Full time ya Liverpool VS Stoke City imeisha hivi…
Vilabu vya Liverpool na Stoke City jioni ya leo vimefunga jalada la mechi ya Barclays Premier League katika siku ya Jumapili August 09 2015 kwa mchezo mkali kati ya Vigogo hao.
Liverpool waliingia kwenye mechi hiyo wakiwa na kumbukumbu ya kupigwa 6-1 msimu uliopita, waliuanza mchezo kwa kasi lakini ngome ngumu ya Stoke iliweza kuhimili mikimikiki mpaka kipindi cha kwanza kilipomalizika.
Kipindi cha pili Liverpool walimuingiza mshambuliaji wao mpya Robert Firmino ambaye alishirikiana vizuri na Mbrazil mwenzie Coutinho katika mashambulizi ya Liverpool… zilipobaki kama dakika 4 kabla ya mchezo kumalizika, Coutinho alifunga goli pekee na la ushindi kwenye mchezo huo.
Kwa habari, matukio na michezo ungana nami hapahapatangakumekuchablog.
No comments:
Post a Comment