Manchester United wamepokea kichapo Anfield dhidi ya Liverpool
Usiku wa March 10 michuano ya
Europa League iliendelea kwa michezo kadhaa kupigwa Barani Ulaya, Uingereza kulikuwa kuna mchezo wa kuvutia zaidi baina ya
Liverpool dhidi ya
Manchester United katika dimba la
Anfield.

Roberto Firmino akishangilia goli
Takwimu za vilabu hivi kabla ya mchezo huu kupigwa ,
Man United alikuwa na takwimu nzuri licha ya kupokea kipigo cha goli 2-0 kwa mujibu wa mechiza mwisho za
Manchester United na
Livepool walivyokutana,
Man United alikuwa kashinda mara nne na
Liverpool mara moja
Hata hivyo takwimu hizo hazikuwa na msaada wowote kwa
Man United kwani vijana wa
Jurgen Klopp walifanikiwa kuifunga
Man United kuanzia dakika ya 20 kupitia kwa
Danny Sturridge kwa mkwaju wa penati, kabla ya dakika ya 73′
Roberto Firmino kupachika goli la pili lililoimaliza
Man United na kufanya mchezo umalizike kwa
Liverpool kuibuka na ushindi wa goli 2-0.
No comments:
Post a Comment