
Wakati
fainali ya Champions League kwa mwaka 2016 ilipotangazwa itachezwa
katika dimba la San Siro, mashabiki wa vilabu vya AC Milan na Inter
Milan vinavyotumia uwanja huo kwa mechi walianza kuwa na ndoto za kupata
ufalme wa soka barani ulaya katika uwanja wao wa nyumbani.
Ni Real Madrid pekee, ambao wameshinda ubingwa wa ulaya mara nyingi
kuliko AC Milan, wakati miaka 5 iliyopita Inter Milan walitwaa ubingwa
huo.
Lakini wakati vigogo viwili vya soka barani ulaya vitakuwa
vikiutafuta ubingwa wa ulaya jijini Milan Mei 2016, hakutakuwa na nafasi
ya wenyeji wa mji huo kupata uwakilishi kwenye michuano hiyo.

Timu
hizo mbili pia hazitopata hata nafasi kushiriki kwenye michuano Midogo
ya Europa – hii ni rekodi ya ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha
miaka 60 kwa aidha AC Milan au Inter kushindwa kucheza katika michuano
ya ulaya.

Vilabu
hivyo vimeshindwa kumaliza katika nafasi 5 za juu za ligi ya Serie A na
hivyo kushindwa kupata nafasi ya kushiriki katika michuano ya ulaya.
Inter Milan imemaliza ligi ikiwa nafasi ya 8, huku AC Milan ikiwa nafasi ya 10.
Kwa habari na matukio ya ukweli na uhakika ni hapa hapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment