Clinton alaumu FBI kwa kushindwa kwake
Clinton amewaambia wafadhili wa chama chake kwamba hatua ya Comey ilisambaratisha kampeini yake, licha ya uchunguzi huo kutompata na hatia.
Mwandishi wa BBC nchini Marekani hata hivyo amesema wengi wanahisi kuna msururu wa sababu zilizomfanya Donald Trump kumshinda katika uchaguzi huo.
Maelfu ya waandamanaji walifanya maandamano kwa siku nne mfululizo dhidi ya rais mteule Donald Trump.
Wengine walielekea katika jumba la Trump Tower,nyumbani kwa bwana Trump pamoja na makao makuu ya biashara za Trump.
No comments:
Post a Comment