Friday, July 29, 2016
NJIWA ASAFIRI FINLAND HADI UGANDA
Ndege aliyesafiri kutoka Finland hadi Uganda
Isaac Mujaasi, afisa wa mauzo na mawasiliano katika UWEC, ameambia BBC kwamba ndege huyo alikuwa ameumia katika mabawa yake baada ya kugongwa na ndege iliyokuwa inapaa.
Bw Mujaasi anasema waliwasiliana na maafisa wa makumbusho hao ambao wamethibitisha kwamba ndege huyo ni wao.
Afisa huyo hata hivyo amesema ni kawaida kwa ndege kuhama kutoka Ulaya, hasa wakati wa majira ya baridi na kukimbilia maeneo yenye joto.
TATIZO LA UGUMBA KWA MWANAUME NA MWANAMKE
Tatizo la Ugumba Kwa Mwanaume na Mwanamke
Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke
wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya
upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata
ujauzito.
Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.
Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.
Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.
Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini. Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.
Je mimba hutungwa vipi?
Mimba hutungwa baada ya mwanamke kutoa yai kutoka katika moja ya viwanda vyake vya mayai ya kike yaani ovaries,kitendo hiki hujulikana kama ovulation. Yai husafiri hadi kwenye mfuko wa uzazi ujulikanao kama uterus (womb) kupitia kwenye mirija ya uzazi inayojulikana kama mirija ya fallopian.
Mbegu moja ya kiume (sperm) ni lazima itungishe au iungane (fertilize) na yai au mayai ya kike (ovum au ova) wakati yai likielekea kwenye uterus. Baada ya mbegu ya kiume na yai la kike kuungana, muunganiko uliotengenezwa yaani kiinitete (embryo) hushuka mpaka kwenye mfuko wa uzazi na kujiwekeza hapo ili kiendelee kuwa kiumbe.
Tatizo la ugumba linaweza likawa ni la nwanaume au mwanamke pekee ingawa wakati mwingine wote wawili wanaweza kuwa na tatizo hili.
Ni sababu zipi zinazoleta tatizo la ugumba (infertility) ?
Kwa wanawake ;
Tatizo la ugumba linaweza kutokea wakati wa;
Kwa wanaume;
Kwa wanawake;
Tiba ni kama ifuatavyo;

- Yai au kiumbe kilicho ndani ya mfuko (uterus) wa uzazi kushindwa kukua hadi kufikia kuwa mtoto.
- Mayai yaliyo ndani ya mfuko wa uzazi kushindwa kujishikiza kwenye ukuta wa mfuko wa uzazi (uterus lining)
- Matatizo kwenye njia ya kupita yai au mayai wakati yanakwenda kwenye mfuko wa uzazi (uterus).
- Matatizo ya mayai ya uzazi (ovaries) kushindwa kutoa mayai (eggs).
- Tatizo la ugumba kwa wanawake husababishwa na;
- Matatizo ya autoimmune disorders kama antiphospholipid syndrome (APS)
- Matatizo katika uterus na shingo ya kizazi (cervix) kama uvimbe (fibroids or myomas) na birth defects
- Matatizo katika mfumo wa kuganda wa damu (clottaing disorders).
- Mazoezi kupita kiasi (excessive exercise), afya iliyodhoofika (poor nutrition), matatizo ya kula (eating disoder).
- Baadhi ya madawa au sumu.
- Msongo wa mawazo (emotional stress)
- Tatizo la kukosekana kwa usawa wa mfumo wa vichocheo mwilini (hormonal imbalance)
- Uzito uliopitiliza (obesity)
- Unywaji pombe kupindukia (heavy alcohol intake)
- Magonjwa ya muda mrefu kama kisukari (diabetes)
- Magonjwa ya kina mama (Pelvic inflammatory infection, PID)
- Ovarian cysts and polycytic ovarian syndrome
- Magonjwa ya zinaa (sexually transmitted disease, STD) au endometriosis
- Saratani
- Uvutaji sigara, madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk.
- Matatizo ya hedhi - wanawake wanaopata hedhi bila kutoa mayai (anovulatory menstrual cycle)
- Kuwepo kwa cervical antigens ambazo huua shahawa za mwanamume na hivyo kusababisha kwa mwanamke kutopata ujauzito.
- Tatizo la ugumba - linaweza kutokea kwa mwanamume wakati wa;
- Kupungua idadi ya shahawa (decrease number of sperm)
- Shahawa kuzuiwa kutolewa (blockage of sperm)
- Shahawa ambazo hazifanyi kazi yake vizuri.
- Kwa mwanamume, tatizo la ugumba husababishwa na;
- Mazingira yaliyo na kemikali zinazoathiri uwezo wa mwanaume kumbebesha mimba mwanamke (environment pollutants)
- Kukaa sehemu zenye joto kali sana kwa muda mrefu (exposure to high heat)
- Matatizo kwenye mfumo wa viashiria vya asili (genetic abnormalities)
- Unywaji pombe kupindukia, matumizi ya madawa ya kulevya kama kokeni, bangi, hashishi nk, hupunguza idadi na kiwango (quality) cha shahawa .
- Kuzeeka (older age)
- Kutumia dawa za vichocheo vya mwilini (hormonal supplements) ama kukosekana kwa baadhi ya vichocheo mwilini (hormonal deficiency)
- Kuasiliwa (impotance)
- Magonjwa ya korodani (testicular infections) au kwenye mishipa ya korodani (epididymis)
- Historia ya matumizi ya baadhi ya dawa za saratani
- Magonjwa ya zinaa (STD), ajali (trauma) au upasuaji
- Historia ya mionzi (radiation exposure)
- Retrograde ejaculation (matatizo ya kukojoa au kutoa shahawa)
- Msongo wa mawazo (emotional stress)
- Uvutaji sigara
- Matumizi ya baadhi ya dawa kama cimetidine, spironolactone, nitrofurantoin.
- Varicocele
- Mumps
Kwa wanaume;
- Semen analysis - Kipimo hiki kinahusisha uchukuaji wa shahawa kutoka kwa mwanamume ambaye amekaa siku 2-3 bila kujamiana na kuzipima kujua wingi, kiwango chake, shepu zake, viscosity of semen, motility and swimming speed.
- Testicular biopsy - Kipimo cha korodani
Kwa wanawake;
- Kipimo cha kiwango cha vichocheo kwenye damu (blood hormone levels)
- Cervical mucus detection - Kipimo cha kuangalia kamasi za kwenye shingo ya kizazi ili kupima jinsi zinavyovutika (stretch), na kama ni za majimaji (wet) wakati wa mzunguko wa hedhi, na kama zina utelezi ambao huusishwa naovulatory phase
- Kipimo cha kiwango cha joto mwilini (body basal temperature) - Kuongezeka kwa kiwango cha joto kwa 1 degree kutoka kiwango cha joto cha kawaida cha binadamu (37 C) kinahusishwa na ovulation ambapo mwanamke ana asilimia kubwa ya kushika ujauzito au yai limetolewa na ovaries.
- Postcoital testing - Kupima kamasi za shingo ya kizazi (cervical mucus) zilizochukuliwa masaa 2-8 baada ya wapenzi kujamiana ili kuangalia mwiingiliano wa shahawa na kamasi za shingo ya kizazi.
- Kipimo cha kichocheo aina ya progesterone kwenye damu (serum progesterone testing)
- Kipimo cha ukuta wa uterus (biopsy of uterine lining or endometrium)
- Kupima kichocheo aina ya Luteinizing hormone kwenye mkojo ili kuweza kutabiri lini yai litatolewa na ovaries ili kupangilia siku za kujamiana kwa wapenzi.
- Hysterosalpingography (HSG) - Kipimo cha X-ray kinachotumia dawa maalum (contrast dye) inayoonyesha njia ya shahawa kutoka kwenye shingo ya kizazi kupitia ndani ya mfuko wa kizazi (uterus) na kwenye mirija ya uzazi(fallopian tubes).
- Laparascopy - Direct visualization of pelvic cavity
- Progestin challenge
- Pelvic exam-hufanywa na daktari.
Tiba ni kama ifuatavyo;
- Ushauri nasaha na kuwaelimisha wapenzi wawili - Matatizo mengi ya ugumba hutokea kutokana na uelewa au ufahamu mdogo wa elimu ya uzazi na ya kujamiana kwa wapenzi au wanandoa.Kuna wanaume wengi ambao hufika kilele haraka wakati wa kujamiana na hivyo kutoa shahawa mapema (au kukojoa) kabla ya muda muafaka (premature ejaculation), hii husababisha kutopata ujauzito ambapo lawama zote hupelekwa kwa mwanamke pasipo mwanamume kugundua kuwa tatizo ni lake. Ifahamike kwamba hakuna muda uliotengwa ambao ni muafaka wa kufika kilele au kukojoa kwa mwanamume lakini watafiti wa mambo ya kujamiana wanashauri angalau mwanamume afike au akojoe baada ya dakika 15 na kuendelea. Hivyo ni bora kwa wapenzi kujiandaa kisaikolojia mwanzo na kuchezeana kabla ya kuanza kujamiana ili kurefusha muda kwa mwanamume.
- Tatizo jengine ni kutofahamu lini hasa ni muda muafaka wa kujamiana ili kushika mimba kwa urahisi. Kuna wanawake ambao hawajui hata mzunguko wao wa hedhi (yaani hawajui wanaanza na kumaliza hedhi lini na wakati wa hedhi wanatumika kwa muda wa siku ngapi). Ongeza nafasi yako ya kushika ujauzito kwa kujamiana angalau mara 3 kwa wiki kuelekea wakati wa ovulation au kujamiana wakati wa kipindi chote cha ovulation. Ovulationhutokea wiki 2 kabla ya mzunguko wako mwengine wa hedhi, kama una mzunguko wa hedhi wa siku 28 (yaani kila baada ya siku 28 unapata hedhi), ni vizuri kujamiana angalau kwa siku 3 kati ya siku ya 7-18 baada ya kupata hedhi.
- Kupunguza kunywa pombe kupindukia, kuvuta sigara, kuacha matumizi ya bangi, kokeni nk.
- Kupunguza kiwango cha mazoezi kwa wanawake.
- Kupunguza unene uliopitiliza
- Kuwa na mpenzi mmoja mwaminifu kwani kuwa na wapenzi wengi huongeza athari ya kupata magonjwa ya zinaa.
- Kuacha tabia ya kuvaa nguo nzito au zenye kuleta joto kali sehemu za siri kwa wanaume kwani joto kali sana hupunguza kiwango na kuathiri utolewaji wa shahawa.
- Kula mlo kamili na wenye virutubisho vyote muhimu kwa afya njema.
- Dawa za kutibu magonjwa kwenye mfumo wa uzazi, magonjwa ya zinaa nk.
- Njia za kitaalamu za kupata ujauzito zijulikanazo kama in vitro fertilization na intrauterine fertilization.
- SOURCE MG BLOG
MBINU ZA KUACHA UVUTAJI SIGARA
Mbinu za kuacha uvutaji wa sigara
Miongoni mwa mambo magumu kabisa katika ufanikishaji wake ni mtu
kuachana na uvutaji wa sigara. Watu wengi wamekuwa wakionywa kuachana na
uvutaji wa sigara kwa sababu ya madhara yake, lakini wamekuwa
wakishindwa kutokana na kukolewa na kiwango cha Nikotini inayopatikana
katika tumbaku.
Vijana wengi wamekuwa wakijiingiza katika uvutaji kwa kufuata mkumbo, lakini baadaye wanapokuja kutambua kuwa wako katika hatari ya kuambukizwa au pengine wana ugonjwa wa kifua kikuu, wanakuwa katika wakati mgumu wa kuachana na uvutaji huo. Wengi wao wamekufa huku makundi kwa makundi wakitangatanga kutafuta suluhu ya kuchana na uvutaji, si tu kwa sababu ya kuhofia ugonjwa, bali hata kukosa uwezo wa kununua bidhaa hiyo.
Hata hivyo idadi kubwa ya wanaojaribu kuacha wamejikuta wakipata majibu ya kutoweza, kutokana na kusumbuliwa na hamu ya uvutaji, umbumbu wa mawazo pindi wanapokaa muda mrefu bila kuvuta, kuumwa na kichwa na hata udhaifu katika kukumbuka vitu au mambo waliyofanya au waliyopanga kuyatenda.
Pamoja na yote hayo watalaam na washauri wa masuala uvuaji wa sigara wanasema wanaopatwa na hayo wamekosa mbinu na muongozo wa kuwasaidia waachane na uvutaji wa sigara bila kupata madhara.
Kwa ufupi somo hili limehusisha uchunguzi wa kina pamoja na kumbukumbu za kitaalamu kutoka kwa washauri kama Anderson JE, Jorenby DE, Scott WJ, Fiore MC, Bailey WC, Cohen SJ, ambao wote kwa pamoja kupitia vituo vyao kikiwemo cha US Department of Health and Human Services na Public Health Service walishawahiwa kueleza mbinu salama za kuachana na uvuaji wa sigara. Zifuatazo ni dondoo kadhaa za kufuata ili mvutaji aache sigara kwa usalama.
Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.

- Mvutaji lazima afahamu ni muda gani ambao huwa anavuta sigara kwa wingi, je ni wakati akiwa amelewa au akiwa na mawazo mengi ya kimaisha? Akishafahamu hilo ajiulize ni kiwango gani cha sigara ambacho huwa unavuta kwa siku?
- Baada ya hapo achukua kitabu chake cha kumbukumbu na aandike muda huo ambao yeye huvuta sigara kwa wingi. Ajiulize kwa nini huwa unavuta, atathimini madhara ya uvutaji wa sigara kwake binafsi na kwa familia yako.
- Kaa chini upitie kwa makini kumbukumbu zako za muda na kiwango cha sigara unazovuta kwa nyakati hizo, kisha panga utaratibu mpya. Kwa mfano kama unavuta sana wakati ukiwa kwenye mawazo hakikisha kuwa unapoanza kufikiria juu ya jambo fulani uwe na kitu mbadala kitachukua nafasi ya sigara. Mfano kahawa au chai? Hakikisha kila penye hamu ya uvutaji unaweka kitu kingine mbadala cha kufanya zaidi ya kuvuta sigara.
- Ondoa masalio ya sigara katika sehemu ambazo unaishi, fua nguo zote na vitambaa ili kuondoa harufu ya sigara katika eneo unalokuwepo. Usikae karibu na mtu anayevuta, usikubali kuwa mshirika wa mvutaji na usiwe mtu wa kuendekeza sana msukumo wa mwili unaotaka uvute, bali kila unapowaza juu ya kuvuta fikiria madhara na nia yako ya kuacha.
- Wafahamishe rafiki zako kuwa umeamua kuachana na uvutaji, ili upate watu wa kuwaonea aibu pale utakapoanguka na kurudia uvutaji wa sigara. Panga tarehe ya kuacha na iwe kwenye kumbukumbu.
- Wakati ukiiendea tarehe hiyo ya kuacha hakikisha unapunguza kiwango cha uvutaji kadiri unavyoisogea siku hiyo. Jipangie muda mrefu zaidi ya kuvuta kulingana na kiwango chako cha uvutaji na kuendelea kuuongeza kila siku ili uzoee kukaa saa nyingi bila kuvuta.
- Fuata ratiba mbadala uliyojiwekea kuziba pengo la uvutaji, kama umepanga kutumia kahawa kila unapokuwa mpweke sebuleni hakikisha unajizoeza ili ikifika tarehe yako ya kuacha usiwe mtu wa kujiuliza cha kufanya nyakati ambazo utakuwa na hamu ya sigara.
- Lengo lako liwe ni kufanikiwa na usikate tamaa utakaposhindwa kufanikisha lengo lako kwa wakati uliojipangia. Mara kwa mara nenda kamuone daktari mshauri ili akupe muongozo zaidi wa kukusaidia na ikiwezekana akupe nafasi ya kuwatembelea wagonjwa waliopata ugonjwa wa kifua kwa sababu ya kuvuta sigara.
Kwa kifupi hizo ni dondoo chache tu za kukusaidia kuachana na uvutaji wa sigara, lakini mara nyingi kinachoweka nguvu za kufanikisha uachaji wa sigara ni utashi wa mtu ambao hutokana na tathimin ya kina ya muhusika na mtazamo wake juu ya sababu za kuacha. Mara nyingi wanaoshindwa ni wale ambao hawakuzitia nguvu sababu za kuacha kwao.
Siku zote mwanadamu anaongozwa na utashi na kila mwenye kutaka hufanikiwa. Hii ina maana kuwa kama mwanadamu atasema hawezi kuacha kitu fulani, haina maana kama hawezi kwa sababu ameshindwa kujizuia bali ameamua kutokutaka na kinachomshinda ni matokeo ya maamuzi yake. Kila anayetaka jambo hufanikiwa na hata wavutao sigara wanaweza kuacha kama wakitaka kufanya hivyo.
source MG
BILIONEA MTANZANIA AELEZA SABABU YA KUTONUNUA NDEGE
Bilionea mtanzania katoa sababu za kwanini hajanunua ndege binafsi
Kama ni msomaji na mtumiaji mzuri wa
mitandao hususani ya kijamii, basi utakuwa ushawahi kukutana na
headlines za mtanzania katika jarida la Forbes, mtanzania Mohammed Dewji ambaye amewahi kutajwa na Forbes kama bilionea wa 24 barani Afrika, amefunguka na kueleza sababu za yeye kutonunua ndege binafsi licha ya kuwa bilionea.
“Nimefanya
Interview na Forbes wakaniuliza kwa nini sijanunua ndege binafsi,
wakati bilioni 10 au 20 unapata ndege, mimi nimepiga mahesabu nikikata
tiketi ya daraja la kwanza kwenda Afrika Kusini kwenda na kurudi natumia
milioni 4, ila kwa ndege binafsi ikiruka angani saa moja gharama yake
milioni 8”
millardayo
UTAFITI, UCHU WA NGONO SWEDEN WASHUKA
Utafiti: Uchu wa ngono Sweden washuka
Taifa la Sweden linazindua utafiti wa miaka mitatu kuhusu maisha ya ngono ya raia wake.
Habari zimechapishwa katika jarida moja zikisema kuwa raia wa taifa hilo wanashiriki ngono kwa kiasi kidogo.Waziri wa Afya Gabriel Wilkstrom amesema kuwa iwapo msongo wa mawazo ama maswala mengine ndio tatizo la watu kushiriki ngono kwa kiasi kidogo basi hilo pia ni swala la kisiasa.
Amesema kuwa huku jamii ikihusishwa na ngono katika kila kitu kuanzia matangazo,mitandao ya kijamii na katika maisha ya kila siku,swala hilo linakabiliwa na aibu na kutokuwepo katika mjadala wa kisiasa .
BBC
AUWAWA KWA KUSHINDWA KULIPA DENI
Wauawa kwa kushindwa kulipa deni la biskuti India
Mtu mmoja na mkewe
kutoka jamii ya Daliti inayobaguliwa tangu jadi nchini India wameuawa,
mmoja akiwa amekatwa kichwa na mwengine kunyongwa kwa kushindwa kulipa
deni la Rupee kumi na tano ambalo ni karibu senti ishirini na mbili tu.
Polisi
kaskazini mwa taifa hilo wamethibitisha kisa hicho ambapo yasemekana
mfanyi biashara anayetokea jamii ya hadhi ya juu,aliwaua wanandoa hao
kwa kushindwa kulipa deni la biskuti walizokuwa wamewachukulia watoto
wao.Mfanyi biashara huyo amekamatwa.
Ubaguzi kwa misingi ya kijamii umeenea sana nchini India, huku watu wa jamii ya Daliti waliokuwa wamebadikwa jina la 'the untouchables' wakiwekwa kwenye daraja la chini kabisa kwenye sera hiyo ya kibaguzi nchini India iitwayo 'caste' ambapo wananyimwa fursa nyingi za kimaendeleo na hivyo kubaki katika lindi la umaskini .
Hata hivyo Visa vya ukatili wa kibaguzi dhidi ya jamii ya Dalit katika jimbo la Gujarat vimeongezeka mnamo siku za hivi karibuni na vimesababisha wimbi la maandamano kutoka watu wa jamii hiyo
MSIMU WA MIHOGO NA VIAZI TANGA
Wafanyabiashara wa mihogo na viazi Soko la Mgandini Tanga, wakipanga kusubiri watja sokoni hap kama walivyokutwa na Camera za Tangakumekucha, Msimu huu wa viazi na mihogo umetajwa kuwa wakulima wa mazao hayo wanaendelea kuvuna kwa wingi hii ikiwa ni kutokana namvua kunyesha kwa wingi sehemu mbalimbali za Mkoa wa Tanga.
Hata hivyo wafanyabiashara na wakulima hao wamelalamikia uhaba wa soko hivyo viazi na mihogo yao kuuza kwa bei ya hasara ili kuepuka kuwaozea mikononi.
Wafanyabashara hao na wakulima wameiambia Tangakumekucha kuwa kama Serikali itajenga kiwanda cha kusindika matunda na mihogo kilimo chao kinaweza kuwa na tija na kuwa mfano kwa wengine ambao mashamba yao wameyatekeleza kwa kuona kilimo hicho hakina tija.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapa hapa tangakumekuchablog

UFARANSA KUPIGA UFADHILI WA NJE WA MISIKITI
Ufaransa kupinga ufadhili wa nje wa misikiti
Waziri mkuu wa
Ufaransa Manuel Valls amesema kuwa huenda akapendekeza kupigwa marufuku
kwa muda ufadhili wa misikiti kutoka nje kufuatia mashambulio ya hivi
karibuni yanayotekelezwa na wana jihad.
Akizungumza na gazeti la
Le Monde ,bwana Valls pia amewataka maimamu wote wa Ufaransa kupewa
mafunzo ndani ya Ufaransa na wala sio nje ya taifa hilo.Amesema ni wakati ambapo Ufaransa inafaa kujenga uhusiano mpya na Islam,akitaja vita dhidi ya itikadi kali kama jukumu la kizazi hiki.
WANYONGWA KWA KUKUTWA NA HATIA (MADAWA YA KULEVYA)
Wanyongwa Indonesia kwa dawa za kulevya
Maafisa nchini
Indonesia wamesema hukumu ya kuwanyonga watu wanne kwa kukutwa na hatia
ya makosa ya dawa za kulevya imetekelezwa.
Mwanasheria mkuu wa
serikali nchini humo Noor Rachmad amesema raia watatu wa Nigeria na
Muindonesia mmoja wameuawa kwa kupigwa risasi katika gereza la kisiwa
cha Nusa Kambangan.Mapema wiki hii mwanasheria mkuu wa serikali nchini humo amesema watu 14, wengi wao wakiwa ni wageni watanyongwa.
Serikali mbalimbali za kigeni, Makundi ya haki za binadamu na ndugu za watu hao walizitaka Mamlaka nchini Indonesia kuacha kuwaua watu hao.
Thursday, July 28, 2016
FAIDA 13 ZIPATIAKANAZO KWENYE CHUNGWA
Faida 13 zipatikanazo kwa kula chungwa kiafya
Ni msimu mwingine wa machungwa, yamejaa tele kila kona. Shilingi 100 tu
unapata chungwa. Lakini siyo ajabu kama kuna watu msimu unaisha hawajala
hata chungwa moja, wala suala la matunda halipo kabisa katika orodha ya
milo yao!
Inawezekana pia hata kwa wale wanaokula, japo kidogo, hula kama kiburudisho tu bila kujua faida zake mwilini. Katika makala ya leo nitakujuza faida 13 unazoweza kuzipata unapokula chungwa, ambalo limesheheni virutubisho kibao.
Kumbuka kuwa hata chungwa moja tu ukila lina kidhi yale mahitaji muhimu ya mwili ya kila siku (daily requirement), iwe chungwa lenyewe au juisi yake halisi.
1. UKOSEFU WA CHOO
Kutokana kuwa na kiwango kikubwa cha kirutubisho aina ya kambalishe (fibre), chungwa husaidia usagaji wa chakula tumbuni na hutoa ahueni kwa mtu mwenye matatizo ya ukosefu wa choo. Aidha, kambalishe huondoa kolestro na huimarisha kiwango cha sukari mwilini, hivyo chungwa ni zuri kwa wagonjwa wa kisukari.
2.UGONJWA WA MOYO
Kiwango kikubwa cha Vitamin C na virutubisho vya ‘flavonoids’, ‘phytonutrients’ vilivyomo kwenye chungwa, huondoa kwa mlaji hatari ya kupatwa na magonjwa ya moyo (Cardiovascular disease)!
3. SHINIKIZO LA DAMU
Virutubisho vya Magnesi (Magnesium) na ‘hesperidin’ vilivyomo kwenye chungwa, husaidia kuondoa tatizo la shinikizo la damu la juu (high blood pressure), hivyo machungwa ni mazuri kwa wagonjwa wa presha.
4. UGONJWA WA MAPAFU
Chungwa pia lina kiasi kikubwa cha Vitamin B6 na Madini ya Chuma (iron), virubisho ambavyo ni muhimu kwa uzalishaji wa seli nyekundu za damu, ambazo hufanya kazi ya kusafirisha hewa ya oksjeni mwilini, hivyo kuwa muhimu kwa kujikinga na ugonjwa wa mapafu.
5. MIFUPA NA MENO
Chungwa lina kiasi kingi cha madini ya kalisi (calcium) ambayo ni muhimu kwa uimarishaji wa mifupa na meno.
6. AFYA YA NGOZI
‘Anti oxidants’ iliyomo kwenye chungwa, hutoa kinga kwenye ngozi ili isiharibike au kushambuliwa na magonjwa ya ngozi yanayoweza kujitokeza kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa. Pia huifanya ngozi ‘isizeeke’.
7. KOLESTRO
Virutubisho vilivyomo kwenye chungwa, hasa kwenye maganda yake, hupunguza kiwango cha mafuta mabaya mwilini (bad cholesterol). Hivyo kwa wenye tatizo la lehemu wanashauriwa kula machungwa pamoja na nyama zake.
8. UKUAJI WA UBONGO
Chungwa moja lina kiasi cha asilimia 10 ya ‘folic acid’ inayohitajika mwilini kila siku. Madini haya ni muhimu kwa afya ya ngozi na ukuaji wa ubongo kwa ajili ya kuimarisha kumbukumbu na uwezo wa mtu wa kufikiri.
9. KINGA YA MWILI
Vitamin C iliyomo kwenye chungwa huimarisha uzalishaji wa seli nyeupe ambazo ni muhimu kwa uimarishaji wa kinga ya mwili. Unapokuwa na kinga imara, huwezi kusumbuliwa na magonjwa mara kwa mara, yakiwemo malaria.
10. UGONJWA WA FIGO
Ulaji wa machungwa mara kwa mara, ukusaidia kujiepusha na ugonjwa wa figo kwa kiasi kikubwa.
11. VIDONDA VYA TUMBO
Unapokuwa na kiwango cha kutosha cha Vitamin C mwilini, una uhakika na kinga dhidi ya ugonjwa wa vidonda vya tumbo, na kama tayari unavyo, ulaji wa machungwa utakupa ahueni.
12. UGONJWA WA MAFUA
Kutokana na wingi wa virutubisho vya kinga vilivyomo kwenye chungwa, ulaji wake mara kwa mara utakuepusha na magonjwa ya kuambukiza na vairasi (virus), kama vile mafua ambayo hivi sasa yanawasumbua watu wengi. Hivyo kula machungwa mengi kadii uwezavyo ili ujiepushe na mafua.
13. KINGA YA MAGONJWA MENGI
Chungwa, siyo tu linatoa kinga kwa magonjwa yaliyoainishwa hapo juu, bali pia hutoa kinga hata kwa magonjwa mengine kama vile baridi yabisi (arthritis, rheumatism), pumu, kikohozi, kifua kikuu, nimonia na kisukari. Nakushauri kula machungwa au juisi yake halisi kuanzia leo ili kupata faida hizo.

SOURCE MG
AMKA NA MAGAZETI NA NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA, 0717 713866
PAPA FRANCISS AANGUKA AKIONGOZA IBADA
Papa Francis Aanguka Akiongoza Ibada Poland
Papa Francis ameanguka wakati akiongoza ibada leo huko nchini Poland mbele ya waumini na wanahabari.
Papa Francis mwenye umri wa miaka 79 ameanguka altareni na kusaidiwa na wasaidizi wake ila hakuumia na kuendelea na ibada hiyo hadi mwisho.
Papa yupo ziarani nchini humo na alikuwa na ibada hiyo kusini mwa mji wa Czestochowa.
SOURCE MG
Subscribe to:
Posts (Atom)