Ukiona wahudumu kwenye ndege hawaonekani, ujue wako huku wengine wamelala… !!
Ukiwa ndani ya ndege unasafiri kuna wale
wahudumu ambao wanakuwa wanazunguka hivi kuhudumia wasafiri, muda
mwingi ni wakarimu na utaona wanatabasamu muda wote, unadhani
hawapumziki?
Nimekutana na story kwenye mitandao
mikubwa Duniani, wamesapoti kabisa story yao kwa ushahidi wa pichaz
kwamba kama ukiona wahudumu hawaonekani katikati ya safari, wakati
mwingine wanakuwa wamelala.. unajua vyumba viliko?
Ndani ya ndege nyingi kubwa kama Boeing 777 au 787
ambazo zinafanya safari ndefu kama kutoka Amsterdam Uholanzi mpaka New
York Marekani ndani kuna hivi vyumba vya wale wahudumu kupumzika wakiwa
safarini.
Unaambiwa
kwenye ndege nyingine mlango ni wa siri kabisa, huu unafunguka kwa juu
kama sehemu ambayo inawekwa mizigo kwa juu ndani ya ndege.
Kwenye
ndege nyingine vitanda vya wahudumu viko juu, hii ni ramani yake, watu
wanaendelea na safari kwa chini alafu wahudumu wanakuwa wamepumzika zao
kwa juu.
No comments:
Post a Comment