Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE
wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stivin Ngonyani (CCM), amewaonya viongozi wa kata
na vijiji kuepuka ubadhirifu kula pesa
za wafadhili na walipa kodi vyenginevyo wataanza kutumbuana majipu wenyewe kwa
wenyewe kabla hayajawa tambazi.
Akizungumza katika mkutano wa
wananchi kuwashukuru kwa kumchagua kwa awanu ya pili kuwa Mbunge wao jana
uliofanyika kata ya Makuyuni, Ngonyani maarufu kama Profesa Majimarefu, alisema
hatukuwa tayari kuona pesa za walipa kodi zinaliwa na wajanja.
Majimarefu katika mkutano huo baada
ya kusikiliza kero za wananchi alitoa shilingi milioni tatu zikiwa msaada kuchonga barabara ya Makuyuni itokayo milimani iliyoharibiwa na
mvua iliyonyesha wiki iliyopita pamoja na ujenzi wa Zahanati ya wazee na
watoto.
“Wananchi wenzangu nimekuja hapa
kutoa shukurani zangu za dhati na taadhima kwa mapenzi yenu kwa kunichagua kwa
nmara ya pili, name fadhila yangu kwenu ni kutoa msukumo kwa shughuli za
maendeleo” alisema Majimarefu na kuongeza
“kuna viongozi wengine wanayatumia
vibaya misaa da ya wafadhili na pesa za wananchi na leo nachangia milioni tatu
ili kuhamasasisha watu kujitolea katika
miradi ya maendeleo” alisema
Akizungumza kuhusu wakulima
kupata pembejeo za kilimo na mikopo
nafuu, Majimarefu alisema atahakikisha bei za pembejeo zinapatikana kwa bei nafuu na kuepukana na
kero ya kufuata mjini.
Alisema atahakikisha pembejeo za
kilimo zinapatikana karibu na wakulima maeneo yao pamoja na kupata mikopo yenye
masharti nafuu ili kuhakikisha mkulima anapata unafuu katika kilimo chake.
Alisema ataita wataalamu wa kilimo
na masoko kufika kutoa elimu ya kilimo na upatikanaji wa masoko lengo likiwa ni
kumuokoa mkulima wa chini na kuwa wa kisasa.
“Hapa tutahakikisha kilimo cha
mkulima mdogo kinakuwa kilimo kama ilivyo cha mkubwa, watakuja walimu wa kilimo
na masoko, pembejeo sio tena kufuata mjini ni hapahapa tena kwa mkopo nafuu”
alisema Majimarefu
Alisema rutba nzuri ya ardhi yenye
kukubali aina mbalimbali za kilimo ni kila mwenye ardhi kuitumilia kwa kilimo
na matumizi bora ya ardhi lengo likiwa ni kutokomeza umasikini Wilayani humo.
Mwisho
No comments:
Post a Comment