Sunday, May 3, 2015

JEURI YA PESA

KISA MAYWEATHER VS PACQUIAO, ANGALIA NDEGE ZA MABILIONEA ZILIVYOJAZANA UWANJANI

Unaweza kusema ni jeuri ya fedha, mastaa mbalimbali mamilionea na mabilionea wamejitokeza kwenye pambano la ngumi kati ya Floyd Mayweather dhidi ya Manny Pacquiao.
Burudani ni kwamba kwenye Uwanja wa Ndege wa Las Vegas linapopigwa pambano hilo, zimejazana ndege ile mbaya.Ndege za matajiri hao, hadi imelazimika ziegeshwe kwa utaratibu usio sahihi kwa kuwa ziko nyingi ile mbaya.Ila imeelezwa wengi wao wanaondoka baada ya mechi hiyo asubuhi ya kurejea sehemu mbalimbali duniani.

YAMETIMIA, TUMEKUBALI

Umati huu ulikuwa kwa ajili ya Pacquiao…Unadhani watakubaliana na matokeo.

watuuuu
Hawa mashabiki wa Manny Pacquaio hawakujua kama mwisho wa pambano ingekuwa hivi, na walikuwa na uhakika kwa asilimia zote kwamba ni lazima Pacquiao angeshinda.
watu4
Lakini mwisho wa siku matokeo yaliamua kuwa Floyd Mayweather ndiye mbabe kwa mwanzake Manny Pacquiao baada ya pambano la raundi 12 ambapo Mayweather alimshinda Pacquiao kwa pointi sita akiwa na pointi 117 huku mwenzake akiwa na 111.
Mashabiki kutoka sehemu mbalimbali huko Ufilipino waliacha kazi zao kwa ajili ya kushuhudia pambano hilo katika maeneo mbalim,bali ya wazi kkwenye Screen  kubwa katika pambano lililokuwa likipigwa Las Vegas, Marekani.
watu3
Ukiachia Ufilipino mashabiki walijitokeza isivyo kawaida kila pande duniani na kila mmoja alikuwa na uhakika na ushindi wa mtu anayemkubali kati ya mastaa hao wawili duniani.
watu
Yote haya yanakuja hapa hapa tangakumekuchablog

SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETINI LEO, MAY 3 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

BRIIF
MWANANCHI
Hatimaye makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano, juzi walipata nafasi ya kutunishiana misuli baada ya kualikwa kuchangia mfuko wa maendeleo wa mkoa mpya wa CCM wa Magharibi visiwani hapa.
Edward Lowassa, Mizengo Pinda, Bernard Membe, Makongoro Nyerere, Mark Mwandosya na Steven Wasira walishiriki kwenye hafla hiyo na kuchangia zaidi ya nusu ya fedha zilizokusanywa juzi kwa ahadi, hundi na taslimu kwenye harambee hiyo iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort mjini hapa.
Hata hivyo, pamoja na cheche za makada hao kuonekana visiwani hapa, Ni Waziri Mkuu Pinda aliyehudhuria harambee hiyo iliyokusanya jumla ya Sh. milioni 644.54 na ambayo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi.
Waziri Pinda ndiye aliyetia fora kwenye hafla hiyo baada ya yeye na marafiki zake kuchangia jumla ya Sh203 milioni, wakati Lowassa, Membe, Wasira, Dk Shein, Mwandosya, Makongoro, Shamsi Vuai Nahodha na Amina Salum Ali walichangia jumla ya Sh101.5 milioni.
Makada hao hawakukutana kwa bahati mbaya kwenye hafla hiyo.
“Tuliwapelekea mwaliko maalumu wote waliotangaza nia ya kugombea urais,” alisema mratibu wa shughuli hiyo, Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kabla ya harambee kuanza.
Kombo alisema si vyema kwa wanachama wa CCM kubaguana wakati viongozi wakuu wa nchi hawajambagua mtu kwa sababu ya makundi ya wagombea uongozi.
Kati ya fedha zilizokusanywa, Sh120.7 milioni zilikuwa fedha taslimu, wakati ahadi zilikuwa Sh490.8 milioni na hundi Sh33 milioni.
Katika hafla hiyo vitu mbalimbali vya asili pamoja na picha za kumbukumbu za kitaifa, ikiwamo picha ya kuchora ya Rais Dk Shein ambayo ilinunuliwa kwa Sh23 milioni.
MWANANCHI
Tishio la ugaidi limezidi kuwa tete baada ya watu wanaoshukiwa kufanya vitendo hivyo kulipua bomu na kusababisha watu watano kujeruhiwa wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Kijiji cha Msolwa Ujamaa, kilichoko Kata ya Sanje wilayani Kilombero.
Hili ni tukio la pili kutokea kwenye Wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro baada ya watu tisa kukamatwa kwenye Msikiti wa Suni wakiwa na silaha na vifaa vingine vinavyohusishwa na harakati za kigaidi.
Mbali na matukio hayo ya Morogoro, hivi karibuni vikosi vya ulinzi na usalama vilipambana vikali na watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi kwenye mapango ya kihistoria ya Amboni mkoani Tanga.
Hadi sasa polisi haijatoa taarifa ya kina kuhusu tukio hilo lililopoteza maisha ya mwanajeshi mmoja.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro hakuweza kupatikana kuzungumzia suala hilo, wakati msemaji wa Jeshi la Polisi alisema tukio hilo liko ndani ya mipaka ya mkoa hivyo linatakiwa lizungumzwe na mamlaka hiyo badala ya makao makuu ya chombo hicho cha dola.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea walieleza kuwa bomu hilo lilirushwa kuelekea kwenye gari la mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero saa 2:00 usiku.
Bomu hilo lilirushwa na watu wawili ambao awali walidhibitiwa na wananchi baada ya kuwashuku kuwa siyo raia wema.
Baada ya kuwatilia shaka, wananchi waliwaweka watu hao chini ya ulinzi na wakati wakiwapekua, walitoa bomu na kulirusha kwenye gari hilo lililokuwa limeegeshwa na kujeruhi  watu watano, akiwamo dereva.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Ligazio aliwataja waliojeruhiwa katika tuko hilo kuwa ni Novatus Ngapi, ambaye ni dereva na Thomas Manjole, ambaye ni mgambo na hali yake inadaiwa kuwa siyo nzuri.
Wengine waliojeruhiwa ni Amos Msopole, Azama Naniyunya, ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo Mikumi wilayani Kilosa na Anna Pius ambaye amepata majeraha kidogo na kuruhusiwa.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongeza nchi kwa muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari la Kudumu la Wapigakura.
Hivi karibuni viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema ni miezi mitatu imebaki kabla ya kampeni za uchaguzi, lakini mpaka sasa ratiba, majimbo yaliyogawanywa, watumishi wala vituo vya uchaguzi bado haviwekwa bayana na wala haifahamiki kazi ya uandikishaji katika Daftari la Wapigakura halijakamilika katika mikoa miwili.
Hiyo ni hatari sana kwa Taifa. Tunaionya NEC isijaribu kufanya mbinu zitakazosababisha kuahirishwa kwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,” Mbowe.
Mrema alisema yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoa wazo la kutaka Rais Kikwete aongezewe muda zaidi wa kukaa Ikulu kwa kuwa kuna mambo mengi ambayo ni ya muhimu kwa Taifa yanayotakiwa kukamilika kabla ya Uchaguzi Mkuu.
Mrema alisema alitoa maoni hayo mwaka jana wakati viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walipokutana na Rais Kikwete mjini Dodoma, lakini alishangaa kuona viongozi wengine wakipinga wazo hilo.
“Nilitoa ushauri Rais Kikwete akiwepo. Nilisema tusogeze Uchaguzi Mkuu mbele kwa miaka miwili ili atuachie nchi ikiwa salama, lakini wapinzani wamejiandaa kuingia Ikulu waliniona mimi kama bundi,” Mrema.
JAMBOLEO
Waziri wa Nishati na madini George Simbachawene ameiagiza menejmenti ya Shirika la Umeme TANESCO kuwachukulia hatua za kinidhamu wahandisi wa shirika hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa mkutano na watendaji wa Tanesco wa kanda ya Dar na Pwani, ambapo alisema Muhandisi wa Wilaya ya Temeke, Tabata na Tazara wameshindwa kusimamia majukumu waliyopewa na Shirika hilo,hivyo amewataka wakurugenzi wahakikishe wanawahadhibu.
Alisema huo ni mwanzo kwani ataendelea kuwachukulia hatua watumishi ambao watashindwa kufanyia kazi majukumu waliyopewa na Shirika katika kuhakikisha wanawapa huduma nzuri Watanzania.
“Wengine wakae mguu sawa, huu ni mwanzo tu, sitaki kuwa na watendaji ambao hawajui wanachokifanya katika vitengo walivyopewa, yeyote atakayeshindwa kufanya kazi yake ni vyema aachie ngazi” Simbachawene.
Alisema wahandisi watatu aliowatolea maagizo wachukuliwe hatua za kinidhamu wanamtosha kwani anaamini litakuwa fundisho kwa wengine.
MTANZANIA
Meli ya Tanzania iliyokamatwa kwenye bahari ya Kaskazini nchini Marekani ikiwa na tani tatu za dawa za kulevya aina ya Cocaine ilisajiliwa Zanzibar.
Taarifa iliyopatikana kutoka vyombo ya habari vya kimataifa ilisema meli hiyo ilikutwa na tani tatu za dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5.
Meli hiyo inayojulikana kwa jina la Mv Hamal ilikamatwa na meli ya kivita ya Uingereza na kikosi chamipaka ikiwa umbali wa kilometa 160 kuelekea katika Pwani ya Aberdeen nchini Scotland na ilikuwa ikiendeshwa na waturuki.
Msemaji wa SUMATRA, David Mziray aamesema wanaendelea kufuatilia kama meli hiyo ilisajiliwa bara ama visiwani na baadaye alisema wao hawahusiki n usajili wa meli hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Zanzibar Abdi Maalim alikiri kuwa meli hiyo ilisajiliwa Zanzibar kupitia kwa wakala wao aliyepo Dubai.
HABARILEO
Wafanyabiashara wadogo na waendesha bodaboda wanaofanya biashara zao kwenye njia kubwa za kusafirishia umeme wapo hatarini kupungukiwa nguvu za kiume.
Kutokana na kuwepo wengi kwenye njia hizo kubwa za kusafirishia umeme, wametahadharishwa kutoendelea kufanya biashara kwenye maeneo hayo.
Hayo yalibainishwa jana na Ofisa Mahusiano Msaidizi huduma kwa wateja wa Tanesco Mwanza, Haji Bwegege  baada ya uzinduzi wa maonyesho ya siku ya wafanyakazi uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye viwanja vya Furahisha, jijini hapa.
Tumekuwa tukiielimisha jamii mara kwa mara kutofanya biashara kwenye njia ya umeme mkubwa unaopita kutokana na madhara wanayoweza kuyapata na hii ya kupungukiwa nguvu za kiume ni moja ya madhara ambayo yanaweza kuwapata hivyo wachukue tahadhari mapema,”
Aliyataja madhara mengine kuwa pamoja na mwili kupoteza nguvu kutokana na mionzi hivyo wananchi kutakiwa kuishi umbali wa mita 30 kila upande pamoja na mjamzito kuharibu mimba.
HABARILEO
Wakimbizi 800 kutoka nchini Burundi wameingia nchini kupitia mkoani Kigoma huku wengine 87 wakirejeshwa nchini mwao baada ya kuingia nchini kwa kupitia wilayani Ngara mkoani Kagera.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Isack Nantanga alisema wakimbizi hao wameingia nchini kwa makundi madogo madogo na watahifadhiwa kwa muda karika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Nantanga alisema wakimbizi wanaofikia 800 wameshaingia nchini huku walioingia kupitia mkoani Kagera ilibidi warejeshwe walipotoka kutokana na kukiuka sheria za kimataifa kwa wakimbizi kuingia nchi nyingine wakivuka nchi moja.
Alisema hawapokei wakimbizi wanaotokea Rwanda kutokana na kuwa sheria za kimataifa haziruhusu wakimbizi kuvuka nchi moja ndiyo maana waliwarejesha wakimbizi hao.
Alisema kati ya wakimbizi hao waliopokelewa mkoani Kigoma wameingia kupitia vijijini ambapo serikali za vijiji wanawapokea na kuwahoji kisha kuwapleka kigoma mjini kwenye kituo maalum.
Alisema serikali za vijiji na wilaya kwa kushirikiana na halmshauri wamekuwa wakaifanya kazi ya kuwahoji kujua sababu hasa ya kuwafanya wakimbilie nchini humu kwani isije kutumika vurugu za Burundi watu kuingia nchini.
“Serikali kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi (UNHCR) baada ya kuwahoji na kuwapa misaada muhimu wanaobainika kupata hifadhi wana mpango wa kuwapeleka kwenye kambi ya Nyarugusu kwa muda,”alisema.
Msemaji huyo alisema baada ya kuhifadhiwa katika kambi hiyo mipango inaendelea kufahamu njia nyingine za kuwahifadhi.
Wengi wa wakimbizi hao wametokea mji wa Bujumbura na wameingia Kigoma kwa usafiri wa boti kupitia bandari ndogo ya Kibirizi mjini Kigoma.
Inaelezwa kuwa kundi kubwa la wakimbizi liliingia nchini juzi katika mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye kijiji cha Kagunga mwambao wa kaskazini wa ziwa Tanganyika ambapo kundi la wakimbizi 200 waliingia kupitia kijiji hicho.
Tayari wakimbizi 68 ambao waliingia na kufikia kambi ya muda ya NMC kibirizi mjini Kigoma wamepelekwa kwenye kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu ambayo kwa sasa ndiyo kambi pekee mkoani Kigoma inayohifadhi wakimbizi.
Akizungumzia kuingia kwa wakimbizi mkoani humo Mkuu wa mkoa Kigoma, Issa Machibya alisema kuwa wameanza kupokea wakimbizi kutoka vijiji mbalimbali vya wilaya za Buhigwe,Kasulu na Kibondo ambao wanakimbia hali ya machafuko nchini Burundi.
Machibya alitaja maeneo ambayo hadi sasa yamekuwa yakipokea wakimbizi hao kuwa ni pamoja na Kijiji cha Kagunga wilaya ya Kigoma, Muyama,Kibande na Kilelema ambavyo vyote vipo katika wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Kuingia kwa wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania kunatokana kuanza kwa machafuko nchini humo kati ya wananchi wanaopinga kitendo cha Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuongoza muhula wa tatu wa uongozi dhidi ya polisi na wanajeshi wanaomtii raisi huyo.
Kwa siku mbili mfululizo kumekuwepo na taarifa za kuchomwa mwa mabasi mawili ya abiria na moja kulipuliwa kwa bomu la kurushwa kwa mkono huku kukiwa na vifo vya watu kadhaa kutokana na makabiliano ya waandamanaji na polisi.
Wageni wamekuwa wakizuiliwa kuingia mji mkuu wa Burundi, Bujumbura ambako kwa kiasi kikubwa maandamano ya kupinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuongoza muhula wa tatu yanaendelea ambapo kwa sasa maandamano hayo yameanza kusambaa mikoa ya jirani na mji Mkuu wa Bujumbura.
NIPASHE
Agizo la serikali la kupiga marufuku uingizaji wa mabehewa ‘feki’ ili kuliokoa taifa dhidi ya ufisadi na ajali zinazogharimu mali na maisha ya watu, limepuuzwa baada ya Kampuni ya Reli (TRL) kupokea mabehewa 47, mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Mabehewa hayo ni sehemu ya yaliyoanza kuingizwa nchini, Julai 24, mwaka jana na kupokelewa na aliyekuwa Waziri wa Uchukuzi wa wakati huo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Hata hivyo, serikali kupitia kwa Waziri wa Uchukuzi, Samwel Sitta, ilizuia uingizwaji wake, Aprili 16, mwaka huu, kwa madai kuwa hayana ubora.
Akitangaza uamuzi wa kuzuia mabehewa hayo, Sitta alisema baada ya bodi kupitia taarifa hiyo, ilibaini  mabehewa mengi kati yaliyoagizwa yalikuwa na kasoro, kuwepo kwa uzembe katika uagizaji na ufuatiliaji kuanzia kiwandani  na kuwapo kwa uzembe katika mchakato wa kuyapokea.
Sitta alisema kilichowashtua ni kubaini ukiukwaji mkubwa wa masharti ya mkataba wa ununuzi ambao ulipangwa kufanyika kwa awamu.
Alisema katika makubaliano ya ununuzi wa mabehewa hayo, malipo yalitakiwa yafanywe kwa awamu kwa kuanza na asimilia 50 awamu ya kwanza,  asilimia 40 awamu ya pili  na awamu ya mwisho ya malipo ilikuwa ni asilimia 10.
Hata hivyo, wiki mbili tangu Sitta atoe agizo hilo, gazeti hili limebaini kuwa mabehewa 47 yaliingizwa nchini na kuhifadhiwa kwenye karakana ya Malindi jijini Dar es Salaam.
Chanzo hicho kimesema inavyoonyesha mkataba wa kuyaleta mabehewa hayo haujavunjwa ndio maana yamewasili tena licha ya Waziri Sitta kusema yaliyobaki yasiingie nchini.
Mabehewa hayo ni kati ya 274, ambapo 150 yalishaingizwa nchini na mengine 124 yalizuiliwa.
Sakata la ununuzi wa mabehewa hayo limesababisha serikali hasara ya Sh. bilioni 230. Kufuatia sakata hilo Sitta aliwasimamisha kazi vigogo watano kutokana na kubainika kuihujumu serikali.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu,  Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiranga na Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinarnd Soka.
NIPASHE
Wakati serikali ikijitetea kuwa kushuka kwa shilingi ya Tanzania kunatokana na kuimarika kwa dola ya Marekani, Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ametaja sakata la Escrow kuchangia pia anguko hilo.
Kafulila alisema hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, iliyokutana na Wizara ya Fedhana mamlaka zake.
Alisema, kwa mujibu wa maelezo ya Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu, sababu za kushuka kwa shilingi ni kuimarika kwa dola ya Marekani na kusababisha sarafu zote duniani kuathirika katika mbadilishano na dola.
Aidha, sababu nyingine ni uhaba wa dola uliosababishwa na kukosekana kwa fedha za wafadhili.
Kafulila alisema misaada iliyokuwa inatarajiwa kutoka kwa wahisani imekwama kutokana na sakata la Escrow.
Alisema mikopo ya  kibiashara ambayo Tanzania ilikuwa ikitarajia kupata dola milioni 800, imekatwa na  kutolewa dola milioni 300, tafsiri inayoonyesha kuwa Tanzania haiaminiki.
Alisema fedha za wafadhili zaidi ya Sh. tirioni 1.0, sawa na dola milioni 740, hazijaidhinishwa kupewa Tanzania na mwaka jana Wizara ya Fedha ilisema zitaidhinishwa Desemba, mwaka jana.
Mwaka huu wanazungumzia labda zitasainiwa Septemba tafsiri yake ni kwamba hiyo hela ambayo ni sawa na tirioni 1.5 haitaletwa hadi hatua zichukuliwe kwenye jambo la Escrow,” Kafulila
Hata hivyo, alisema mikopo ya biashara ya dola milioni 500-800 iliyoahidiwa kuletwa imekwama kwa sababu ya sakata la Escrow.
Alisema tatizo la serikali ni kusema hatua zimechukuliwa wakati,  IPTL inalipwa zaidi ya Sh bilioni 5 kila mwezi, kama tozo ya uzalishaji  (Capacity Charge).
Kama kawaida tangakumekuchablog inakuta yote yaliyoandikwa katika magazeti, ni hapa hapa

MANNY WEATHERE BINGWA WA DUNIA

Floyd Mayweather VS Manny Pacquiao kazi imeisha !! Points 6 tu zimeamua mshindi tayari..

fight-8a_rnd_5_3289903b
Najua watu wengi waliisubiri hii kwa hamu.. wengine hata sio mashabiki wa boxing lakini walijikuta wakivutiwa na hii.. Promo ilikuwa kubwa sana, pambano la kihistoria ambalo dunia nzima ililisubri ni hili kati ya Floyd ‘Money’ Mayweather na Manny Pacquiao.
Points tayari zimeamua, pambano limeenda kwa round 12, Floyd Mayweather kamshinda Pacquiao kwa points sita tu.. Floyd ana points 117 na Pacquiao ana points 111.
wattt_3289915b

Kwa matokeo hayo Mayweather kaendeleza kuweka rekodi yake kubwa ya kutoshindwa pambano hata moja tangu amekuwa professional boxer.
fight-6-a_rnd_2_3289901b
fight-end-manny_3289916b
fight-floyd-manny-_3289909b
fight-floyd-win-be_3289919b
fight-manny-floyd-_3289911b
fight-manny-floyd-_3289914b

Shilingi yako uliweka upande upi mtu wangu ?? Uliamini upande wa Mayweather au Pacquiao..

Saturday, May 2, 2015

HAYAWI HAYAWI SASA YAMEKUWA

MAYWEATHER, PACQUIAO WAPIMA UZITO, SASA KILICHOBAKI NI NDONGA TU

Mabondia Floyd Mayweather na Manny Pacquiao wamepima uzito ikiwa ni hatua muhimu ya kuthibitisha pambano la kesho.Kukutana kwao na kupima uzito, maana yake kila kitu kimekamilika na kinachosubiriwa ni ndonga tu kesho.Ndiyo pambano ghali zaidi katika historia ya ngumi duniani na linasubiriwa kwa hamu duniani kote wakati wawili hao wakipambana jijini Las Vegas, Marekani.









SOMA MAKUBWA YALIOANDIKWA MAGAZETINI LEO MAY 02, TZ

Uchambuzi huu unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wale ambao wanajiendeleza kielimu. Pia wanatoa kozi ya Kiingereza na Computer na kutoa Certificate. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

Newspaper
MWANANCHI
Kwa mara nyingine, Jina la nchi limeendelea kuchafuka baada ya Meli ya MV Hamal iliyosajiliwa Tanzania kukamatwa Ulaya ikiwa imebeba shehena ya dawa za kulevya aina ya cocaine yenye uzito wa tani tatu, kama dawa hizo zingeuzwa mitaani nchini Uingereza zingekuwa na thamani ya Sh1.5 trilioni, kiasi ambacho nchi wafadhili zinatarajiwa kuichangia Tanzania kwenye bajeti ya mwaka 2015/16.
Mwaka 2013 meli ya mizigo ya Gold Star iliyosajiliwa Tanzania ambayo ilikamatwa Septemba 2013 katika bahari ya Mediterranian, Italia wakati ikielekea Uturuki ikiwa na tani 30 za bangi zenye thamani ya Pauni 50 milioni za Uingereza (sawa na Sh125 bilioni).
Kiwango hicho cha dawa zilizokamatwa kimeweka rekodi ya ukubwa wa mzigo wa dawa hizo haramu zilizowahi kukamatwa Uingereza..
Upekuzi wa meli ulikuwa mrefu na unaosababisha maumivu, na uliofanywa na watu wenye utalaamu mkubwa wa kufanya kazi kwenye mazingira magumu”—alisema John McGowan, afisa mwandamizi wa Uchunguzi wa NCA.
Rekodi za mtandao wa shughuli za baharini unaonyesha kuwa katikati ya Februari, meli hiyo ilikuwa Uturuki na wiki mbili zilizopita ilianza safari kutoka visiwa vya Tenerife, Hispania.. ilipokamatwa ilikuwa inaelekea Hamburg, mji wa pili kwa ukubwa nchini Ujerumani ambako ingefika jana usiku.
Meli hiyo imekutwa na watu tisa wenye umri kati ya miaka 26 na 63 wote raia wa Uturuki na wameshitakiwa kwa kukutwa na dawa za kulevya.
JAMBO LEO
Chama cha Wamiliki wa Mabasi TABOA kimesema uwepo wa mizani ya kupima mizigo ya Kibaha imekuwa sababu mojawapo kubwa ya madereva kwenda mwendokasi ili kufidia muda mwingi ambao wanaupoteza kwenye mizani hiyo.
Hii mizani mpya imekuwa ni tatizo kwetu, imekuwa ikichangia dereva kuendesha mwendo mkali kwani katika kupima mizani pale unachukua muda mrefu kukaa”—Enea Mrutu, Katibu Mkuu TABOA.
Alisema kwamba katika Kamati ambayo waliunda kuchunguza tatizo hilo la ajali wamegundua kwamba mwendo kasi pamoja na mizani hiyo vimechangia tatizo la ajali.
JAMBO LEO
Viongozi wa CHADEMA Rungwe, Mbeya wametwangana makonde mkutanoni baada ya kupishana kauli kwa kila mmoja kumpigia chapuo mtia nia ya Ubunge na kusababisha mmoja wao kuchanwa uso na kushonwa nyuzi sita.
Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye alijeruhiwa amesema kisa cha ugomvi huo ni mgogoro wa maslahi binafsi anayoyaendekeza Katibu Uenezi wa Wilaya.
Kisa cha mgogoro wao ni suala la CHADEMA kupata nyumba ya kupanga ambayo wanaitumia kama ofisi, viongozi wote walichanga pesa kwa ajili ya ofisi hiyo lakini kiongozi mmoja ambaye ni Godogo aligoma akitaka ofisi hiyo ihamie nyumbani kwake kitu ambacho Kamati ilikataa.
Katibu wa Chama hicho Wilaya hiyo, Nsajigwa Bonifas amekiri kutokea tukio hilo na kusema ni kitendo cha aibu japo haweza kuzungumzia zaidi kwa sasa.
HABARI LEO
Wakati wateja wa umeme wameendelea kutaabika, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetoa malekezo zaidi ya namna ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi.
Taarifa ya Tanesco imekuja baada ya tatizo lililojitokeza kwa baadhi ya mawakala wa LUKU kushindwa kutoa huduma ya kuuza umeme kutokana na Kampuni ya SELCOM ambaye ni wakala wa kuuza na kuziunganisha baadhi ya kampuni za simu kwa TANESCo kusitishiwa huduma kutokana na kile kilichoelezwa kushindwa kutekeleza baadhi ya majukumu yake ikiwamo kughushi nyaraka na kukiuka taratibu za kulipa kodi.
Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo, na kusainiwa na Ofisa Habari wake, Adrian Sevelin ilisema kuwa huduma zinaendelea kupatikana kupitia Makampuni mengine na huduma za Mabenki.
Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa”– alisema Adrian Sevelin, Afisa Uhusiano wa TANESCo.
Gazeti la HABARI LEO lilizunguka katika vituo mbalimbali vya kutoa huduma hiyo na kukuta misululu ya wananchi wakisubiri huduma hiyo huku kukiwa na tatizo la mtandao.
MTANZANIA
Mwenendo wa uchunguzi wa madai ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kutaka kuuawa na mlinzi wake binafsi, Khalid Kangezi, umezua shaka kutokana na ukimya wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ambapo kwa zaidi ya mwezi mmoja limeshindwa kuwahoji watuhumiwa waliotajwa.
Uchunguzi wa gazeti la MTANZANIA umebaini Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ambao kwa pamoja wanashutumiwa kula njama ya kutaka kumzuru Dk. Slaa,hawajahojiwa.
Si Mangula wala Kinana aliyehojiwa.. inasikitisha kuona watu walioendesha njama ya kutaka kuteketeza maisha yangu wanaendelea kuranda randa pasipo hatua yoyote kuchukuliwa,” alisema Dk. Slaa.
Alipotafutwa Philip Mangula ili athibitishe kama ameshahojiwa na Jeshi la Polisi au la, alishindwa kukataa wala kukubali badala yake alimwambia mwandishi kuwa yupo kwenye kikao na hata alipotafutwa Kinana simu yake haikupatikana.
 “Ngoja niulize wasaidizi wangu…Lakini kwanini umeniuliza swali hilo wakati sipo ofisini? Nitafute Jumatatu,” alijibu Kamishna Kova baada ya kuulizwa kuhusu suala hilo.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog.com

AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wale ambao wanajiendeleza kielimu. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746


Na Awadh Ibrahim

Friday, May 1, 2015

WATUHUMIWA WA MALALA WAFUNGWA MAISHA JELA

Hii ni hukumu ya waliompiga risasi mwanaharakati mdogo Pakistan

malala-yousafzai-nobel-prize-winnerJina la Malala Yousafzai liliwahi kukaa kwenye vichwa vya habari vya Kimataifa mwaka 2012 kutokana na tukio la msichana huyo kupigwa risasi akiwa ndani ya basi lao la shule.
Malala alikuwa na umri wa miaka 15 wakati huo, tukio la kupigwa risasi linahusishwa na ishu yake kujihusisha na harakati za kudai haki za watoto hasa wa kike kwenye suala la elimu.
Mwaka 2014 jina lake likarudi tena kwenye headlines baada ya kupewa Tuzo ya amani ya Nobel, kilichoripotiwa leo kinarudisha kumbukumbu ya tukio la kupigwa risasi mwaka 2012.
Watuhumiwa 10 ambao walikamatwa kwa kesi ya kuhusika na tukio la kumpiga risasi Malala wamehukumiwa kifungo cha maisha jela.
Malala Yousafzai lying in hospital bed
Malala baada ya shambulio akiwa Hospitali.
Baada ya kupigwa risasi Malala alifanyiwa upasuaji Uingereza, baada ya hali yake kukaa sawa ameendelea na kampeni zake Kimataifa.
Malala ni mmoja ya watu wenye umri mdogo na wana rekodi kubwa.. wakati anatunukiwa Tuzo ya Nobel alikuwa na umri wa miaka 17 tu.
Nobel Peace Prize laureate Malala Yousafzai poses with her medal during the Nobel Peace Prize awards ceremony at the City Hall in Oslo December 10, 2014. Pakistani teenager Malala Yousafzai, shot by the Taliban for refusing to quit school, and Indian activist Kailash Satyarthi received their Nobel Peace Prizes on Wednesday after two days of celebration honouring their work for children's rights. REUTERS/Cornelius Poppe/NTB Scanpix/Pool   (NORWAY  - Tags: SOCIETY CIVIL UNREST TPX IMAGES OF THE DAY) NORWAY OUT. NO COMMERCIAL OR EDITORIAL SALES IN NORWAY.
Malala alipotunukiwa Tuzo ya Nobel
Hutopitwa na habri yoyote na kuwa karibu nami nitakusogezea muda na wakati wowote hapa hapa tangakumekuchablog.com

NGASSA MCHEZAJI BORA LIGI KUU TANZANIA BARA

Yanga ndiyo mabingwa TZ Bara..  headlines za mchezaji wao, Mrisho Ngassa

yanga-standd
Jopo maalum la makocha ambao huchagua wachezaji bora kwa kila mchezo kwenye ligi kuu ya soka Tanzania bara wametoa matokeo ya wachezaji waliochaguliwa kuwa bora kwenye ligi hiyo kwa mwezi April.
Mshambuliaji wa Yanga na timu ya Taifa, Mrisho Ngassa amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom ya mwezi April.
Ngassa ametajwa kuwa mshindi katika nafasi hiyo, wenzake ambao walikuwa wakishiriki ni pamoja na mchezaji Amos EdwardFrank Domayo na Emmanuel Okwi baada ya kupata alama nyingi za mchezaji bora kwa kila mchezo.
Mbali na Ngassa pia James Ambrose ametajwa kuwa mchezaji bora wa Ligi hiyo kwa mwezi March 2015.
Zawadi ambayo watapatiwa mastaa hao kila mmoja ni pesa kiasi cha Tshs. Mil. 1 kutoka kwa wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom.

DROBA ANYAKUA TUZO YA HESHIMA ENGLAND

Tuzo nyingine ya heshima aliyopewa Didier Drogba…

droooMbali na uwezo wake mkubwa wa kumiliki mpira uwanjani, Didier Drogba raia wa Ivory Coast amekuwa na mchango mkubwa katika shughuli za kijamii ambazo ambazo amekuwa akishiriki ndani ya nchi yake na Afrika kwa ujumla.
Uongozi wa ligi kuu ya England umeona ni vyema ukaonyesha kuridhishwa na kazi zake na kuamua kumpa tuzo kutokana na mchango wake mkubwa wa kuhamasisha soka la vijana Afrika kupitia michango yake na uamuzi wake wa kufungua Didier Drogba Foundation ambayo itakuwa ikifanya kazi ya kuwasaidia wenye matatizo.
Staa huyo wa soka wa Chelsea amepewa heshima hiyo kubwa na uongozi huo kama sehemu ya kumpongeza kwa kazi nzuri za kijamii anazofanya.
Tayari Drogba amejenga hospitali kubwa ya kisasa nchini kwao Ivory Coast.

SIMA MAKUBWA YALIYOJIRI MAGAZETINI LEO, MEY 01 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita kwa wanaofanya mitihani ya Taifa na wale wanaojiendeleza kielimu. Kituo kipo Tanga mkbala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

MAY
MTANZANIA
Vyama vinavyoundwa na Umoja wa katiba ya Watanzania UKAWA vimeibua madai mapya ya kuwepo njema za Serikali za kutaka kusogeza uchaguzi mkuu hadi 2017.
Kwa mujibu wa Umoja huo Serikali ipo katika maandalizi ya kupeleka muswada wa sheria Bungeni ili kumwongezea miaka miwili Rais Jakaya Kikwete abaki madarakani.
Viongozi wa UKAWA walisema njama hizo za Serikali zitaungwa mkono na  na wabunge wote wakiwemo baadhi wapinzani kwa maslahi yao wenyewe.
“Wanaona wakifanya uchaguzi huu mwaka huu wataanguka kwa sababu dalili zinaonyesha hata mgombea wao wa Urais ataanguka, wanaona wasogeze kidogo ili iwe rahisi kwao”
“Wanafikiri kwa vile wabunge wanasema wana njaa, tukisema tuwaongezee miaka miwili watapigiwa makofi wawe wa upinzani au wa CCM…hayo ndiyo matumaini yao.
Mwenyekiti wa NEC Damian Lubuva alikanusha taarifa hizo na kusema ni hisia za viongozi hao na hakuna mpango wa aina hiyo.
NIPASHE
Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaweza kujikaanga kwa mafuta yake, iwapo kitachelewa kutangaza mgombea urais katika kinyang’anyiro cha Uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Sumaye alisema hayo baada ya kuombwa na waandishi wa habari mjini hapa, wakimtaka azungumzie hali ya kisasa nchini, uchaguzi mkuu ndani ya CCM na hali ya utekelezaji wa adhabu ya kifo dhidi ya watu waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa.
Alisema wengi wana shauku ya kufahamu atakayepeperusha bendera ya CCM kugombea urais, hiyo ikiwa ni kutokana na kupewa nafasi kubwa ya kushinda uchaguzi huo, na kwamba katika hali isiyo ya kawaida kimechelewa kumtaja.
“Anapotangazwa mapema watu wanatafiti, kufahamu ubora wake na kuwa na msimamo wa kumchagua, hata mgombea anapata muda wa kutosha kufikiri na kufanya kampeni za kutosha,” alieleza.
Alisema pia hiyo itasaidia wapinzani kukosa muda wa kutosha kumshambulia mgombea anapotangazwa kwa kuchelewa, hata yeye mgombea anaathiriwa kwa kutopata muda wa kutosha kufanya kampeni.
Wananchi nao hawapati muda wa kutosha kutafiti ili kufahamu ubora wake, ikiwa ni pamoja na kumhoji maswali, ili wasifanye uchaguzi kwa kufuata mkumbo.
“Hata mimi hali hii sijaielewa, katika hali ya kawaida sasa hivi wenye nia ya kugombea wangeshachukua fomu na kuingia mikoani kutafuta wadhamini, kwa mfano, uchaguzi wa mwaka 2005, mgombea alitangazwa Mei 05,Sumaye,
Sumaye alisema anaamini siku siyo nyingi ratiba ya wenye nia ya kuwakilisha chama katika kugombea urais, ubunge na udiwani itatolewa na chama hicho.
NIPASHE
Siku tatu baada ya Chama cha Wamiliki wa Mabasi yaendayo mikoani (TABOA), kuendelea na msimamo wa kugoma nchi nzima kupinga nauli mpya, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), imenywea na kufuta agizo lake la awali la kupunguza nauli hizo.
Badala yake, Sumatra imetangaza kusitishwa utekelezaji wa viwango vipya vya nauli vilivyotangazwa hivi karibuni na kutaka vya zamani viendelee.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Sumatra kwa vyombo vya habari, jana jijini Dar es Salaam, na kusainiwa na Mkurugenzi Mkuu, Gilliard Ngewe, utekelezaji utasitishwa hadi marejeo yatakapofanyika tena.
“Sumatra imepokea kutoka kwa msafirishaji ABC Trans na Afritrans Limited maombi ya kupitia upya maamuzi yake ya kushusha viwango vya nauli za mabasi ya masafa marefu yalitolewa Aprili 15, mwaka huu.  Maombi ya Kampuni mbili yalipokelewa Sumatra Aprili 29, mwaka huu, ,” alisema.
Alisema kwa sasa viwango vya nauli vya zamani vitaendelea kutumika hadi hapo umma utakapotaarifiwa vinginevyo.
Afisa Uhusiano wa Sumatra, David Mziray, alisema sheria inatoa haki kwa wahusika kukata rufaa ndani ya siku 14 na kwamba kwa sasa wanapitia hoja zao kuona kama zina mashiko ndipo watatoa maamuzi ambayo yatawekwa wazi.
Alisema viwango vipya vya nauli vilitolewa baada ya kukokotoa na kwamba kwa mujibu wa kanuni na kwamba mambo yatawekwa wazi ndani ya siku 14.
MWANANCHI
Mwanasiasa mkongwe aliyevuliwa uanachama wa CCM, Hassan Nassor Moyo  amesema yeye ndiye aliyefanya kazi kubwa, usiku kucha, kumshawishi Maalim Seif Sharrif Hamad, aliyekuwa mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CUF, akubaliane na matokeo ya Uchaguzi Mkuu mwaka 2010 kabla ya hata kutangazwa.
 Moyo alisema alitumwa na Rais Amani Abeid Karume kufanya kazi hiyo kwa bidii, utiifu na uadilifu hadi akafanikiwa.
Moyo alifanya kazi mbalimbali akiwa waziri kwenye Baraza la Mapinduzi Zanzibar na akiwa waziri katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika maisha yake ya utumishi wa kisiasa, lakini akajikuta akipata tuzo ya kuvuliwa uanachama wa CCM akiwa ameshastaafu siasa kwa madai ya kuhudhuria mikutano ya hadhara ya CUF.
Moyo alisema kuwa Mohamed Riyami, ambaye ni mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Maridhiano, alikwenda nyumbani kwake na kumpa ujumbe huo kutoka kwa Rais Karume, na baada ya majadiliano naye, alikubali.
“…Ni kweli Mohamed Riyami alikuja kuniamsha saa 10:00 alfajiri hivi akisema ametumwa na Rais Karume aje aniambie nikamwombe Maalim Seif aridhie matokeo ya uchaguzi mkuu yatakayotangazwa,”  Moyo.
Alipoulizwa kama ni kweli maneno hayo tu ndiyo yalimlainisha Maalim Seif aridhie matokeo hayo, Moyo alijibu; “Hapana, nilizungumza naye kwa kina historia ya mabadiliko, tulikotoka, kufikia kuundwa kwa kamati za miafaka mpaka sasa, naye alikubali.”
MWANANCHI
Ndege iliyokuwa imembeba rais mstaafu wa Marekani, Bill Clinton na mwanaye Chelsea, juzi ilipata hitilafu katika moja ya injini zake na kulazimika kutua Dodoma kwa ajili ya matengenezo kabla ya kuendelea na safari.
Ndege hiyo aina ya DHC 7 yenye namba za usajili 5Y-CDK, iliyokuwa ikitokea mkoani Iringa kuelekea Ziwa Manyara, ilitua saa 10.15 jioni juzi  na kuondoka saa 10.24 jioni.
Chanzo cha habari kutoka uwanja huo wa ndege, kilisema ndege hiyo ilikuwa na tatizo dogo na lilirekebishwa wakati Clinton na abiria wengine wakiwa ndani ya ndege.
“Tulimuuliza rubani wa ndege hiyo kama angehitaji msaada wowote kutoka kwetu, lakini alisema kuwa ni tatizo dogo tu na angeweza kutua mwenye bila msaada na akafanya hivyo,” .
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, meneja wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga, (TCAA),  Ludovic Ndumbaro alikataa kulizungumzia kwa madai yeye si msemaji wa mamlaka hiyo.
Mtafute mkurugenzi ndiyo msemaji wa mambo yote yanayohusu mambo ya anga,”
Clinton na binti yake Chelsea walifika Tanzania kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayofadhiliwa na mfuko wa familia ya Clinton.
Clinton ataendelea na ziara yake ya siku tisa katika nchi za Kenya, Liberia na Morocco. Miradi inayosimamiwa na mfuko wa Clinton ni ya kilimo cha kibiashara.
MWANANCHI
Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa amemtaka Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli kuangalia uwezekano wa kuongeza fedha za Mfuko wa Barabara katika mkoa wa Dar es Salaam ili kujihakikishia kura ikiwa atagombea Urais kama anavyotajwa.
Silaa alitoa kauli hiyo juzi wakati wa hafla ya kuweka jiwe la msingi la upanuzi wa barabara ya Uhuru iliyopo katika Manispaa ya Ilala.
Alisema mkoa wa Dar es Salaam una wapigakura wengi wanaoweza kuamua kupita au kushindwa kwa mgombea katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Meya huyo kijana alibainisha kuwa Manispaa ya Ilala na zile za Temeke na Kinondoni, zimekuwa zikipata fedha kidogo kutoka Mfuko wa Barabara, licha ya kuchangia fedha nyingi kwenye mfuko huo.
Nakuomba  katika bajeti yako ya 2015/16 iangalie Dar es Salaam kwa jicho la huruma. Nikuhakikishie katika takwimu za makadirio ya Sensa za Watu na Makazi za mwaka 2012, jiji hili lina wapigakura 2.3 milioni sasa mzee kama yanayosemwa semwa na yenyewe yamo, hebu iangalie Dar es Salaam kwa jicho la huruma,”  Silaa
Silaa alisema manispaa yake inapata Sh 4.1 bilioni kwa mwaka, lakini barabara ya kilomita moja inajengwa kwa Sh2.95 bilioni, hivyo uwezo wa halmashauri hiyo kuzihudumia barabara zote ni mdogo mno.
MWANANCHI
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chama Kikuu cha Ushirika mkoani Kilimanjaro (KNCU) Maynard Swai, ametangaza kuwania ubunge katika Jimbo la Hai kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwa tangazo hilo, Swai sasa atakuwa na kibarua kizito cha kukabili upinzani kutoka kwa mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Freeman Mbowe (CHADEMA) ambaye tayari ametangaza nia ya kutetea nafasi yake katika Uchaguzi Mkuu ujao.
Hata hivyo, wakati kurudi kwa Mbowe kwenye kinyang’anyiro cha ubunge jimboni humo kutategemea uamuzi wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) ambao utalazimika kumkubali au kumkataa kupitia vikao vyake vya kupanga wagombea.
Swai anatakiwa kupita kwenye kura ya maoni ndani ya CCM, kabla hajawa mgombea rasmi.
Swai ambaye ni kada wa kwanza wa CCM kufungua pazia la kutangaza nia ya kugombea ubunge katika jimbo la Hai, alisema jana kuwa dhamira yake ni kufanya kazi na wananchi ndani ya jimbo hilo, tofauti na sasa ambapo wawakilishi wengi wanaomba kura na wakipata wanahamia Dar es Salam.
Nimeamua kuingia kwenye siasa niendelee kuwatumikia wananchi. Ifike mahali kiongozi anayechaguliwa aishi na wananchi ili ajue shida zao, matatizo yao na changamoto walizonazo na siyo unapewa heshima na wananchi, lakini ukipata huonekani ukiwatumiakia,” Swai.
Alisema iwapo chama kitampa ridhaa ya kugombea, atahakikisha anawaweka vijana pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili likiwemo suala la ajira.
HABARILEO
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema ajali za barabarani zinachangiwa na uzembe wa taasisi inayosimamia sekta ya usafiri jambo linalogharimu maisha ya watu wasio na hatia, na kuitaka taasisi hiyo kuchukua hatua na kuhakikisha nidhamu inarejea kwenye sekta hiyo.
Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) ndiyo yenye dhamana ya kusimamia na udhibiti wa sekta ya usafiri katika nchi kavu na majini.
Sitta aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na waandishi wa habari wakati Kamati ya Bunge ya Miundombinu ilipokuwa ikizungumza na viongozi wa wizara hiyo.
Sitta alisema “Hakuna kitu kinachoniuma kama ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na uzembe, ubovu wa magari na matairi ya mtumba, halafu baya zaidi ni kwamba Mamlaka husika ya kudhibiti vyombo hivyo ipo, inaona na kuwasamehe makosa,” Sitta.
Aliongeza, mamlaka husika zina wajibu wa kusimamia vyombo hivyo na kuhakikisha vile vinavyofanya makosa vinachukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kuvifutia leseni, kwani matukio mengi ya ajali yanatokana na uzembe na kuanzia sasa masuala ya msamaha yasiwepo.
Sitta aliongeza, wamiliki wa vyombo vya moto na madereva, wanapaswa kufuata sheria za barabarani na kuhakikisha wanazitii na kwamba vyombo hivyo vinapaswa kuwa na vipuri vyenye viwango na kuhakikisha mabasi yanayokwenda umbali zaidi ya kilometa 700, yawe na madereva wawili.
“Ipo sheria inayozungumzia umbali unaotakiwa dereva mmoja aendeshe gari, lakini pia nilizungumza na daktari kuhusu umbali unaokubalika kwa madereva kuendesha chombo cha moto, aliniambia dereva mmoja hatakiwi kuendesha gari kwa umbali wa zaidi ya kilometa 700, zaidi ya hapo inabidi wawe madereva wawili,” Sitta.
Alisema hiyo inatokana na ukweli kwamba kwa umbali huo, wa kilometa 700 dereva huwa amechoka na akienda zaidi ya hapo anaweza kusababisha ajali kwa kuwa akili na mwili vimechoka hivyo hawezi kuwa makini barabarani.
Akizungumzia ubovu wa mabasi ya abiria na daladala, Sitta alisema magari yote mabovu, yanapaswa yasiwepo barabarani, kwani kuwepo kunachangia ajali kwa njia moja au nyingine.
Kuhusu mgomo, Sitta alisema nchi inaongozwa kwa sheria na kwamba sio kila kitu kinachofanywa na serikali ni masuala ya siasa, hivyo sio sahihi madereva na wamiliki wa mabasi kugoma kutoa huduma kwa abiria.
HABARILEO
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuamuru Mbunge wa Jimbo la Dimani Zanzibar, Abdallah Sharia Ameir (CCM) kutoa Sh 200,000 kila mwezi kwa ajili ya matunzo ya mtoto wake wa kiume, mwenye umri wa miaka mitatu na nusu, anayedaiwa kumtelekeza.
Pamoja na amri hiyo, Hakimu Mkazi, Hellen Liwa alisema mbunge huyo atatoa kiasi hicho cha fedha kuanzia siku alipokoma kutoa matunzo na matibabu kwa mtoto huyo, anayetajwa kuwa ni mlemavu.
Pia, aliamuru mtoto huyo kulelewa na wazazi wake na siyo bibi yake, kama alivyokuwa akitaka mbunge huyo. Hivyo ataendelea kukaa na mama yake.
Kwa upande wake, Wakili Gideon Mandes aliyekuwa akimtetea Hawa Deus aliyekuwa mke wa mbunge huyo, alisema kupitia hukumu hiyo Mahakama imetoa uamuzi wa haki.
“Kupitia hukumu hii nimebaini wazazi wanawajibu wa kumtunza mtoto wanayemzaa bila ya kujali hali yake hata kama ni ya ulemavu asitelekezwe na imedhihirisha hakuna mtu aliye juu ya sheria na kwamba sheria ipo sawa kwa kila mtu,”.
Wakili huyo aliwashauri Watanzania wenye matatizo na changamoto kama hizo, kuweka bidii ya kuijua sheria na taratibu zake ili waweze kuitumia kupata haki na suluhisho kupitia Mahakama.
Yote haya unayapa hapa hapa tangakumekucablog