Zaidi ya falimia 11 mtaa wa Mikanjuni A kata ya Mabawa Tanga hazina mahala pa kuishi baada ya nyumba zao kuzingirwa na maji baada ya mvua iliyonyesha kwa siku mbili mfululizo.
Kujaa kwa maji hayo pia imedaiwa kusababishwa na kutokuwepo kwa miundombinu ya kupitisha maji na hivyo kuwa sababu ya maji kuingia majumbani.
Wakizungumza na tangakumekuchablog mapema leo, wakazi hao walisema kwa muda mrefu wamekuwa wakiwaeleza viongozi juu ya kero hiyo lakini hakuna jitihada zozote zinazochukuliwa.
Wakazi wa mtaa wa Mikanjuni A kata ya Mabawa Tanga, wakiangalia
nyumba iliyozingirwa na maji baada ya mvua kubwa kunyesha kwa siku mbili
mfululizo ambapo jumla ya familia 11 hazina pahala pakuishi. Maji hayo hayana
njia za kupita baada ya kutokuwepo kwa miundombinu ya mifereji ya kupitisha
maji.
Kwa habari, matukio na burudani ni hapa hapa tangakumekuchablog
Sunday, May 31, 2015
FERDINAND ATUNDIKWA MADALUGA
Kauli ya Rio Ferdinand na hatma ya soka lake..
Akiwa bado kwenye majonzi makubwa ya mkewe aliyefariki duniani mwanzoni mwa mwezi huu, beki wa zamani wa Manchester United na timu ya Taifa ya England Rio Ferdinand ameweka wazi mikakati yake mipya katika mahojiano aliyoyafanya.
Mchezaji huyo ambaye kwa sasa ana miaka 36 ametangaza nia ya kustaafu soka baada ya klabu ya Queens Park Rangers kutangaza kumtema kwenye kikosi chake.
Alitangaza uamuzi wake katika mahojiano ya moja kwa moja na BT Sport, na aliandika kwenye akaunti yake ya Twitter kuwashukuru waliomtakia kila la heri baada ya kifo cha mkewe, Rebecca aliyekuwa akisumbuliwa na maradhi ya saratani, ambaye wamezaa naye watoto watatu.Ferdinand hakuacha kumsifia kocha wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson kwamba ni mfano wa kuigwa kutokana na ujuzi wake.
Manchester United ilitoa Pauni Milioni 30 kumnunua Ferdinand Julai mwaka 2002 na kumfanya awe beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza wakati akisajiliwa kutoka Leeds United.
Unahitaji cho
Kwa habari, matukio na burudani, ni hapa hapa tangakumekuchablog
ALIPANDIKIZWA USO WA MAREHEMU BAADA YA KUPATA AJALI MBAYA
Jana tuliweka post hii ya Richard Norris aliepata ajali na kuwekwa uso wa marehemu na leo nimekuwekea mwendelezo wa tukio hilo ambalo limekuwa gumzo kwa washabiki wa blog hii
Ajali
nyingi duniani zimekua zikisababisha vifo vya watu wengi huku zikiacha
wengine wakiwa na ulemavu wa maisha ambao huwasababishia kupoteza
mwelekeo wa maisha yao na kukata tamaa kabisa.
Pamoja
na wengi kubaki na ulemavu, lakini pia madaktari wamekuwa kijitahidi
kadri wawezavyo kuwarudisha watu hao katika hali zao lakini moja ya
tukio la kushangaza ni la kijana Richard Norris ambaye alipata ajali mbaya na kumpelekea kuharibika vibaya sura yake.
Picha ikimwonyesha Norris kabla hajapata ajali, alivyopata ajali na baada ya kuwekewa uso mwingine wa marehemu
Unaambiwa
baada ya ajali hiyo kijana huyo alishindwa kutoka nyumbani kwa
takribani miaka 15 na amini usiamini kijana huyo alifanyiwa upasuaji wa
kihistoria uliochukua masaa 36 na kupandikizwa uso mpya wa mtu ambaye
alishafariki baada ya kupata ajali.
Upasuaji huo ulifanyika katika hospitali ya University of Maryland Medical Center na ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa na sasa kijana huyo anaendelea vyema akiwa mwenye furaha.
Kwa kawaida kwa sababu ya maadili ya
utabibu watu waliopewa mabaki ya viungo vya wafu hawaruhusiwi kukutana
na jamaa au ndugu wa marehemu, lakini Norris hakuweza kujizuia kukutana
na Aversano, kutoka Maryland ambaye ni dada wa marehemu.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog
SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA NA MAGAZETI YA LEO, MAY 31 TZ
Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wale wanaojiendeleza kielimu. Kituo kimesajiliwa na NECTA na kiko na Hostel. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu, 0715 772746
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Ngoyai Lowassa
amesema ana ari, shauku na uwezo wa kuongoza Taifa wakati alipotangaza
nia yake ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika mkutano wa hadhara
uliohudhuriwa na maelfu ya watu kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.
Lowassa, ambaye ni mbunge wa Monduli akihutubia maelfu ya wakazi wa Arusha, katika Uwanja a Sheikh Amri Abeid Aluta, alisema ameamua kujitokeza tena kuwania urasi kwa kuwa anaamini yeye ndiye mtu sahihi wa kuiongoza nchi wakati huu.
Zaidi ya watu 30,000 walifurika kwenye
uwanja huo wakiwa wamekaa kwenye viti na wengine ndani ya kiwanja cha
mpira huku, mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombare Mwiru
akiongoza mlolongo wa watu mashuhuri waliojitokeza kumuunga mkono
mbunge huyo wa Monduli katika mbio za kuelekea Ikulu anazoziita “safari ya Matumaini”.
Akihutubia mkutano huo, Lowassa alisema
pamoja na kuwa viongozi waliopita wameliongoza taifa hili vizuri, bado
linahitaji kiongozi mwenye uthubutu na uongozi madhubuti unaoweza
kufanya maamuzi magumu.
“Kuamini
kama una uwezo na shauku, hakuna budi kwenda sambamba na uwezo wa
kusimamia yale unayoyaamini. Na kwangu haya mawili ni dhahiri. Nina ari,
nina shauku na nina uwezo, kama rekodi yangu inavyothibitisha,” alisema Lowassa huku akishangiliwa.
“Tunapomtafuta
Rais wa Jamhuri ya Muungano ni lazima tukumbuke kwamba tunamtafuta mtu
ambaye atakuwa pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama
katika nchi yetu. Na kwa Chama cha Mapinduzi tunamtafuta mtu ambaye
atakuwa pia mwenyekiti wa chama chetu.
“Naamini
kwa vigezo vyote, nina kila sifa ya kubeba dhamana hizo nzito. Katika
mambo ambayo najivunia, na sitayasahau katika historia yangu ni
kushiriki kwangu kuilinda nchi yetu pale nilipohitajika. Nilishiriki
kikamilifu katika Vita vya Kagera nikiwa miongoni mwa askari wa mstari
wa mbele wa mapambano.”
Lowassa pia alikumbusha tukio la mwaka 1995 alipojitokeza kugombea urais kwa pamoja na Rais Jakaya Kikwete.
“Natarajia safari hii, Kikwete ataniunga mkono.”
Hata hivyo, Kikwete hakupitishwa na CCM
mwaka huo na akagombea peke yake 2005, mwaka ambao Lowassa alisema
aliamua kwa dhati kumuunga mkono mwenzake.
MWANANCHI
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema
uandikishaji wa wananchi kwenye Daftari la Wapigakura nchini
utamalizika mwishoni wa mwezi ujao baada ya mashine 1,600 zaidi za
kielektroniki kwa ajili ya kazi hiyo kuwasili juzi.
Ofisa ugavi mwandamizi wa NEC, Datus Matuma alisema mashine hizo zinazotumia teknolojia ya utambuzi wa alama za mpigakura (Biometric Voter’s Registration), zitaanza kupelekwa mikoa ya Mara, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.
“Ule
uvumi ambao ulikuwa ukienea nchini kwamba Tume ya Taifa haiwezi kumaliza
uandikishaji, sasa umefikia mwisho kwani hizi mashine ni za kisasa na
zitaanza kazi moja kwa moja kwenye mikoa hiyo niliyoitaja na mwishoni
mwa mwezi Juni au mwanzoni mwa mwezi wa Julai watu wote watakuwa
wameshaandikishwa,” Matuma.
Alisema wananchi wajitokeze kwa wingi
kujiandikisha ili wasikose haki yao ya msingi ya kupiga kura kwani kila
aliyefikisha umri wa kupiga kura anatakiwa kujiorodhesha kwenye daftari
hilo.
Alisema Serikali ni sikivu ndio maana
imekata kiu ya Watanzania kwa kuleta mashine hizo ambazo sasa zimefikia
8,000 na zinakidhi kabisa mahitaji ya Watanzania wote kwani zinafika
kila mkoa na zitagawiwa kwenye halmashauri kwa ajili ya kuzisambaza
kwenye vituo vya uandikishaji .
Hata hivyo, mwezi uliopita NEC
ilitangaza kwamba hakuna mpango wowote wa kuahirisha Uchaguzi Mkuu na
kusisitiza kuwa utafanyika kama ilivyopangwa.
MWANANCHI
Mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi jana uligeuka shubiri kwa Waziri Samuel Sitta wakati alipobanwa na wabunge kutokana na Serikali kushindwa kuboresha usafiri wa reli na anga.
Wabunge hao, mbali na kuibua ufisadi
mbalimbali unaofanywa na watendaji wa Serikali, wakiwamo wa wizara hiyo,
walihoji sababu za Serikali kuwa na ndege moja tu na kushindwa na nchi
ndogo ya Rwanda ambayo ina ndege saba za serikali.
Licha ya kuipitisha, walisema kuwa nchi bila kuwa na usafiri unaoeleweka wa reli, anga na barabara ni vigumu kupata maendeleo.
Akichangia mjadala huo, mbunge wa Kawe,
(Chadema), Halima Mdee aliibua suala la ukiukwaji wa mauzo ya nyumba za
Shirika la Reli Tanzania na Zambia (Tazara), kwamba mbali na ukiukwaji
wa mauziano na ununuzi, pia mfanyabiashara aliyenunua nyumba hizo
amekwepa kodi ya Serikali inayokadiriwa kufikia Sh4 bilioni
“Haiwezekani,
tuna taarifa hizo, nyumba zimeuzwa kwa bei ya soko na Serikali pia
ilipaswa kupata kodi yake inayofikia wastani wa Sh4 bilioni… Serikali
hii ni ya aina gani ambayo kila mwaka kuna kashfa za ufisadi katika
wizara zake,” Mdee.
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila,
alisema katika serikali ya Awamu ya Nne kila wizara inakabiliwa na
wizi, akifafanua jinsi Mamlaka ya Manunuzi Nchini (PPRA) ilivyoshindwa
kufuata vigezo ya ununuzi wa mabehewa 124 ya Kampuni ya Reli (TRL).
Alivitaja vigezo hivyo kuwa ni pamoja na utangazaji wa zabuni kutozingatiwa na pia kutofanyika kwa uchunguzi.
Alisema waziri wa uchukuzi na katibu
mkuu wa wizara hiyo na waziri wa fedha ambao ndio waidhinishaji wa fedha
hizo za ununuzi wa mabehewa wanatakiwa kuwajibika. Alisema suala hilo
linalohusu Sh230 bilioni haliwezi kufunikwa na kupita.
Alisema Rwanda ni nchi ndogo lakini ina
ndege saba wakati Tanzania ni nchi kubwa lakini ina ndege mmoja tena
inahitaji matengenezo kila siku.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa kamati ya Ulinzi na usalama Wilayani Bukombe Amani Mwenegoha
amesematangu kutokea kwa mauaji ya mtoto albino Yohana Bahati Wilayani
Chato, kumeibuka madai mbalimbali ya utapeli na vitisho vinavyofanywa na
watu wenye ulemavu huo.
Mwenegoha alisema kuna utapeli unadaiwa
kufanywa na wasichana wenye ulemavu wa ngozi wanaofanya biashara ya
kujiuza miili yao Wilayani humo.
Imedaiwa kuwa wasichana hao huwageuka wanaume wanapofika kwenye nyumba za kulala wageni licha ya kukubaliana toka awali.
“Kuna
taarifa ambazo zimetufikia ofisini kwetu kwamba hawa wasichana
wanasimama barabarani sehemu za vichochoro wakiona wanaume wakawapenda
wanawaita na kuwalazimisha wawape fedha, wakikataa wanapiga kelele na
kudai kuwa wanataka kuwakata viungo vyao”Mwenegoha.
Pia wanapokuwa kwenye biashara yao ya
kujiuza wanapokutana na wanaume hukubaliana kiwango cha fedha, lakini
wanapofika ndani hubadilika na kuwalazimisha watoe fedha zaidi ya
makubaliano na wakikataa kuwa wanataka kukatwa viungo.
NIPASHE
Watu wawili wamefariki dunia mkoani
Simiyu katika matukio tofauti akiwamo mtoto wa miezi mitatu
aliyenyakuliwa na fisi akiwa mgogoni mwa mama yake.
Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Simiyu, Gemin Mushy jana alisema kuwa mtoto Ng’wanza Samwel,
akiwa amebebwa na mama yake alinyakuliwa na fisi Mei 25, majira ya
saa 1;30 jioni katika kijiji cha Ngugunu,Tarafa ya Kisesa wilayani
Meatu.
Alisema katika kufuatilia tukio hilo,
mabaki ya mtoto huyo yalipatikana mita 200 tu fisi kutoka eneo
alilonyakuliwa huku kichwa, kifua, tumbo, mikono na miguu ikiwa haipo.
Katika tukio jingine mpanda baiskeli
aliyefahamika kwa jina la Magina Supa(20), mkazi wa Nyaumata mtaa wa
Kisiwani wilayani Bariadi, aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali
shingoni na bega la kushoto na mtu aliyekuwa amempakiza kama abiria
wake.
Akifafanua, Kamanda Mushy alisema kuwa
tukio hilo lilitokea Mei 26 majira saa 1;00 jioni katika mtaa wa
Izunya, kata ya Somanda tarafa ya Ntuzu wilayani Bariadi kwa mtuhumiwa
wa mauaji hayo anayedaiwa kuwa abiria wa mpanda baiskeli huyo aliyekuwa
anajishughulisha na biashara ya daladala ya baiskeli.
Kamanda huyo alisema kuwa mara baada ya
mauaji hayo, mtuhumiwa ambaye hajafahamika na anasakwa baada uhalifu
huo alitoroka. Chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.
NIPASHE
Walemavu wa aina mbalimbali karibu
milioni nne huenda wasipige kura kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu
kutokana na kukosekana vifaa vya kuwawezesha kushiriki zoezi hilo.
Baadhi ya vifaa hivyo ni kama maandishi ya nukta nundu kwa wasioona, hadi sasa havijanunuliwa.
Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec), Jaji Mstaafu John Mkwawa, alisema matarajio ya kupatikana kwa vifaa hivyo yanasubiri kufunguliwa zabuni katikati ya mwezi ujao.
Alitoa maelezo hayo baada ya kuulizwa
iwapo Nec ina vifaa vya kuwasaidia walemavu hao na kama wamepewa elimu
kuhusu matumizi ya vifaa hivyo, kwa vile mwaka 2010 walilalamikia
ukosefu wa elimu na vifaa vya kuwawezesha kushirika zoezi hilo.
Jaji Mkwawa alisema jitihada zinafanywa
na tangazo la kutafuta wazabuni wa kuagiza vifaa hivyo lilitolewa Mei
12, mwaka huu kwenye vyombo vya habari.
Alisema idadi ya walemavu wenye sifa za
kupiga kura mwaka huu ni milioni nne hivyo Nec haipo tayari kuwakosesha
haki wananchi hao.
Kuhusu suala la utoaji wa elimu kwa watu
hao ambalo mwaka 2010 walilikosa, Jaji Mkwawa aliahidi kueleza zaidi
taarifa hizo kabla ya kupatikana vifaa hivyo.
Hata hivyo, alipoulizwa idadi ya vifaa
wanavyokusudia kuviagiza, Jaji Mkwawa alisema ni mapema kulielezea
kabla ya zabuni kufunguliwa.
NIPASHE
Hatima ya Mpango wa Taifa wa Damu Salama (NBTS) upo kwenye hati hati baada ya mfadhili mkuu aliyekuwa anagharamia uendeshaji wake kuondoka rasmi leo na kuiacha ikichechemea.
Serikali ya Marekani kupitia kituo cha
Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC), ilikuwa akigharamia sehemu kubwa ya
mishahara ya wafanyakazi, vifaa vya kuhifadhia na kusafirishia damu.
Uchunguzi wa umebaini kuwa, NBTS ina
hali mbaya kwa vile mafadhili anaiacha wakati benki hiyo inakabiliwa
na uhaba wa damu ambayo ni tegemeo kwa wagonjwa waliopo mahospitalini
hasa wanawake wajawazito, wazazi na watoto wachanga.
Msemaji wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Nsachris Mwamwaja,
alikiri kujitoa kwa mfadhili huyo na kuongeza kuwa, serikali imejipanga
kukabiliana na changamoto hiyo ikiwa ni pamoja kubeba mzigo wote wa
ulipaji mishahara kwa wafanyakazi na kuhakikisha damu na vifaa
vinavyohitajika vinakuwepo wakati wote.
“Tunatambua
umuhimu wa damu kwa wagonjwa, hata bajeti yetu itakayowasilishwa
keshokutwa bungeni tutalitilia mkazo suala hili kwa sababu mfadhili huyu
alikuwa anatusaidia na sasa amejitoa hivyo hatuna jinsi,”.
Kuhusu uhaba wa damu, aliwataka
Watanzania kujitokeza kuchangia damu kwa sababu mahitaji yake ni makubwa
na kila mtu anaweza kuhitaji msaada huo.
“Suala
la damu halihusiani na mfadhili bali watu wajitolee kwa sababu damu
inasaidia kila mtu bila kujali ni nani unacheo gani, niwaombe muwe na
utaratibu wa kuchangia damu ili tuokoe maisha ya watoto, wanawake,
wanaume, wazee,” alihimiza.
NBTS imekuwa ikitegemewa kusambaza
vitenganishi kwenye kanda zake sita ambazo ni Mwanza, Moshi, Tabora,
Mbeya, Mtwara na Dar es Salaam.
HABARILEO
Maofisa watano wa Serikali, wanatarajiwa
kupandishwa kizimbani hivi karibuni, kutokana na kashfa ya uagizaji wa
mabehewa 274 kutoka India, huku wengine wakitarajiwa kuchukuliwa hatua
za kiutawala.
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta, ameliambia Bunge jana kuwa Kamati Maalumu iliyoundwa na wizara yake, imemaliza kazi na kumkabidhi ripoti hiyo.
“Wamenikabidhi ripoti juzi na iliundwa na watu wa Ofisi ya CAG, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Takukuru na wahandisi,” alisema Sitta.
Alikuwa akifanya majumuisho ya hoja za
wabunge kuhusu makadirio ya bajeti yake kwa mwaka wa fedha 2015/16,
ambayo aliyawasilisha bungeni jana asubuhi na kupitishwa na Bunge
baadaye mchana.
Waziri huyo mkongwe alisema kamati hiyo ilienda hadi Calcutta, India ambako mabehewa hayo 274 yalitengenezwa na kwa mujibu wake, mabehewa hayo si chakavu, kama ilivyodaiwa awali.
Hata hivyo alisema
“kuna makosa mawili hapa ambayo ni uzembe wa pande mbili, waagizaji na
watengenezaji. Kuna tatizo katika specification (vipimo). “Hapa kuna
majina ya watu wote waliohusika katika suala hili.
Watano tunawapeleka mahakamani, wengine tutawachukulia hatua za kiutawala.” Aidha,
aliweka bayana kuwa katika maofisa hao watano watakaopelekwa
mahakamani, wawili ni wanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA).
Aidha, Sitta alisema si kweli kuwa
hasara iliyopatikana ni Sh bilioni 200, bali ni Sh bilioni 12 na wote
waliohusika watachukuliwa hatua stahili.
“Pia tumemwomba Mwanasheria Mkuu ili sehemu ya hasara hii ibebwe na
mtengenezaji na nyingine itabebwa na Serikali kutokana na uzembe
uliofanyika,” Sitta.
Kwa habari, matukio na burudani ni hapa hapa tangakumekuchablog
AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Pia wako na Hostel. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 7727246
Saturday, May 30, 2015
ALIEPANDIKZWA USO AKUTANA NA DADA WA MAREHEMU
Aliyepandikizwa uso akutana na dadake marehemu
Mwanamke ambaye kakake alikufa katika ajali mbaya ya barabarani amekutana na mtu aliyepewa uso wake.
Amini
usiamini mtu huyo aliyefanyiwa upasuaji huo wa kihistoria alipandikizwa
uso mpya baada yake kuishi kwa miaka 15 akiwa bila pua.Richard Norris alimshukuru mwanamke huyo kwa niaba ya kakake marehemu aliyemwezesha kupata mwanzo mpya maishani.
Mwanamke huyo Rebekah Aversano alionekana akiugusa uso wa kakake akiwa haamini macho yake.
Richard Norris, anayetokea Virginia, Marekani alijeruhiwa katika ajali ya ufyatulianaji wa risasi miaka 15 iliyopita.
Yamkini Norris hakuwa amewahi kutoka nyumbani kwake katika kipindi hicho chote.
Aversano, kutoka Maryland.
Na alipomuona Aversano, alibubujikwa na machozi na kusikika akisema ''hii ndiyo uso na sura niliyokuwa nayo''
Kakake Joshua Aversano, alipoteza maisha yake katika ajali mbaya ya barabarani akiwa na umri wa miaka 21.
kauli yake ya kutoa viungo vya mwili wake haikupokelewa vyema na familia yake na haswa mamake Gwen Aversano.
''Baada ya kukutana na Norris aghalabu nimeweza kumuona mwanangu tena''
''Nahisi vyema kuwa nimemsaidia Norris kuanza upya maisha yake japo tumempoteza mpendwa wetu'' alisema mamake Joshua .
Upasuaji huo wa kihistoria ulifanywa katika chuo kikuu cha Maryland yapata miaka mitatu iliyopita.
Upasuaji ambao ulidumu kwa zaidi ya saa 36.
UJERUMANI NDIO NCHI PEKEE YENYE IDADI NDOGO YA WATOTO DUNIANI
Ujerumani ina idadi ndogo zaidi ya watoto duniani
Idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Ujerumani imepungua zaidi ya mataifa yote duniani.
Utafiti
umeonesha kuwa idadi ya watoto wanaozaliwa nchini Ujerumani ndiyo ya
chini zaidi duniani na sasa kunahofu kuwa kupungua kwa uzazi kutaathiri
pakubwa uwezo wa vijana kuendeleza kasi ya ukuaji wa uchumi wa taifa
hilo tajiri zaidi barani Ulaya.Watafiti wanaonya kuwa endapo jitihada mahsusi hazitafanywa ilikuimarisha idadi ya watoto nchini humo basi uchumi wa taifa hilo utaathirika vibaya.
Kulingana na utafiti huo,watoto 8.2 pekee walizaliwa miongoni mwa watu wazima 1000.
Awali idadi ya chini zaidi ilikuwa ya Japan ambayo huandikisha idadi ya watoto 8.4 wanaozaliwa miongoni mwa watu wazima 1000.
Barani Ulaya, Ureno na Italia ziliorodheshwa katika nafasi ya tatu na nne zikiwa na jumla ya watoto 9.0 na 9.3 mtawalia.
Ufaransa na Uingereza zinasajili watoto 12.7 wanaozaliwa miongoni mwa watu wazima 1000.
Niger iliyoko Afrika ndiyo inayoandikisha idadi kubwa zaidi ya watoto wanaozaliwa duniani.
Nchini humo watoto 50 huzaliwa miongoni mwa watu wazima 1000.
Aidha afisa wa BDO Arno Probst, aliwatahadharisha wajerumani kuwa kiwango cha malipo na mishahara ya wafanyikazi kitaongezeka maradufu kadri ya upungufu wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi .
Probst alisema Ujerumani italazimika kuwaruhusu wahamiaji kuingia nchini humo na kufanya kazi ilikuepuka kuzorota kwa uchumi wake.
Hutopitwa na habari na niko tayari kukusogezea muda na wakati kupitia hapa hapa tangakumekuchablog
BLATTER ACHAGULIWA TENA KWA KISHINDO
FIFA:Blatter ailaumu UEFA na Marekani
Rais
wa shirikisho la soka duniani FIFA Sepp Blatter ameikashifu shirikisho
la soka barani Ulaya UEFA na Marekani kwa kuendesha kampeini ya kuipaka
tope jina zuri la FIFA.
Blatter ambaye ameanza muhula wake wa
tano kama rais wa shirikisho hilo amesema kuwa alipigwa na mshangao
alipopata habari za ufisadi ulaji na rushwa ndani ya FIFA.Akizungumza na runinga moja ya Uswisi Blatter alimtaja mkuu wa sheria wa Marekani Loretta Lynch na rais wa UEFA Michel Platini kwa kuichukia FIFA.
''Kwa kweli chuki inayosikika katika tuhuma za ufisadi na ulaji rushwa dhidi ya FIFA kwa hakika sio kitu cha kudhaniwa na mtu mmoja hiyo ni chuki ya shirikisho lote la UEFA.
''Lakini mimi nitawasamehe tu '' alisema Blatter.
Blatter alitawazwa rais wa FIFA baada ya kujiondoa kwa mpinzani wake Ali Bin al Hussein mwanamfale wa Jordan baada ya kushindwa katika mkondo wa kwanza wa uchaguzi kwa kura 133 kwa 73.
Blatter, ambaye ameongoza shirikisho hilo kwa miaka 17 amewataka wajumbe wa FIFA kushirikiana na kuwa imara. .
Akifungua mkutano mkuu wa FIFA mjini Zurich, Bwana Mr Blatter alibainisha kuwa shirikisho hilo linakabiliwa na matatizo - lakini akatoa wito kwa wajumbe kushughulikia matatizo hayo kwa pamoja.
Lakini kabla upigaji kura , mpinzani mkuu wa bwana Blatter , Ali Bin al Hussein mwanamfale wa Jordan, aliwaomba wajumbe wa mkutano huo kumuunga mkono -- kwa ajili ya kuboresha mchezo wa soka
Ali Bin al Hussein mwanamfale wa Jordan alijiondoa kabla ya kupigwa kura ya mkondo wa pili.
Wakati huohuo,wafadhili wakuu wa shiriko la kandanda duniani FIFA wanasema kuwa wanatarajia raisi wake aliyechaguliwa kwa mara nyingine Sepp Blatter kuchukua hatua madhubuti ili kurejesha hadhi ya shirikisho hilo iliyochafuka.
Kampuni za Coca-Cola na McDonalds zimeitaka FIFA kuchukua hatua za haraka kwa munufaa ya mchezo wa soka na mashabiki kote duniani.
Blatter alichaguliwa tena kwa muhula wa tano siku ya Ijumaa licha ya kuwepo uchunguzi unaofanywa na Marekani na Uswisi kuhusu kashfa zinazolikumba shirikisho hilo za ufisadi na ulaji rushwa dhidi ya maafisa wake wakuu.
Subscribe to:
Posts (Atom)