Tukio la mauaji yaliyotokea Hotelini.
Mhudumu wa Hoteli hiyo amesema wateja hao walilipia room kwa siku moja na kesho yake mwanaume huyo aliwaambia kuwa anaendelea na angelipia, baadae walimgongea ili alipie mteja huyo aliwaambia kuwa hafungui hadi Polisi waje, walichukulia utani ndipo walipomchukua mtu mmoja nakujifanya Polisi na kwenda kumgongea ndipo alipofungua na kukuta damu zimetapakaa kwenye chumba hicho.
Baada ya kukuta hali hiyo waliamua kuita Polisi ambao walifika na kukumkuta bado yuko ndani na walipomuuliza alisema kuwa amemuuwa mke wake, huku na yeye akiwa na majeraha yanayosemekana kuwa alitaka kujiuwa mwenyewe.
Ndungu wa mtuhumiwa amesema kuwa aliyeuwawa ni mke wa ndoa wa mtuhumia ambao walikuwa na ugomvi muda mrefu uliosababisha waishi tofauti na walipomwuliza mtuhumiwa kuhusu tukio hilo aliwaambia kuwa ameamua kumuuwa lakini hakutoa sababu ya kufanya mauaji hayo na baada ya kupatiwa matibabu mtuhumiwa yuko kituo cha Polisi Magomeni.
No comments:
Post a Comment