Mkusanyiko wa Stori kubwa zilizopewa headlines kwenye Magazeti ya leo February 2, 2015
MWANANCHI
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amedokeza kuwa atakayekuwa mgombea wake wa urais baadaye mwaka huu ni yule ambaye hajajitokeza mpaka sasa.
Akihutubia jana katika sherehe za miaka 38 ya kuzaliwa kwa chama hicho mjini Songea, mkoani Ruvuma, Rais Kikwete alisema: “Wapo
watu wenye sifa zote za urais lakini hawajitokezi na hata wakiambiwa
kuwa wanaweza husema hawajajiandaa. Hawa ndiyo tunaowahitaji kwa kuwa
wanahitaji kukumbushwa tu.”
Kauli hiyo ya Rais Kikwete inaweza kuwa mwiba mchungu kwa baadhi ya
makada wa CCM ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakipita huku na kule
kutafuta uungwaji mkono, huku baadhi yao wakiwa wamepewa onyo kali
kutokana na kushiriki kampeni kabla ya muda na kushiriki vitendo ambavyo
ni kinyume na maadili.
Katika hotuba yake iliyorushwa moja kwa moja na vituo vitatu vya
televisheni, Rais Kikwete alisema chama hicho kitakuwa na mgombea bora
wa urais kwa kuwa upo utaratibu mzuri wa kumpata kwa kutumia kanuni
walizojiwekea. Pia alieleza kwa msisitizo kwamba kinachokatazwa ni
‘kukiuka kanuni na taratibu.’
“Oktoba tunachagua rais, mimi
nataka rais huyo atoke CCM. Chama kina mfumo wa kumpata mgombea mzuri wa
urais na nawahakikishia kuwa tutakuwa na mgombea bora wa urais na
wananchi hawatanung’unika:-Kikwete
Rais alieleza kuwa ni lazima CCM ishinde katika uchaguzi mkuu ujao
hasa kwa kuzingatia kuwa imekuwa ikifanya hivyo tangu mfumo wa vyama
vingi uanzishwe, zaidi ya miaka 20 iliyopita.
Hata hivyo, mwenyekiti huyo aliwatahadharisha wanachama wake kuwa ni
lazima wajiandae kukabiliana na upinzani uliopo na ili kufanikisha hilo,
aliwataka wale wote wenye nia kuanza kuwa karibu na wananchi ili
kusikiliza kero walizonazo.
NIPASHEJeshi la Polisi Wilaya ya Ludewa mkoani Njombe, limeingia katika kashfa baada ya askari wake kutuhumiwa kumuua raia.
Raia huyo ambaye ni mkazi wa mtaa wa Mdonga, fundi wa magari, Januari Mtitu (20), inadaiwa kuwa aliuawa kwa risasi na askari mwenye namba G 6352, Abduel Nyuki.
Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Juma Madaha, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa tayari askari anayetuhumiwa na raia wengine wawili, wamekamatwa.
Habari zinaeleza kuwa wakazi wa eneo la tukio, walipandwa na hasira na kumfanya Mkuu wa huyo wa Wilaya kulazimika kuwatuliza kwa kuwataka wapunguze hasira ili wasiwadhuru polisi wengine kwa sababu siyo wote waliohusika na tukio hilo.
Kauli ya Mkuu huyo wa Wilaya ilitokana na mgomo wa mafundi wa magari kukataa kutengeneza jeneza na kutaka kuandamana huku wakilitaka Jeshi la Polisi kulitengeneza wenyewe ama kulipa fedha kwanza ndipo litengenezwe.
“Sasa hivi tumechoka kuteswa na kunyanyaswa na polisi, wanaacha kukamata wahalifu badala yake wamewageukia wananchi ambao hawana hatia na leo hii wamemuua mwenzetu bila kosa,” mmoja wa mafundi hao alisema.
NIPASHE
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, amesema ameanza mchakato wa kuonana na Rais Jakaya Kikwete, kuwasilisha kilio na kushauriana naye juu ya nguvu kubwa inayotumiwa na Jeshi la Polisi kuwashambulia na kuwakamata wapinzani.
Kadhalika, amesema mazungumzo hayo yatalenga kuwekwa utaratibu wa Jeshi la Polisi kuvitendea haki vyama vya upinzani kuelekea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba, mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Prof. Lipumba alisema nguvu kubwa inayotumiwa na polisi dhidi ya vyama vya upinzani, haina lengo jema, bali kukandamiza haki za binadamu na demokrasia.
“Tunataka vyama vyote vitendewe haki na usawa mbele ya nguvu ya dola na siyo kukandamiza upande mmoja, hali hii ikiruhusiwa kuendelea na mwaka huu wa uchaguzi, ni wazi kuwa nchi itaingia katika machafuko:-Lipumba
“Vijana wa sasa siyo wa mwaka 2001, Polisi wasifikiri kuwa vijana na wananchi wataendelea kunyamaza na siku wakiamua kulipiza, hakika hakuna atakayepona…nawaomba wananchi wasilipize kisasi kwa askari wanaoishi nao uraiani.”
NIPASHE
Umoja wa Nchi Huru za Afrika (AU) umetoa heshima pekee kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na kumuenzi kwa kuamua kuwa moja ya majengo yake muhimu katika makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia, litapewa jina la Mwalimu Julius Nyerere.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere anapewa heshima hiyo kubwa kwa mchango wake katika ukombozi wa Bara la Afrika na kuliondoa Bara la Afrika kutoka kwenye ukoloni.
Uamuzi wa kuliita Jengo la Baraza la Amani na Usalama (Peace and Security Council) la Umoja huo Mwalimu Julius Nyerere Hall ulifikiwa juzi Jumamosi wakati wa kikao cha ndani cha marais wa nchi wanachama wa AU kilichofanyika makao makuu ya AU mjini Addis Ababa.
Akizungumza baadaye kwenye kikao hicho, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete aliwashukuru viongozi wenzake, wakiongozwa na Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, kwa kutoa heshima hiyo kubwa kwa mwanzilishi wa Taifa la Tanzania na kwa nchi ya Tanzania yenyewe.
Hoja ya kufanya uamuzi wa kuliita jengo hilo Mwalimu Julius Nyerere Hall ilitolewa ufafanuzi na Rais Mugabe ambaye ni Mwenyekiti mpya wa AU.
MTANZANIA
ASKARI wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Kikosi cha 27 Makoko kilichopo Musoma, Praiveti Wilfred Koko amekutwa ameuawa na kuondolewa sehemu ya viungo vya mwili katika eneo la kikosi hicho.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi mkoani Mara ilisema askari huyo MT-78227, aliokotwa katika eneo la jeshi Januari 30, mwaka huu saa sita mchana mwili wake ukiwa hauna baadhi ya viungo ukiweamo mguu wa kulia, viganja vya mikono yote na sehemu za siri.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Ernest Kimola, alisema upande wa mguu wa kushoto wa marehemu ulikutwa na jeraha lililokatwa na kitu chenye ncha kali hali inayoonyesha huenda askari huyo aliuawa na kutupwa kwenye eneo hilo.
Alisema huenda viungo vya askari huyo ambavyo havikukutwa vilikuwa vimeliwa na wanyama baada ya mwili huo kuonekana kukaa muda mrefu, kuanza kuharibika na kuingiliwa na wadudu.
MTANZANIA
JAJI Mkuu, Mohammed Othman Chande, amewahamisha majaji 27 wa Mahakama Kuu Tanzania akiwamo Jaji John Utamwa aliyehamishiwa Mahakama Kuu Tabora na Jaji Dk. Fauz Twaib aliyehamishiwa Mahakama Kuu Mtwara.
Uhamisho huo ulifanyika mwishoni mwa wiki ambako majaji wengine walibadilishwa vituo vya kazi na wengine kuteuliwa kuwa wafawidhi wa kanda.
Majaji waliohamishwa ni Jaji Agathon Nchimbi aliyekuwa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara kwenda Mahakama Kuu Ardhi, Jaji Sophia Wambura aliyekuwa Mahakama Kuu Kazi amehamishiwa Mahakama Kuu Ardhi Dar es Salaam.
Jaji Rehema Mkuye kutoka Mahakama Kuu Dodoma kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi, Jaji Kassim Nyangarika aliyekuwa Mahakama Kuu Biashara amehamishiwa Mahakama Kuu Sumbawanga.
Wengine waliohamishwa ni Jaji Hamisa Kalombola kutoka Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kwenda Mahakama Kuu Dodoma, Jaji Utamwa aliyekuwa Mahakama Kuu Dar es Salaam kahamia Mahakama Kuu Tabora, Jaji Richard Kibela alikuwa Mahakama Kuu Mtwara kahamia Mahakama Kuu Dar es Salaam, Jaji Haruna Songoro kutoka Mahakama Kuu Tabora kwenda Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara.
HABARILEO
Waziri wa Ujenzi Dk John Magufuli amevitaka vyombo vya dola kuingilia kati suala la rushwa kwenye vituo vya mizani za kupimia uzito wa magari yanayosafirisha mizigo, akisema rushwa hiyo imekithiri.
Magufuli alitoa agizo hilo alipotembelea na kukagua kituo cha mizani cha Mpemba wilayani Momba, ambapo alipita kituoni hapo kwa kushtukiza, alipokuwa katika ziara yake ya kukagua barabara akielekea wilayani Ileje
Kupita kwa Magufuli kwenye mizani hiyo, kulitokana na yeye kujionea namna barabara ya kati ya Mbeya na Tunduma ilivyoharibiwa, kutokana na malori yanayosafirisha mizigo inayozidi uzito unaotakiwa kutoka Bandari ya Dar es Salaam kwenda mpaka wa Tunduma kabla ya kuvushwa kuelekea nchi jirani.
Baada ya kufika kituoni hapo, alihoji maofisa waliokuwa zamu ni kwa nini barabara ionekane kuharibika upande mmoja wa magari yanayotoka Mbeya kwenda Tunduma badala ya pande zote mbili. Maofisa hao walimweleza kuwa kuharibika kwa upande huo wa barabara, kunatokana na malori kutoka Mbeya kwenda Tunduma, kutopimwa uzito kwakuwa hakuna mizani nyingine kabla ya kufika kituoni hapo.
Hata hivyo, majibu ya maofisa hayo hayakumridhisha waziri huyo na ndipo akatupia lawama utendaji kazi wa maofisa wa vituo vya mizani, akisema umekithiri kwa kupokea rushwa.
Alisema licha ya serikali kuwafukuza kazi watumishi 400 wa idara hiyo mwaka jana na kuajiri upya, bado tatizo la upokeaji rushwa kwa watumishi waliopo ni kubwa mno.
HABARILEO
Wabunge wametakakuwepo na udhibiti wa ongezekola watu kwa kutaka wanaume wadhibitiwe katika uzazi kama ilivyo kwa wanawake huku wengine wakitaka Serikali kuboresha rasilimali watu bila kudhibiti uzazi.
Miongoni mwa waliotaka wanaume wafungwe kizazi kama wanawake ni Mbunge wa jimbo la Ulanga Mashariki Selina Kombani.
Wakichangia mada katika sense ya watu na makazi ya mwaka 2012 kwa wabunge walisema ni vyema kudhibiti uzazi kwani inaweza kusababisha athari kwa siku za baadaye kuwa na wazee wengi kuliko vijana.
No comments:
Post a Comment