TANGA KUMEKUCHA

Tuesday, August 11, 2015

WAANDISHI WA HABARI WAASWA KUANDIKA HABARI KWA WELEDI UCHAGUZI MKUU


Tangakumekuchablog

Moshi, WAANDISHI wa habari nchini wametakiwa kuandika habari kwa usahihi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka huu na kuepuka kushabikia vyama na wagombea jambo ambalo linaweza kuwa chanzo cha kuharibika kwa amani.

Nasaha hizo zilitolewa jana na Mwandishi mwandamizi, Atilio Tigalile  wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kanda ya Kaskazini yaliyofanyika Mkoani Kilimanjaro na kuitishwa kwa pamoja na Baraza la Habri la Taifa (MCT)  na BBC Media Action.

Alisema mara nyingi waandishi wa habari nyakati za chaguzi wamekuwa wakiingia katika misuguano na vyama baada ya kuandika habari za upande mmoja na hivyo kuwataka kubadilika na kurejea katika maadili yao ya kazi.

Alisema mwandishi wa habari anapaswa kuzingatia taaluma yake ya upashaji wa habari na kuepuka vishawishi vya kuandika habari upande mmoja na kuacha kurubuniwa kwa vitu vidogo.

“Nawaomba ndugu zangu waandishi wa habari muliopata nafasi ya kuwepo hapa na wale ambao hawapo----jiepusheni  kuandika habari za upande mmoja na kuepuka kudanganyika na  vitu vidogo vidogo” alisema Tigalile na kuongeza

“Zingatieni maadili yenu ya habari kwa kuandika kwa weledi kwani kutawafanya kuwa salama na uwepo wenu popote muendapo kuchukua habari za wagombe wakati wa kampeni” alisema

Alisema mwandishi wa habari anaweza kuwa chanzo cha uvunjifu wa amani endapo atakiuka maadili ya kazi yake na hivyo kuwataka kuepuka kufanya hivyo na kurejea katika mstari wa ukweli na uhuru usiopitiliza mipaka.

Kwa upande wake, Mwandishi wa siku nyingi, Kyondo Mshana, aliwataka waandishi hao kuyatumia mafunzo hayo na kuwa mfano wa kuingwa kwa waandishi wengine wa vyombo vya habari.

Alisema kuandika habari kwa usahihi kutamfanya mwandishi kuwa salama wakati wowote na pahala popote na hivyo kukisaidia chombo chake jambo ambalo linaweza kukiletea sifa chombo chake anachofanyia kazi.

“Kuandika habari kwa usahihi kutawafanya kuwa huru na salama jambo ambalo chombo chako unachofanyia kazi kuaminika na kupendwa jambo litakalowafanya walaji kulipenda” alisema Mshana

Alisema kuelekea uchaguzi mkuu mwaka huu mwandishi anatakiwa kuepuka vishawishi na kuzingatia maadili ya taaluma ya habari ili kuepuka mizozo wakati anapoenda kufuata habari kwa vyama vyote wakati wa kampeni hadi uchaguzi.

                                             Mwisho

Mwandishi wa habari mwandamizi, Atilio Tigalile, akitoa somo kwa  waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka kanda ya Kaskazini juu ya kuandika habari kwa usahihi bila kuegemea upande wowote wa vyama  wakati wa uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika   Octobar mwaka huu,  mafunzo yaliyoitishwa  kati ya  Baraza la Habari la Taifa (MCT)  na BBC Media Action Moshi Mkoani Kilimanjaro jana . Kushoto ni mwandishi wa siku nyingi, Kyondo Mshana


People (2)

mwananchipapers


Show details

 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari kutoka  kanda ya Kaskazini wakiwa katika mafunzo mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro jana juu ya kuandika habari za uchaguzi  kwa Ukweli na Uwazi bila kuegemea upande wowote wa vyama wakati wa  uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Octobar mwaka huu. Mafunzo hayo yaliratibiwa kwa pamoja na Baraza la Habri la Taifa na BBC Media Action



Imechapishwa na Unknown kwa 1:12 AM
Email ThisBlogThis!Share to XShare to FacebookShare to Pinterest

No comments:

Post a Comment

Newer Post Older Post Home
Subscribe to: Post Comments (Atom)

Time

 Time in Tanga

Total Pageviews

My Blog List

Blog Archive

  • ►  2014 (563)
    • ►  November (97)
    • ►  December (466)
  • ▼  2015 (3131)
    • ►  January (417)
    • ►  February (332)
    • ►  March (351)
    • ►  April (308)
    • ►  May (263)
    • ►  June (255)
    • ►  July (260)
    • ▼  August (246)
      • KAMPUNI INAYOSHIKA RIKODI YA KUNUNUA NDEGE KWA MPIGO
      • DC AOMBA AMANI WAKATI WA UCHAGUZI
      • HIFADHI YA TAIFA TANZANIA YAWAZINDUA WATANZANIA KU...
      • UNGEPENDA KUWA NA GARI NZURI KAMA AINA HII
      • HADITHI SEHEMU (11)
      • VIMBWANGA VYA WALIMWENGU
      • ARSENAL KUMKOSA BENZEMA
      • BALOTEL KUTUPIWA VIRAGO VYAKE ANFIELD
      • MAAMUZI YA RAIS WA GABON
      • KAMA ULIPITWA NA MATOKEO YA MAN U Vs CLUB BRUGGE, ...
      • VITUKO VYA BALOTELLI KILA AINA
      • KERPO, MITAANI
      • AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
      • HADITHI SEHEMU YA (12)
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO NA MAGAZETI YA ...
      • VIWANJA VINAVYOVUTIA WAKATI NDEGE IKITUA
      • OSCAR PISTORIUS KUTUMIKIA KIFUNGO CHA NJE
      • POMBE YADAIWA KUSABABISHA SARATANI
      • ALEX SONG ANAHAHA KUPATA TIMU
      • MJUU WA MANDELA MATATANI AKIDAIWA KUBAKA
      • KIWANDA CHA SARUJI CHA SIMBA CEMENT CHATOA MSAADA ...
      • BIASHARA KITUO CHA MABASI , SEGERA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MENGI YAIBUKA BAADA YA OSCAR KUTOKA GEREZANI
      • WIZI WA MITANDAO WABAMBWA CHINA
      • ZIJUE HOTELI KALI ZILIZO KATIKATI YA BAHARI
      • RAHEEM STERLING KULIUZA JUMBA LAKE
      • AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
      • BANDARINI DEEP SEA
      • HADITHI SEHEMU (13)
      • MAAJABU NA KWELI
      • WOSHINGTON NA HAVANA WAMALIZA TOFAUTI ZAO
      • AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MAN U KIZUNGUZUNGU
      • MIJENGO MIKALI YA WANASOKO WAKALI DUNIANI
      • SOKONI NGAMIANI, TANGA
      • SUMAYE NAE ATIMKIA UKAWA
      • MUUNGANISHO WA WAJASIRIAMALI (MUVI) TANGA WAWAWEZE...
      • HADITHI SEHEMU YA (14)
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • CHALSEA HAINA MCHEZO KATIKA USAJILI, ANGALIA KIFAA...
      • MADARAJA 10 GHALI ZAIDI DUNIANI
      • PETRO AONYESHA MAKALI YAKE DARAJANI
      • NYOMI LA CCM
      • AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
      • KAMA ULIPITWA NA MATOKEO YA MAN CITY NA EVETON , H...
      • USIPITWA NA MATOKEO YA FC BARCELONA NA ATHLETIC BI...
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • JEURI YA PESA
      • ZINEDIN ZIDANE HATAKI MCHEZO KAMA KOCHA WA ZAMANI ...
      • VIWANJA 10 KATIKA HISTORIA UINGEREZA
      • WASHABIKI WA ARSENAL WAKATA TAMAA YA KUMNASA BENZEMA
      • KAMA ULIPITWA NA MATOKEO YA ARSENAL NA LIVAPOOL, N...
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MCHEZAJI WA LIGI KUU YA UINGEREZA MBARONI
      • PIRLO AIBUKIA JUVENTUS
      • RAIS KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA MTOTO WA JAJI MKU...
      • KUTOKA MSIBANI KWA JAJI MKUU WA TANZANIA, OTHMAN C...
      • AMKA NA MAGAZETI NA TANGAKUMEKUCHABLOG
      • MAJI YAFURIKA NA KUTISHIA KUINGIA KATIKA MAKAZI YA...
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • BALOTELI AWEKEWA MASHARTI KIBAO , AC MILAN
      • NDEGE 10 ZA KIFAHARI DUNIANI
      • MASHA USIKU MMOJA SEGEREA TOSHA
      • WAANDISHI WAWILI MAREKANI WAPIGWA RISASI NA KUFA
      • NDINGA UTAKAOTUMIKA MICHUANO KLABU BINGWA ULAYA
      • KAMA ULIPITWA NA MTANANGE WA MAN U NA BRUGGE, YAKO...
      • MATOKEO YA MECHI ZA JANA USIKU ULAYA
      • VIZIWI TANGA WATAKA MKALIMANI KAMPENI ZA UCHAGUZI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • BALOTELL ATOA KAULI TATU BAADA YA KUTUA MILAN
      • MANCHESTER YAMUWINDA NEYMAR
      • OSCAR PISTORIUS SHAKANI KURUDI GEREZANI
      • MBIO ZA UBUNGE TANGA ZAPAMBA MOTO
      • ZOMEAZOMEA BUNGENI YAMKUMBA MUGABE
      • WENGER AWATULIZA MZUKA WASHABIKI WA ARSENAL
      • RATIBA YA MAKUNDI KLABU BINGWA ULAYA
      • MESSI MCHEZAJI BORA ULAYA
      • SEKESEKE LA STONES KWENDA CHALSEA LATOKOTA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • USAIN BOLT HASHIKKIKI
      • MAITI 71 ZAKUTWA KATIKA LORI ZIKISAFIRISHWA
      • TOTTENHAM YAMSAJILI KINDA WA KIJERUMANI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • VIWANJANI LEO, AUG 29
      • YASIKUPITE MATOKEO YA LIKU KUU ENGLAND
      • LIVAPOOL YALOWA KWA VIBONDE
      • CHALSEA YADUNDWA
      • UKANJANJA WAWAPELEKA JELA WAANDISHI WA HABARI MISRI
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO...
      • MANCHESTER YAMNYEMELEA NEYMAR KABLA DIRISHA KUFUNGWA
      • WAFURAHIA KUICHAPA LIVAPOOL
      • MOPEROO YAKABIDHIWA PIKIPIKI 20 KUKOPESHANA
      • DE BRUYNE AVUNJA ROKODI YA RAHEEM STERLING
      • NUNDU TANGAMANO, TANGA
      • SOMA HABARI KUBWA ZILIZOANDIKWA MAGAZETI YALE LEO,...
      • DE GEA AKWAA KISIKI REAL MADRID
      • WANAOTUMIA MITANDAO YA KIJAMII VIBAYA CHA MOTO HIK...
      • ALLINCE FOR DEMOCRATIC CHENGE (ADC) TANGAMANO , TANGA
    • ►  September (237)
    • ►  October (210)
    • ►  November (142)
    • ►  December (110)
  • ►  2016 (1913)
    • ►  January (121)
    • ►  February (102)
    • ►  March (131)
    • ►  April (198)
    • ►  May (196)
    • ►  June (197)
    • ►  July (197)
    • ►  August (186)
    • ►  September (159)
    • ►  October (160)
    • ►  November (138)
    • ►  December (128)
  • ►  2017 (562)
    • ►  January (134)
    • ►  February (106)
    • ►  March (113)
    • ►  April (77)
    • ►  May (72)
    • ►  June (11)
    • ►  September (1)
    • ►  October (36)
    • ►  November (10)
    • ►  December (2)
  • ►  2018 (1)
    • ►  February (1)
Picture Window theme. Powered by Blogger.