Monday, April 3, 2017

KILIMO CHA UMWAGILIAJI AMBONI TANGA



Mkulima wa mbogamboga shamba la Mkurumuzi Amboni Tanga, Robarts Jonathan, akimwagilia maji katika shamba lake la mbogamboga na nafaka.
Kufuatia uhaba wa mvua wakulima wengi wanalazimika kuchiota maji ya mito kumwagilia mbogamboga zao.







MAHARAMIA WATEKA MELI PWANI YA SOMALIA

maboti bahariniTaarifa kutoka Somalia zinasema maharamia wa Kisomali wameiteka meli ya mizigo ya India.
Kumezuka utata kuhusu eneo halisi ambako meli hiyo ya kutoka India ilikotekwa.
Baadhi ya vyombo vya habari nchini vinaarifu kuwa tukio hilo linaarifiwa kutokea Somalia ya kati, eneo la Elhur kiasi ya kilomita 50 kusini mwa Hobyo, eneo ambalo miaka michache iliyopita lilikuwa ndio kitovu cha maharamia wa Kisomali.
Kaimu rais wa eneo la Galmud, Somalia ya kati ameithibitishia BBC kwamba meli ya mizigo imetekwa siku ya Jumamosi karibu na eneo la Haradhere.
Ameeleza kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Kismayo.
Wakati huo huo maafisa huko Puntland wanasema utekaji huo umefanyika katika eneo lao.
Inaarifiwa kuwa meli hiyo ilikuwa inaelekea Yemen kutoka India wakati ilipotekwa na ina mabaharia 11 ndani.
Mapema mwezi uliopta maharamia katika eneo la Puntland waliiteka meli ya mafuta ambayo baadaye waliachia huru.
Kilikuwa ni kisa cha kwanza cha uharamia kushuhudiwa tangu 2012.
BBC

MSHIKAJI WA SAMATTA ATAKIWA KUKIPIGA EMMARATIES

Mshikaji wake Samatta ameripotiwa kuhitajika na Man United na Arsenal

Kuelekea kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu England na kuelekea kipindi cha usajili cha majira ya joto, tayari majina ya wachezaji wanaonekana kufanya vizuri yameanza kuhusishwa kujiunga na timu fulani, Wilfred Ndidi ambaye alijiunga na Leicester City January akitokea KRC Genk ya Ubelgiji jina lake limerudi kwenye headlines za usajili tena.
Kutoka kushoto ni Ndidi, Omar Colley na Mbwana Samatta
Ndidi ambaye ana miezi michache toka ajiunge na Leicester City akitajwa kama mbadala sahihi wa kiungo N’golo Kante aliyejiunga na Chelsea, ameanza kuripotiwa kuhitajika na timu za Arsenal na Man United, mtandao wa 90min.com umeripoti timu hizo kuanza kumfuatilia kwa karibu kutokana na kiwango chake.
Kumordizi, Samatta na Ndidi
Wilfred Ndidi ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa KRC Genk waliyompokea Samatta wakati anajiunga na timu hiyo mwaka 2016, kutokana na Ndidi kutokea Nigeria, Omar Colley kutoka Gambia na Samatta kutokea Tanzania wameonekana mara kadhaa kuwa karibu hiyo inatokana na wote kutokea Afrika.
Samatta, Ndidi na Nikolaos Karelis wakiwa uwaja wa ndege Cork wakati wakicheza pamoja
milardayo

ADONOLEWA NA KUKU NA KUPATA KILEMA CHA MAISHA



Maryam Abrahman (kushoto) akionyesha mkono wa mume wake, Abdalla Nassir, wakazi wa kijiji cha Mtimbwani Wilayani Mkinga Mkoani Tanga  wenye makovu uliopata kilema baada ya kung’atwa na kuku na kumsababishia kilema cha mkono kupinda.
Kijana huyo mwenye ndoto ya maendeleo alipatwa na mkasa huo na kwa sasa amepata kilema cha mkono wa kushoto ambao umepinda na haufanyi kazi ya aina yoyote.
Akisimulia mkasa huo kwa umakini na utulivu alisema alishangazwa na kuku huyo kumdonoa ambapo hakusikia maumivu yoyote zaidi ya ubaridi ambao ulimshangaza.
Alisema ubaridi huo ulidumu kwa hadi siku ya pili asubuhi wakati alipoamka na kusikia maumivu ambayo familia yake na yeye pia walishangaa.
Aliongeza na kusema kuwa wakati wa kutafuta tiba alipanda milima na mabonde na mwisho kugundua kuku huyo hakuwa kuku wa kawaida.
Alibainisha na kuongeza kuwa kama kuku huyo angemchelewesha kidogo kumuuza angelimuweka na  kila siku angemuliza "Kwanini amenipatia kilema cha maisha" 




ARSENAL WENGER LICA YA SHINIKIZO, AWASIFU WASHABIKI WA ARSENAL

ArsenalMeneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema mashabiki wa klabu hiyo walikuwa wazuri sana wakati wa mechi dhidi ya Manchester City ambayo iliisha kwa sare ya 2-2 uwanjani Emirates.
Amesema hayo licha ya kwamba bado wapo mashabiki walioandamana kumpinga wakati wa mechi hiyo ya Jumapili.
Wenger, ambaye anakabiliwa na shinikisho baada ya kushindwa mechi moja pekee kati ya sita walizocheza karibuni amekuwa akitakiwa na baadhi ya mashabiki ajiuzulu.
"Lazima niseme kwamba, licha ya yote yaliyofanywa na baadhi ya mashabiki, mashabiki wetu walikuwa wazuri sana leo," alisema Mfaransa huyo baada ya mechi.
Arsenal, ambao wameshuka hadi nafasi ya sita kwenye Jedwali, walitoka nyuma mara mbili kulazimisha sare hiyo dhidi ya vijana hao wa Pep Guardiola.
"Katika nyakati ngumu sana, tukiwa 1-0 chini na 2-1 chini, wangetugeuka lakini nafikiri walikuwa wazuri sana na walituwezesha kupitia vipindi hivyo vigumu."
BBC

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990



Sunday, April 2, 2017

SIMULIZI, NIMEKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU SEHEMU YA 3

SIMULIZI
 
NIMEKIONA CHA MOTO URITHI WA BABU 3
 
Alinisalimia kwa Kingreza kwa kutumia jina la marehemu babu yangu. Na yeye nikamjulisha kuwa Mzee Fumbwe alikuwa amefariki dunia na kwamba mimi nilikuwa mjukuu wake.
 
“Ulikuwa unataka nini?” akaniuliza.
 
“Kumbukumbu za babu zinaonesha kwamba anakudai dola milioni moja na laki tano. Mikataba yenu  ninayo hapa. Mimi ndiye mrithi wake”
 
Simu ya upande wa pili ikawa kimya. Nilipoona amenyamaza nilimwambia.
 
Ninazo hati za mahakama zinazothibitisha kuwa mimi ndiye mrithi wa marehemu. Nina cheti cha kifo chake na nina mkataba wa makubaliano yenu”
 
“Utakuja kunionesha?” Benjamin akaniuliza.
 
“Nitakuja kukuonesha ili uthibitishe kuwa Mzee Fumbwe amefariki na kwamba mimi ndiye ninayepaswa kulipwa madeni yake”
 
SASA ENDELEA
 
“Utakuja lini?”
 
“Nitakujulisha siku ambayo nitakuja”
 
“Sawa”
 
Nikakata simu kisha nikampigia Dumessan Dube wa Afrika Kusini.
 
Yeye nilizungumza naye kama nilivyozungumza na wenzake lakini yeye hakushangaa nilipomwambia Mzee Fumbwe amefariki. Aliniambia ameshapata habari.
 
“Umepata habari hiyo kutoka wapi?” nikamuuliza.
 
“Nimeipata kutoka kwa marafiki mbalimbali ambao anafanya nao biasharara”
 
“Ni vyema kama umeshapata habari. Kwa hiyo mimi ndiye mrithi wake. Nimekuta una deni la dola milioni tatu ambazo babu anakudai”
 
“Umelikuta wapi deni hilo?”
 
“Kwenye kumbukumbu zake na mkataba wenu wa makubaliano pia ninao hapa”
 
“Sawa” Dube aliniambia baada ya kimya kifupi kisha akaniuliza.
 
“Sasa ulitakaje?”
 
“Nimeona tarehe ya malipo ya hizo pesa imeshapita. Nilitaka nije Afrika  Kusini unipatie pesa hizo. Nitakuja na hati zote”
 
Baada ya kimya kingine kifupi, Dube aliniambia.
 
“Sawa. Unatarajia kuja lini?”
 
“Nitakujulisha”
 
“Sawa”
 
Kusema kweli baada  ya kuzungumza na wafanyabiashra hao waliokuwa nje ya nchi nilifarijika sana. Yule mfanyabiashara aliyekuwa Dar es Salaa ambaye simu yake ilikuwa haipatikani nilimuacha kiporo.
 
Niliona sasa urithi wa babu ulikuwa unakuja mikononi mwangu taratibu. Nikajiambia kama pesa hizo nitazipata zote ningekuwa miongoni mwa matajiri wakubwa katika jiji hili.
 
Nilimshangaa marehemu babu yangu kwa kuacha kiasi kikubwa cha pesa  nje ya nchi bila kunishirikisha mimi mjukuu wake. Kwa kweli alikuwa msiri sana na pia alikuwa tajiri japokuwa mali alizokuwa akimiliki hapo Dar bado zilikuwa ni kitendawili.
 
Sikwenda kumueleza wakili kuhusu madeni hayo. Niliacha yabaki kuwa siri yangu. Sasa nikaanza kujiandaa kwa safari ya nchi hizo tatu huku ndoto za utajiri zikiwa zimetawala akili yangu.
 
Baada ya wiki mbili nikawa nimeshapata pesa za kuniwezesha kuzuru katika nchi hizo. Mipango yangu ya safari ilipokamilika nikaanza safari yangu. Kwanza nilipanga kwenda Harare Zimbabwe. Kabla ya kuondoka  nilimpigia simu Isaac Chusama kumjulisha kuwa ninakwenda Zimbabwe.
 
“Sawa. Ukifika utanipigia simu kunijulisha kuwa umefika” akaniambia.
 
“Sawa”
 
Nilifika Harare kama saa nane mchana. Nikiwa katika kiwanja cha ndege cha Harare nilimpigia simu Chusama kumjulisha kuwa nilikuwa uwanja wa ndege wa Harare. Nilitumia simu ya malipo iliyokuwa pale kiwanja cha ndege.
 
“Kama umeshafika kodi teksi. Mwambie dereva akupeleke Chapachapa Hotel. Nimekukodia chumba namba 35”
 
“Natumaini madereva wa teksi watakuwa wanaifahamu ilipo hoteli hiyo”
 
“Wanaifahamu. Ni hoteli maarufu”
 
“Sawa. Ngoja nikodi teksi”
 
Baada ya kumaliza kuzungumza na mwenyeji wangu huyo nilitoka nje ya uwanja wa ndege na kukodi teksi. Sasa nilikuwa natumia kingereza kitupu.
 
Nilimwammbia dereva wa teksi anipeleke Chapachapa Hotel. Baada ya mwendo wa saa moja kasorobo akanifikisha katika hoteli hiyo iliyokuwa katikati ya jiji la Harare.
.
Baada ya kumlipa dereva pesa aliyotaka niliingia hotelini humo. Unapoingia unakutana na ukumbi mwanana uliokuwa na viti na meza.
 
Kwenye meza moja iliyokuwa karibu na mlango aliketi msichana mmoja mrembo aliyekuwa akinywa soda huku akisoma gazeti. Upande wa kushoto wa ukumbi huo ndio palikuwa mapokezi.
 
Nikaenda hapo mapokezi na kujitambulisha kuwa nilikuwa mgeni wa Isaac Chusama na kwamba aliniambia kuwa amenikodia chumba namba 35.
 
“Oh ndiye wewe! Hebu lete paspoti yako tuione” Mhudumu wa mapokezi ambaye alikuwa msichana akaniambia.
 
Nikampa paspoti yangu iliyokuwa mkononi kama kitambulisho changu huku tukizungumza Kiingereza.
 
Baada ya kuifungua paspoti yangu na kuiona picha yangu alinirudishia.
 
Nikapelekwa chumba namba 35 kilichokuwa ghorofa ya kwanza. Nilikuta kiyoyozi, tv na simu ya mezani iliyowekwa kwenye kimeza kilichokuwa kando ya kitanda. Pia kulikuwa na  kochi moja refu na kabati la  kuwekea nguo pamoja na meza ya kuvalia iliyokuwa na kioo kikubwa.
 
Nilipoona ile simu niliweka begi langu juu ya kochi nikaketi kitandani na kuinua mkono wa simu.
 
Simu zilikuwa zinapitia kwa opereta aliyekuwa hapo hoteli ambaye alipopokea simu yangu nilimpa namba ya Isaac Chussama.
 
Sekunde chache tu baadaye nikaisikia sauti ya Chusama.
 
“Helow!”
 
“Mimi ni yule mgeni wako kutoka Tanzania, nimeshafika katika hoteli ya Chapachapa”
 
“Umepewa chumba?”
 
 
ITAENDELEA kesho Usikose Uhondo huu nini kitatokea baada ya kuwasili Harare na kutinga katika hoteli

Saturday, April 1, 2017

WATU 250 WAPOROMOKEWA NA GOROFA , WAHOFIWA KUFA, COLOMBIA

Watu 250 waangamia kwenye maporomoko ya ardhi ColombiaWatu 250 waangamia kwenye maporomoko ya ardhi ColombiaWatu 250 waangamia kwenye maporomoko ya ardhi ColombiaMamlaka ya jeshi la Colombia inasema idadi ya waliofariki katika maporomoko ya ardhi nchini humo imefikia watu 250 huku waliojeruhiwa wakiwa 400.
Hata hivyo idadi hiyo huenda ikaongezeka kwani bado kuna zaidi ya watu 200 ambao hawajapatikana .
Vikosi vya wafanyikazi wanaoendesha shughuli za uokoaji wanasema nyingi ya barabara za kulipotekea maporomoko hayo huko eneo la mji wa kusini mwa taifa hilo, Mocoa hazipitiki kutokana na mkasa huo.
BBC

AMKA NA MAGAZETI NA FREYS LUXURY COACH TANGA HADI SINGIDA KILA SIKU, 0622 292990


Magazetini leo Jumapili Aprili 2,2017

LIVAPOOL YAITANDIKA EVARTON BAO 3 , 1

Liverpool yaitandika Everton 3-1Liverpool iliongezea matumaini ya kuendelea kusalia katika kundi la timu nne bora baada ya kuwatandika Everton mabao 3-1 katika Champions League.
Sadio Mane aliwapa Liverpool bao la mapema kufuatia ushirikiano mzuri na Roberto Firmino.
Bao la pili lilifungwa na Philipe Coutinho baada ya kuwabwaga wachezaji wawili wa Everton.
Matokeo hayo yanaipa Liverpool uongozi wa pointi 7 mbele ya  Manchester United, ambao wana mechi tatu za kucheza, ikiwemo ya nyumbani dhidi ya West Brom siku ya Jumapili.

SOKONI MLANGO WA CHUMA MASIWANI TANGA

 Wafanyabiashara wa mbogamboga na matunda soko la Mlango wa Chuma Masiwani Tanga wakipanga bidhaa zao kusubiri wateja, Msimu huu wa matunda na mbogamboga wafanyabiashara wamedai kukosa soko baada ya watu wengi kulalamika ugumu wa maisha hivyo biashara kuwawia ngumu.
Tangakumekucha ilifika sokoni hapo na kujionea matunda nanmbogamboga zikiwa zimezagaa baada ya kukosa sokona na kuwa na hofu ya kuwaozea mikononi.