Monday, February 2, 2015

AMKA NA MAGAZETI NA TANGA KUMEKUCHABLOG


Kama kawaida,tangakumekuchablog inakupa makubwa yaliandikwa katika magazeti kurasa za mbele na nyuma katika magazeti kila siku kupiti www.tangakumekcha.blogspot.com





















         Hutopitwa na habari yoyote mtu wangu tembelea www.tangakumekucha.blogspot.com kila wakati na muda wowote na kupata habari kedekede                                                         

BAADA YA MAZISHI YA BABA YAO , KILICHOFUATA NI KUJIRUSHA KWA SANA

Baada ya mazishi ya baba yao P Square, Peter alitumia muda huu na marafiki zake…

.
Jennifer Enwemnwa, mfanyabiashara Abdulsamad Rabiu, Freda Francis Edewor, Lola Omotayo na Peter Okoye
Siku ya Ijumaa January 30 ndugu jamaa na marafiki wa familia ya mzee Moses Okoye ambaye ni baba mzazi wa mastaa wa muziki kutoka Nigeria, Peter na Paul OkoyeP Square‘ ambapo mazishi hayo yamefanyika miezi miwili tangu mzee huyo afariki kwa kuanguka akiwa anashuka ngazi ndani ya nyumba.
.
Peter akiwa na mkewe pamoja na marafiki zake.
Baada ya kufanyika kwa mazishi hayo, Peter aliamua kujumuika na familia yake pamoja na marafiki zake ikiwemo mfanyabiashara mkubwa wa Nigeria, Abdulsamad Rabiu ndani ya boti yao.
Hizi ni baadhi ya picha zikimuonyesha Peter pamoja na mkewe Lola Omotayo wakifuraji.
peter2
peter3
peter
peter9
peter6
peter5
Peter I
Peter II
.
Mfanyabiashara Abdulsamad Rabiu na Peter Okoye.
Hakuna story itakayokupita mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakuimekucha.blogspot.com

MTOTO AWAFYATULIA RISASI WAZAZI WAKE

Pale ambapo mtoto anachukua bastola na kuwapiga wazazi wake…

boy yrs
Wazazi wana jukumu kubwa la kuhakikisha wanalinda watoto wao kila wakati ili waweze kuwa salama ikiwa ni pamoja na kuwaweka kwenye mazingira mazuri.
Lakini wazazi wa mtoto huyu wamejikuta wakiwa hoi hospitali baada ya mtoto wao wa miaka mitatu katika mji wa New Mexico kuchukua bastola iliyokua ndani ya mkoba wa mama yake na kuwafyatulia wazazi wake.
Justin Reymond ambaye ni Baba wa mtoto huyo alipigwa risasi ya sehemu ya mgongo huku mama yake, Gabrielle Burkhart ambaye ni mjamzito wa miezi nane naye akijeruhiwa vibaya katika bega lake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakuimekucha.blogspot.com

MUME AMUUA MKE WAKE HOTELINI MAGOMENI ,DAR

 Tukio la mauaji yaliyotokea Hotelini.

images (16)Tukio la mauaji  Magomeni Dar inahusu   lililotokea hivi karibuni katika Hoteli moja maeneo ya Magomeni Kagera baada ya mteja aliyefika kwenye Hoteli moja na kumuua mke wake.
Mhudumu wa Hoteli hiyo amesema wateja hao walilipia room kwa siku moja na kesho yake  mwanaume huyo aliwaambia kuwa anaendelea na angelipia, baadae walimgongea ili alipie mteja huyo aliwaambia kuwa hafungui hadi Polisi waje, walichukulia utani ndipo walipomchukua mtu mmoja nakujifanya Polisi na kwenda kumgongea ndipo alipofungua na kukuta damu zimetapakaa kwenye chumba hicho.
Baada ya kukuta hali hiyo waliamua kuita Polisi ambao walifika na kukumkuta bado yuko ndani na walipomuuliza alisema kuwa amemuuwa mke wake, huku na yeye akiwa na majeraha yanayosemekana kuwa alitaka kujiuwa mwenyewe.
Ndungu wa mtuhumiwa amesema kuwa aliyeuwawa ni mke wa ndoa wa mtuhumia ambao walikuwa na ugomvi muda mrefu uliosababisha waishi tofauti na walipomwuliza mtuhumiwa kuhusu tukio hilo aliwaambia kuwa ameamua kumuuwa lakini hakutoa sababu ya kufanya mauaji hayo na baada ya kupatiwa matibabu mtuhumiwa yuko kituo cha Polisi Magomeni.

KUTOKA JUKWAANI HADI KUMILIKI MGHAHAWA

Baada ya duka la nguo,Feruz amekuja na biashara hii nyingine.

bzncKwenye spika zako hajasikika muda mrefu kimuziki ingawa kuna stori tofauti ambazo zimekua zikimhusisha staa wa Bongo Fleva Feruz ikiwemo inshu ya kuchimba madini na duka la nguo.
Ferooz_SafariGood news ambayo Feruz leo ameshare nasi ni kuhusu biashara nyingine ambayo anategemea kuizindua Jumatano ya February 04,biashara ambayo anaifungua Feruz ni biashara ya mgahawa ambao utakua ukihudumia maeneo ya Darfree Market.
Feruz kasema mgahawa huo umegharimu kama milion 30 za Kitanzania na utakua ukitoa huduma ya chakula cha aina yoyote baada ya uzinduzi wake kufanyika.

FRANCISS CHEKA JELA MIAKA MITATU

BreakingNews: Bondia Francis Cheka amehukumiwa kwenda jela.

Breaking NewsBondia Francis Cheka leo February 2 2015 amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu na faini ya Milioni moja laki sita kwa kosa la kumpiga mmoja kati ya wafanyakazi wake kwenye bar yake iliyopo Morogoro.
cheka
Muda mfupi uliopita Francis Cheka ameongea na tangakumekucha na kusema ndio alikua anajiandaa kuachia simu yake na vitu vingine muhimu ili achukue karandinga kuelekea gerezani ambapo namnukuu akisema ‘imeshakua hivi tayari ila hamna noma, niko na wanangu wengine wamepigwa miaka 10 nitakua nao fresh tu ila hamna noma ni miaka mitatu tu mimi’
Hukumu imetolewa na Hakimu Mkazi Said Msuya ambapo baada ya hayo upande wa Francis Cheka unasemekana kujiandaa kukata rufaa.

HABARI NJEMA UGONJWA WA EBOLA AFRIKA

Habari njema kuhusiana na majaribio chanjo ya Ebola…

trial
Stori kuhusu ishu ya Ebola huenda ni moja ya story zilizochukua headlines kubwa kwa mwaka wote 2014, tangu iliporipotiwa kuibuka kwa maambukizi ya ugonjwa huo Afrika Magharibi mwanzo wa mwaka 2014.
Hii inaweza kuwa habari njema kwa Waafrika na dunia nzima kwa ujumla, taarifa iliyopo ni kwamba jaribio la kwanza la chanjo ya ugonjwa wa Ebola kutarajiwa kuanza kutumika Liberia wakati wowote kuanzia sasa.
Wataalamu wanatarajia zaidi ya watu 30,000 watajitokeza katika zoezi la majaribio hayo wakiwemo wahudumu wa afya.
ebola
Katika kipindi cha mwaka mmoja zaidi ya watu elfu tisini wamefariki kutokana na ugonjwa huo ambao uliandama zaidi Mataifa ya Guinea, Sierra Leone na Liberia.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia,www.tangakumekucha.blogspot.com

KAKA AMCHOMA MDOGO WAKE KISU CHA TUMBO KISHA AITA POLISI

Baada ya kuchoshwa na uonevu unaofanywa kwa mama yake, jamaa aamua kumfanyia ukatili dada yake…

HANDCUFFS (1)Jamaa mmoja huko Taiwan mama yake alikuwa anaumwa, baada ya kutibiwa Hospitali alirudishwa nyumbani kwa mapumziko lakini mtoto wake wa kike hakuonekana kujali hali hiyo ya mama yake, alikuwa akimsumbua mama huyo mara kwa mara kudai hela kitu ambacho kaka yake hakupendezwa nacho.
Kaka huyo ambaye anaitwa Wang aliamua kumchoma kisu dada yake kutokana na kutopendezwa na usumbufu anaofanyiwa mama yake huo, ambapo dada huyo alifariki.
Wang muda mwingi hukaa nyumbani kumhudumia mama yake na kufanya kazi zote za nyumbani, ikiwemo kupika na kufanya usafi lakini dada yake hakuwa msaada wowote kwa mama yake, ni mtu wa kushinda na rafiki zake.
Baada ya kufanya mauaji hayo alishafisha eneo hilo, akamuandalia mama yake breakfast na chakula cha mchana, baada ya mama yake kupumzika Wang aliwaita Polisi na kukiri kuhusika na tukio hilo kutokana na kuchoshwa na matatizo ya nyumbani kwao na kudai kuwa  dada yake mara nyingi amekuwa akimuonea mama yao ikiwemo kumdai fedha kila siku na kwenda kutumia na rafiki zake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,www.tangakumekucha.blogspot.com

SOMA HABARI KUU ZILIZOPEWA UZITO MAGAZETI YA LEO,TZ

Mkusanyiko wa Stori kubwa zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo February 2, 2015

good
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amedokeza kuwa atakayekuwa mgombea wake wa urais baadaye mwaka huu ni yule ambaye hajajitokeza mpaka sasa.
Akihutubia jana katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho mjini Songea, mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema: “Wapo watu wenye sifa zote za urais lakini hawajitokezi na hata wakiambiwa kuwa wanaweza husema hawajajiandaa. Hawa ndiyo tunaowahitaji kwa kuwa wanahitaji kukumbushwa tu.
Kauli hiyo ya Rais Kikwete inaweza kuwa mwiba mchungu kwa baadhi ya makada wa CCM ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipita huku na kule kutafuta uungwaji mkono, huku baadhi yao wakiwa wamepewa onyo kali kutokana na kushiriki kampeni kabla ya muda na kushiriki vitendo ambavyo ni kinyume na maadili.
Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja na vituo vitatu vya televisheni, Rais Kikwete alisema chama hicho kitakuwa na mgombea bora wa urais kwa kuwa upo utaratibu mzuri wa kumpata kwa kutumia kanuni walizojiwekea. Pia alieleza kwa msisitizo kwamba kinachokatazwa ni ‘kukiuka kanuni na taratibu.’
Oktoba tunachagua rais, mimi nataka rais huyo atoke CCM. Chama kina mfumo wa kumpata mgombea mzuri wa urais na nawahakikishia kuwa tutakuwa na mgombea bora wa urais na wananchi hawatanung’unika:-Kikwete
Rais alieleza kuwa ni lazima CCM ishinde katika uchaguzi mkuu ujao hasa kwa kuzingatia kuwa imekuwa ikifanya hivyo tangu mfumo wa vyama vingi uanzishwe, zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo aliwatahadharisha wanachama wake kuwa ni lazima wajiandae kukabiliana na upinzani uliopo na ili kufanikisha hilo, aliwataka wale wote wenye nia kuanza kuwa karibu na wananchi ili kusikiliza kero walizonazo.
NIPASHE
Jeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, limeingia katika kashfa baada ya askari wake kutuhumiwa kumuua raia.
Raia huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mdonga, fundi wa magari, Januari Mtitu (20), inadaiwa kuwa aliuawa kwa risasi na askari mwenye namba G 6352, Abduel Nyuki.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Juma Madaha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa tayari askari anayetuhumiwa na raia wengine wawili, wamekamatwa.
Habari zinaeleza kuwa wakazi wa eneo la tukio, walipandwa na hasira na kumfanya Mkuu wa huyo wa Wilaya kulazimika kuwatuliza kwa kuwataka wapunguze hasira ili wasiwadhuru polisi wengine kwa sababu siyo wote waliohusika na tukio hilo.
Kauli ya Mkuu huyo wa Wilaya ilitokana na mgomo wa mafundi wa magari kukataa kutengeneza jeneza na kutaka kuandamana huku wakilitaka Jeshi la Polisi kulitengeneza wenyewe ama kulipa fedha kwanza ndipo litengenezwe.
Sasa hivi tumechoka kuteswa na kunyanyaswa na polisi, wanaacha kukamata wahalifu badala yake wamewageukia wananchi ambao hawana hatia na leo hii wamemuua mwenzetu bila kosa,” mmoja wa mafundi hao alisema.
NIPASHE
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema ameanza mchakato wa kuonana na Rais Jakaya Kikwete, kuwasilisha kilio na kushauriana naye juu ya nguvu kubwa inayotumiwa na Jeshi la Polisi kuwashambulia na kuwakamata wapinzani.
Kadhalika, amesema mazungumzo hayo yatalenga kuwekwa utaratibu wa Jeshi la Polisi kuvitendea haki vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Prof. Lipumba alisema nguvu kubwa inayotumiwa na polisi dhidi ya vyama vya upinzani, haina lengo jema, bali kukandamiza haki za binadamu na demokrasia.
Tunataka vyama vyote vitendewe haki na usawa mbele ya nguvu ya dola na siyo kukandamiza upande mmoja, hali hii ikiruhusiwa kuendelea na mwaka huu wa uchaguzi, ni wazi kuwa nchi itaingia katika machafuko:-Lipumba
Vijana wa sasa siyo wa mwaka 2001, Polisi wasifikiri kuwa vijana na wananchi wataendelea kunyamaza na siku wakiamua kulipiza, hakika hakuna atakayepona…nawaomba wananchi wasilipize kisasi kwa askari wanaoishi nao uraiani.”
NIPASHE
Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) umetoa heshima pekee kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kumuenzi kwa kuamua kuwa moja ya majengo yake muhimu katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, litapewa jina la Mwalimu Julius Nyerere.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anapewa heshima hiyo kubwa kwa mchango wake katika ukombozi wa Bara la Afrika na kuliondoa Bara la Afrika kutoka kwenye ukoloni.
Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama (Peace and Security Council) la Umoja huo Mwalimu Julius Nyerere Hall ulifikiwa juzi Jumamosi wakati wa kikao cha ndani cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa.
Akizungumza baadaye kwenye kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliwashukuru viongozi wenzake, wakiongozwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, kwa kutoa heshima hiyo kubwa kwa mwanzilishi wa Taifa la Tanzania na kwa nchi ya Tanzania yenyewe.
Hoja ya kufanya uamuzi wa kuliita jengo hilo Mwalimu Julius Nyerere Hall ilitolewa ufafanuzi na Rais Mugabe ambaye ni Mwenyekiti mpya wa AU.
MTANZANIA
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 27 Makoko kilichopo Musoma, Praiveti Wilfred Koko amekutwa ameuawa na kuondolewa sehemu ya viungo vya mwili katika eneo la kikosi hicho.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Mara ilisema askari huyo MT-78227, aliokotwa katika eneo la jeshi Januari 30, mwaka huu saa sita mchana mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo ukiweamo mguu wa kulia, viganja vya mikono yote na sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ernest Kimola, alisema upande wa mguu wa kushoto wa marehemu ulikutwa na jeraha lililokatwa na kitu chenye ncha kali hali inayoonyesha huenda askari huyo aliuawa na kutupwa kwenye eneo hilo.
Alisema huenda viungo vya askari huyo ambavyo havikukutwa vilikuwa vimeliwa na wanyama baada ya mwili huo kuonekana kukaa muda mrefu, kuanza kuharibika na kuingiliwa na wadudu.
MTANZANIA
JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande, amewahamisha majaji 27 wa Mahakama Kuu Tanzania akiwamo Jaji John Utamwa aliyehamishiwa Mahakama Kuu Tabora na Jaji Dk. Fauz Twaib aliyehamishiwa Mahakama Kuu Mtwara.
Uhamisho huo ulifanyika mwishoni mwa wiki ambako majaji wengine walibadilishwa vituo vya kazi na wengine kuteuliwa kuwa wafawidhi wa kanda.
Majaji waliohamishwa ni Jaji Agathon Nchimbi aliyekuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara kwenda Mahakama Kuu Ardhi, Jaji Sophia Wambura aliyekuwa Mahakama Kuu Kazi amehamishiwa Mahakama Kuu Ardhi Dar es Salaam.
Jaji Rehema Mkuye kutoka Mahakama Kuu Dodoma kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Jaji Kassim Nyangarika aliyekuwa Mahakama Kuu Biashara amehamishiwa Mahakama Kuu Sumbawanga.
Wengine waliohamishwa ni Jaji Hamisa Kalombola kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenda Mahakama Kuu Dodoma, Jaji Utamwa aliyekuwa Mahakama Kuu Dar es Salaam kahamia Mahakama Kuu Tabora, Jaji Richard Kibela alikuwa Mahakama Kuu Mtwara kahamia Mahakama Kuu Dar es Salaam, Jaji Haruna Songoro kutoka Mahakama Kuu Tabora kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.
HABARILEO
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuingilia kati suala la rushwa kwenye vituo vya mizani za kupimia uzito wa magari yanayosafirisha mizigo, akisema rushwa hiyo imekithiri.
Magufuli alitoa agizo hilo alipotembelea na kukagua kituo cha mizani cha Mpemba wilayani Momba, ambapo alipita kituoni hapo kwa kushtukiza, alipokuwa katika ziara yake ya kukagua barabara akielekea wilayani Ileje
Kupita kwa Magufuli kwenye mizani hiyo, kulitokana na yeye kujionea namna barabara ya kati ya Mbeya na Tunduma ilivyoharibiwa, kutokana na malori yanayosafirisha mizigo inayozidi uzito unaotakiwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda mpaka wa Tunduma kabla ya kuvushwa kuelekea nchi jirani.
Baada ya kufika kituoni hapo, alihoji maofisa waliokuwa zamu ni kwa nini barabara ionekane kuharibika upande mmoja wa magari yanayotoka Mbeya kwenda Tunduma badala ya pande zote mbili. Maofisa hao walimweleza kuwa kuharibika kwa upande huo wa barabara, kunatokana na malori kutoka Mbeya kwenda Tunduma, kutopimwa uzito kwakuwa hakuna mizani nyingine kabla ya kufika kituoni hapo.
Hata hivyo, majibu ya maofisa hayo hayakumridhisha waziri huyo na ndipo akatupia lawama utendaji kazi wa maofisa wa vituo vya mizani, akisema umekithiri kwa kupokea rushwa.
Alisema licha ya serikali kuwafukuza kazi watumishi 400 wa idara hiyo mwaka jana na kuajiri upya, bado tatizo la upokeaji rushwa kwa watumishi waliopo ni kubwa mno.
HABARILEO
Wabunge wametakakuwepo na udhibiti wa ongezekola watu kwa kutaka wanaume wadhibitiwe katika uzazi kama ilivyo kwa wanawake huku wengine wakitaka Serikali kuboresha rasilimali watu bila kudhibiti uzazi.
Miongoni mwa waliotaka wanaume wafungwe kizazi kama wanawake ni Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki Selina Kombani.
Wakichangia mada katika sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwa wabunge walisema ni vyema kudhibiti uzazi kwani inaweza  kusababisha athari kwa siku za baadaye kuwa na wazee wengi kuliko vijana.

AMBER ROSE NDANI YA NIGERIA

Amber Rose ndani ya Nigeria kwenye party ya miaka 10 ya D’Banj kwenye muziki

01
Kokomaster’, D’Banj mtu mkubwa kwenye muziki anayeiwakilisha Nigeria na Afrika kwenye ramani ya dunia hakika anajivunia mengi kwenye safari yake, mafanikio ya kufanya kazi na lebo ya GOOD MUSIC ya Kanye West ni zawadi kubwa kwake kwenye hii miaka kumi.
Dbanjfirstphotos-8-
Juzi January 31 kafanya  party Lagos, Nigeria, staa mwanamitindo kutoka Marekani ambaye alikuwa mpenzi wa Rapper Wiz Khalifa, Amber Rose unambiwa alishuka zake Lagos Naija, kumpa shavu Banj kwenye celebration ya miaka 10, Amber alikuwa MC kwenye event hiyo.
.
Amber Rose na D’Banj muda mfupi baada ya Amber kuwasili Nigeria.
.
Amber Rose baada ya kuwasili Nigeria.
Amber & Koko
Amber &KokO
Shaydee, Banky W, Ifeanyi Nwune
Shaydee, Banky W, Ifeanyi Nwune ni baadhi ya mastaa waliojitokeza kwenye party hiyo.
.
Amber Rose na D’Banj, mbele zinaonekana baadhi ya Tuzo alizowahi kushinda staa huyo.
 Kwenye stage Amber Rose hapa alijaribu kucheza Shoki wimbo wa Kesh, staa wa Nigeria

Huu ni wimbo wenyewe wa Kesh ft. Davido & Olamide, Unaitwa Shoki 

Sunday, February 1, 2015

SOKONI NGAMIANI TANGA, KUKU TUNAMYONYOA

 Wafanyabiashara wa kuku soko kuu la Ngamiani Tanga, wakinyonyoa kuku wa mteja baada ya kununua ukiwa ni utaratibu wa wachuuzi sokoni hapo endapo mteja atapendezwa na kulipa ujira wa shilingi elfu moja kwa kuku mmoja. Kuku mmoja alikuwa akiuzwa kati ya shilingi 8,000 hadi 10,000 kulingana na ukubwa wake.








Wachuuzi wa kuku soko kuu la Ngamiani Tanga wakiwanadi kuku sokoni hapo leo asubuhi. Kuku mmoja  alikuwa akiuzwa kati ya shilingi 8,000 hadi 10,000 kulingana na ukubwa wake.