
Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu
nchini Nigeria ambaye anadaiwa alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia
akiwa na umri wa miaka 93.
Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa
Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili.
Gazeti
la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka
2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo inadaiwa ilipanda hadi
wake 130 wakati wa kifo chake.
BBC
No comments:
Post a Comment