Viwango vipya vya sukari vimetangazwa leo, onyo latolewa kwa watakaobainika kupandisha bei
Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
kutangaza zuio la uingizwaji wa bidhaa ya sukari kutoka nje ya nchi,
leo March 8 2016 Serikali kupitia bodi ya sukari Tanzania, imetangaza
viwango vipya vya bei ya sukari nchini vitakavyoanza kutumika hivi
karibuni, akiongea na waandishi wa habari Mkurugenzi wa bodi ya sukari
Tanzania Henry Semwanza amesema>>
Serikali,
kupitia bodi ya Sukari Tanzania, inawaarifu wananchi wote kuwa bei ya
rejareja ya sukari sasa itakuwa sh. 1,800 kwa kilo moja‘
‘wafanyabiashara
wote wanapaswa kuzingatia agizo hili, pamoja na kuhakikisha kuwa sukari
inaendelea kusambazwa na kuuzwa kwa wananchi bila kuihodhi‘
‘Maafisa
biashara wa mikoa na wilaya watafuatilia na kusimamia utekelezaji wa
agizo kuhusu bei elekezi ya sukari, na hawatasita kuchukua hatua stahiki
za kisheria kwa wale watakaobainika kupandisha bei ya bidhaa hiyo‘
No comments:
Post a Comment