika kwa kuandika vizuri sera zake, lakini utekelezaji wake ni shida. Mfano sera hii haielezi ni kwa kiasi gani itaondoa ubaguzi au matabaka ya elimu hasa viwango vya elimu. Pia haielezi nini maana ya kufuta ada ikiwa kuna michango mingi kuliko ada yenyewe,” alisema.
Dk. Kawambwa
Awali akiwasilisha hotuba yake, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa alisema kwa kushirikiana na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mikakati ya Matokeo Makubwa Sasa (BRN) imetekelezwa.
Alisema sekta ya elimu imefanikiwa kwa asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mikakati hiyo.
Dk. Kawambwa aliainisha vipaumbele vya sekta ya elimu vilivyomo katika mwongozo wa taifa wa maandalizi ya mpango wa bajeti kwa mwaka 2015/2016 kuwa ni
pamoja na kuongeza upatikanaji wa fursa ya elimu kwa usawa katika ngazi zote za elimu na mafunzo, kuinua ubora wa elimu na kujenga stadi stahiki, kuimarisha taasisi za usimamizi wa ubora wa elimu na ufuatiliaji na tathmini ili zitekeleze majukumu yake.
NIPASHE
Mbunge wa Vunjo (TLP), (pichani), amemshukia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdularhman Kinana, kwamba anamchonganisha na wapiga kura wake kwa  kudai kuwa serikali imetoa Sh. milioni 400 katika jimbo hilo kupitia Mfuko wa Jimbo wakati siyo kweli.
Akichangia bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka 2015/16 bungeni jana, Mrema alisema ni jambo la kushangaza kwa Kinana kutoa taarifa za uongo kwa lengo la kumchonganisha na wapiga kura wake, ili CCM ijijengee mazingira mazuri katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu.
“CCM kwanini mnaanza kushiriki uongo, mnataka kunichonganisha kwa wapiga kura wangu ili kuning’oa Vunjo, nawahakikishia CCM hang’oki mtu Vunjo, hizo Sh. milioni 400 hazijaletwa jimboni kwangu labda mmepeleka kwa wabunge wa CCM,” alisema.
Mrema alisema mbinu zinazofanywa na CCM kumshambulia katika jimbo lake kama mpira wa kona haziwezi kuzaa matunda.
HABARILEO
SEKTA ya Elimu imefanikiwa kwa asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Matokeo ya utekelezaji wa mikakati iliyowekwa na BRN ni kupanda kwa ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Msingi (Darasa la Saba) na kupanda ufaulu wa mtihani wa kumaliza Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne).
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa aliyasema hayo bungeni jana wakati alipowasilisha Bajeti ya Mwaka 2015/16.
Dk Kawambwa alisema, “Kwa mujibu wa taarifa ya mwaka mmoja (2013/14) sekta ya elimu imefanikiwa kwa asilimia 81 na kushika nafasi ya kwanza katika utekelezaji wa awamu ya kwanza ya mikakati hiyo.”
Aliyajata baadhi ya mafanikio ambayo yamehakikiwa na ‘Presidential Delivery Bureau’ ni kutoa tuzo kwa shule na wanafunzi waliofanya vizuri kwenye matokeo ya darasa la saba na kidato cha nne.
Alisema jumla ya tuzo 3,044 zilitolewa kwa shule zilizopata ufaulu uliotukuka na zile zilizopanda kwa ufaulu ikilinganishwa na mwaka 2013.
Pia alisema walimu 4,103 wa masomo ya Sayansi, Hisabati na Lugha walipatiwa mafunzo ya kuwajengea uwezo wa kutambua wanafunzi wenye uwezo mdogo wa kumudu masomo.
Aidha, alisema ujenzi wa miundombinu ya shule 47 za sekondari kati ya 264 zilizolengwa katika awamu ya kwanza ulikamilika. Lengo ni kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya shule 1,200 katika awamu tatu.
“Madeni ya shilingi 1,852,162,158.21 ya malimbikizo ya mishahara yalilipwa kwa watumishi 916 wa wizara,” aliongeza Dk Kawambwa.
Alisema matokeo ya utekelezaji wa mikakati hiyo ni kupanda kwa ufaulu wa darasa la saba kutoka asilimia 50.6 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 56.99 mwaka 2014.
“Na kupanda kwa ufaulu wa Mtihani wa kumaliza Elimu ya Sekondari (Kidato cha Nne) kutoka asilimia 57.09 mwaka 2013 hadi kufikia asilimia 69.76 mwaka 2014,” alieleza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi.
Akizungumzia utungaji wa Sera za Elimu, alisema rasimu ya andiko la uanzishwaji wa Bodi ya Kitaalamu ya Walimu imekamilika, na kuwasilishwa katika mamlaka husika.
Aidha, alisema katika mwaka 2014/15, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ilitoa mikopo kwa wanafunzi 99,590 wakiwemo 2,117 wa Stashahada ya Elimu ya Ualimu wa masomo ya Sayansi na Hisabati.
Alisema Bodi hiyo ilikusanya marejesho ya mikopo kiasi cha Sh 15,978,993,320.04 sawa na asilimia 45.5 ya lengo la makusanyo kwa mwaka 2014/15 na hivyo kufikia Sh 75,575,793,215 sawa na asilimia 45.45 ya Sh 165,008,246,475 za madeni yaliyoiva.
Kuhusu changamoto katika mwaka wa fedha uliopita, ilisema mojawapo ilikuwa ni kulipa madeni ya wazabuni na huduma nyingine sasa yanafikia Sh 45,855,370,632.7.
Alisema kati ya hizo, Sh 25,195,672,974.2 ni deni la wazabuni wa vyuo vya ufundi na Sh 5,148,207,930.00 ni deni la posho za wahadhiri.
Akizungumzia vipaumbele kwa mwaka 2015/16, alisema Wizara itasimamia utungaji na utekelezaji wa Sera za Elimu, ithibati ya shule na udhibiti wa ubora wa elimu.
Kwa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania, alisema itaendelea kuratibu na kusimamia udahili na ukaguzi wa wanafunzi 60,000 ili kufikia lengo la kuwa na wanafunzi 300,000 katika taasisi za elimu ya juu ifikapo mwaka 2016.
Kuhusu Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, alisema itakusanya Sh 51,001,034,808.24 za marejesho ya mikopo iliyotolewa kati ya mwaka 1994/95 na 2014/15.
Kwa habari na matukio na mengi mengineo ni hapa hapa tangakumekuchablog