Monday, April 4, 2016

KIKAO CHA KWANZA BARAZA LA MADIWANI JIJI LA TANGA LAVUNJIKA



 Mbunge wa jimbo la Tanga mjini (CUF), Mussa Mbarouk , akifanyiwa upekuzi kabla ya kuingia katika ukumbi wa baraza la Madiwani halmashauri ya jiji la Tanga, na kikao hicho kuahirishwa baada ya Madiwani wa CUF kudai kutomtambua Meya (CCM) Seleman Mustafa hivyo kutaka uchaguzi urudiwe au kuvunjwa kwa baraza.
Kikao hicho ambacho kilikuwa kiketi kuanzia saa 3 asubuhi ndani na nje ya jengo la halmashauri ya jiji la Tanga kulikuwa na ulinzi maradufu.
Njia ipitayo katika jengo hilo ielekeayo Posta na Bandari ya Tanga na njia ielekeayo Mombasa Kenya ilikuwa imefungwa.
Wakati wa kuanza kikao hicho mara baada ya kuingia katika ukumbi wa Baraza la Madiwani, Meya na Kaimu Mkurugenzi wa jiji la Tanga Madiwani wa CUF walimtaka Meya wa jiji kuondoka mbele ya meza kuu kwa madai sio Meya halali.
Madiwani hao wa CUF walidai kuwa Meya huyo wa alietoka Chama Cha Mapinduzi kuwa hakushinda kihalali wakati wa uchaguzi wa kumtafuta Meya hivyo kudai kuwa Meya alipaswa kutoka Chama Cha Wananchi CUF, Rashid Jumbe kwa madai kuwa ndie mshindi.
Diwani wa kata ya Msambweni, Abrahman Hassan (CUF) alisema msimamo wao ni kurudiwa Uchaguzi wa Umeya au kuvunjwa kwa Baraza.
"Hatuko tayari kuongozwa na Meya ambaye ameupora ushindi halali wa CUF, turudie uchaguzi au Baraza livunjwe iwe hakuna baraza" alisema Abrahman
Alisema endapo mambo hayo mawili hayatafanyika hakutakuwa na kikao chochote kitakachofanyika hadi hapo maamuzii yaliyofanywa na Madiwani wakati wa kumchagua Meya yatakapoheshimiwa. 
Chama Cha Wananchi CUF kiko na madiwani 20, na Chama Cha Mapinduzi kiko na Madiwani 17.




 Madiwani wa CUF halmashauri ya jiji la Tanga wakijadiliana nje ya ukumbi wa mikutano halmashauri ya jiji baada ya kikao chao cha kwanza kuahirishwa kwa madai ya kutomtambua Meya (CCM) Seleman Mustafa na kudai kuwa Baraza hilo livunjwe au kufanyika tena uchaguzi wa Umeya.

Diwani wa kata ya Msambweni halmashauri ya jiji la Tanga, Abrahman Hassan (CUF) akitoa hoja kwenye kikao cha Baraza la Madiwani kabla ya kuahirishwa kutaka uchaguzi wa Umeya urudiwe au kuvunjwa kwa Baraza la Madiwani kwa madai kuwa hawamtambui Meya (CCM) Seleman Mustafa.

No comments:

Post a Comment