Wednesday, March 29, 2017

KARAFUU TIBA YA MAGONJWA KWA BINADAMU

Karafuu ni zao linalotokana na  mkarafuu, ingawa karafuu hazimo katika kundi la vyakula wala vinywaji lakini ni kiungo na dawa  muhimu sana kwa maisha ya binadamu.                                                                                     
Mikarafuu ilianza kupandwa kwenye visiwa vya Shelisheli, Mauritius na sehemu nyinginezo katika karne ya 19. Miche ya mikarafuu ililetwa Zanzibar kutoka Indonesia, mashariki ya mbali mwaka 1818.

Mikarafuu inastawi zaidi Visiwani vya Unguja na Pemba ambapo katika miaka 30 iliyopiata Zanzibar ilikuwa inazalisha asilimia 80 ya karafuu zote zinazohitajika duniani ambapo uchumi wake ulitegemea sana zao la karafuu.

Karafuu zina matumizi mengi, ambapo hutumika kama kiungo katika vyakula na vinywaji, dawa kwa maradhi ya tumbo, meno na misuli vile vile hutumika katika kuleta harufu nzuri ya kinywa, mwili na mazingira ya nyumbani.

Pia karafuu zinatumika katika uzalishaji wa bizaa nyengine ikiwemo sigara, mafuta ya karafuu ambayo hutumika kwa kuchulia misuli inayouma, kutengezea dawa za meno na perfume kwa ajili ya manukato.
MGBLOG

WENGERE NI MUHIMU KWETU, IWOBI

Iwobi amesema kila mtu anayejua historia ya Wenger hapaswi kumpingaMshambuliaji wa Arsenal Alex Iwobi anataka meneja wa klabu hiyo Arsene Wenger kusalia Emirates na kusema kuwa kukosolewa kwake sio sahihi.
Wenger mwenye umri wa miaka 67 amekuwa akikosolewa na mashabiki wa timu hiyo baada ya timu yake kushuka mpaka nafasi ya sita katika msimamo wa ligi ya EPL kufuatia kufungwa katika michezo mitano iliyopita.
Magoli 10-2 ikiwa ni uwiano waliofungwa na Bayern Munich katika michuano ya Ulaya imeongeza msukumo kwa meneja huyo, huku akisema kuwa atafanya maamuzi sahihi katika siku za usoni.
BBC

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990



Tuesday, March 28, 2017

SARAFU YENYE PICHA YA MALKIA ELIZABETH WA UINGEREZA YAIBWA MAKUMBUSHO YA UJERUMANI

Vienna, AustriaSarafu kubwa iliyotengenezwa kwa dhahabu, ambayo ina picha ya Malkia Elizabeth wa Uingereza, ambayo inakadiriwa kuwa na thamani ya $4m (£3.2m), imeibiwa kutoka kwenye makumbusho Ujerumani.
Sarafu hiyo kutoka Canada imeandikwa kuwa ya thamani ya $1m, lakini kwa sababu imetengenezwa kwa kilo 100 za dhahabu, thamani yake ni ya juu sana kwa kutumia bei ya sasa ya dhahabu.
Iliibiwa usiku kutoka makavazi ya Bode mjini Berlin.
Haijabainika ni vipi wezi walifanikiwa kuingia bila kugunduliwa na mtambo wa kuzuia wezi, na kisha wakafanikiwa kutoroka na sarafu hiyo ambayo nusu kipenyo chake ni cha nusu mita.
BBC

THIERY HENRY ADAIWA KUMRITHI MIKOBA YA WENGER

Thiery Henry kumrithi Wenger

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Thierry Henry (39) huenda akarithi mikoba ya Arsene Wenger anayemaliza mkataba wake mwishoni mwa msimu huu.
Mchezaj huyo aliyeacha jina kwenye klabu yake hiyo ya zamani, hata hivyo amesema hana uhakika iwapo ndiye atakarithi mikoba hiyo ya bosi wake  wa zamani ambaye amekuwa kwenye wakati mgumu kutokana na presha ya kutakiwa kuondoka klabuni hapo.
Mkabata wa Wenger unaelekea ukingoni mwishoni mwa masimu huu na mpaka sasa hajui hatima yake klabuni hapo kutokana na kuwapo mvutano iwapo abaki au aendelee kukinoa kikosi hicho.
Msukumo mkuwa wa kutakiwa kuondoka ulishinikizwa na mashabiki wa timu hiyo baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya Ligi ya Europa, huku wakimpa presha kuhakikisha kikosi hicho kinakuwa katika nafasi za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England.

Monday, March 27, 2017

NAY WA MITEGO ACHIWA HURU

Wa Mitego baada ya kuachiliwa huruMwanamuziki Emmanuel Elibariki maarufu kama Nay wa Mitego, ambaye alikuwa amekamatwa na kuzuiliwa na maafisa wa polisi Tanzania kuhusiana na wimbo wake, ameachiliwa huru.
Wa Mitego ameachiliwa huru saa chache baada ya Waziri wa Habari nchini Tanzania Dkt Harrison Mwakyembe kuagiza aachiliwe huru.
"Saa hizi sina kubwa la kuongea. Wimbo umeruhusiwa. Nashukuru. Nafurahi kusikia taarifa ya serikali kwamba wameruhuru wa Wapo upigwe. Upigwe kwa nguvu," amesema Wa Mitego baada ya kuachiliwa huru.
Kuhusu kuuboresha wimbo huo, amesema: "Hili nitalifanyia kazi. Siwezi kusema saa hizi ni vitu gani kwa sababu ndio nimetoka huko. Lakini nitalifanyia kazi kwa sababu tayari ni wimbo wa kila mtu, wimbo wa Watanzania, wimbo wa watu wote."
Dkt Mwakyembe hata hivyo alimtaka Nay wa Mitego auboreshe zaidi wimbo wake, kwa mujibu wa ujumbe uliopakiwa katika ukurasa Rasmi wa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania kwenye Twitter.
Sehemu ya maudhui ya wimbo huo inagusia tuhuma za kughushi vyeti ambazo zimekuwa zikigonga vichwa vya habari nchini Tanzania
Wimbo huo mpya wa Ney wa Mitego, ulianza kusambaa katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Ulrich Matei alikuwa amesema mwanamuziki huyo alikamatwa kwa kosa la kutoa wimbo wenye maneno ya kashfa dhidi ya serikali.
BBC

ARSENAL YATOLEWA KOMBE LA FA

Marisa Ewers alijiunga na Birmingham City kutoka Bayer Leverkusen Aprili 2016Mabingwa watetezi wa Kombe la FA la Wanawake nchini Uingereza, Kinadada wa Arsenal, wametupwa nje ya michuano ya mwaka huu.
Hii ni baada ya kuchapwa 1-0 na kinadada wa Birmingham City katika hatua ya robo fainali.
Bao la Birmingham lilifungwa na Marisa Ewers dakika ya 77.
BBC

BIASHARA KUELEKEA TANGA MJINI



 Wafanyabiashara wa mkaa kutoka Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga wakielekea Tanga mjini kusaka wateja wa biashara yao, Gunia moja la mkaa lilikuwa likiuzwa 20,000 hadi 25,000.




Mfanyabiashara wa matenga kutoka Maramba Wilayani Mkinga Mkoani Tanga akielekea Tanga mjini kutafuta wateja, Tenga moja alikuwa akiuza 7,000.

MBOWE ATINGA TANGA



Mwenyekiti wa Taifa wa Chadema, Freeman Mbowe, akizungumza na viongozi wa kata, Wilaya na Mkoa wa Tanga wakati wa kikao cha ndani cha Chama hicho kilichofanyika ukumbi wa YDPC Tanga jana.
.




Wanachama na viongozi wa kata na Wilaya wa Chadema Wilaya ya Tanga wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, Freeman Mbowe kwenye kikao cha ndani cha chama hicho kilichofanyika ukumbi wa YDPC jana.

KOCHA WA UHOLANZI ATIMULIWA

Danny Blind ni baba wa mlinzi wa Man United Daley BlindUholanzi imemtimua kocha wa timu yake ya taifa Danny Blind baada ya kudumu kwa takriban miaka miwili.
Hii inafuatia kichapo cha magoli 2-0 dhidi ya Bulgaria siku ya Jumamosi na kuwaacha Uholanzi katika nafasi ya nne kwenye mbio za kufuzu kushiriki kombe la dunia.
Blind mwenye miaka 55 alichukua nafasi hiyo kutoka kwa Guus Hiddink mwaka 2015 huku ikishuhudiwa kikosi chake kikishindwa kufuzu fainali za michuano ya Ulaya mwaka jana.
Chama cha soka nchini Uholanzi kimesema kuwa ameicha timu hiyo katika wakati mgumu kufuzu kucheza kombe la dunia nchini Urusi.
Fred Grim ameteuliwa kuwa kocha wa mpito na atakiongoza kikosi hicho siku ya Jumanne dhidi ya Ufaransa.

WASICHANA WALIOKUWA WAMEVALIA SURUALI YA KUBANA WAZUIWA KUPANDA NDEGE

Ndege za United AirlinesShirika la ndege la United Airlines nchini Marekani limeshutumiwa sana baada ya kudaiwa kuwazuiwa wasichana wawili waliokuwa wamevalia suruali ndefu za kubana kuabiri ndege hiyo.
Kisa hicho kilitokea kwenye safari ya ndege iliyokuwa ikitokea Denver kuelekea Minneapolis Jumapili asubuhi, mwanaharakati Shannon Watts amesema.
Shirika la United limesema wasichana hao walikuwa wanasafiria hati maalum, ambayo hutumiwa na wafanyakazi wa shirika la ndege na wageni wao.
United wamesema huwa kuna kanuni za mavazi kwa wanaotumia hati hiyo kusafiria.
Shirika hilo limefafanua kwamba abiria wa kawaida, ambao wanalipia tiketi zao, wako huru kuvalia mavazi yao ya kubana.
BBC

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH, TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990