HADITHI hii inaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Tiba Cha Mkombozi Sanitarium Clinic Tanga, Mkombozi ni mabingwa wa tiba na hutoa ushauri wa kitaalamu. Mkombozi wako na vifaa vya kisasa vya kupimia mwili mzima. Mkombozi wapo Tanga barabara ya 12 kituo cha zamani cha mabasi yaendayo Mikoani, simu 0654 361333
MWANAMKE
ALIYENICHUNUKA
12
ILIPOISHIA
Nikainuka
na kushuka kitandani. Juma alikuwa amelala fofofo.
“Vaa
nguo zako” akaniambia.
Nikavaa
suruali, shati na viatu.
“Sasa
twende”
Akanishika
mkono.
Tukatoka
mle chumbani. Akafungua mlango wa mbele na kuniambia nitangulie kutoka nje.
Nilipotoka na yeye akafuatia.
Aliinama
chini akachora msitari mbele yangu kisha akaniambia.
“Vuka
huo msitari”
Nikiwa
kama zezeta ambaye sikuwa na uwezo wa kuwaza chochote, nilitii alichoniambia,
nikapiga hatua na kuvuka ule msitari. Kufumba na kufumbua nikajiona niko katika
eneo jingine ufukweni mwa bahari. Banuna alikuwa amesimama kando yangu,
akanishika mkono na kuniambia.
SASA
ENDELEA
“Twende
kule”
Alinionesha
kule baharini.
Tukawa
tunatembea kwenye ufukwe kuelekea
baharini. Sikuju tulikwa tunakwenda wapi. Ulikuwa usiku mwingi na
kulikwa kunatisha lakini sikupata hofu yoyote.
Punde
tu tukayafikia maji, sasa tukawa tunatembea kwenye maji huku nguo zetu
zikitota. Tangu maji yalikuwa kwenye viwiko vya miguu hadi yakawa kwenye magoti.
Tukaendelea kwenda hadi maji yakatufikia kifuani.
Sasa
nikawa ninayumbishwa na maji. Ilibidi Banuna anishikilie ili maji yasinichukue.
“Tunakwenda
hadi wapi?” nilimuuliza Banuna nilipoona maji yametufika shingoni.
“Tunakwenda
kwetu” Banuna akanijibu.
“Kuna
mji huku?”
“Ndio
upo”
“Uko
wapi?”
“Utauona,
twende tu”
“Tutafika
saa ngapi?”
“Usiwe
na wasiwasi. Tutafika sasa hivi”
Banuna
aliendelea kunipeleka hadi maji yakawa yananikosesha pumzi kwani mawimbi
yalikuwa yanapiga kwenye uso wangu. Banuna akaniambia nipande kwenye mgongo
wake.
“Panda
ukae kwenye mabega yangu”
Banuna
akanisaidia nikaweza kukaa kwenye mabega yake. Jambo la ajabu ni kuwa Banuna
aliweza kunibeba na kutembea na mimi kwenye maji huku kichwa chake kikiwa
kimeshazama baharini Sikuweza kujua alikuwa akipumua kwa namna gani.
Muda
si muda niliona ananizamisha cihini ya bahari. Nikapiga kelele.
“Sasa
tunakufa!”
“Usiogope,
hutakufa” niliisikia sauti yake ikitokea ndani ya maji.
Licha
ya kunitoa wasiwasi kuwa sitakufa, sikuamini. Nikizama chini ya bahari. nitapata
wapi pumzi?
“Banuna
sitaweza kupumua ndani ya maji!” nikamwambia Banuna kwa sauti ya kutetemeka.
“Utaweza.
Mbona mimi ninaweza”
Banuna
akazidi kunizamisha. Sasa maji yalikuwa kwenye shingo yangu. Nilikuwa nimefunga
mdomo lakini ndani ya moyo wangu nilikuwa ninapiga kelele.
“Nakufa…nakufa…nakufa…!”
Ghafla
kichwa changu chote kikazama chini ya bahari. Nilikuwa nimetaharuki kwa hofu
lakini niliona miujiza mikubwa. Vile ninazama tu chini ya bahari niliona
tumetokea mahali kweupe kusiko na bahari.
Banuna
akiwa amenibeba kwenye mabega yake alikuwa amesimama kwenye mnara mrefu
ulioteremka chini. Huko chini kulikuwa na mji mkubwa uliokuwa unawaka taa.
Kulikuwa na minara kadhaa iliyoonekana kila upande
Ulikuwa mji wa ajabu na mzuri usio na magari wala pikipiki isipokuwa
watu wa ajabu walioonekana wakienda huku na huku kama
vile ni mchana.
Kwa upande mmoja niliona kulikuwa na gulio. Watu walikuwa wamejazana
wakinunua mahitaji.
Wengi wa watu niliowaona walikuwa wamevaa nguo zilizofanana na nguo
zenyewe zilikuwa shuka, ama shuka nyeupe ama nyekundu. Wengine walikuwa wamechanganya
shuka nyeupe na nyekundu. Baadhi ya watu hao walikuwa wamejifunga vilemba
vikubwa kama waarabu.
Mbali ya watu hao, pia niliona punda wengi na farasi wa rangi
mbalimbali.
Banuna akaniambia nishuke kutoka kwenye mabega yake. Huwezi kuamini
kuwa msichana huyo aliweza kunibeba, labda kwa vile alikuwa ni jini kwani hata
kwa uzito nilikuwa nimemzidi.
“Umeuona mji wetu?” Banuna akaniuliza.
“Nimeuona. Ndiyo mji wenu huu?”
“Ndio huo. Wale wote unaowaona chini ni majini!”
“Sasa huu mji ndio uko chini ya bahari?”
“Ndiyo. Na hapa tulipotokea ndio nyumbani kwetu”
“Huu mnara ndio nyumbani kwenu?”
“Hii ni ghorofa, imekwenda chini. Humu ndani kuna wazazi wangu”
Nikawa nimeshangaa.
“Hii ni nyumba kabisa. Tutaingia na utaiona” Manuna akaniambia.
Mnara huo wa mawe ulikuwa na matundu kama madirisha na kulikuwa na
sehemu yenye uwazi mrefu kama mlango. Banuna
akaniambia nimfuate.
Akatangulia kuingia kwenye ule uwazi na mimi nikamfuata nyuma. Kulikuwa
na kiza sana.
Nilikuwa sioni.
“Nishike bega twende” Banuna akaniambia.
Nikanyoosha mkono wangu wa kulia na kumshika bega.
Kulikuwa na ngazi. Tukashuka taratibu. Tulikuwa kama tunaoshuka kwenye
shimo. Kila tulivyozidi kushuka ndio kiza kilivyozidi.
“Huoni kabisa?” Banuna akaniuliza baada ya ukimya mrefu.
“Sioni!”
“Mimi naona. Tunapita katika kuta za mawe, karibuni tutafika”
“Sasa mnaishije kwenye kiza namna hii?”
“Tunapokuwa kwenye mwanga, mboni zetu za macho zinakuwa
Ndogo lakini tukiwa kwenye kiza
mboni zinakuwa kubwa na kutuwezesha kuona”
“Kwa hiyo mimi sitaweza kuona”
“Tutatokea kwenye mwanga muda si mrefu”
“Kiza hiki kinatisha sana
bora mngeweka taa”
“Usijali, utazoea tu”
Mara nikasikia Banuna akisemeshana na mwenzake mwenye sauti ya kiume ambaye
sikuweza kumuona kutokana na kiza. Lugha waliyozungumza haikuwa ya Kiswahili.
Hapo hapo nikaona mlango unafunguliwa. Nikaona mwanga mzuri mweupe
umetokea.
“Tuingie” Banuna akaniambia.
Itaendelea kesho
|
Wednesday, April 13, 2016
HADITHI , MWANAMKE ALIENICHUNUKU SEHEMU YA (12)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment