Pichaz 18 za Makocha wa zamani Ligi Kuu Uingereza ambao walikuwa Wachezaji pia…
Makocha wa timu za ligi kuu ya England wengi wao wamewahi kucheza soka katika ngazi ya juu wakitumikia klabu kubwa na zile za madaraja ya kati na hata timu za Taifa huku wakishiriki Michuano mikubwa kama Kombe la Dunia , Ligi Kuu ya England, michuano ya Kombe la Ulaya na mingine mingi.
Katika makocha wanaofundisha timu za ligi ya England kocha wa Aston Villa, Tim Sherwood amewahi kutwaa Ligi hiyo akiwa mchezaji wa klabu ya Blackburn Rovers katika msimu wa mwaka 1994/95.
Hapa Sherwood alikuwa nahodha wa kikosi cha Blackburn Rovers kilichotwaa ubingwa wa Ligi ya England.
Kocha wa Tottenham Hotspurs, Mauricio Pochettino aliwahi
kuwa sehemu ya timu ya taifa ya Argentina akishiriki kwenye Kombe la
Dunia ambapo alikuwa sehemu ya idara ya kiungo kwenye timu hiyo.
Hapa Pochettino alikuwa kiungo wa timu ya Taifa ya Argentina kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 1998.
Kocha wa Crystal Palace, Alan Pardew aliwahi kuichezea timu hiyo na aliwahi kuifungia bao muhimu kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la FA dhidi ya Liverpool kabla ya kufika hatua ya fainali ambapo walifungwa na Manchester United.
Picha inayoonyesha makocha 18 wa timu 18 za EPL enzi zao wakiwa kwenye nafasi zao kama Makocha na Wachezaji pia.
No comments:
Post a Comment