NIPASHE
Serikali imeruhusu wanafunzi wa shule za msingi na sekondari waliopata ujauzito kuendelea na masomo wanapojifungua.
Mratibu wa Masuala ya Jinsia wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi,
Chimpaye Marango, wakati wa mjadala wa sababu za kuongezeka kwa idadi ya watoto ya mabinti wanaokosa elimu baada ya kupata mimba.
Mjadala huo ulioitishwa na asasi ya kiraia ya uchambuzi wa sera ya
Policy Forum iliwakutanisha wadau mbalimbali wa elimu.
Marango alisema lazima wasichana waliopewa ujauzito kuhakikisha
wanarudishwa haraka shuleni mara watakapojifungua, vinginevyo hatua kali
watachukuliwa watakaowazuia.
“
Wizara imeliona hilo na tayari
imewekwa sera mpya, kwani kumuadhibu kwa kumfukuza shuleni hakutaweza
kuwasaidia watoto wa kike kumudu maisha badala yake tunaongeza
umasikini ndani ya jamii:- Marango.
Awali, Dk.
Rebecca Balira, kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Tiba Afrika (Amref) alisema tatizo la mimba kwa wanafunzi wa kike limekuwa sugu nchini.
Alisema katika utafiti uliofanyika katika Wilaya za Kilindi, Mkalama,
Iringa vijijini na Same jumla ya wanafunzi wa kike 55,000 walishindwa
kuendelea na masomo kwa kipindi cha mwaka 2003 hadi 2011.
NIPASHE
Waziri wa Uchukuzi,
Samuel Sitta, ametangaza kuwashughulikia watu wote waliohusika kulihujumu Shirika la Ndege Tanzania (
ATCL), ambalo ‘limekufa’, huku akionyesha masikitiko yake kuona mpaka sasa hatua kali hazijachukuliwa dhidi yao.
Sitta alisema hayo, wakati akijibu hoja za wabunge, waliochangia
mjadala kuhusu taarifa za kazi za Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Miundombinu na ya Nishati na Madini, kuanzia Januari 2014 hadi Januari
2015, zilizowasilishwa bungeni jana.
Alisema makosa yaliyotendeka huko nyuma dhidi ya ATCL, ni ya ovyo
ovyo kabisa na kushauri Bunge liweke utaratibu wa kutunga sheria za
kuwabana watu wanaoyatenda.
Sitta alisema hali mbaya iliyopo ATCL inayotokana na deni
linaloikabili, inachangiwa kwa kiasi kikubwa na uzembe unaokaribiana na
hujuma.
“
Sina hakika kama wahusika
wamepatiwa dawa yao. Si ajabu wanatamba tu, wako mahali fulani tu
wanaangalia. Basi kuna udhaifu fulani lazima tuurekebishe ili tuweze
kwenda vizuri:-Sitta.
Kuhusu usafiri wa treni ya Dar es Salaam, maarufu kama “
Treni ya Mwakyembe“,
alisema baada ya mkutano kati ya wizara na Wajerumani unaotarajia
kufanyika jijini humo, Jumanne ijayo, itaboreshwa zaidi ya ilivyo hivi
sasa.
NIPASHE
Mkazi wa Tabata Mawenzi,
Remi Joseph (36)
anashikiliwa na polisi kwa tuhuma za kumuua mkewe kwa kumkata kichwa
kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner ya jijini Dar es Salaam.
Aliyeuawa ni
Josephena Moshi (35), ambaye alikatwa kichwa na kuchomwa na kitu chenye ncha kali kifuani wakiwa kwenye nyumba ya wageni ya Friends Corner.
Akihojiwa kuhusiana na tukio hilo, Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kipolisi wa Kinondoni, Augustine Senga, alikiri kutokea mauaji hayo.
Senga alisema mwanamke huyo alifariki papo hapo baada ya kushambuliwa
na kwamba chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika na uchunguzi
unaendelea.
Kamanda alipoulizwa kuhusiana na mtuhumiwa huyo kutaka kujiua, alisema kuwa uchunguzi unaendelea.
“
Bado ni mapema sana kueleza kila
kitu hayo niliyokueleza ni taarifa za awali kwani na huyu mtuhumiwa
amekutwa na majeraha shingoni, hivyo masuala ya kazi yake na sababu
vinachunguzwa:- Senga.
MWANANCHI
Wakati Serikali ikitafuta njia ya kumaliza tatizo la mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi ‘
albino’
katika Mikoa ya kanda ya ziwa,imedaiwa watoto ambao hawajafikisha umri
na kufariki dunia wakati wa kuzaliwa viungo vyao huuzwa kwa waganga wa
kienyeji.
Hayo yalibainika juzi mbele ya Katibu tawala wa Mkoa wa Simiyu,
Mwamvua Jilumbi katika kikao cha pamoja kilichofanyika katika ukumbi wa
KKKT ulioko Bariadi wakati wa uzinduzi wa mpango mkakati wa kukomesha vifo vya wajawazito.
Wadau hao walibainisha kuwa hali hiyo hujitokeza kila mara katika
hospitali ya Wilaya ya Bariadi na walieza pia mtandao wa wahusika wa
viungo hivyo hufanyika kati ya wauguzi na madaktari ambao ndio huzalisha
wamama wajawazito.
Wadau hao waliendelea kueleza kuwa viungo hivyo vimekuwa vikiuzwa kuanzia 400,000 hadi 500,000.
MWANANCHI
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar,
Mohamed Aboud Mohamed amesema wananchi hawana imani tena na Jeshi la Polisi kwa kuwa vitendo vya uhalifu vinafanyika, lakini hakuna wanaotiwa mbaroni.
Waziri Aboud alitoa kauli hiyo wakati wa kufunga mkutano wa wakuu
waandamizi wa Jeshi la Polisi uliokuwa ukifanyika mjini hapa, huku
chombo hicho cha dola kikizidi kurushiwa lawama kutokana na ongezeko la
uhalifu ambao umefikia hatua ya vituo vya polisi kuvamiwa na askari
kuuawa na kuporwa silaha.
Jeshi hilo pia linalaumiwa kutokana na jinsi linavyoshindwa
kushughulikia vurugu kwa weledi na hivyo kujikuta ikitumia nguvu nyingi
zinazosababisha wananchi kuuawa na kujeruhiwa.
Waziri Aboud alibainisha kuwa wananchi wengi kwa sasa hawana imani
tena na polisi kwa kuwa vitendo vya uhalifu vinafanyika lakini hakuna
watuhumiwa wanaokamatwa na kutiwa mbaroni.
“
Tabu inakuja pale uhalifu
unapotokea na polisi kushindwa kuwapata wahalifu… wananchi wanapenda
wahalifu wote watiwe mbaroni na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria:- Aboud.
MWANANCHI
Mbunge wa Bukoba Mjini kwa tiketi ya CCM,
Khamis Kagasheki amemtuhumu
Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa ndiye aliyekuza mgogoro wa Bukoba
uliosababisha madiwani wa halmashauri kushindwa kufanya vikao, akidai
kuwa mtendaji huyo mkuu wa Serikali ameshindwa kuchukua hatua.
Tuhuma hizo za Kagasheki ni za nadra kwa mbunge huyo wa chama hicho
tawala kuelekeza kwa mtendaji mkuu wa Serikali na mmoja wa wajumbe wa
vikao vya juu vya CCM.
Kagasheki, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, alitoa
tuhumu hizo wakati wa mahojiano maalumu na gazeti hili wiki iliyopita,
akisisitiza kuwa ni makosa kuutazama mgogoro huo kuwa ni kati ya yake na
meya na akataka ijulikane kuwa kinachoendelea Bukoba ni suala la wizi.
Mgogoro huo wa kisiasa, ambao umedumu kwa takriban miaka miwili na
unaotishia kugawanyika kwa CCM, umekolezwa na kufunguliwa kwa kesi tatu
ambazo zimezuia utekelezaji wa shughuli za maendeleo na umekuwa
ukihusishwa na vita vya ubunge baina ya Kagasheki na Meya wa Manispaa ya
Bukoba, Anatory Amani.
“
Hii ni mara yangu ya kwanza kupata
nafasi ya kuzungumzia suala hili. Hakuna unafiki hapa, hili
nitalisimamia mahali popote na nitalisema mahali popote kuwa Pinda,
ndiye tatizo katika mgogoro huu ulioinyima Bukoba maendeleo:-Kagasheki.
MTANZANIA
Wanakiji wa Namonge mkoani Geita, wameua watu wawili ambao ni askari
wa wanyama pori na msaidizi wake, baada ya kuwashambulia kwa mawe,
mapanga, rungu na nondo wakiwatuhumu kuwa ni majambazi.
Kufuatia mauaji hayo yaliyotokea wilayani Bukombe, watu 24 akiwamo ofisa mtendaji wa kijiji hicho wanashikiliwa na polisi.
Tukio hilo limetokea juzi jioni baada ya wananchi hao kukusanyana na
kuivunja ofisi ya serikali ya kijiji hicho ambako walinzi hao walikuwa
wamehifadhiwa na ofisa mtendaji wa kijiji hicho,
Andrea Malise.
Wananchi walioshuhudia mauaji walisema juzi alasiri watu watano,
mmoja wao akiwa na silaha aina ya SMG walipita kijijini baadaye
kuingia baa wakiwa na pikipiki lakini safari hiyo bila silaha.
Kutokana na kuonekana wageni wanakijiji walianza kuhoji na kuwasiliana juu ya wageni hao.
Pasipo subira inadaiwa wananchi walianza kuwatupia mawe na
kuwashambulia ndipo ofisa mtendaji alipoingilia kati na kuwaweka katika
ofisi yake kukwepa vipigo kutoka kwa wananchi hao.
Hofu ya wananchi inadaiwa inachangiwa na kuwapo kwa matukio ya
kihalifu ya mara kwa mara katika ukanda huo, likiwamo la mnada wa
ng’ombe kuvamiwa na watu wenye silaha Januari 16 mwaka huu na wengine
wenye silaha kuingia katika kijiji cha Ilyamchele siku tatu baadaye na
kuwateka wanakijiji baada ya kuwakirimu.
HABARILEO
WAKATI Jeshi la Polisi likilaumiwa kutokana na namna lilivyoshughulikia maandamano ya Chama cha Wananchi
(CUF)
wiki iliyopita, Serikali imetahadharishwa kuwa makini na harakati za
kisiasa zinazotumia mbinu za kuchokoza Jeshi la Polisi na kuvunja sheria
halali.
Wakizungumza na gazeti hili wiki hii kuhusu dhana ya udhaifu wa jeshi
hilo, baadhi ya watu wakiwemo wasomi wameitaka Serikali kuwa makini na
kauli za wanasiasa, ambao wamewahi kushiriki au kutoa matamko ya
kihalifu na leo wanatuhumu jeshi hilo.
Baadhi ya matukio ya kihalifu yaliyotajwa kufanywa katika mazingira
ya siasa, tamko la maandamano na migomo isiyokoma, bila kibali cha
Polisi, lililotolewa hivi karibuni na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa,
Freeman Mbowe na udhalilishwaji wa Mkuu wa Wilaya, wakati wa uchaguzi
mdogo wa Igunga uliokuwa na ushindani wa kisiasa mwanzoni mwa 2011.
Tahadhari hiyo imetolewa, wakati Serikali ikielezea kuridhishwa na
kazi ya kutunza amani nchini inayofanywa na jeshi hilo, na kuagiza
lijiandae na siasa za 2015; siasa za kabla ya Kura ya Maoni ya kupata
Katiba Mpya na za kabla ya Uchaguzi Mkuu ujao.
Maandamano ya CUF Akitoa tamko kuhusu kudhibitiwa kwa maandamano ya CUF wiki iliyopita, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mathias Chikawe, akizungumzia hoja ya mwenyekiti mwenza wa Ukawa,
James Mbatia (
NCCRMageuzi), kuhusu polisi walivyodhibiti maandamano ya CUF, alisema
Prof. Ibrahimu Lipumba, ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, alikaidi zuio la Jeshi la Polisi.
Nitaendelea kukupatia kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com