Mabadiliko ya bei za Petroli, Diesel na mafuta ya Taa Tanzania kwa March 2016 yametangazwa
Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya Petrol, Diesel na ya mafuta ya taa katika masoko yote ya jumla na rejareja ambapo bei hizo zitaanza kutumika kuanzia Jumatano siku ya pili ya mwezi March 2016.
Mkurugenzi wa huduma za nishati na maji (EWURA), Felix Ngamlagosi amesema >>> ‘kuanzia tarehe 2 March bei za mafuta zimebadilika ikilinganishwa na toleo lililopita la February 2016, kwa
March 2016 bei ya rejareja za petroli imepungua Tsh 31 kwa lita sawa na
1.70%, Diesel imepungua Tsh 114 kwa lita sawa na 7.10% na mafuta ya taa
yamepungua kwa Tsh 234 kwa lita sawa na 13.75%’
‘kwa
kiasi kikubwa , kupungua huku kwa bei za mafuta kwenye soko la ndani
kumetokana na kuendelea kushuka kwa bei za mafuta katika soko la dunia‘
Nimekuwekea hapa Orodha ya bei za mafuta kwa mikoa yoteKwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment