Tangakumekuchablog
Tanga,NAIBU
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Zuberi
Samataba, amewagiza wakurugenzi na walimu wakuu nchini kusimamia agizo la Rais John Pombe Magufuli la kukomesha michango shuleni.
Akifungua mkutano Mkuu wa mwaka wa
Camfed na wadau wa elimu Tanga jana, Samataba alisema mwalimu mkuu yeyote
ambaye atabainika kuchangisha na kusababisha kero kwa wananchi achukuliwe hatua kali za kisheria.
Alisema moja ya sababu zinazofanya
malengo ya uandikishaji wananfunzi yasifikie kwa asilimia mia moja ni michango
holela wakati wa uandikishaji wanafunzi
darasa la kwanza.
“Natoa wito kwa maofisa elimu na
walimu wakuu nchini kusimamia agizo la Rais la kukomesha michango
shuleni----yoyote ambaye atabainika hatua kali za kisheria atachukuliwa”
alisema Samataba na kuongeza
“Familia masikini zinaogopa
kuwapeleka watoto wao shuleni kisa michango ovyo ovyo----ninasema yoyote
atakaebainika tutamshughulikia” alisema
Alisema wajibu wa mwalimu mkuu ni
kusimamia uandikishaji wa watoto wote wenye umri wa kwenda shule katika eneo lake
kwa kushirikiana na viongozi wa mtaa na vijiji .
Aliwataka viongozi hao wa Serikali
kushirikiana na wadau wa elimu kuwaandikisha watoto wenye umri wa kwenda shule
lengo likiwa ni kutokomeza ujinga na wasiojua kusoma na kuandika.
Kwa upande wake Afisa Elimu Wilaya
ya Kilolo Mkoani Iringa, Gloria Kang’oma, amekiri kuwa michango ilikuwa ikiwapa
changamoto kutoka kwa wazazi hasa wa vipato vya chini.
Alisema kufutwa kwa michango hiyo
itajenga mahusiano mazuri baina ya wazazi na walimu pamoja na kamati za shule
ambapo baadhi ya wazazi walikuwa wakiwakosesha maxsomo watoto wao kwa kuhofia
kuchangishwa.
“Kufutwa kwa michango shuleni ni
furaha kwa walimu na wazazi kwani kesi na malalamiko kila siki ofisni zilikuwa
haziishi----hii nadhani ni fursa kwa wazazi na walezi kuwabidiisha watoto wao
kupenda shule na masomo” alisema Kang’oma
Alisema agizo hilo la Rais walimu
wamelipkea kwa furaha kubwa na hivyo ni wajibu wao wa kusimamia kuhakikisha
hakuna michango yoyote inayojitokeza shuleni.
Mwisho
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri
Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Zuberi Samataba, akifungua kongamano
la Mkutano Mkuu wa Comfed uliofanyika juzi Tanga.
No comments:
Post a Comment