Tangakumekuchablog
Tanga, AFISA
Elimu shule za msingi halmashauri ya jiji la Tanga, Godfrey Mkingo, amewataka
wazazi na walezi kuwa na ada ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao shuleni na
kuacha kuzurura mitaani.
Akizungumza kwenye mahafali ya 8
shule ya India Ocean English Midium jana, Mkingo alisema watoto wengi wamekuwa
wakizagaa mitaani muda wa shule na hivyo kuwataka wazazi kushirikiana na walimu
kuhakikisha kila mtoto anahudhiria masomo darazani.
Alisema ili kuweza kukabiliana na
wimbi hilo amezitaka kamati za shule na wazazi pamoja na walezi kushirikiana
katika maendeleo ya watoto darasani na kuunda timu moja ya ufuatiliaji watoto
majumbani na darasani.
“Leo hapa tuko pamoja na wazazi na
walezi pamoja na watoto wetu katika mahafali haya ya nane-----utoro darasani
tukemee na majumbani kwetu tusiwaruhusu ucheza” alisema Mkingo na kuongeza
“Kuna baadhi ya wazazi wamekuwa
wakiwatumikisha watoto wao muda wa masomo shuleni jambo hili ni baya na
halikubaliki linamkosesha haki ya elimu mtoto” alisema
Kwa upande wake Mkurugenzi wa shule
hiyo, Samwel Kimbute, amewataka walimu shuleni hapo kuzidisha bidii ya
ufundishaji darasani na kutobweteka na mafanikio yaliyofikiwa.
Alisema shule hiyo imejiwekea
mikakati ya kuhakikisha inashika nafasi ya kwanza katika ufaulishaji na hivyo
kuwataka walimu dhima hiyo kuwa kipaumbele chao wakati wa ufundishaji darasani.
“Nawaomba walimu kuzidisha kasi ya
ufundishaji darasani na kuacha kubweteka na mafanikio tuliyopata----hii ni
faida kwa vijana wetu kuwa viongozi bora na mahiri wa baadae” alisema Kimbute
Aliwataka wazazi na walezi kuwa na
mawasiliano na uongozi wa shule na kupeana taarifa za maendeleo ya vijana wao
lengo likiwa ni kuhakikisha watoto wanahudhuria masomo darasani kwa wakati.
Mwisho
No comments:
Post a Comment