Monday, June 1, 2015

AC MILAN YAVUNJA REKODI MIAKA 60

AC Milan na Inter zavunja rekodi ya miaka 60 michuano ya ulaya

  Wakati fainali ya Champions League kwa mwaka 2016 ilipotangazwa itachezwa katika dimba la San Siro, mashabiki wa vilabu vya AC Milan na Inter Milan vinavyotumia uwanja huo kwa mechi walianza kuwa na ndoto za kupata ufalme wa soka barani ulaya katika uwanja wao wa nyumbani.
Ni Real Madrid pekee, ambao wameshinda ubingwa wa ulaya mara nyingi kuliko AC Milan, wakati miaka 5 iliyopita Inter Milan walitwaa ubingwa huo.
Lakini wakati vigogo viwili vya soka barani ulaya vitakuwa vikiutafuta ubingwa wa ulaya jijini Milan Mei 2016, hakutakuwa na nafasi ya wenyeji wa mji huo kupata uwakilishi kwenye michuano hiyo.
  Timu hizo mbili pia hazitopata hata nafasi kushiriki kwenye michuano Midogo ya Europa – hii ni rekodi ya ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka 60 kwa aidha AC Milan au Inter kushindwa kucheza katika michuano ya ulaya.
  Vilabu hivyo vimeshindwa kumaliza katika nafasi 5 za juu za ligi ya Serie A na hivyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya ulaya.
Inter Milan imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 8, huku AC Milan ikiwa nafasi ya 10.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika ni hapa hapa tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Kituo kinatoa huduma ya Hostel na kutoa kozi ya Kiingezeza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bnk ya CRDB simu 0715 772746















MTI UNAOAMBUKIZA UGONJWA WA EBOLA WAGUNDULIKA GUINEA

Mti wa Ebola nchini Guinea

Mti wa Ebola
Kuna mti unaodaiwa kusababisha mlipuko wa Ebola nchini Guinea.Kundi moja la wavulana lilimpeleka mwandishi wa BBC katika mti huu.
Walielezea kwamba siku moja waliwasha moto katika mti huo na popo wakaanguka kutoka kwa mti huo.
Waliwajaza popo hao katika mifuko na kuwala.Wakati huo hakuna mtu ambaye alikuwa amewahi kufariki na mlipuko wa Ebola.

WAANDAMANA WAKIWA UCHI, UGANDA

Waandamana wakiwa uchi Uganda

Wanawake katika kijiji kimoja cha kaskazini mwa Uganda wamefanya maandamano wakiwa uchi kutokana na mgogoro wa ardhi kati ya utawala wa eneo hilo na jamii ambao umeendelea kwa takriban miaka 10.
Wakati wa maandamano hayo ,mawaziri wa serikali na watafiti walipanga kukata kipande cha ardhi katika kijiji cha Apaa huko Amuru.
Utawala wa wanyama pori nchini Uganda unaamini kwamba watu wanavamia ardhi ya uhifadhi wa wanyama pori huku  wakidai kwamba ardhi hiyo ilikuwa ya mababu zao.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa katika kabila la Acholi ,mwanamke anapovua nguo na kusalia uchi ni zaidi ya kupigana kwa kuwa inatoa laana kwa mpinzani wake

JURGEN KLOPP KUTIMKIA LIVAPOOL

Jurgen Klopp haendi Liverpool.

klopp

Kocha ambaye ameamua kuondoka kwenye klabu ya Borrusia Dortmund Jurgen Klopp amethibitisha kuwa hatajiunga na klabu ya Liverpool kama inavyovumishwa kwenye baadhi ya vyombo vya habari barani ulaya .
Klopp majuzi aliiongoza Dortmund kwenye fainali ya kombe la ujerumani ambapo timu yake ilifungwa 3-1 na Wolfsburg akiwa tayari ametangaza kuondoka kwenye klabu hiyo baada ya kuwa nayo kwa misimu 7 .
Vyombo vya habari nchini England vimekuwa vikimhusisha na kocha huyo na mpango wa kujiunga na klabu ya Liverpool ambayo kwa nyakati tofauti imetajwa kuwa mbioni kumfukuza kazi kocha wake Brendan Rogers .
Jurgen Klopp amesema kuwa atakaa nje ya mchezo kwa muda akipumzika na kujipanga upya tayari kwa kurudi mchezoni huku akisema kuwa anahitaji kupumzika baada ya miaka saba ya kazi ngumu .
Kocha huyo pia hakuondoa uwezekano wa kujiunga na wapinzani wa Borrusia Dortmund Bayern Munich endapo fursa itajitokeza hapo baadae .

TANK LA MAFUTA LARIPUKA NA KUUWA WATU 70, NIGERIA

Nigeria na ajali nyingine mbaya ya lori la mafuta!! 

moto
Nigeria imeendelea kukumbwa na matukio ya vifo, baada ya tukio la kundi la Boko Haram kuvamia msikiti na kuuwa watu 16 jana, kuna taarifa nyingine ambayo si nzuri kutoka nchini humo.
Watu wasiopungua 70 wamefariki dunia Mashariki mwa Nigeria baada ya lori la kubeba mafuta kushika moto huku magari mengine 15 nayo yakishika moto.
Mashuhuda wa ajali hiyo iliyotokea jana wamesema dereva wa gari hilo alishindwa kudhibiti mwendo kazi wa gari hilo ndipo likakosa mwelekeo na kutoka barabarani na kuwagonga watu waliokuwa wakisubiri usafiri katika kituo kimoja cha mabasi.
Miaka mitatu iliyopita ajali mbaya kama hiyo iliua zaidi ya watu 100 huko Niger katika ajali ilisababishwa na watu kuchota mafuta yaliomwagika baada ya gari kubwa la mafuta kupata ajali.
Kwa habari, matukio na mengi mazuri, ni hpa hapa tangakumekuchablog

USHABIKI WA MPIRA BALAA

Azinduka baada ya wiki 2 na kitu cha kwanza alichoulizia kinahusu Barca vs Juventus 

Fainali ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya ambayo itafanyika mwishoni mwa wiki hii siku ya Jumamosi, kati ya FC Barcelona dhidi ya Juventus, itakuwa ni tukio la aina yake kwa mtoto mmoja wa kitaliano aishiye Jiji la Milan.
Kijana huyo ana umri 14, kwa bahati mbaya alipata ajali ya kukwama kwenye maji yenye kina kirefu kwa zaidi ya dakika 40, akapoteza fahamu kwa muda wa wiki mbili.
Gazeti la The Independent linaripoti kwamba mtoto huyo ambaye jina lake ni Michael, alipata ajali hiyo baada ya yeye na rafiki zake watano kutoka kwenye daraja la mto mmoja katika Jiji la Milan, mwisho wake baada ya kuzama mapigo yake ya moyo yalisimama kwa muda huo, baada ya vipimo ilionesha alipata tatizo zaidi kwenye ubongo.
Wiki nne baada ya kulazwa hospitali alizinduka na jambo la kwanza kuuliza ilikuwa kuhusu timu yake anayoishabikia kama bado ipo kwenye michuano ya mabingwa wa ulaya.
Daktari ambaye alikuwa anamsimamia, Alberto Zangrillo daktari binafsi wa mmiliki wa AC Milan, Silvio Berlusconi alisema kupona kwa mtoto huyo ni jambo kubwa zaidi lililowahi kumtokea katika maisha yake ya udaktari kutokana na hali mbaya aliyokuwa nayo.
Mtoto Michael, Jumamosi hii tarehe 6 atakuwa miongoni mwa mashabiki wa Juventus watakaokuwa wakiombea ushindi timu yao itakapokuwa ikipambana na FC Barcelona, Jiji la Berlin, Ujerumani.

SHERIA ZA NDOA ZA JINSIA MOJA ZAPAMBA MOTO ULAYA

Sheria ya ndoa za jinsia moja yaanzishwa

wapenzi wa jinsia moja
Kinara mkuu wa chama cha upinzani cha Labour nchini Australia, ameanzisha sheria inayokubalia ndoa ya wapenzi wa jinsia moja, sheria ambayo inapingwa na Waziri mkuu wa nchi hiyo, Tony Abbott.
Kiongozi huyo, Bill Shorten, amemtaka  Abbott kuwakubalia wanachama wa serikali wawe na uhuru wa kupiga kura kuhusiana na swala hilo.
Abbot ambaye ni mfuasi wa kanisa katoliki alikataa kura ya uhuru wa ndoa za jinsia moja na kusema kuwa lengo lake kuu ni kuimarisha uchumi na usalama wa taifa.

MWANAMKE WA KUIGWA

 Mkazi wa kijiji cha Jirihini  kata ya Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga, Mwanakombo Said, akisonga ugali na kuwauzia wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO)  eneo la Mbugani kunakofanyika  utafiti wa awali na  kuonyesha   uwepo wa mafuta na gesi umbali wa zaidi ya  kilometa 10 kutoka kijiji cha Jirihini.
Tangakumekuchablog
Mkinga
MWANAKOMBO amewataka wanawake wenzake waache kujikalia vibarazani na kuunda umbea pamoja na kuwategemea wanaume zao au mabwana  na badala yake watafute njia za kujipatia pesa kwa njia za halali.
Alisema haikuwa rahisi kwake kuweza kujitoa mhanga na kuwafuata wafanyakazi wa kampuni ya uchimbaji Madini kupika na kuwauzia chakula ambapo kwa siku amekuwa akipata zaidi ya shilingi laki moja tokea asubuhi.
Alisema eneo hilo limekuwa likitembelewa na watu mbalimbali kujionea namna ya hatua za Uchorongaji huo unaofanywa na Kampuni ya  Madini ya STAMICO.
Alisema amekuwa kitoka alfajiri nyumbani kwake kwa kukodi pikipiki (bodaboda) kupakiza maji, na vyombo vyengine vya kutayarishia chai na chakula ambao mwanzo watu wengi walikuwa wanambeza na kuonekana kujihangaisha.
Alisema kwa sasa amekuwa akivuna pesa na mara baada ya mradi huo kukamilika atakuwa na mtaji wa kufungua biashara au saloon ya kisasa na hivyo kuwataka wanawake wenzake kujituma kwani fursa nyingi za kujipatia kipato kwa nia za halali zipo.





UKIENDA CHINA , EPUKA UVUTAJI SIGARA HADHARANI

Ukivuta sigara hadharani China kuna faini zake!!

mchinaa
China iliwahi kupitisha sheria ya kusitisha uvutaji wa sigara katika maeneo ya wazi pamoja na maeneo ya shule na hospitali lakini haikuweza kutekelezeka kwa mara ya kwanza.
Ingawa kuna baadhi ya nchi kama Jamaica ambapo uvutaji sigara ama bangi si kitu cha ajabu lakini kwa upande wa China sasa kitendo hicho kimeonekana ni kosa kubwa na Serikali imeanza mikakati ya kuhakikisha inatokomeza uvutaji sigara.
Nchi hiyo imerudi kwenye headlines tena na safari hii Serikali imeweka wazi mikakati yake hiyo ya kuzuia uvutaji wa sigara kuanza leo katika maeneo ya wazi hasa ya mji mkuu wa nchini hiyo Beijing na kinyume na hapo kuna faini ambazo zitatolewa kwa wanaokaidi agizo hilo.
Ripoti ya Wizara ya afya imesema nchi hiyo ina wavutaji wa sigara zaidi ya milioni 300,
Sheria hiyo imesema watakaoukiuka makubaliano hayo watatozwa faini ya fedha ya China yuan 32.25 ambayo ni sawa na dola 1.60 huku watakaorudia kosa hilo kwa zaidi ya mara tatu watatozwa faini ya dola 1600 pamoja na kuwekwa kwenye website ya Serikali.
Pia Serikali imetoa onyo kwa wauzaji wa sigara kuhakikisha wanauza kuanzia mita 100 kutoka katika ameneo ya wazi na karibu na shule ama hospitali ili kukwepa faini hizo.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika usiwe mbali nami, ni hapa hapa tangakumekuchablog

SOMA MAKUBWA YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO, JUNE 01 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaltwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

TODAY
MWANANCHI
Mwenyekiti wa CCM, Simiyu Musa Ntimizi amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kumlawiti kijana mmoja mkazi wa Manispaa ya Tabora.
Mwenyekiti huyo alisomewa mashtaka mbele ya hakimu na kudaiwa kufanya koda hilo nyumbani kwake kwa kumrubuni kijana huyo kwa kumnunulia bia mbili kwenye baa moja mjini Tabora kabla ya kutenda kosa hilo.
Wakili Jocktan Rusherwa alidai kuwa baada ya kijana huyo kulewa na kupoteza fahamu, mshtakiwa alimpeleka nyumbani kwake na kufanya kitendo hicho.
Hata hivyo mshtakiwa alikana tuhuma hizo na yupo nje kwa dhamana na wakili kuahirisha kesi hiyo hadi itakaposomwa tena kesho.
MWANANCHI
Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ametangaza nia yake ya kugombea urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba akieleza jinsi atakavyoivusha Tanzania kuwa nchi yenye uchumi wa kati utakaopatikana kwa kutoa haki kwa watu wote.
Akitangaza nia hiyo jana kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere katika Chuo cha Mipango Dodoma, Nchemba alisema: “Ahadi yangu kubwa kwenu ni kwamba nitawavusha. Nitawavusha wanaCCM wenzangu pamoja na Watanzania kwa ujumla… wakati ni sasa tunataka Taifa letu lifike kuwa nchi yenye uchumi wa kati,” alisema Nchemba na kuongeza:
“Ninachoomba kutoka kwenu, mniamini na mniunge mkono katika hili… nitawavusha. Lakini tukumbuke kwamba kila mmoja lazima atimize wajibu wake katika utendaji kazi ili tufikie huko tunapotaka kufikia.”
Nchemba aliyekuwa ameongozana na mkewe, Neema na watoto wake watatu, Isaack, Grecious na Joshua pamoja na ndugu jamaa na marafiki, alisisitiza kuwa ili kufikia malengo hayo, lazima nchi iwe na mfumo wa uwajibikaji utakaowezesha kulinda rasilimali za Taifa na kuongeza Pato la Taifa.
Huku akitumia kauli mbiu ya ‘Mabadiliko ni Matendo, Wakati ni Sasa’, ambayo ataitumia katika safari yake ya kuelekea Ikulu, Nchemba aliyetumia dakika 115, kuanzia saa 10.10 jioni hadi saa 11.25 jioni, alisema atapambana na tabia za watu kufanya kazi kwa mazoea, rushwa, ufisadi na kwamba Serikali ya Awamu ya Tano atakayoiongoza endapo atachaguliwa, itakuwa ya uadilifu na uaminifu.
Alisema iwapo atachaguliwa, ataifanya nchi kuwa ya kipato cha kati sambamba na watu wake, kujenga Taifa linalojitegemea kibajeti na kuwajengea uwezo wananchi kumiliki uchumi wao wenyewe.
Jambo la kwanza na la msingi ni kuitambua ajenda ya Watanzania, Watanzania watamuunga mkono kiongozi kwa kuitambua ajenda yake,” alisema.
Alisema wakati akijitathimini kutangaza nia ya kugombea alikuwa akifahamu ajenda ya Watanzania, huku akisisitiza kuwa umaskini hakuusoma katika vitabu, bali amekulia katika maisha ya kimaskini.
NIPASHE
Wakuu  wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wameishauri serikali ya Burundi kusogeza mbele mwezi mmoja na nusu uchaguzi mkuu nchini humo.
Uchaguzi wa wabunge ulitarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii na wa urais ukipangwa kufanyika mwezi huu.
Hatua hiyo imetokana na kutoimarika kwa hali ya amani na utulivu kufuatia baadhi ya vyama vya upinzani na mashirika yasiyo ya kiserikali kuendelea na maandamano kupinga hatua ya Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza, kutangaza kuwania urais kwa muhula wa tatu.
Taarifa ya kuomba kusogezwa mbele kwa uchaguzi huo ilitolewa jana na wakuu wa nchi hizo katika mkutano wao uliofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa EAC, Dk. Richard Sezibela, alisema  wakuu hao waliishauri serikali ya Burundi kusogeza uchaguzi huo kutokana na nchi hiyo kutotengemaa kisiasa.
Alisema wakuu hao pia walitoa wito kwa makundi yenye silaha kuziweka chini. Pia, waliishauri serikali ya Burundi  kuwarejesha raia wake wote waliokimbilia nchi jirani.
Dk. Sezibera alisema wakuu wa EAC pia walitoa wito kwa wadau wa amani ukiwamo Umoja wa Mataifa  (UN) na Umoja wa Afrika (AU), kuingilia kati mgogoro huo.
Waliohudhuria mkutano huo ni Mwenyekiti wa AEC, Rais Jakaya Kikwete (Tanzania); Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta; Rais wa Uganda, Yoweri Museveni huku Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, akihudhuria kama mlezi wa Burundi.
Rwanda iliwakilishwa na Waziri wake wa Mambo ya Nje, Valentine Rugwaiza huku Burundi ikiwakilishwa na Waziri wa Mambo ya Nje, Allen Nyamizwe.
NIPASHE
Shirika lisilo la Kiserikali la Sikika limewaasa wabunge kuishinikiza serikali iongeze bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba kwa mwaka 2015/16, ili kuhakikisha upatikanaji wa dawa nchini  unaongezeka kufikia asilimia 80, kama inavyotarajiwa na mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN).
Aidha, imewataka waishinikize itoe fedha zote zinazoidhinishwa na Bunge kwa wakati, ili kuviwezesha vituo vya huduma za afya vya umma kuondokana na uhaba wa mara kwa mara wa dawa muhimu na vifaa vya tiba, na hivyo kuimarisha afya za wananchi walio wengi.
Wito huo ulitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Sikika, Irenei Kiria (pichani) na kuongeza kuwa wabunge wanapaswa kulichukulia suala hili kwa umuhimu wa kipekee na kuachana na itikadi za vyama, ili kuokoa maisha ya Watanzania, hasa wanaotegemea kupata matibabu katika vituo vya huduma za afya vya umma nchini.
“Ukiangalia bajeti iliyotengwa kwa ajili ya dawa muhimu na vifaa tiba kwa mwaka wa fedha wa mwaka 2015/16, kwenye bajeti ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inayosomwa kesho, ni Shilingi bilioni 37 tu kati ya mahitaji halisi ya zaidi ya Shilingi bilioni 500, fedha ambazo ni kidogo sana,” alisema.
Alisema bajeti hiyo imepungua kwa kiwango kikubwa ukilinganisha na bajeti ya miaka ya nyuma kwa mfano kuanzia mwaka 2011/12, kuonyesha namna serikali isivyotoa kipaumbele kwa eneo hilo lililo muhimu kwa ustawi wa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Kiria alisema mwaka 2011/12, mahitaji halisi ya bajeti ya dawa muhimu na vifaa tiba yalikuwa Sh. bilioni 188, lakini  jumla ya bajeti iliyopitishwa ilikuwa Sh. bilioni 123.4, na serikali ikatoa Sh. bilioni 98 (79.4%) ya fedha iliyoidhinishwa.
Alisema mwaka 2012/13 mahitaji halisi ya fedha kwenye eneo hilo yalikuwa Sh. bilioni 198, lakini bajeti iliyopitishwa ilikuwa Sh. bilioni 80.5 na serikali ikatoa fedha zote hizo.
“Japo tatizo likabaki kuwa ni fedha kuchelewa kutolewa kwa wakati na hivyo kuzorotesha utoaji wa huduma kwa wananchi, ikizingatiwa kuwa upatikanaji wa dawa muhimu na vifaa tiba katika vituo vya huduma za afya  vya umma, ni moja ya viashiria  vya huduma bora za afya katika nchi yoyote ile,” alisema.
Aidha alisema mwaka 2013/14, mahitaji halisi ya fedha yalikuwa Sh. bilioni 549, lakini bajeti iliyoidhinishwa ilikuwa Sh. bilioni 64, na serikali ikatoa Sh. bilioni 50 (78.9%).
Kwa mujibu wa Kiria, mahitaji halisi ya fedha kwa mwaka 2014/15, yalikuwa Sh. bilioni 577, lakini fedha iliyoidhinishwa ilikuwa Sh. bilioni 70.5, na fedha iliyotolewa hadi sasa ni Sh. bilioni 23.5.
NIPASHE
Bodi ya Mikopo ya  Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB), imesema ilichelewa kutoa mikopo kwa wanafunzi wa vyuo vikuu nchini kutokana na sababu mbalimbali, zikiwamo kuchelewa kwa fedha kutoka serikalini, marejesho madogo ya mikopo na uchache wa fedha zilizokusanywa.
Mkurugenzi Msaidizi wa Habari, Elimu na Mawasiliano wa HESLB, Cosmas Mwaisobwa, alisema HESLB ilishindwa kupeleka fedha kwa wakati kutokana na vyanzo vilivyotegemewa kutoa fedha kuchelewesha huku akisisitiza kuwa fedha iliyokwisha kusanywa haikuweza kutosheleza idadi ya wanafunzi wenye mahitaji.
“Siyo kama inavyoelezwa na vyombo vya habari, mikopo katika mihula yote ya kwanza ilitolewa kwa wakati, katika kipindi hiki cha muhula wa mwisho wa masomo mikopo imechelewa kwa sababu ya fedha zinazotengwa kwa ajili ya mikopo kuchelewa na urudishaji wa mikopo usioridhisha, Mwaisobwa.
Aidha, alisema mikopo haikuchelewa kupelekwa katika vyuo vyote vyenye wanafunzi wenye mahitaji na kuongeza kuwa hata vyuo vilivyofanya migomo, baadhi ya vitivo vilikuwa vimepatiwa mikopo.
Alisisitiza kuwa HESLB imeshapeleka fedha za mikopo kwenye  vyuo vyote na kuwa vyuo ambavyo wanafunzi hawajapokea, vina utaratibu wake wa kuwapatia fedha hizo.
Hivi karibuni, wanafunzi wa Vyuo Vikuu nchini vikiwamo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph, Chuo Kikuu cha Iringa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Ualimu cha Dar es Salaam (DUCE) waligomea masomo kuishinikiza serikali kupitia HESLB kuwapatia fedha za kujikimu.
NIPASHE
Serikali  imeombwa kuangalia upya tatizo la ukubwa wa kodi kwa hospitali binafsi kwani lengo kuu ni kutoa hudumu bora kwa gharama nafuu kwa kila Mtanzania.
Ombi hilo lilitolewa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Regency ya jijini Dar es Salaam (RMC), Dk. Amish Kanabar, wakati wa ujio wa Mwenge wa Uhuru kwenye hospitali hiyo ambao ulizindua jengo jipya la ghorofa 10 la hospitali hiyo.
Alisema hospitali binafsi na za serikali zina lengo la kuwahudumia Watanzania kupata afya bora, hivyo hakuna haja ya kutoza kodi kubwa kwani hali hiyo inazidumaza na kushindwa kukua kwa kasi.
Alisema katika kuhakikisha wanaendelea kutoa huduma bora, RMC imechukua mkopo ghali kutoka benki na hata kuweka rehani hisa za wanachama wake ili kufanikisha ujenzi wa jengo jipya.
“RMC  inafanya jitihada kuhakikisha inakuwa chuo cha mafunzo ya uuguzi na utaalam wa tiba na afya ili kupunguza pengo la nguvu kazi katika sekta ya afya Tanzania. Mara zote RMC imekuwa ikishirikiana na sekta ya umma, Manispaa ya Ilala na Lions Club ya Dar es Salaam Host na Shirika La Nyumba La Taifa, “ alisema.
Alisema hospitali inatoa huduma kwa wastani wa wagonjwa 500 kwa siku na kwamba upanuzi wa jengo una maslahi mapana kitaifa kama vile kuwezesha upatikanaji wa huduma za matibabu kwa gharama nafuu, kutekeleza kwa vitendo sera za Mkukuta II na Dira ya Taifa 2025 na kuongeza wigo wa ajira na mafunzo kwenye sekta ya afya Tanzania
MTANZANIA
Utangazaji nia ya kuwania urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) umeanza kwa kishindo, huku machifu wote wa Mkoa wa Mbeya wakitarajiwa kumuunga mkono Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Prof. Mark Mwandosya, ambaye leo anatarajiwa kutangaza nia mkoani Mbeya.
Miongoni mwao ni Chifu wa Rungwe, Mbozi na Chifu wa Jiji la Mbeya, Mwashiga ambaye atawaongoza pia wazee wote wa jiji hilo.
Wakati hayo yakijiri, wakazi wa Jiji la Mbeya wakiwamo vijana, pia wanatarajiwa kujitokeza kwa wingi kumsindikiza Profesa Mwandosya kutangaza nia.
Hafla hiyo inayotarajiwa kufanyika saa nne asubuhi, itafanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mkapa uliopo eneo la Soko Matola jijini Mbeya.
Katika hafla hiyo, viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyo nje ya Ukawa wanatarajiwa kuhudhuria ikiwa ni pamoja na kupata nafasi ya kutoa msimamo wao wa kumuunga mkono Profesa Mwandosya.
Vyama hivyo ni TLP, ACT-Wazalendo, APPT- Maendeleo,  UDP, PP, SAU na UPDP.
Wakati Mwandosya akiwa Mbeya, Mbunge wa Afrika Mashariki, Makongoro Nyerere naye anatarajia kutangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Mwitongo wilayani Butiama.
Wakati hayo yakijiri, Mbunge wa Sengerema mkoani Mwanza, William Ngeleja pamoja na Waziri wa Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi, Dk. Titus Kamani wao wakitarajiwa kutangaza kesho jijini Mwanza.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu, amesema siku saba zijazo kuanzia sasa atachukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kugombea urais wa Tanzania.
Alitoa kauli hiyo jana jijini Arusha baada ya kumalizika ibada ya kwanza aliyoshiriki katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Kati, Usharika wa Arusha mjini.
“Nimekuja kanisani kuabudu, nimefarijika kwa neno la Mungu. Nataka kusema, nilishatangaza nia miezi saba iliyopita, Desemba mwaka jana,” Nyalandu
Kwa upande waje Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema atatangaza nia ya kuwania urais Juni 6, mwaka huu jimboni kwake Mtama mkoani Lindi.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika, ni hapa hapa tangakumekuchablog

AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wanaojiendeleza kielimu. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

















Kwa habari na matukio za ukweli na uhakika , ni hapa hapa tangakumekuchablog