SITASAHAU NILIVYOKUMBANA NA MWANAUME WA KIJINI 2
ILIPOISHIA
Nilipomtajia namba yangu aliiandika kwenye simu yake kisha akanipigia hapo hapo.
Simu yangu ilipoita aliniambia.
“Namba yangu ndiyo hiyo, ahsante sana”
Hakurudi tena kwenye meza yake akatoka. Kwa vile mtu aliyefanya niamue
kuondoka alishatangulia kutoka nikaona niendelee kukaa kidogo.
Lakini sikutimiza hata nusu saa nikainuka na kutoka. Nilirudi nyumbani
kwa teksi. Nikafikia kuoga na kujilaza kitandani.
Wakati usingizi unataka kunichukua, simu yangu ikaita. Nilipoichukua na
kutazama kwenye sikrini ya simu niliona namba ya yule mzungu. Nikaipokea simu
yake.
“Hello!” nikasema kwenye simu.
SASA ENDELEA
“Hello! Mambo vipi?” Sauti ya yule mzungu ikasikika kwenye simu.
Nilifurahi alivyoniuliza “Mambo vipi?” Niliona alikuwa mzungu aliyebobea katika
lugha ya Kiswahili.
“Poa” Na mimi nikamjibu kwa kutumia
lugha ile ile ya mitaani.
“Uko
poa kabisa?” akaniuliza.
“Mimi niko poa, sijui wewe?”
“Mimi pia niko poa. Umesharudi
nyumbani?”
Mara moja nikagundua kuwa mzungu huyo alikuwa anataka kurefusha mazungumzo.
“Nimesharudi.
Hapa niko kitandani” nikamjibu.
“Samahani sana.
Mimi naitwa Mr Smith, sijui mwenzangu unaitwa nani?”
“Naitwa Enjo”
“Okey. Jina lako zuri sana.
Unaishi wapi?”
“Naishi Sinza”
“Unafanya kazi?”
“Hapana. Kwa sasa niko nyumbani tu”
“Okey. Mimi ni Muingreza. Ninapenda kuja Afrika Mashariki mara kwa mara
kutembea. Huwa ninafikia hoteli tu”
“Ndio…ndio”
“Nimefurahi kukufahamu Enjo na ninapenda uwe rafiki yangu”
“Kuna aina nyingi za urafiki, wewe
umependelea urafiki
wa aina gani?”
“Urafiki
wowote tu lakini tutazungumza zaidi tutakapokutana. Enjo una mchumba?”
“Sina mchumba”
“Vizuri. Unadhani tunaweza kukutana wapi kwa ajili ya mazungumzo zaidi”
“Sema wewe”
“Mimi si mwenyeji sana
hapa Dar”
“Umefikia katika hoteli gani?”
“Hoteli ya Lux hapa Masaki. Niko chumba namba 35. Unaweza kufika.
Mzungu kanitajia
hadi namba ya chumba chake akidhani
ningeweza kwenda kwake.
“Kwanini tusikutane mahali pengine?” nikamwambia.
“Tunaweza. Sasa sema wewe ni mahali gani”
“Ngoja, kesho nitakupigia kukufahamisha”
“Kesho saa ngapi”
Nikafikiri kidogo kisha
nikamjibu.
“Kesho mchana”
“Ningefurahi zaidi kama utanitajia saa
ili nisubiri simu yako”
“Tuweke saa tano”
“Sawa. Nipige mimi au utanipigia wewe?”
“Nitakupigia mimi”
“Sawa. Nitasubiri simu yako saa tano”
“Nashukuru. Usiku mwema”
“Usiku mwema na kwako”
Nikatangulia mimi kukata simu kisha
nikaiweka kwenye kimeza cha mchagoni. Baadaye niliona niizime kabisa kwani
sikupenda nikatishwe usingizi wangu kwa milio ya simu.
Usingizi haukuchelewa kunipitia, nikalala. Wakati niko usingizini
nikaota niko kwenye ufukwe wa bahari mimi na yule mzungu tukikimbizana huku
tukirushiana michanga. Sote wawili tulikuwa tumevaa mavazi hafifu ya kuogelea.
Mimi nilivaa chupi na sidiria yake na mzungu alivaa chupi peke yake.
Lakini rangi ya chupi yake na yangu zilikuwa zikifanana.
Baada ya kufukuzana na kuangushana kwa dakika kadhaa tuliingia kwenye
maji na kuanza kuogelea kwa pamoja. Tuliogelea hadi tukafika maji mengi.
Mimi nilikuwa nyuma, yule mzungu alikuwa mbele yangu. Ghafla tukajikuta
tuko katikati ya bahari. Ule ufukwe wa bahari hatukuuona tena.
Itaendelea kesho hapahapa kuwa nami
Sikuwahi kuamini kitu kama hiki kingeweza kunitokea hadi ndoa yangu ilipokaribia kuisha kabisa.
ReplyDeleteMume wangu alibadilika ghafla. Mwanaume ambaye hapo awali alinipenda na kunijali akawa baridi, asiyejali, na mwenye hasira bila sababu. Aliacha kuonyesha nia katika ndoa yetu, akaniepuka kabisa, na hatimaye akaniomba talaka. Nilivunjika moyo kwa sababu nilimpenda mume wangu kwa moyo wangu wote.
Mambo yalizidi kuwa mabaya aliponizuia kila mahali — WhatsApp, Facebook, Instagram — kana kwamba sijawahi kuwepo. Nililia kila usiku nikijiuliza nilifanya nini kibaya.
Siku moja, rafiki wa karibu alinitembelea na kunitambulisha kwa mtu wa kiroho anayeitwa Dkt. Dawn. Kwa kweli, mwanzoni nilikuwa na shaka, lakini niliamua kumweleza kila kitu kwa sababu sikuwa na chochote cha kupoteza.
Dkt. Dawn alinisomea mambo ya kiroho, na nilishtuka. Alifichua siri kuhusu ndoa yangu na maisha yangu binafsi ambayo hakuna mtu aliyejua. Kila kitu alichosema kilikuwa sahihi 100%. Kisha akafichua kwamba mwanamke mwingine alikuwa amemloga mume wangu. Mwanamke huyu alikuwa akimtembelea mara nyingi, na kwa upumbavu niliamini ilikuwa kuhusu kazi tu.
Dkt. Dawn alinisaidia kuvunja uchawi na akafanya ibada yenye nguvu ya kurejesha upendo kwa ndoa yangu.
Kwa mshangao wangu mkubwa, muda mfupi tu baadaye, mume wangu alinifungulia kizuizi mwenyewe na kuanza kunipigia simu na kunitumia ujumbe mwingi, akiniomba nimsamehe na nirudi nyumbani. Mwanzoni nilimpuuza kwa sababu ya maumivu aliyonisababishia, lakini hatimaye alirudi nyumbani akiwa na zawadi na machozi machoni mwake akiomba nafasi nyingine.
Leo, ndoa yetu ni imara zaidi, yenye furaha zaidi, na yenye amani zaidi kuliko hapo awali. Mapenzi kati yetu yanahisi upya kabisa.
Kana kwamba hiyo haitoshi, Dkt. Dawn baadaye alinisaidia na ibada ya ujauzito kwa sababu tulikuwa tumejitahidi kwa miaka mingi kupata watoto. Ndani ya wiki 8, nilipata mimba kiasili, na leo tumebarikiwa na wavulana wawili wazuri wenye afya njema.
Nitaendelea kushukuru milele.
Ukihitaji: Uchawi wa mapenzi wa kuungana tena na mpenzi wako wa zamani
. Usaidizi wa kurejesha ndoa
. Tamaduni za ujauzito za kupata mimba
. Usaidizi wa kiroho kwa kesi za mahakamani au kupona urithi
. Mwongozo na ulinzi wa kiroho
Ninapendekeza sana Dkt. Dawn. Ushuhuda wangu ni wa kweli, na furaha yangu leo ni uthibitisho. WhatsApp yake: +2349046229159 dawnacuna314@gmail.com