Aliyepandikizwa uso akutana na dadake marehemu
Mwanamke ambaye kakake alikufa katika ajali mbaya ya barabarani amekutana na mtu aliyepewa uso wake.
Amini
usiamini mtu huyo aliyefanyiwa upasuaji huo wa kihistoria alipandikizwa
uso mpya baada yake kuishi kwa miaka 15 akiwa bila pua.Richard Norris alimshukuru mwanamke huyo kwa niaba ya kakake marehemu aliyemwezesha kupata mwanzo mpya maishani.
Mwanamke huyo Rebekah Aversano alionekana akiugusa uso wa kakake akiwa haamini macho yake.
Richard Norris, anayetokea Virginia, Marekani alijeruhiwa katika ajali ya ufyatulianaji wa risasi miaka 15 iliyopita.
Yamkini Norris hakuwa amewahi kutoka nyumbani kwake katika kipindi hicho chote.
Aversano, kutoka Maryland.
Na alipomuona Aversano, alibubujikwa na machozi na kusikika akisema ''hii ndiyo uso na sura niliyokuwa nayo''
Kakake Joshua Aversano, alipoteza maisha yake katika ajali mbaya ya barabarani akiwa na umri wa miaka 21.
kauli yake ya kutoa viungo vya mwili wake haikupokelewa vyema na familia yake na haswa mamake Gwen Aversano.
''Baada ya kukutana na Norris aghalabu nimeweza kumuona mwanangu tena''
''Nahisi vyema kuwa nimemsaidia Norris kuanza upya maisha yake japo tumempoteza mpendwa wetu'' alisema mamake Joshua .
Upasuaji huo wa kihistoria ulifanywa katika chuo kikuu cha Maryland yapata miaka mitatu iliyopita.
Upasuaji ambao ulidumu kwa zaidi ya saa 36.
No comments:
Post a Comment