Tangakumekuchablog
Korogwe, MBUNGE
wa jimbo la Korogwe Vijijini, Stivn Ngonyani (CCM) amewataka wananchi wa jimbo
hilo kushirikiana na kuacha makundi na kuijenga Korogwe katika nyanja mbalimbali za kilimo na Uchumi.
Akizungumza katika mkutano wa
hadhara jana uwanja wa sokoni mji mdogo
wa Mombo, Majimarefu aliwataka wananchi kuvunja makundi ya ushabiki wa ksiasa
na badala yake kuijenga Korogwe kimaendeleo.
Alisema wananchi wa Korogwe ambao
wengi ni wakulima wa kilimo cha mbogamboga na matunda pamoja na kilimo cha
mkonge, wako na nafasi nzuri ya kuboresha maisha yao kwa kujiongozea kipato
kupitia kilimo cha mbogamboga na zao la mkonge.
“Ndugu zangu wananchi wa mji mdogo
wa mombo nimekuja hapa kuwashukuruni kwa kunichagua kwa mara ya pili kuwa
mbunge wenu, niseme kuwa uchaguzi umeisha na sasa niwajibu wetu wa kushirikiana
kufanya kazi” alisema Majimarefu na kuongeza
“Wakati wa kampeni mengi yamesemwa
juu yangu na mwisho wa siku sanduku la kura lilijibu, ila niseme hata ambao
hawakunichagua wote ni wananchi wangu na niko tayari kufanya kazi nao lengo ni kuleta maendeleo” alisema
Mbunge huyo ambaye mara nyingi hujiita Mganga
wa kienyeji, aliombwa na Diwani wa kata ya Mombo, Halima Juma (CCM) kumtaka
kipindi hiki akiwa mbunge kuhakikisha mji huo unapata hadhi ya kuwa halmashauri
ya mji.
Diwani huyo alimtaka pia Majimarefu baada
ya kufanikisha upelekaji umeme vijijini na uchimbaji wa kisima kuzichonga
barabara zitokazo kwa wakulima ili kuwapa unafuu nyakati za mvua.
Alisema vipindi vya mvua wakulima wa
mazao wamekuwa na wakati mgumu na kuingia gharama kubwa hivyo kuuza kwa hasara
hivyo kuchongwa kwa barabara hizo itakuwa msaada kwa wakulima na
wafanyabiashara.
“Mheshimiwa mbunge tunatambua
michango yako kwa hali na mali na umekuwa ukiwatetea wananchi wako, kwa hayo na
mengine lakini pia tunakuomba utupiganie mji wetu wa Mombo kuwa halmashauri ya
mji” alisema Halima
Alimtaka mbunge huyo kusimamia
miradi ya maendeleo ya wananchi na ya wafadhili pamoja na kuziba mianya ya
ubadhrifu ili kuhakikisha pesa itolewayo inatumika kama ilivyopangwa.
Mwisho
Mbunge wa jiombo la Korogwe Vijijini , Profesa Majimarefu akimpa hongera mzazi , Sharifa Juma baada ya kujifungua salama wakati wa ziara yake hospitali ya Wilaya ya Magunga ya Korogwe kujua kero za wagonjwa na wafanyakazi wa hospitali hiyo
No comments:
Post a Comment