Uchambuzi huu unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, Kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita na wale ambao wanajiendeleza kielimu. Pia wanatoa kozi ya Kiingereza na Computer na kutoa Certificate. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746
MWANANCHI
Kwa mara nyingine, Jina la nchi
limeendelea kuchafuka baada ya Meli ya MV Hamal iliyosajiliwa Tanzania
kukamatwa Ulaya ikiwa imebeba shehena ya dawa za kulevya aina ya cocaine
yenye uzito wa tani tatu, kama dawa hizo zingeuzwa mitaani nchini
Uingereza zingekuwa na thamani ya Sh1.5 trilioni, kiasi ambacho nchi
wafadhili zinatarajiwa kuichangia Tanzania kwenye bajeti ya mwaka
2015/16.
Mwaka 2013 meli ya mizigo ya Gold Star
iliyosajiliwa Tanzania ambayo ilikamatwa Septemba 2013 katika bahari ya
Mediterranian, Italia wakati ikielekea Uturuki ikiwa na tani 30 za
bangi zenye thamani ya Pauni 50 milioni za Uingereza (sawa na Sh125
bilioni).
Kiwango hicho cha dawa zilizokamatwa kimeweka rekodi ya ukubwa wa mzigo wa dawa hizo haramu zilizowahi kukamatwa Uingereza..
“Upekuzi
wa meli ulikuwa mrefu na unaosababisha maumivu, na uliofanywa na watu
wenye utalaamu mkubwa wa kufanya kazi kwenye mazingira magumu”—alisema John McGowan, afisa mwandamizi wa Uchunguzi wa NCA.
Rekodi za mtandao wa shughuli za
baharini unaonyesha kuwa katikati ya Februari, meli hiyo ilikuwa Uturuki
na wiki mbili zilizopita ilianza safari kutoka visiwa vya Tenerife,
Hispania.. ilipokamatwa ilikuwa inaelekea Hamburg, mji wa pili kwa
ukubwa nchini Ujerumani ambako ingefika jana usiku.
Meli hiyo imekutwa na watu tisa wenye
umri kati ya miaka 26 na 63 wote raia wa Uturuki na wameshitakiwa kwa
kukutwa na dawa za kulevya.
JAMBO LEO
Chama cha Wamiliki wa Mabasi TABOA
kimesema uwepo wa mizani ya kupima mizigo ya Kibaha imekuwa sababu
mojawapo kubwa ya madereva kwenda mwendokasi ili kufidia muda mwingi
ambao wanaupoteza kwenye mizani hiyo.
“Hii
mizani mpya imekuwa ni tatizo kwetu, imekuwa ikichangia dereva kuendesha
mwendo mkali kwani katika kupima mizani pale unachukua muda mrefu kukaa”—Enea Mrutu, Katibu Mkuu TABOA.
Alisema kwamba katika Kamati ambayo
waliunda kuchunguza tatizo hilo la ajali wamegundua kwamba mwendo kasi
pamoja na mizani hiyo vimechangia tatizo la ajali.
JAMBO LEO
Viongozi wa CHADEMA Rungwe, Mbeya
wametwangana makonde mkutanoni baada ya kupishana kauli kwa kila mmoja
kumpigia chapuo mtia nia ya Ubunge na kusababisha mmoja wao kuchanwa uso
na kushonwa nyuzi sita.
Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye
alijeruhiwa amesema kisa cha ugomvi huo ni mgogoro wa maslahi binafsi
anayoyaendekeza Katibu Uenezi wa Wilaya.
Kisa cha mgogoro wao ni suala la CHADEMA
kupata nyumba ya kupanga ambayo wanaitumia kama ofisi, viongozi wote
walichanga pesa kwa ajili ya ofisi hiyo lakini kiongozi mmoja ambaye ni Godogo aligoma akitaka ofisi hiyo ihamie nyumbani kwake kitu ambacho Kamati ilikataa.
Katibu wa Chama hicho Wilaya hiyo, Nsajigwa Bonifas amekiri kutokea tukio hilo na kusema ni kitendo cha aibu japo haweza kuzungumzia zaidi kwa sasa.
HABARI LEO
Wakati wateja wa umeme wameendelea
kutaabika, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limetoa malekezo zaidi
ya namna ya upatikanaji wa huduma hiyo kwa urahisi.
Taarifa ya Tanesco imekuja baada ya
tatizo lililojitokeza kwa baadhi ya mawakala wa LUKU kushindwa kutoa
huduma ya kuuza umeme kutokana na Kampuni ya SELCOM ambaye ni wakala wa
kuuza na kuziunganisha baadhi ya kampuni za simu kwa TANESCo kusitishiwa
huduma kutokana na kile kilichoelezwa kushindwa kutekeleza baadhi ya
majukumu yake ikiwamo kughushi nyaraka na kukiuka taratibu za kulipa
kodi.
Taarifa iliyotolewa jana na shirika
hilo, na kusainiwa na Ofisa Habari wake, Adrian Sevelin ilisema kuwa
huduma zinaendelea kupatikana kupitia Makampuni mengine na huduma za
Mabenki.
“Shirika linaomba radhi kwa usumbufu wowote unaojitokeza, wanafanya kila linalowezekana kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa”– alisema Adrian Sevelin, Afisa Uhusiano wa TANESCo.
Gazeti la HABARI LEO lilizunguka katika
vituo mbalimbali vya kutoa huduma hiyo na kukuta misululu ya wananchi
wakisubiri huduma hiyo huku kukiwa na tatizo la mtandao.
MTANZANIA
Mwenendo wa uchunguzi wa madai ya Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Slaa kutaka kuuawa na mlinzi wake binafsi, Khalid Kangezi,
umezua shaka kutokana na ukimya wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar
es Salaam ambapo kwa zaidi ya mwezi mmoja limeshindwa kuwahoji
watuhumiwa waliotajwa.
Uchunguzi wa gazeti la MTANZANIA umebaini Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula pamoja na Katibu Mkuu wa chama hicho, Abdulrahman Kinana ambao kwa pamoja wanashutumiwa kula njama ya kutaka kumzuru Dk. Slaa,hawajahojiwa.
“Si
Mangula wala Kinana aliyehojiwa.. inasikitisha kuona watu walioendesha
njama ya kutaka kuteketeza maisha yangu wanaendelea kuranda randa pasipo
hatua yoyote kuchukuliwa,” alisema Dk. Slaa.
Alipotafutwa Philip Mangula
ili athibitishe kama ameshahojiwa na Jeshi la Polisi au la, alishindwa
kukataa wala kukubali badala yake alimwambia mwandishi kuwa yupo kwenye
kikao na hata alipotafutwa Kinana simu yake haikupatikana.
“Ngoja niulize wasaidizi wangu…Lakini kwanini umeniuliza swali hilo wakati sipo ofisini? Nitafute Jumatatu,” alijibu Kamishna Kova baada ya kuulizwa kuhusu suala hilo.
Hutopitwa na habari yoyote inayonifia na niko tayari kukutumia muda wowote kupitia hapa hapa tangakumekuchablog.com
No comments:
Post a Comment