Kampuni ya Liquid Telecom ipo katika hatua za mwisho kufanikisha mradi
mpya wa kutandaza mkongo wa mawasiliano wa baharini ambao pamoja na
kuunganisha kusini mwa Afrika pia utaunganisha na Mashariki ya kati
pamoja na Ulaya.
Iwapo mkongo huu utakamilika basi itakuwa ni habari nzuri kwa watumiaji
na watoa huduma wa intaneti hapa Tanzania kwani itakuwa ni nafasi ya
kuongeza ufanisi na ubora wa huduma katika sekta hii.
Bosi wa kampuni hiyo ya Liquid Telecom ambayo imejikita zaidi nchi za
kusini mwa Afrika alikuwa na mazungumzo na aliyekuwa katibu mkuu wa
jumuiya ya Afrika Mashariki DR Richard Sezibera alipotembelea makao
makuu ya jumuiya.
Nkusi amesema kwamba Cable hii itapita katika njia ambayo haina
watumiaji wengi zaidi kwenda Ulaya, hii itasaidia watoa huduma na
watumiaji wa tanzania kuweza kapata intaneti yenye spidi kubwa na pia ya
uhakika zaidi.
Mkongo huu utatambazwa chini ya bahari ukiambaa na ukanda wa Afrika
Mashariki kuelekea katika bahari ya Shamu ambapo baada ya kuvuka bahari
hiyo mkonga huu utaishia Ulaya, utakapoweza kuunganishwa na mikonge
mingine.
Aliyekuwa katibu mkuu wa jumuiya ya Afrika Mashariki aliahidi
ushirikiano na wawekeaji hao huku akitilia mkazo umuhimu wa jumuiya ya
afrika mashariki kuunganishwa na ulimwengu.
Kwa mtanzania wa kawaida kuongezeka kwa mkono wa cable ya chini ya
bahari ni dalili nzuri kwamba watoa huduma kama vile mitandao ya simu
itakuwa na nafasi kubwa ya kufanya machaguo juu ya mkongo upi utumike
kitu ambacho kinaweza kuchangia kushuka wa gharama au kuongezeka kwa
ubora wa huduma za intaneti.
Kwa habari, matukio na michezo ni hapahapa Tangakumekuchablog
No comments:
Post a Comment