Tuesday, November 8, 2016

KUMEKUCHA UCHAGUZI MAREKANI

Marekani yaamua: Kuhusu Trump, Clinton na Bangi

Marijuana leaf on American flag
Kando na kumpa rais mpya, wamarekani wanakaribia kuamua ikiwa watapanua eneo kubwa zaidi ambako bangi inakubalika kisheria.
Katika majimbo tisa , katika siku ambayo uchaguzi unafanyika, wapiga kura watapata fursa pia kuwa na kauli yao kuhusu kuidhinishwa kisheria kwa matumizi ya bangi.
Ikiwa watapiga kura ya ndio karibu robo ya wamarekani watakuwa na kibali cha sheria cha kuvuta mmea huo kwa kujifurahisha ama sababu za matibabu watakapotimiza umri unaokubalika kisheria.
Katika kipindi cha miaka 20 suala hili lilikuwa ni mwiko nchini Marekani.
Jimbo la California lenye wakazi karibu milioni 39 itashuhudia mabadiliko hayo Jumanne.
Masanduku ya kupigia kura katikja majimbo matano - Nevada, Arizona, Massachusetts na Maine, pamoja na California - yatajumuisha chaguo la kuwaruhusu watu wenye umri wa miaka 21 kutumia dawa hiyo ya kulevya kujifurahisha.
Wapiga kura katika majimbo mengine manne - Florida, Montana, North Dakota na Arkansas - watapiga kura kuruhusu wagonjwa kupata bangi kwa sababu za kimatibabu ama kupanua zaidi kanuni za sheria ya sasa juu ya kuhalalisha kisheria mmea huo kwa sababu za tiba.
Nchini Marekani majimbo 25 tayari yameidhinisha kisheria matumizi ya marijuana kwa sababu za kimatibabu , huku mengine manne yakiidhinisha muhadarati huo kwa matumizi ya kujifurahisha : Washington, Oregon, Colorado and Alaska, pamoja na mji mkuu wa Marekani Washington DC.
Mabadiliko ya sheria yanaonekana kufanikiwa, kwa mujibu wa kura za maoni, na yatawabadilisha wakazi wa maeneo ya mwambao wa magharibi mwa Marekani, kuanzia New Mexico hadi jimbo la Washington na Alaska, kuwa waraibu wa uvutaji wa bangi.
Walau bangi inaweza kuwasaidia kupunguza maumivu yao, ikiwa hawatapata rais wampendao.

No comments:

Post a Comment