Tuesday, January 31, 2017

EMMANUEL EDABAYOUR AIBUKIA UTURUKI

 Emmanuel Adebayor aibukia Uturuki kwa miezi 18

Nahodha wa timu ya taifa ya Togo Emmanuel Adebayor ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga na timu kadhaa, leo January 31 tukiwa tunaelekea kufunga dirisha la usajili, ametangazwa kusajiliwa na timu ya Istanbul Basaksehir na atakuwa akivaa jezi namba 26.
Adebayor amejiunga na timu ya  Istanbul Basaksehir ya Ligi Kuu Uturuki kwa mkataba wa miezi 18, Adebayor ambaye alikuwa hana klabu toka aachane na Crystal Palace mwishoni mwa mwaka jana, alikuwa Uturuki kwa ajili ya kufanya mazunguzo na Besiktas  lakini walishindwana mshahara na vinara hao wa Ligi.

Emmanuel Adebayor alikuwa anataka Besiktas  wamlipe mshahara wa pound milioni 3 wakati wao walikuwa wanataka wamlipe pound milioni 2, hivyo akaamua kuachana nao na kujiunga na Istanbul Basaksehir waliyopo nafasi ya pili katika msimamo wa Ligi Kuu Uturuki inayoshirikisha timu 18.

WASAFIRI WA PEMBA HADI TANGA KUMEKUCHA



Tanga, KILIO cha muda mrefu cha wakazi wa Pemba na Tanga cha usafiri wa majini kimepata muarobani baada ya kampuni ya usafirishaji abiria na mizigo ya Azam Sealink 2, kuanzisha safari yake kwa mara ya kwanza juzi.
Usafiri huo utakuwa chachu kwa abiria na wafanyabiashara wa Tanga na Zanzibar ambao awali walikuwa wakitumia usafiri ambao sio salama na baadhi ya nyakati kutokea maafa na mizigo  kuzama baharini .
Akizungumza na waandishi wa habari, meneja wa meli hiyo ya  Azam Marinelink2, Hussein Said, amesema kilio cha Wanzanzibar hususani wakazi wa Pemba na Tanga wakiwemo wafanyabiashara kilikuwa kinawasononesha.
Alisema meli iko na uwezo wa kuchukua watu zaidi ya 2,000 waliokaa katika viti na shehena ya  mizigo pamoja na ubebaji wa magari.
“Kwa muda mrefu kilio cha wafanyabiashara na wasafiri kwa upande wa Tanga na Pemba tulikuwa tunajua ila muda muafaka ulikuwa bado, leo hii niseme kuwa muarobaini wake umepatikana” alisema Said na kuongeza
“Ujio huu wa meli utafufua uchumu na  biashara kwa pande zote mbili na Serikali kuongeza mapato yake hasa kuelekea ujengaji wa bomba la mafuta ambapo kuna fursa nyingi” alisema
Kwa upande wake mmoja wa wasafiri hao kutoka Pemba aliewasili kwa mara ya kwanza kwa kutumia meli hiyo, Ali Makame, amesema meli hiyo itakuwa mkombozi wa watu wa Pemba waishio Tanga na wafanyabiashara wa Tanga Pemba.
Alisema awali walikuwa wakitumia usafiri wa mashua ambao sio rasmi na baadhi ya nyakai kulazimika kupitia Unguja hadi Dar es Salaam ambako hutumia gharama kubwa.
“Ujio wa usafiri huu niseme kuwa ni mapinduzi makubwa kwa wasafiri wa majini kati ya Tanga na Pembao ambao tulikuwa tunahatarisha uhai wetu mikononi” alisema Makame
Aliyataka makampuni mengine kujitokeza hasa kipindi hiki cha ujio wa bomba la mafuta ambapo wafanyabiashara na wawekezaji wataweza kufika na kuangalia fursa za uwekezaji Tanga.
                                        















 Abiria kutoka kisiwani Pemba wakishuka kwenye meli ya Azama Sealink2 iliyotia nanga kwa mara ya kwanza katika bandari ya Tanga juzi.


 Moja ya vyumba vya VIP na viti vyake katika muonekano wake.

 Life Jarket zikiwa zimehifadhiwa  katika moja ya vyumba katika meli hiyo

Monday, January 30, 2017

MNIGERIA ALIEDAIW AKUWA NA WAKE 86 AFARIKI DUNIA

Mohammed Bello Abubakar huenda alikuwa na zaidi ya wake 1Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye anadaiwa  alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93.
Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo inadaiwa ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake.
BBC

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY BUS TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990



SOKO LA BAMIA TANGA LADODA

Mkulima wa bamia shamba la Ngomeni kata ya Chumbageni Tanga, Suleiman Lugendo, akivuna kupeleka masokoni. Mkulima huyo amelalamika kukosa soko la uhakika na badala yake wamekuwa wakipeleka masokoni na kutegemea wateja wa  rejareja na baadhi ya nyakati kuuza kwa hasara kuepika kuwaharibikia mikononi.








Mkuliama wa bamia shamba la Ngomeni kata ya Chumbageni Tanga, Saleh Omary Ngole, akionyesha bamia ya mbegu kutoka Holland, mkulima huyo amekuwa akipeleka bamia zake katika masoko na kuuza rejareja baada ya kukosa soko la uhakika na baadhi ya nyakati kuuza kwa hasara kuepuka kuwaozea mikononi. Kisado kimoja kwa jumla alikuwa akiuza,2,000.