Mshikaji wake Samatta ameripotiwa kuhitajika na Man United na Arsenal
Kuelekea kumalizika kwa msimu wa Ligi Kuu
England
na kuelekea kipindi cha usajili cha majira ya joto, tayari majina ya
wachezaji wanaonekana kufanya vizuri yameanza kuhusishwa kujiunga na
timu fulani,
Wilfred Ndidi ambaye alijiunga na
Leicester City January akitokea
KRC Genk ya
Ubelgiji jina lake limerudi kwenye headlines za usajili tena.

Kutoka kushoto ni Ndidi, Omar Colley na Mbwana Samatta
Ndidi ambaye ana miezi michache toka ajiunge na
Leicester City akitajwa kama mbadala sahihi wa kiungo
N’golo Kante aliyejiunga na
Chelsea, ameanza kuripotiwa kuhitajika na timu za
Arsenal na
Man United, mtandao wa
90min.com umeripoti timu hizo kuanza kumfuatilia kwa karibu kutokana na kiwango chake.

Kumordizi, Samatta na Ndidi
Wilfred Ndidi ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa
KRC Genk waliyompokea
Samatta wakati anajiunga na timu hiyo mwaka 2016, kutokana na
Ndidi kutokea
Nigeria,
Omar Colley kutoka
Gambia na
Samatta kutokea
Tanzania wameonekana mara kadhaa kuwa karibu hiyo inatokana na wote kutokea Afrika.

Samatta, Ndidi na Nikolaos Karelis wakiwa uwaja wa ndege Cork wakati wakicheza pamoja
milardayo
No comments:
Post a Comment