Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akipima eneo la barabara inayohitajika katika eneo la hifadhi ya uwanja wa ndege wa Tanga. |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawaakitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko. |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa meneja wa Tanroads Mkoa wa Tanga, Alfred Ndumbaro kuhusu ujenzi wa barabara ya mchepuko. |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo katika makutano ya barabara ya mchepuko eneo la Duga. |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama
ramani ya gati ya Bandari ya pangani ambayo inajengwa kwa gharama ya
sh. bilioni 2.3.
Muonekano wa gati inayojengwa katika bandari ya Pangani iliyogharimu kiasi cha sh. bilioni 2.3. |
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitazama
ramani ya daraja la Mto Pangani ambalo upembuzi yakinifu wa ujenzi wake
umekamilika na litaanza kujengwa hivi karibuni.
SERIKALI
ipo kwenye hatua za mwisho za kuanza ujenzi wa Barabara ya
Tanga,Pangani ,Saadani mpaka Bagamoyo yenye urefu wa kilometa 242 kwa
kiwango cha
lami ambapo mpaka sasa tayari kazi iliyobaki ni kupata mzabuni wa kuendesha mradi huo.
Waziri wa ujenzi,uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa alisema kuwa ujenzi
wa Barabara hiyo utaanza rasmi kutekelezwa kwenye bajeti
ya mwaka wa fedha 2016/2017 na kwamba serikali ipo kwenye mazungumzo na
Benki ya Maendeleo ya Afrika(ADB)ambayo imeonesha nia ya kufadhili mradi
huo.
Mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa Daraja katika
Mto Pangani lenye urefu wa mita 550 ambalo linategemewa
kuwa kiunganishi cha mawasiliano ya kuimarisha shughuli za utalii katika
ukanda wa Pwani ya Bahari ya Hindi.
Kwa
mujibu wa Prof.Mbarawa ni kwamba wakati wa utekelezaji wa mchakato huo
serikali itawalipa fidia wananchi ambao wanastahili na wameshafanyiwa
tathimini
kwa mujibu wa sheria ya Barabara ya mwaka 2007 iliyofanyiwa marekebisho
mwaka 2009.
“Nasisitiza
kwamba kama sheria inavyotamka kwamba nani anastahili kulipwa basai
kila mwenye haki na anayestahili kulipwa atalipwa na kama hastahili
hatalipwa
na hii itakuwa ni kulingana na tathmini iliyokwishafanyika......”, alisema Waziri huyo.
Alisema
kuwa serikali inatambua umuhimu wa ujenzi wa Barabara hiyo kwamba ndiyo
kiini na moyo wa uchumi wa wilaya ya Pangani hasa kwa kutambua namna
ambavyo
ina vivutio vingi vya kitalii hatua itakayolenga kuwaongezea fursa za
kibiashara wananchi na kukuza Pato lao.
“Daraja
hili litakuwa na uwezo wa kupitisha magari na watembea kwa miguu kwa
wakati mmoja na hivyo ni mkombozi wa wananchi hasa kwa kuzingatia kuwa
walikuwa
wakitegemea kuvuka ng’ambo ya pili ya mto kwa kutumia kivuko tu ambacho
wakati mwingine kinakumbwa na hitilafu”,alifafanua Prof.Mbarawa ambaye
yupo mkoani Tanga katika ziara ya kikazi.
Akizungumza
wakati wa majumuisho ya ziara yake baada ya kukagua Kivuko cha Mto
Pangani,Barabara ya Tanga,Saadani mpaka Bagamoyo na eneo linalotakiwa
kujengwa
Daraja,Prof.Mbarawa aliuagiza Uongozi wa Wakala wa ufundi na Umeme(Temesa)kuhakikisha wanaweka kumbukumbu za utendaji wa kivuko kwa kila siku.
Aliwaagiza
kutumia mfumo wa malipo kwa njia ya elektroniki ili kuepusha vitendo
vya ubadhirifu wa fedha wakati serikali ikiwa kwenye mpango wa
ukusanyaji
wa fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi.
“Suala
la kutumia mashine za kieletroniki halina mjadala habari ya kutumia
vitabu vya risiti ili muongeze sifuri mbele hatuzitaki....hapa kuna
shida kuna
siku I naandikwa imeingia shilingi milioni moja lakini Benki zimeenda
laki nane na hamsini hii laki moja na hamsini zinaishia wapi hili ni
tatizo”,alisema.
Hata
hivyo alisema ipo haja kwa Temesa kuajiri manahodha wa vivuko ambao
wanafanya kazi kwa viwango vya kitaaluma ambavyo vinakubalika badala ya
kutumia
Wazee ambao wanafanya kazi kwa mazoea.
IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO WIZARA YA UJENZI,UCHUKUZI NA MAWASILIANO
No comments:
Post a Comment