Sunday, January 1, 2017

MWAKA MPYA, ZAWADI, WALIOJIFUNGUA HADI SHEREHE BEACH RASKAZONE TANGA



Tanga, WATOTO saba wamezaliwa mkesha wa Mwaka Mpya hospitali ya Rufaa ya Bombo Tanga mmoja kati yao akiwa wa kiume ikiwa ni idadi pungufu ya mkesha wa mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari wodi ya wazazi Leo, Muuguzi wa zamu, Halima Rico, alisema awali walidhani wangepokea idadi kubwa ya wazazi na kuwa walikuwa wamejipanga vya kutosha.
Alisema mara nyingi vipindi vya mikesha ya Sikukuu huongezeka wajawazito katika vituo vya aafya na hospitali na kwa kulitambua hilo huwa wanajipanga.
“Mkesha wa mwaka huu tumezalisha watoto saba na mmoja kati yao ni wakiume, hii ni tofauti na mwaka jana ambapo idadi ilizidi zaidi ya kumi” alisema Ricco na kuongeza
“Jambo ambalo tunalishukuru wazazi wote afya zao ni nzuri pamoja na watoto wao na kulikuwa hakuna wa upasuaji, ila jambo ambalo limejitokeza ni kuwa kati ya saba waliozaliwa mmoja tu ndio wa kiume” alisema
Akizungumza na wazazi mara baada ya kutoa zawadi ya miche mitatu ya sabuni kwa kila mzazi, Katibu Tawala Mkoa, Zena Said, aliwataka wazazi kuwa na ada ya kuhudhuria kliniki ili kujua tarehe zao.
Alisema kuna baadhi ya wajawazito wamekuwa hawana ada ya kuhudhuria kliniki hivyo kuwa na wakati mgumu wakati wa kujifungua.
“Tuko miongoni mwetu hatuna ada ya kuhudhuria kliniki jambo ambalo linawakwaza mauguzi wakati wa kujifungua” alisema Zena
Zena aliwatakia kila la heri wazazi na watoto wao waliozaliwa mkesha huo wa mwaka mpya na kulitakia Taifa lidumu katika amani na utulivu ili kila mmoja afanye kazi zake za kujiletea maendeleo.
                                               










Tanga na maeneo ya jirani  wakiogelea Beach ya Raskazone kusherehekea mwaka mpya Leo.









RAIS MAGUFULI, UMEME HAUPANDI

Magufuli: Bei ya umeme haitapanda

Rais John Magufuli amesema licha ya Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati maji (Ewura) kuridhia ombi la Tanesco kupandisha bei ya umeme kuanzia Januari Mosi, 2017 bei ya umeme haitapanda.

Rais Magufuli amezungumza hayo leo katika Kanisa Kuu Katoliki la Bukoba aliposali wakati wa kuanza ziara ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera.

Rais ameshangazwa na kitendo cha watendaji waliopandisha bei ya umeme bila hata ya kushauriana na yeye, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu au Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo.

''Ninamshukuru sana Waziri wa Nishati na Madini kwa maamuzi ya kusitisha hayo. Kwa hiyo umeme hakuna kupanda bei, Amesema.

Ameongeza kuwa, “Haiwezekani unapanga mikakati ya kujenga viwanda na hasa katika mikakati mikubwa ya nchi ya kusambaza umeme mpaka vijijini kwa watu maskini halafu mtu mmoja kwa sababu ya cheo chake anapandisha bei, hili haliwezekani.''
MGBLOG

MVUA KIDOGO TU SOKO LA MLANGO WA CHUMA MASIWANI TANGA, NI BALAA

 Wafanyabiashara ndani ya soko la Mlango wa Chuma Masiwani Tanga wakiwa wamezingirwa na maji ya mvua iliyonyesha jana usiku na kusababisha kero kwa wateja na wauzaji wa bidhaa jambo ambalo linalotishia afya ya mlaji.
Maji hayo ambayo yamejaa na kusomba bidhaa zilizopangwa chini na kutishia kuibuka kw amagonjwa ya miripuko,
Inadaiwa kuwa miundombinu chakavu imekuwa chanzo cha maji katika soko hilo kutokuwa na njia ya kupitia.




UTURUKI YAUKARIBISHA MWAKA KWA MAJONZI

Watu 39 wauawa wakikaribisha mwaka mpya UturukiMshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa

Kulingana na waziri wa maswala ya ndani takriban watu 39 wamefariki huku 69 wakijeruhiwa Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.Mshambuliaji aliyetekeleza mashambulio hayo alitoroka na hajakamatwa hadi kufikia sasa
Takriban watu 39 wakiwemo wageni 15 wanahofiwa kuuawa katika shambulio la klabu ya burudani mjini Istanbul Uturuki, kulingana na waziri wa maswala ya ndani nchini humo.
Mtu aliyekuwa amejihami kwa bunduki aliwafyatulia risasi watu waliokuwa wakijiburudisha katika mkahawa huo wa Reina saa saba usiku wakati ambapo watu walikuwa wakisherehekea kuingia kwa mwaka mpya.
Waziri huyo Süleyman Soylu ameelezea waliojeruhiwa kuwa 69 .
Mtu huyo aliingia katika klabu hiyo akijifanya kikaragosi kilichovaa mavazi ya Santa Claus na punde kuanza kuwafyatulia risasi kiholela waliokuwepo.
Baadhi yao iliwabidi kujirusha baharini kuepuka msusuru wa risasi zilizokuwa zinafyatulia.
Polisi mmoja ni miongoni mwa waliofariki.
Huku waliojeruhiwa wakikimbizwa hospitali, maafisa wa usalama wanaendelea kufanya upekuzi katika eneo hilo lakini muhusika wa shambilo hilo hajakamatwa
BBC

UZEE NI DAWA BADO NIMO NIMO



Mzee Mwinyi Shaban maarufu (Maembe) mkazi wa barabara ya 15 Ngamiani Tanga akipaka rangi maua moja ya kawa lililoletwa na mteja. Kawa moja hupaka rangi kwa shilingi 3,000 na mkoba mmoja wa ukili hupaka kwa shilingi 5,000.










WAKAZI WA NGAMIANI KUSINI TANGA WAFANYA USAFI WA MAZINGIRA



Wakazi wa kata ya Ngamiani Kusini wakiufanyia usafi mfereji wa maji barabara ya Taifa Road jana ikiwa ni sehemu ya zoezi la usafi kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi.
Zoezi la Usafi la kila Jumamosi ya mwisho ya mwezi limeuweka jiji la Tanga katika mazingira ya usafi na wadau wa Mazingira wametaka kufanyika kila jumamosi ya mwisho wa wiki ili kuweza kutokomeza magonjwa ya miripuko ambayo husababishwa na uchafu.






AMKA NA MAGAZETI NA FREYS TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 2929