Huyu ndio kocha mpya wa Chelsea atakayejiunga na timu mwisho wa msimu 2015/2016
Baada ya klabu ya Chelsea ya Uingereza kumfukuza aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Jose Mourinho miezi kadhaa iliyopita na nafasi yake kuchukuliwa na kocha wa muda Guus Hiddink, April 4 uongozi wa Chelsea umetangaza kocha wa kudumu atakayejiunga na klabu hiyo mwishoni mwa msimu.
Chelsea imetangaza kuingia mkataba wa miaka mitatu na kocha wa timu ya taifa ya Italia Antonio Conte, Chelsea imempa mkataba Conte ambaye atajiunga na timu hiyo baada ya michuano ya Euro 2016 kumalizika akiwa anaiongoza timu ya taifa ya Italia katika michuano hiyo.
“Klabu
ya Chelsea na soka la Uingereza kwa ujumla unaangaliwa sana popote
uendapo, mashabiki wa soka Uingereza wanamapenzi na soka kweli,
natumaini nitafurahia mafanikio hapa kama ilivyokuwa Italia”
>>> Antonio Conte
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Antonio Conte aliwahi kuichezea timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 1994 hadi mwaka 2000, lakini amewahi kuvifundisha vilabu vya Juventus ya Italia kuanzia mwaka 2011-2014, Siena na timu ya taifa ya Italia kuanzia mwaka 2014 hadi 2016. Conte kwa sasa ana umri wa miaka 46.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment