HADITHI
NILIJUA NIMEUA (6)
ILIPOISHIA
“Wafukuze wapangaji wote
halafu uikarabati hii nyumba” nikamwambia.
“Unataka tuishi peke yetu?”
“Ndiyo. Sitaki kero. Chumba
kimoja uweke sebule”
“Kwa vile nakupenda nitafanya
hivyo”
Baada ya wiki moja
nikaufanyia kazi ushauri wa Halima. Niliwapa notisi wapangaji wote,
nikaikarabati nyumba na kuweka chumba kimoja kama
sebule.
Nilikuwa na shamba langu la
minazi. Fedha nilizopata kutokana na mauzo ya nazi zilinisaidia sana kukamilisha nyumba
yangu.
Halima aliendelea
kunitembelea mara kwa mara. Alipohakikisha nimetimiza matakwa yake akanielekeza
kwa wazazi wake nipeleke barua ya uchumba.
Wazazi wa Halima walikuwa
wakishi Pongwe, mwendo wa karibu kilometa kumi na tano kutoka Tanga mjini. Baba
yake Halima mzee Moto Bwagizo alikuwa mtu mzima sana. Niliambiwa kuwa Halima alikuwa mtoto
wake wa mwisho na alizaliwa bila kutegemewa kwani tayari baba yake alikuwa mzee.
Mama yake mzazi alishafariki.
SASA ENDELEA
Mzee Moto Bwagizo alikuwa na
wake wawili, mama yake Halima na mke mwingine. Baada ya kufariki mama yake
Halima, mzee Moto aliendelea kuishi na mke wake wa pili.
Niliwasilisha ujumbe wangu
kwa wazazi wa Halima. Baba mkwe aliponiona aliniambia hazitambui mila za kutuma
barua ya uchumba kwani mimi sikuwa nikiomba kazi. Ukiomba kazi ndio unatuma
barua.
“Mila ninazizijua mimi za
kutpka enzi na enzi ni za kutuma mshenga, anakuja na maneno tu”
“Samahani baba yangu, sikujua
ndio kama unanielimisha”
Mzee akacheka.
“Umenijibu vizuri. Sasa
fungua barua yako unisomee”
Nikafungua ile barua yangu na
kumsomea yale niliyoandika.
Mzee akafurahi akaniambia.
“Nimekuelewa. Unataka kuunga
udugu na sisi. Mimi kama baba wa Halima nakujibu hapa hapa kuwa nimekukubali.
Halima ni mchumba wako tangu sasa”
Mzee Moto alinitajia kiasi
cha pesa alichotaka ili aniozeshe binti yake.
Siku ya pili yake nilimchukua
rafiki yangu nikaenda naye kupeleka pesa hizo.
Mipango ya harusi ikafanywa.
Baada ya wiki mbili nikaenda
Ponwe kumuoa Halima.
Baada ya kuoana na Amina
ndipo nilipoanza kufaidi maisha ya ndoa. Kuse,ma kweli yalikuwa matamu kinyume
na kuishi kihuni.
Kwanza gharama ya maisha
ilipungua sana.
Pesa ambayo hapo mwanzo nilitumia peke yangu kwa siku kwa kula kwenye mikahawa, ilitumika kwa siku
mbili nilipokuwa na mke wangu.
Kadhalika nilikuwa na
mwenzangu wa karibu wa kuniliwaza, kunishauri na kunisaidia pale nilipohitaji
mwenza wa kunisaidia.
Kwa kweli nilihisi raha na
nilijilaumu kwa kuchelewa sana
kumuoa Halima.
Niliendelea na kazi yangu ya
teksi. Fedha nilizopata ntulitumia, kiasi kingine tuliwek kama
akiba yetu. Miezi michache tu baad ya kuoana, ndoa ilijibu. Halima akapata
ujauzito.
Halima alinijulisha usiku
kuwa alikuwa mjamzito. Wakati tunataka kulala aliniambia.
“Subiri”
“Nisubiri nini?” nikamuuliza.
“Subiri nikuoneshe kitu”
“Kitu gani?”
“Una haraka gani?”
Halima akasimama mbele yangu
na kuushika mkono wangu kisha akaushikisha kwenye tumbo lake chini
ya kitovu. Akawa anautomasisha kwenye tumbo lake.
“Unaona nini?” akaniuliza.
“Sioni kitu” nikamjibu.
“Huoni kitu kigumu gumu?”
“Nakiona, ni nini?”
Halima akauachia mkono wangu
kisha akapanda kitandani. Wakati anavuta shuka nilimuuliza.
“Mbona hukiambii ni nini?”
“Mimba!” akanijibu huku
akiendelea kijifinika.
“Hiyo ni mamba?”
Ndiyo”
“Mbona ndogo sana?”
“Si ndio inaanza, ina mwezi
mmoja. Ujue mwezi uliopita sikupata siku zangu”
Ni kweli ilikuwa mamba ya
mwezi mkmoja. Ilitupa furaha sote wawili. Tukaona karibuni tutaitwa baba na
mama.
Lakini kadiri siku
zilivyoendelea Halima alikuwa akiniambia anapolala usiku anaota ndoto
amejifungua watoro wawili mapacha. Watoto hao ni wazuri na weupe kama wazungu!
Nikadhani labda ni kweli
atajifungua mapacha. Mimba ilipoiza miezi mitatu Halima aliota akifanya tendo
la ndoa na mwendawazimu. Alipoamka akaanza kuumwa tumbo!
“Una nini?” nikamuuliza
nilipomuona akifurukuta.
Akanihadithia ile ndoto
aliyoota kasha akaniambia alipoamka aliona tumbo linamuuma.
Wakati ananieleza hali
ilizidi kuwa mbaya. Nikafikiria nimpeleke hospitali lakini ile mamba ikatoka
muda ule ule.
Sikujua alikuwa amepatwa na
tatizo gani. Ilikuwa saa kumi na mbili asubuhi. Nikatoka naye na kumpakia
kwenye teksi, tukaenda hospitali ya Bombo.
Tulipofika hospitali
nilimpigia simu rafiki yangu Dk Augostino Kweka. Kwa bahati njema alikuwa pale
pale hospitali, akaja kumtazama mke wangu kisha
akaniambia.
“Anahitaji kusafishwa. Mimba
haikutoka yote”
Dk Kweka alinisaidia sana. Alilichukua jukumu
lile kirafiki. Mpaka inafika saa tatu mke wangu alikuwa ameshasafishwa.na
kupelekwa wodini. Mimi mwenyewe nilikuwa hapo hapo hospitali muda wote.
Usikose uhiondo huu ni kitajitokeza katika mfululizo huu wa hadithi hii ya kusisimua, hapahapa tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment