Baada ya kuchoshwa na uonevu unaofanywa kwa mama yake, jamaa aamua kumfanyia ukatili dada yake…
Jamaa mmoja huko Taiwan
mama yake alikuwa anaumwa, baada ya kutibiwa Hospitali alirudishwa
nyumbani kwa mapumziko lakini mtoto wake wa kike hakuonekana kujali hali
hiyo ya mama yake, alikuwa akimsumbua mama huyo mara kwa mara kudai
hela kitu ambacho kaka yake hakupendezwa nacho.
Kaka huyo ambaye anaitwa Wang aliamua kumchoma kisu dada yake kutokana na kutopendezwa na usumbufu anaofanyiwa mama yake huo, ambapo dada huyo alifariki.
Wang muda
mwingi hukaa nyumbani kumhudumia mama yake na kufanya kazi zote za
nyumbani, ikiwemo kupika na kufanya usafi lakini dada yake hakuwa msaada
wowote kwa mama yake, ni mtu wa kushinda na rafiki zake.
Baada ya kufanya mauaji hayo alishafisha
eneo hilo, akamuandalia mama yake breakfast na chakula cha mchana,
baada ya mama yake kupumzika Wang aliwaita Polisi na kukiri kuhusika na
tukio hilo kutokana na kuchoshwa na matatizo ya nyumbani kwao na kudai
kuwa dada yake mara nyingi amekuwa akimuonea mama yao ikiwemo kumdai
fedha kila siku na kwenda kutumia na rafiki zake.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupiti,www.tangakumekucha.blogspot.com
No comments:
Post a Comment