Saturday, July 2, 2016

WAKUU WAPYA WA WILAYA TANGA WAAPISHWA LEO



 Mkuu wa Mkoa wa  wa Tanga, Martin Shigella(kushoto) akimuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Muheza, Mwanasha Rajab wakati wa hafla fupi ya kuwaapicha Wakuu wapya wa Wilaya wa Mkoa wa Tanga Leo




  Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella akimuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wa Wilaya Mkoa wa Tanga leo.

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigella, akimuapisha mkuu mpya wa Wilaya ya Korogwe,Robarts Gabiel, wakati wa hafla fupi ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya leo . Hafla iliyofanyika ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

KIZAAA ZAAA, ABIRIA WAGOMA KUFAULISHWA NGAMIANI TANGA



Abiria  kutoka Mikanjuni kuelekea Raskazone Tanga wakizingira  daladala kupinga gari hiyo kukatisha safari kituo cha Ngamiani na kutaka kupelekwa hadi mwisho wa kituo.
Inadaiwa kuwa madereva wengi wamekuwa na ada ya kukatisha Rout na kuwa kero kwa abiria hivyo kuzusha mitafaruku ya abiria na wenye gari.
Hii imekuwa mwiba na Polisi wa Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Sumatra wamekuwa wakilivalia njuga kwa kuwatoza Faini jambo ambalo linaonekana kana kwamba adhabu hiyo iliyowekwa kisheria ni ndogo.







MAHAKAMA YA MAFISADI NA UHUJUMU UCHUMI KUANZA KARIBUNI




WAKATI Mahakama Maalumu ya Ufisadi na Uhujumu Uchumi ikitarajiwa kuanza wakati wowote, majengo ya mahakama hiyo yanatarajiwa kukabidhiwa kesho kutwa jumatatu.


Jaji Mkuu, Mohamed Othman Chande, alisema jana kuwa mkandarasi aliyekabidhiwa kazi ya kukarabati majengo hayo yaliyopo katika Shule Kuu ya Sheria, pembeni mwa kituo cha mabasi cha Simu 2000, Ubungo Dar es Salaam, yako katika hatua za mwisho za ukarabati.


Akizungumza katika viwanja vya Karimjee baada ya kuapisha mawakili wapya 623 wa Mahakama Kuu, Jaji Chande alisema tayari Bunge limeshapitisha muswada wa sheria ya uanzishwaji wa mahakama hiyo.


Alisema kwa sasa muswada huo utawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa ajili ya kuusaini ili uwe sheria, kisha sheria hiyo itatangazwa katika gazeti la Serikali ili kuruhusu shughuli za mahakama hiyo kuanza.


Kwa mujibu wa Jaji Mkuu, Mahakama iko tayari kuendesha Divisheni hiyo ya Mahakama na baada ya kukabidhiwa majengo hayo, wataanza kutoa semina kwa majaji na watumishi wengine wa mahakama hiyo, kuhusu divisheni hiyo itakavyoendesha shughuli zake.


Aliweka wazi kuwa mpaka sasa hakuna kesi hata moja iliyokwishatambuliwa kwamba itashughulikiwa na mahakama hiyo.
 

Friday, July 1, 2016

HADITHI , MWANAMKE SEHEMU YA 32

SIMULIZI ZA FAKI A FAKI

MWANAMKE  32

ILIPOISHIA

Mgosingwa alitia mkono kwenye mfuko wa shati lake akatoa ganda kama la kitambulisho akaniwekea mezani.

“hii si leseni yako Mgosingwa?’ akaniuliza.

Nikalichukua lile ganda na kulifungua. Naam. Ilikuwa ni leseni yangu niliyokuwa nimeitupa kule makaburini. Pale pale uso wangu ulibadilika rangi kwa hofu iliyochanganyika na fadhaa. Nikamtazama mgosingwa huku nikijiuliza ameipata wapi leseni yangu.

“Huku nikiendelea na tabasamu langu la kulazimisha nilimuuliza.

“Mgosingwa umeipata wapi hii leseni yangu?’

“Si nimekwambia unatakiwa polisi?”

Jibu lake hilo lilizidi kunichanganya na kunifadhaisha. Midomo yangu niliyokuwa ninailazimisha kutabasamu huku nikiwa na fadhaa ilianza kutatizika na kutetemeka. Sasa haikuweza tena kutabasamu.

“Mgosingwa unanichanganya. Sasa nani kakupa hii leseni na kakupa kwa madhumuni gani?” nikamuuliza huku nikiizuia modomo yangu isitetemeke wakati nikimuuliza hivyo.

Mgosingwa aligundua kuwa nilikuwa nimetaharuki. Akacheka. Hata hivyo kwa vile uso wake ulikuwa umekunjana kutokana na kuendeleza kilevi, kicheko chake hakikuufanya uso wake upendeze, bali ulionekana kama anataka kulia.

“Mgosingwa hukumbuki uliiacha wapi leseni yako?” akaniuliza.

Nikatikisa kichwa.

“Sikumbuki” Nilimjibu hivyo ili nijue ataniambia nini.

“Mgosingwa jana usiku si ulikuja kule makaburi ukafukua lile kaburi nikakukurupusha”

SASA ENDELEA

Aliponiambia hivyo nikanywea na kumtazama. Alipoona nipo kimya aliendelea kunieleza.

“Wakati unakimbia mgosingwa uliiangusha hii leseni yako”

“Kumbe wewe ndiye unayelinda pale?” nikamuuliza.

“Nilipoacha kazi STC niliajiriwa na kanisa kulinda yale makaburi. Sasa jana usiku niliondoka kidogo kwenda kupata ulabu (kilevi), niliporudi nikakuta mtu amechimba kaburi na kuingia ndani. Hii leseni niliiokota asubuhi ndio nikagundua kuwa ulikuwa wewe”

“Sasa Mgosingwa umeshakwenda kutoa ripoti polisi?”

Polisi nimeshakwenda lakini nilipoona hii leseni yako sikuwapa. Niliwambia huyo mtu sikumuona vizuri”

Hapo hapo nilitia mkono mfukoni nakutoa pochi yangu. Niliifungua na kuchomoa noti za shilingi elfu ishirini, nikampa.

“Asante sana Mgosingwa, umenisaidia sana”

SASA ENDELEA

“Tunajuana Mgosingwa , hatuwezi kusalitiana” Mgosingwa aliniambia wakati akipokea zile pesa.

“Unajua lile kaburi ni la shemeji yake mhasibu wetu. Mimi sikujua kabisa”

“Kwani ulikuwa unataka nini Mgosingwa?”

“Kuna kitu nilikuwa nataka”

“Kitu gani?”

Kwanza nilisita kumwambia nilikuwa nataka nini lakini nikaona ni vizuri nimwambie.

“Nilikuwa nataka kucha za maiti”

“Mgosingwa unataka kwenda kuroga au kuua mtu?”

“Hapana. Ni kwa mambo yangu binafsi”

“Mgosingwa ungeniambia, ningekupatia. Mimi Ndio nalinda yale makaburi”

“Bado ninazihitaji Mgosingwa, nifanyie huo mpango”

“Utanipa shilingi ngapi?”

“Ukiniletea hizo kucha nitakuongezea kumi nyingine”

“Fanya ishirini Mgosingwa, kumi ndogo sana”

“Si kitu, nitakupa hizo ishirini”

“Sasa Mgosingwa nitafutie shepe na kiwembe. Niletee pale saa nne usiku. Mimi nitafukua kaburi, asubuhi nitakuletea hizo kucha nyumbani kwako”

“Hakuna tatizo. Nitakuletea hilo shepe. Kiwembe utanunua mwenyewe”

“Sasa Mgosingwa fanya kitu kimoja, nipatie kianzio cha shilingi elfu kumi, hiyo kumi nyingine utanipa asubuhi”

Nilitaka kucheka lakini nilisita kwa sababu tulikuwa katika suala nyeti sana kwa upande wangu.

“Kwanini usisubiri hadi hiyo asubuhi nikupe zote?” nikamuuliza.

“Ninahitaji hiyo pesa kwa sasa”

“Mgosingwa si nimekupa elfu ishirini za bure?”

“Mgosingwa si za bure, polisi ungetoa ngapi ili wakuachie”

“Sawa. Sasa si hizo nimekupa”

“Hazitoshi Mgosingwa”

“Wewe unataka kwenda kulewa tu” nikamwambia huku nikitia mkono kwenye mfuko wa suruali yangu.

Nilitoa pochi yangu nikaifungua na kumpa shilingi elfu kumi alizotaka.

“Umeridhika?” nikamuuliza.

“Hapa Mgosingwa umeniokoa sana”

“Utapata chupa ngapi”

“Acha mzaha Mgosingwa. Mimi siendi kulewa. Mke wangu amekwenda kwao kujifungua. Nilitaka kumtumia hzi pesa”

“Sawa Mgosingwa mtumie, nilikutania tu”

“Sasa Mgosingwa niletee shepe saa nne usiku pale pale”

“Sawa, nitakuletea”

Nikaagana na Mgosingwa na kuondoka.

Nilipotoka kazini jioni nilikwenda kununua shepe jingine nikaenda nalo nyumbani. Nikawa nasubiri saa nne usiku ifike nimpelekee Mgosingwa.

Kwa mara ya kwanza niligundua hata mlevi anaweza kuwa na manufaa yake. Sikutarajia kuwa Mgosingwa mlevu wa gongo na pombe ya mnazi angeweza kunisaidia. Licha ya msaada wa kucha za maiti alioniahidi, kile kitendo chake cha kuiokota leseni yangu na kuja kunipa mwenyewe bila kuipeleka polisi ulikuwa msaada mkubwa kwangu.

Nilimshukuru sana nikijua kama si yeye ningeumbuka. Pengine muda ule ningekuwa niko mahabusi.

Ilipofika saa nne usiku nililifunga lile shepe sehemu ya nyuma ya siti ya pikipiki yangu nikatoka.

Nilikwenda katika lile eneo la makaburi analolinda Mgosingwa. Niliposimamisha tu pikipiki, Mgosingwa akajitokeza. Alitazama kila upande, alipoona kuko kimya akasogea kwenye pikipiki yangu na kunisaidia kulifungua lile shepe.

Ile hewa yake ya mwilini tu ingetosha kumlewesha mtu. Alikuwa akinuka pombe aina ya gongo kama vile alikuwa mtambo wa kuitengenezea. Muda ule tayari alikuwa ameshalewa.

Sikumlaumu. Kulinda makaburi wakati wa usiku ilikuwa kazi ya kutisha. Alihitaji kupata kitu cha kutuliza akili yake, vinginevyo anaweza kuota ndoto za maiti waliozikwa usiku kucha.

Hatukuungumza chochote. Alipochukua lile shepe, alinionesha ishara kuwa tukutane asubuhi akatokomea makaburini.

Nikapanda pikipiki yangu na kuondoka. Nilipofika nyumbani nilifikia kuoga na kulala.

Kulikuwa kunaanza kupambazuka nilipoamshwa usingizini kwa kishindo cha mlango wa mbele uliokuwa unabishwa. Nikatazama saa yangu na kuona ilikuwa saa kumi na mbili kasorobo. Nikajiuliza ni nani abishae mlango? Sikupata jibu.

Nikashuka kitandani na kuvaa suruali yangu kisha nikafungua mlango wa chumbani mwangu na kutoka ukumbini. Nilikwenda kwenye mlango wa mbele na kuuliza.

“Nani abishaye?”

“Ni mimi Mgosingwa!” nikaisikia sauti ya Mgosingwa ikisikika kwa nje.

“Ahaa ni wewe!” nikasema huku nikifungua mlango.

JE MGOSINGWA AMEPATA HIZO KUCHA? JIBU UTALIPATA KESHO

UCHUNGUZI BWAWA LA NDEGE LILILOKOTWA PEMBA LACHUNGUZWA

PEMBA-ZANZIBARNa Masanja Mabula –Pemba
————————–
MAMLAKA ya Usafiri wa Anga Tanzania  imesema uchunguzi  wa kitaalamu bado unaendelea ili  kubaini iwapo bawa la ndege lililookotwa na wavuvi  katika Kisiwa cha Kojani Pemba ni  mabaki ya ndege  ya Malyasia . 
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Vallery Luanda Chamlungu ameyabainisha hayo wakati wa makabidhiano ya  bawa hilo yaliyofanyika  katika bandari ya Kojani na kushuhudiwa na Viongozi wa mbali mbali wa Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Wete .
Alisema , pamoja na uchunguzi wa kitaalamu unaofanywa na mamlaka hiyo , lakini pia Uongozi unaendelea kuwasiliana na mashirika ya ndege ya  kimataifa ya ili kusaidia kukamilisha machakato wa kutambua asili ya ndege hiyo .
“Uchunguzi bado unaendelea ili kubaini kwamba bawa hilo ni mabaki ya ndege ya Malyasia iliyopotea miaka kadhaa iliyopita , tunafanya mawasiliano na mashirika ya ndege ya kimataifa na hili bawa tunatarajia wenzetu kutoka  Malyasia watakuja  ”alifahamisha Chamlungu .
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo alisema wataendelea kushirikiana na wananchi kufanya utafiti hasa sehemu za baharini sambamba na kuwashukuru wavuvi wa Kojani kwa kuweza kulihifadhi bawa hilo .
Aidha , Mkuu wa Wilaya ya Wete Rashid Hadid Rashid akikabidhi bawa hilo   aliwataka wananchi kuwasiliana na vyombo vya ulinzi wanapookota vitu  baharini , na kuacha kuvihifadhi majumbani kwani baadhi vinaweza kuwa ni hatari kwa maisha yao .
Alisema , Serikali ya Wilaya ilisimamia ili kuona kwamba bawa hilo linahifadhiwa , na linabaki  katika mazingira yaliyo salama ili kupisha uchunguzi wa kitaalam ufanyike .
“Pamoja na juhudi zenu , lakini pia naomba nitoe wito kwa wavuvi kutoa taarifa Serikalini ili kuepisha utokea kwa madhara yasiyotarajiwa  , baada ya kuhifadhi majumbani mwenu ” alisisitiza Mkuu wa Wilaya.
Mmoja wa mashuhuda waliookota bawa hilo Chungua Hamad Chungua aliishauri mamlaka ya Usafiri wa Anga kuwaandalia mazingira mazuri ya kuwapatia mashine ya uvuvi ambayo itawasaidia  katika kazi zao za uvuvi .
Alisema ,  ni vyema Mamlaka hiyo kuwazawadia mashine ya supa kumi au kumi na tano kutokana na usumbufu walioupata wakati wa kulikokota kwani ni zito na bahari ilikuw aimechafuka .
Hata hivyo Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga iimekabidhi shilingi milioni mbili wavuvi waliofanikisha kuliokota na kulihifadhi kama ni zawadi .
Kwa mujibu wa taratibu na sheria , Mamlaka ya Usafiri wa Anga haina ulazima wa kuwalipa wananchi wanaokota vitu aidha baharini au nchi kavu , isipokuwa hulazimika kutoka zawadi ili kuwajenga imani wananchi ya kuvihifadhi vitu wanavyo viokota

AMKA NA MAGAZETI NA NEW AGE EDUCATION CENTRE TANGA, 0717 713866

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kituo Cha Elimu cha New Age Education Centre Tanga, New Age ni mabingwa wa kufaulisha wanafunzi kidato cha Pili hadi cha Sita na wanaojiendeleza kielimu, New Age wapo Tanga mkabala na TANESCO simu 0717 713866
























Kila siku asubuhi na mapema tangakumekuchablog inakupa kurasa mwanzo mwisho ya magazeti ya Tanzania na Uingereza

TAIWAN YARUSHA KOMBORA FYONGO

Taiwan yarusha kombora la kulipua meli kimakosa

Jeshi la wanamaji la Taiwan limezindua kimakosa kombora la kulipua meli kutoka kambi yake ya Kaohsiung, maafisa wanasema.
Boti moja iliokuwa ikipiga doria ilikuwa inafanyiwa zoezi la ukaguzi wakati kombora hilo Hsiung Feng 3 liliporushwa .
Kombora hilo lilianguka katika maji ya kisiwa cha Penghu karibu na China lakini halikusababisha madhara yoyote.
Kisa hicho kinajiri wakati ambapo China inasheherekea maadhimisho ya miaka 95 tangu kuanzishwa kwa chama cha Kikomyunisti.
Alisema kuwa kisa hicho kinachunguzwa na kitaangaziwa vilivyo.
Haijulikani iwapo Bejing ilijulishwa.
Kombora hilo linaweza kurushwa umbali wa kilomita 300.China inaichukulia Taiwan kama mkoa wake uliojitenga.
BBC

MATENGA NACHUUZA



Wafanyabiashara wa Matenga ya kuku  kutoka Gombero Wilayani Mkinga Mkoani Tanga  wakitafuta wateja mitaani  barabara ya Pangani Road jana, Tenga moja waliuza kwa bei ya 25,000 hadi 30,000.
Matenga ni moja ya upakiaji wa mizigo pamoja na uchuuzi wa samaki hasa Tanga ikiwa ni eneo la bahari na utoaji wa samaki wengi jambo ambalo huwavutia wachuuzi wa ndani na nje ya Mkoa huo.





ATELEZA AKIJIPIGA SELF GOROFANI

Mtalii afariki akijipiga picha Peru

Machu
Mtalii kutoka nchini Ujerumani amefariki dunia baada ya kuanguka akijipiga picha nchini Peru.
Oliver Park, 51, alianguka kwenye eneo la mabaki ya kale ya Machu Picchu katika milima ya Andes nchini Peru.
Park alipuuza tahadhari za kiusalama  kutoka kwa walinzi na kwenda eneo lisiloruhusiwa watu kujipiga picha.
Taarifa zinasema alienda kujipiga picha eneo la mwamba Jumatano.
Alijaribu kuruka juu ndipo ajipiga picha akiwa hewani lakini akateleza na kutumbukia kwenye bonde.
Maafisa wa uokoaji waliupata mwili wake Alhamisi na kuupeleka kituo cha polisi kilichoko karibu.
Polisi wamesema mwili wake utapelekwa chumba cha kuhifadhia maiti katika mji wa Cusco.
BBC

KATUNI ZA LEO MAGAZETINI