Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
MWANANCHI
Hatimaye makada wa CCM wanaotajwa kuwania urais wa Jamhuri ya
Muungano, juzi walipata nafasi ya kutunishiana misuli baada ya kualikwa
kuchangia mfuko wa maendeleo wa mkoa mpya wa CCM wa Magharibi visiwani
hapa.
Edward Lowassa, Mizengo Pinda, Bernard Membe, Makongoro Nyerere, Mark Mwandosya na Steven Wasira
walishiriki kwenye hafla hiyo na kuchangia zaidi ya nusu ya fedha
zilizokusanywa juzi kwa ahadi, hundi na taslimu kwenye harambee hiyo
iliyofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort mjini hapa.
Hata hivyo, pamoja na cheche za makada hao kuonekana visiwani hapa,
Ni Waziri Mkuu Pinda aliyehudhuria harambee hiyo iliyokusanya jumla ya
Sh. milioni 644.54 na ambayo Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alikuwa mgeni rasmi.
Waziri Pinda ndiye aliyetia fora kwenye hafla hiyo baada ya yeye na
marafiki zake kuchangia jumla ya Sh203 milioni, wakati Lowassa, Membe,
Wasira, Dk Shein, Mwandosya, Makongoro, Shamsi Vuai Nahodha na Amina
Salum Ali walichangia jumla ya Sh101.5 milioni.
Makada hao hawakukutana kwa bahati mbaya kwenye hafla hiyo.
“Tuliwapelekea mwaliko maalumu wote waliotangaza nia ya kugombea urais,” alisema mratibu wa shughuli hiyo, Naibu Waziri wa Afya Mahmoud Thabit Kombo kabla ya harambee kuanza.
Kombo alisema si vyema kwa wanachama wa CCM kubaguana wakati viongozi
wakuu wa nchi hawajambagua mtu kwa sababu ya makundi ya wagombea
uongozi.
Kati ya fedha zilizokusanywa, Sh120.7 milioni zilikuwa fedha taslimu,
wakati ahadi zilikuwa Sh490.8 milioni na hundi Sh33 milioni.
Katika hafla hiyo vitu mbalimbali vya asili pamoja na picha za
kumbukumbu za kitaifa, ikiwamo picha ya kuchora ya Rais Dk Shein ambayo
ilinunuliwa kwa Sh23 milioni.
MWANANCHI
MWANANCHI
Tishio la ugaidi limezidi kuwa tete baada ya watu wanaoshukiwa
kufanya vitendo hivyo kulipua bomu na kusababisha watu watano kujeruhiwa
wakati wakitoka kwenye maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi katika Kijiji
cha Msolwa Ujamaa, kilichoko Kata ya Sanje wilayani Kilombero.
Hili ni tukio la pili kutokea kwenye Wilaya ya Kilombero mkoani
Morogoro baada ya watu tisa kukamatwa kwenye Msikiti wa Suni wakiwa na
silaha na vifaa vingine vinavyohusishwa na harakati za kigaidi.
Mbali na matukio hayo ya Morogoro, hivi karibuni vikosi vya ulinzi na
usalama vilipambana vikali na watu wanaoshukiwa kuwa ni magaidi kwenye
mapango ya kihistoria ya Amboni mkoani Tanga.
Hadi sasa polisi haijatoa taarifa ya kina kuhusu tukio hilo lililopoteza maisha ya mwanajeshi mmoja.
Hadi sasa polisi haijatoa taarifa ya kina kuhusu tukio hilo lililopoteza maisha ya mwanajeshi mmoja.
Kamanda wa polisi mkoani Morogoro hakuweza kupatikana kuzungumzia
suala hilo, wakati msemaji wa Jeshi la Polisi alisema tukio hilo liko
ndani ya mipaka ya mkoa hivyo linatakiwa lizungumzwe na mamlaka hiyo
badala ya makao makuu ya chombo hicho cha dola.
Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea walieleza kuwa bomu hilo
lilirushwa kuelekea kwenye gari la mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya
ya Kilombero saa 2:00 usiku.
Bomu hilo lilirushwa na watu wawili ambao awali walidhibitiwa na wananchi baada ya kuwashuku kuwa siyo raia wema.
Bomu hilo lilirushwa na watu wawili ambao awali walidhibitiwa na wananchi baada ya kuwashuku kuwa siyo raia wema.
Baada ya kuwatilia shaka, wananchi waliwaweka watu hao chini ya
ulinzi na wakati wakiwapekua, walitoa bomu na kulirusha kwenye gari hilo
lililokuwa limeegeshwa na kujeruhi watu watano, akiwamo dereva.
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo, David Ligazio aliwataja waliojeruhiwa katika tuko hilo kuwa ni Novatus Ngapi, ambaye ni dereva na Thomas Manjole, ambaye ni mgambo na hali yake inadaiwa kuwa siyo nzuri.
Wengine waliojeruhiwa ni Amos Msopole, Azama Naniyunya,
ambao wamelazwa katika Hospitali ya Mtakatifu Kizito iliyopo Mikumi
wilayani Kilosa na Anna Pius ambaye amepata majeraha kidogo na
kuruhusiwa.
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema
amesema hakuna ubaya Rais Jakaya Kikwete akiachwa kuongeza nchi kwa
muda ili akamilishe mchakato wa Katiba Inayopendekezwa pamoja na Daftari
la Kudumu la Wapigakura.
Hivi karibuni viongozi wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), walidai kuwa Serikali na Tume ya Uchaguzi (NEC) inachelewesha uboreshaji wa Daftari la Wapigakura kwa lengo la kutaka kumwongezea Rais Kikwete muda wa kukaa Ikulu.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema ni
miezi mitatu imebaki kabla ya kampeni za uchaguzi, lakini mpaka sasa
ratiba, majimbo yaliyogawanywa, watumishi wala vituo vya uchaguzi bado
haviwekwa bayana na wala haifahamiki kazi ya uandikishaji katika Daftari
la Wapigakura halijakamilika katika mikoa miwili.
“Hiyo ni hatari sana kwa Taifa.
Tunaionya NEC isijaribu kufanya mbinu zitakazosababisha kuahirishwa kwa
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,” Mbowe.
Mrema alisema yeye ndiye aliyekuwa mtu wa kwanza kutoa wazo la kutaka
Rais Kikwete aongezewe muda zaidi wa kukaa Ikulu kwa kuwa kuna mambo
mengi ambayo ni ya muhimu kwa Taifa yanayotakiwa kukamilika kabla ya
Uchaguzi Mkuu.
Mrema alisema alitoa maoni hayo mwaka jana wakati viongozi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) walipokutana na Rais Kikwete mjini Dodoma, lakini alishangaa kuona viongozi wengine wakipinga wazo hilo.
“Nilitoa ushauri Rais Kikwete
akiwepo. Nilisema tusogeze Uchaguzi Mkuu mbele kwa miaka miwili ili
atuachie nchi ikiwa salama, lakini wapinzani wamejiandaa kuingia Ikulu
waliniona mimi kama bundi,” Mrema.
JAMBOLEO
Waziri wa Nishati na madini George Simbachawene ameiagiza menejmenti ya Shirika la Umeme TANESCO kuwachukulia hatua za kinidhamu wahandisi wa shirika hilo.
Kauli hiyo ilitolewa jana wakati wa
mkutano na watendaji wa Tanesco wa kanda ya Dar na Pwani, ambapo alisema
Muhandisi wa Wilaya ya Temeke, Tabata na Tazara wameshindwa kusimamia
majukumu waliyopewa na Shirika hilo,hivyo amewataka wakurugenzi
wahakikishe wanawahadhibu.
Alisema huo ni mwanzo kwani ataendelea
kuwachukulia hatua watumishi ambao watashindwa kufanyia kazi majukumu
waliyopewa na Shirika katika kuhakikisha wanawapa huduma nzuri
Watanzania.
“Wengine
wakae mguu sawa, huu ni mwanzo tu, sitaki kuwa na watendaji ambao
hawajui wanachokifanya katika vitengo walivyopewa, yeyote atakayeshindwa
kufanya kazi yake ni vyema aachie ngazi” Simbachawene.
Alisema wahandisi watatu aliowatolea
maagizo wachukuliwe hatua za kinidhamu wanamtosha kwani anaamini
litakuwa fundisho kwa wengine.
MTANZANIA
Meli ya Tanzania iliyokamatwa kwenye
bahari ya Kaskazini nchini Marekani ikiwa na tani tatu za dawa za
kulevya aina ya Cocaine ilisajiliwa Zanzibar.
Taarifa iliyopatikana kutoka vyombo ya
habari vya kimataifa ilisema meli hiyo ilikutwa na tani tatu za dawa za
kulevya zenye thamani ya shilingi trilioni 1.5.
Meli hiyo inayojulikana kwa jina la Mv Hamal
ilikamatwa na meli ya kivita ya Uingereza na kikosi chamipaka ikiwa
umbali wa kilometa 160 kuelekea katika Pwani ya Aberdeen nchini Scotland
na ilikuwa ikiendeshwa na waturuki.
Msemaji wa SUMATRA, David Mziray
aamesema wanaendelea kufuatilia kama meli hiyo ilisajiliwa bara ama
visiwani na baadaye alisema wao hawahusiki n usajili wa meli hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya Usafiri Zanzibar Abdi Maalim alikiri kuwa meli hiyo ilisajiliwa Zanzibar kupitia kwa wakala wao aliyepo Dubai.
HABARILEO
Wafanyabiashara wadogo na waendesha
bodaboda wanaofanya biashara zao kwenye njia kubwa za kusafirishia umeme
wapo hatarini kupungukiwa nguvu za kiume.
Kutokana na kuwepo wengi kwenye njia
hizo kubwa za kusafirishia umeme, wametahadharishwa kutoendelea kufanya
biashara kwenye maeneo hayo.
Hayo yalibainishwa jana na Ofisa Mahusiano Msaidizi huduma kwa wateja wa Tanesco Mwanza, Haji Bwegege baada ya uzinduzi wa maonyesho ya siku ya wafanyakazi uliofanywa na Mkuu wa mkoa wa Mwanza, Magesa Mulongo kwenye viwanja vya Furahisha, jijini hapa.
“Tumekuwa
tukiielimisha jamii mara kwa mara kutofanya biashara kwenye njia ya
umeme mkubwa unaopita kutokana na madhara wanayoweza kuyapata na hii ya
kupungukiwa nguvu za kiume ni moja ya madhara ambayo yanaweza kuwapata
hivyo wachukue tahadhari mapema,”
Aliyataja madhara mengine kuwa pamoja na
mwili kupoteza nguvu kutokana na mionzi hivyo wananchi kutakiwa kuishi
umbali wa mita 30 kila upande pamoja na mjamzito kuharibu mimba.
HABARILEO
Wakimbizi 800 kutoka nchini Burundi
wameingia nchini kupitia mkoani Kigoma huku wengine 87 wakirejeshwa
nchini mwao baada ya kuingia nchini kwa kupitia wilayani Ngara mkoani
Kagera.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya ndani ya Nchi, Isack Nantanga
alisema wakimbizi hao wameingia nchini kwa makundi madogo madogo na
watahifadhiwa kwa muda karika kambi ya wakimbizi ya Nyarugusu.
Nantanga alisema wakimbizi wanaofikia
800 wameshaingia nchini huku walioingia kupitia mkoani Kagera ilibidi
warejeshwe walipotoka kutokana na kukiuka sheria za kimataifa kwa
wakimbizi kuingia nchi nyingine wakivuka nchi moja.
Alisema hawapokei wakimbizi wanaotokea
Rwanda kutokana na kuwa sheria za kimataifa haziruhusu wakimbizi kuvuka
nchi moja ndiyo maana waliwarejesha wakimbizi hao.
Alisema kati ya wakimbizi hao
waliopokelewa mkoani Kigoma wameingia kupitia vijijini ambapo serikali
za vijiji wanawapokea na kuwahoji kisha kuwapleka kigoma mjini kwenye
kituo maalum.
Alisema serikali za vijiji na wilaya kwa
kushirikiana na halmshauri wamekuwa wakaifanya kazi ya kuwahoji kujua
sababu hasa ya kuwafanya wakimbilie nchini humu kwani isije kutumika
vurugu za Burundi watu kuingia nchini.
“Serikali
kwa kushirikiana na Shirika la umoja wa mataifa la kuhudumia wakimbizi
(UNHCR) baada ya kuwahoji na kuwapa misaada muhimu wanaobainika kupata
hifadhi wana mpango wa kuwapeleka kwenye kambi ya Nyarugusu kwa muda,”alisema.
Msemaji huyo alisema baada ya kuhifadhiwa katika kambi hiyo mipango inaendelea kufahamu njia nyingine za kuwahifadhi.
Wengi wa wakimbizi hao wametokea mji wa
Bujumbura na wameingia Kigoma kwa usafiri wa boti kupitia bandari ndogo
ya Kibirizi mjini Kigoma.
Inaelezwa kuwa kundi kubwa la wakimbizi
liliingia nchini juzi katika mpaka wa Tanzania na Burundi kwenye kijiji
cha Kagunga mwambao wa kaskazini wa ziwa Tanganyika ambapo kundi la
wakimbizi 200 waliingia kupitia kijiji hicho.
Tayari wakimbizi 68 ambao waliingia na
kufikia kambi ya muda ya NMC kibirizi mjini Kigoma wamepelekwa kwenye
kambi ya Nyarugusu wilayani Kasulu ambayo kwa sasa ndiyo kambi pekee
mkoani Kigoma inayohifadhi wakimbizi.
Akizungumzia kuingia kwa wakimbizi
mkoani humo Mkuu wa mkoa Kigoma, Issa Machibya alisema kuwa wameanza
kupokea wakimbizi kutoka vijiji mbalimbali vya wilaya za Buhigwe,Kasulu
na Kibondo ambao wanakimbia hali ya machafuko nchini Burundi.
Machibya alitaja maeneo ambayo hadi sasa
yamekuwa yakipokea wakimbizi hao kuwa ni pamoja na Kijiji cha Kagunga
wilaya ya Kigoma, Muyama,Kibande na Kilelema ambavyo vyote vipo katika
wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
Kuingia kwa wakimbizi wa Burundi nchini
Tanzania kunatokana kuanza kwa machafuko nchini humo kati ya wananchi
wanaopinga kitendo cha Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunzinza kuongoza
muhula wa tatu wa uongozi dhidi ya polisi na wanajeshi wanaomtii raisi
huyo.
Kwa siku mbili mfululizo kumekuwepo na
taarifa za kuchomwa mwa mabasi mawili ya abiria na moja kulipuliwa kwa
bomu la kurushwa kwa mkono huku kukiwa na vifo vya watu kadhaa kutokana
na makabiliano ya waandamanaji na polisi.
Wageni wamekuwa wakizuiliwa kuingia mji
mkuu wa Burundi, Bujumbura ambako kwa kiasi kikubwa maandamano ya
kupinga hatua ya Rais Nkurunzinza kuongoza muhula wa tatu yanaendelea
ambapo kwa sasa maandamano hayo yameanza kusambaa mikoa ya jirani na mji
Mkuu wa Bujumbura.
NIPASHE
Agizo la serikali la kupiga marufuku
uingizaji wa mabehewa ‘feki’ ili kuliokoa taifa dhidi ya ufisadi na
ajali zinazogharimu mali na maisha ya watu, limepuuzwa baada ya Kampuni
ya Reli (TRL) kupokea mabehewa 47, mwanzoni mwa wiki iliyopita.
Mabehewa hayo ni sehemu ya yaliyoanza
kuingizwa nchini, Julai 24, mwaka jana na kupokelewa na aliyekuwa Waziri
wa Uchukuzi wa wakati huo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Hata hivyo, serikali kupitia kwa Waziri
wa Uchukuzi, Samwel Sitta, ilizuia uingizwaji wake, Aprili 16, mwaka
huu, kwa madai kuwa hayana ubora.
Akitangaza uamuzi wa kuzuia mabehewa
hayo, Sitta alisema baada ya bodi kupitia taarifa hiyo, ilibaini
mabehewa mengi kati yaliyoagizwa yalikuwa na kasoro, kuwepo kwa uzembe
katika uagizaji na ufuatiliaji kuanzia kiwandani na kuwapo kwa uzembe
katika mchakato wa kuyapokea.
Sitta alisema kilichowashtua ni kubaini ukiukwaji mkubwa wa masharti ya mkataba wa ununuzi ambao ulipangwa kufanyika kwa awamu.
Alisema katika makubaliano ya ununuzi wa
mabehewa hayo, malipo yalitakiwa yafanywe kwa awamu kwa kuanza na
asimilia 50 awamu ya kwanza, asilimia 40 awamu ya pili na awamu ya
mwisho ya malipo ilikuwa ni asilimia 10.
Hata hivyo, wiki mbili tangu Sitta atoe
agizo hilo, gazeti hili limebaini kuwa mabehewa 47 yaliingizwa nchini na
kuhifadhiwa kwenye karakana ya Malindi jijini Dar es Salaam.
Chanzo hicho kimesema inavyoonyesha
mkataba wa kuyaleta mabehewa hayo haujavunjwa ndio maana yamewasili tena
licha ya Waziri Sitta kusema yaliyobaki yasiingie nchini.
Mabehewa hayo ni kati ya 274, ambapo 150 yalishaingizwa nchini na mengine 124 yalizuiliwa.
Sakata la ununuzi wa mabehewa hayo
limesababisha serikali hasara ya Sh. bilioni 230. Kufuatia sakata hilo
Sitta aliwasimamisha kazi vigogo watano kutokana na kubainika kuihujumu
serikali.
Waliosimamishwa ni Mkurugenzi Mtendaji, Kipallo Kisamfu, Mhandisi Mkuu wa Mitambo, Ngosomwile Ngosomiles, Mhasibu Mkuu, Mbaraka Mchopa, Mkaguzi Mkuu wa Ndani, Jasper Kisiranga na Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinarnd Soka.
NIPASHE
Wakati serikali ikijitetea kuwa kushuka
kwa shilingi ya Tanzania kunatokana na kuimarika kwa dola ya Marekani,
Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila ametaja sakata la Escrow kuchangia pia anguko hilo.
Kafulila alisema hayo jana alipozungumza
na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, wakati wa kikao cha
Kamati ya Bunge ya Uchumi, Viwanda na Biashara, iliyokutana na Wizara ya
Fedhana mamlaka zake.
Alisema, kwa mujibu wa maelezo ya Gavana wa Benki Kuu (BoT), Profesa Benno Ndulu,
sababu za kushuka kwa shilingi ni kuimarika kwa dola ya Marekani na
kusababisha sarafu zote duniani kuathirika katika mbadilishano na dola.
Aidha, sababu nyingine ni uhaba wa dola uliosababishwa na kukosekana kwa fedha za wafadhili.
Kafulila alisema misaada iliyokuwa inatarajiwa kutoka kwa wahisani imekwama kutokana na sakata la Escrow.
Alisema mikopo ya kibiashara ambayo
Tanzania ilikuwa ikitarajia kupata dola milioni 800, imekatwa na
kutolewa dola milioni 300, tafsiri inayoonyesha kuwa Tanzania
haiaminiki.
Alisema fedha za wafadhili zaidi ya Sh.
tirioni 1.0, sawa na dola milioni 740, hazijaidhinishwa kupewa Tanzania
na mwaka jana Wizara ya Fedha ilisema zitaidhinishwa Desemba, mwaka
jana.
“Mwaka
huu wanazungumzia labda zitasainiwa Septemba tafsiri yake ni kwamba
hiyo hela ambayo ni sawa na tirioni 1.5 haitaletwa hadi hatua
zichukuliwe kwenye jambo la Escrow,” Kafulila
Hata hivyo, alisema mikopo ya biashara ya dola milioni 500-800 iliyoahidiwa kuletwa imekwama kwa sababu ya sakata la Escrow.
Alisema tatizo la serikali ni kusema hatua zimechukuliwa wakati, IPTL inalipwa zaidi ya Sh bilioni 5 kila mwezi, kama tozo ya uzalishaji (Capacity Charge).
Kama kawaida tangakumekuchablog inakuta yote yaliyoandikwa katika magazeti, ni hapa hapa
No comments:
Post a Comment