Saturday, April 2, 2016

AFARIKI AKIWA NA MTOTO WAKE AKIJARIBU GARI ALOITAKA KUINUNUA



Gari aina ya Noah ikiwa imebondeka  sehemu ya mbele baada ya kugonga lori kwa nyuma lililokuwa limeegesha eneo la mezani ya zamani Majanimapana  Tanga na watu wawili kufariki papo hapo na wengine wawili kujeruhiwa.
Inadaiwa kuwa aliefariki ni Mkenya ambaye alikuja kuinunua gari hiyo akiwa na mke wake pamoja na mtoto na wakati akiijaribu ndipo mauti hayo yalipomkuta akiwa na mtoto wake mdogo mbele.
Mke wa Marehemu alikuwa siti ya nyuma na kupata majereha makubwa na miili li wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya Mkoa wa Bombo.
Mashuhuda wameiambia Tangakumekuchablog kuwa dereva alikuwa mwendo kasi na kushindwa kutambua kuwa lori hilo lililokuwa limepaki ama liko katika mwendo.
 






No comments:

Post a Comment