
China imepiga hatua nyingine katika
mpango wake wa anga za juu, baada ya kuanza kufanyia majaribio mpango wa
kupeleka binadamu wakaishi kwa muda mrefu kwenye Mwezi.
Wanafunzi wa sayansi wamehamia katika chumba maalum chenye mazingira yanayofanana na ya Mwezi ambapo watakaa kwa siku 200.
Lengo
ni kuwaanda kwa safari ya kuishi kwa muda mrefu kwenye kituo cha anga
za juu kwenye Mwezi, bila kupokea usaidizi wowote kutoka ardhini.
China imewekeza pesa nyingi sana katika mpango wake wa anga za juu, ikilenga kushindana na Marekani an urusi.
No comments:
Post a Comment