Thursday, April 2, 2015

SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETI YA LEO APRIL 02 TZ

Uchambuzi huu unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya Kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga. Kituo kinaongoza kwa kufaulisha wanafunzi wanaorisiti kidato cha pili hadi sita. Kituo kimesajiliwa na NECTA. Kipo Tanga mkabala na CRDB Bank simu 0715 772746

egMWANANCHI
Treni ya kisasa (Delux), kwenda Bara yenye mabehewa 22 ilianza safari yake ya saa 30 kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma ikiwa ni tofauti ya saa sita ikilinganishwa na safari ya treni ya zamani.
Kutokana na tofauti hiyo, abiria walioanza safari kwa furaha na matumaini jana saa tano asubuhi wanatarajiwa kufika Kigoma leo saa 11 jioni badala ya saa tano usiku.
Hata hivyo, abiria hao watalazimika kuingiza mikono yao zaidi mifukoni, kutokana na kiwango kipya cha nauli kuwa Sh79,400 badala ya Sh75,700 za awali kwa daraja la kwanza.
Huku nauli za daraja la pili ikishuka kutoka Sh55,400 hadi Sh,47,600 zile za daraja la tatu zimepanda kutoka Sh27,700 hadi Sh35,700.
Kwa mtazamo wa haraka, mabehewa hayo yanavutia yakilinganishwa na yale ya awali yaliyokuwa yamekithiri kwa uchakavu, yaliyokuwa yamejaa mende na yenye milango na madirisha mabovu.
Mabehewa hayo yana viti vya kutosha, huduma ya intaneti, swichi za umeme za kuchajia simu na kuunganisha kompyuta na safari zake zimeongezeka kutoka mbili hadi tatu kwa wiki.
Akizungumza muda mfupi kabla uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli Tanzania (TRL), Mhandisi Kipallo Kisamfu alisema wamelazimika kupandisha viwango vya nauli kutokana na gharama zitakazokuwa zinatumika katika uendeshaji wa treni hiyo.
Licha ya kuongeza kidogo kiwango cha nauli, dhamira yetu ni kuwapatia abiria huduma safi na ya raha… kila msafiri atasafiri akiwa ameketi kwenye kiti chake. Hakuna abiria atakayesafiri akiwa amesimama,” alisema na kuongeza:
“Treni inayozinduliwa leo inatumia mabehewa mapya 22 yaliyonunuliwa kutoka Korea Kusini na kichwa cha treni kiliundwa upya kwenye karakana ya TRL iliyopo Morogoro mabehewa mapya yamegharimu Serikali Sh28.6 bilioni.”
Kuhusu vituo vya ambavyo treni hiyo alisema itasimama kwenye vituo vikubwa ambavyo vingi ni vile vya miji, wilaya na mikoa.
Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Dk Shabaan Mwinjaka aliwataka abiria kuwa walinzi wa treni hiyo ili kuhakikisha usafiri huo unadumu.
“Kumekuwa na tabia ya watu kujiamulia kuharibu mali za umma, ninawaomba abiria mtakaopanda treni hii muwe walinzi wa wenzenu kwa sababu baadhi ya abiria wamekuwa na tabia ya kuchora kwenye viti,”  Dk Mwinjaka.
Mmoja wa abiria, Saida Roman alisema Serikali inahitaji kupewa pongezi kwa hatua hiyo kwani hivi sasa abiria wanaotumia usafiri wa treni kutoka Dar es Salaam kwenda Kigoma watasafiri kwa raha tofauti na ilivyokuwa zamani.
MWANANCHI
Wabunge wa upinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) jana walianzisha tafrani bungeni na kusababisha kikao cha Bunge kuvunjika saa 5.18 asubuhi baada ya kusimama na kupaza sauti wakishinikiza Serikali itoe kauli juu ya hatima ya uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapigakura na upigaji wa Kura ya Maoni kupitisha Katiba Inayopendekezwa.
Huku wakiwa wamesimama walikuwa wanapiga kelele wakisema, ‘hatutaki kuburuzwa’, ‘tumechoka kupelekeshwa’, Watanzania wapo njia panda’ na ‘tunataka majibu,’ ‘Bunge lisitumiwe kuilinda Serikali’, ‘Waziri Mkuu yupo bungeni kwa nini asitoe kauli’ na maneno mengine mengi bila mpangilio.
Wabunge hao wa vyama vya NCCR-Mageuzi, Chadema na CUF, kwa umoja wao walimtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutoa majibu hayo muda huohuo, kabla ya jioni kutoa hutuba na kuahirisha mkutano huo wa 19 wa Bunge.
Baadaye jana usiku katika hotuba yake ya kuahirisha Bunge hadi Mei 12, utakapoanza Mkutano wa 20, Waziri Mkuu Pinda alisema Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) itatoa taarifa siku za hivi karibuni kuhusu upigaji wa kura ya maoni.
“Ni dhahiri muda uliobaki kuanzia sasa ni mfupi lakini Tume ndiyo itakayotujulisha ratiba kamili,” alisema.
Kelele hizo zilitokana na hoja za wabunge wawili, Suleiman Jafo wa Kisarawe na yule wa Ubungo, John Mnyika waliotaka Bunge lisitishe shughuli zake zote lijadili suala hilo kwa kuwa ni muhimu na Taifa halielewi hatima yake, wakati Bunge lilikuwa linaahirishwa jana.
Spika wa Bunge, Anne Makinda alikataa suala hilo kujadiliwa, akisema ni hoja iliyowasilishwa katika mkutano uliopita, akataka Bunge liendelee na shughuli zake, lakini wabunge wa upinzani walikataa kukaa na wakaendelea kupaza sauti.
Hata alipobadili kauli akasema, “nimesema kauli itatolewa, wabunge hao walisisitiza itolewe papohapo. Hata alipowataka waondoke ndani ya ukumbi huo, wabunge hao ambao ni wachache ukilinganisha na wale wa CCM, walikataa, wakisema; “hatutoki hadi kauli itolewe.”
Kelele za wabunge hao zilimfanya Spika Makinda kutoa kauli kali, “Njooni mwendeshe (kikao) nyinyi basi. Njooni hapa mkae tena wote.”
Baada ya kuona kelele hizo zimedumu kwa dakika tatu, Spika Makinda alilazimika kusitisha shughuli za Bunge hadi baadaye (jioni), bila kutaja muda ambao Bunge lingerejea na kuwaacha wabunge wakiwa wamesimama katika makundi ndani ya ukumbi wakijadili tukio hilo.
Jafo ndiye aliyeanza kuomba mwongozo wa Spika akitaka chombo hicho cha kutunga sheria kisitishe kujadili jambo lolote lile, badala yake kijadili mustakabali wa Katiba Mpya, akitaka Serikali iwasilishe muswada wa sheria kwenye mkutano wa 20 wa Bunge (wa Bajeti) ili Katiba ya Mpito ipitishwe.
MWANANCHI
Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu, Jaji Mark Bomani ameshauri Kura ya Maoni ya Katiba Inayopendekezwa iahirishwe na badala yake Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) iendelee kuboresha Daftari la Wapigakura.
Pia, alisema Serikali iachane na mfumo wa uandikishaji wananchi wa Biometrick Voters Registration (BVR) kwa kuwa ilikurupuka bila ya kufanya maandalizi ya kutosha na fedha na vifaa havitoshi kuendeshea mpango huo.
Jaji Bomani alisema jana kuwa mujibu wa Tangazo la Rais, Kura ya Maoni itapigwa Aprili 30 mwaka huu, lakini walioandikishwa hawazidi milioni moja.
Alisema Serikali ikilazimisha upigaji kura, itasababisha mgogoro mkubwa na manung’uniko mengi nchini.
“Hadi hii leo, uandikishaji wapigakura bado unasuasua, zaidi ya watu milioni 20 wataweza kweli kuandikishwa katika wiki nne zilizobaki?
“Itakuwa ni muujiza kufanya hivyo na ni Mkoa wa Njombe tu ambao wanaendelea kuandikishwa,” Jaji Bomani.
Alisema Tume ya Jaji Joseph Warioba ya kukusanya maoni, ilifanya kazi kwa umakini na kukamilisha Desemba 2013 na kuitishwa Bunge Maalumu la Katiba liangalie ripoti ya Rasimu Iliyopendekezwa.
Alisema Bunge lilifanya kazi yake, lakini ilikuwa siyo nzuri, hivyo kusababisha baadhi ya wajumbe kutoka nje ya ukumbi kwa kutofautiana.
Pia, alisema baadhi ya mambo mazuri yaliyomo kwenye Katiba Inayopendekezwa yafanyiwe mabadiliko ili yatumike kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu.
NIPASHE
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Dodoma Mjini, Roda Ngimilanga, imemrudishia dhamana Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini, Johnson Minja.
Hatua ya kumfutia dhamana mfanyabiashara huyo ilizua mjadala mkali bungeni juzi, baada ya wabunge wengi kuilalamikia na kuituhumu serikali kwamba inahusika kuishawishi mahakama kuchukua hatua hiyo.
Wabunge hao walitaka Minja arudishiwe dhamana yake ili kuwezesha kufanyika kwa majadiliano kati ya serikali na wafanyabiashara ambao walikuwa wamegoma na kufunga maduka katika sehemu mbalimbali za nchi kushinikiza kiongozi wao arejeshewe dhamana yake.
Mahakama hiyo ilimfutia dhamana kiongozi huyo wa wafanyabiashara na kuamuru awekwe rumande kwa muda wa wiki moja kwa tuhuma za kuvunja kanuni za dhamana aliyopewa na mahakama hiyo Januari 28, mwaka huu.
Jana baada ya kusikiliza hoja zilizowasilishwa mahakamani hapo na  pande za utetezi na Jamhuri, Hakimu Ngimilanga alieleza kuwa Mahakama haioni sababu yoyote ya kuendelea kumshikilia Minja gerezani, kwani madai yaliyowasilishwa na Mwendesha Mashitaka wa Serikali, Rose Shio, hayana mashiko ya kisheria ya kumuondolea dhamana Minja.
Aidha, alisema kuwa kwa mujibu wa jalada la kesi hiyo, hakuna kifungu chochote cha dhamana ambacho mtuhumiwa amekivunja na kwamba kwa mujibu wa masharti ya dhamana husika, hakuna kifungu chochote kinachomkataza Minja kufanya mkutano na wanachama wake.
Baada ya kusikiliza hoja za pande zote mbili na kupitia jalada la kesi, ninatamka kuwa Minja ataendelea kuwa huru kwa masharti ya dhamana yake ya Shilingi milioni nne na wadhamini wawili,Hakimu Ngimilanga.
Kadhalika, alisema kuwa masharti mengi yanayodaiwa kuwa chanzo cha kufutwa kwa dhamana ya mtuhumiwa katika kesi iliyosomwa mahakamani hapo wiki moja iliyopita, hayakuandikwa katika jalada la kesi hiyo.
Shio aliitaka Mahakama kuendelea kumshikilia mshtakiwa kwa tuhuma kwamba hali ya amani nchini bado siyo shwari kutokana na migomo ya wafanyabiashara inayoendelea maeneo mengi nchini.
Pia Shio alidai kuwa wafanyabiashara wengi bado wanaigomea Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutumia mashine maalum ya kufanyia malipo  (EFD).
Kwa upande wake, Wakili wa Minja, Godfrey Wasonga, aliieleza Mahakama kuwa kwa mujibu wa ibara (13 (6) b na 15 (1) za Katiba ya nchi, mteja wake hakustahili kufutiwa dhamana na kuwa  jukumu la kuhakikisha kwamba wafanyabiashara wanafungua maduka siyo la mteja wake, bali la Jeshi la Polisi.
Hata hivyo, mwanasheria huyo aliiambia Mahakama kuwa kama kweli mteja wake alikuwa na makosa ambayo yalisababisha kufutiwa dhamana, Polisi walitakiwa kumkamata wakati ule ule walipobaini akiwa katika mwendelezo wa kufanya makosa hayo.
Hakimu huyo aliahirisha kesi hiyo kwa ajili ya kutajwa hadi Aprili 9, mwaka huu huku  Jeshi la Polisi likiendelea na upelelezi.
Kabla ya kuanza kwa kesi, idadi kubwa ya wafanyabiashara kutoka maeneo mbalimbali nchini walikusanyika kwenye eneo la Mahakama, wakisubiri kuletwa kwa Mwenyekiti wao huku polisi waliovaa sare na makachero wakiwa wamelizunguka eneo hilo kuimarisha ulinzi. Kabla mahakama hiyo haijamrejeshea dhamana mshtakiwa huyo, maduka katika maeneo kadhaa nchini yalikuwa yamefungwa.
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, aliwataka wafanyabiashara kufungua maduka yao wakati serikali ikiendelea kushughulikia tatizo hilo.
NIPASHE
Mchungaji Christopher Mtikila, ameiondoa mahakamani kesi ya kupinga serikali kupeleka bungeni Muswada wa kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi, baada ya jopo la majaji kumshauri kufanya hivyo kutokana na taarifa za kuondolewa bungeni.
Kesi hiyo ilifunguliwa na Mtikila dhidi ya Mwanasheria Mkuu, Watendaji wakuu wa serikali akiwamo Warizi Mkuu, Mizengo Pinda.
Hatua hiyo ilifikiwa jana mbele ya jopo la majaji watatu, likiongozwa na Mwenyekiti, Richard Mziray, akisaidiana na Jaji Lawrence Kaduri na Said Kihio katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.
Jaji Kaduri alihoji kama kuna haja ya kuendelea na kesi hiyo mahakamani wakati Ikulu imesema serikali haina mpango wa kuanzisha Mahakama hiyo na Bunge limeshauondoa muswaada huo.
Alisema kusikiliza kesi inayozungumzia muswada huo uliondolewa bungeni haina maana na hata maamuzi yake yatakuwa hayana mashiko kisheria.
“Watanzania hatujaelimishwa nini kinaanzishwa na kitakuwa na majukumu gani hali ambayo imetuacha tumechanganyikiwa … kuna mgawanyiko mkubwa mara maaskofu wanasema hili mara wabunge na wananchi pia wanasema mengine ili mradi tu kila pande inashindwa kuelewa nini haswa kipo mbele yetu,” alisema Mwenyekiti na kuongeza:
“Tuache kwanza wananchi wapate elimu ya kutosha ili wajue nini kinajadiliwa na hata kitapopitishwa wajue kuna faida gani wanapata.”
Akizungumza na Majaji hao, Mtikila alidai kuwa lengo la kufungua kesi hiyo ni pamoja na kunyoosha mkondo wa sheria kwa sababu wapo wanaovunja sheria na kupuuza kazi za Mahakama.
Jopo hilo lilimshauri Mtikila kwamba kama ana nia ya kuendelea na maombi mengine yaliyopo kwenye kesi hiyo aiondoe mahakamani  na kwenda kuandaa upya maombi yake yasiyokuwa na kipengele cha Muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Mtikila alikubaliana na ushauri wa jopo hilo liliondoa kesi iliyosajiliwa kwa namba 14, ya mwaka huu.
Mtikila alisema baada ya kuliondoa shauri hilo mahakamani anatarajia kuandaa maombi mapya dhidi ya Waziri Mkuu, Pinda na wenzake ili waende waieleze mahakama kwa nini waliandaa muswada huo.
MTANZANIA
Watoto 140 wenye umri kati ya miaka 10 na 21 wamekamatwa wilayani Hai mkoani Kilimanjaro wakilelewa katika misikiti mitatu tofauti.
Taarifa zilizopatikana wilayani hapa zinasema watoto hao wamekuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam kinyume cha sheria.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, watoto hao waligundulika baada ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Hai kupata taarifa na kuwafuatilia kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi, kati ya Machi 25 na 27 mwaka huu.
Taarifa hizo zimeyataja maeneo waliyokutwa watoto hao kuwa ni Misikiti ya Masjid Bilal, Masjid Othiman na Msikiti wa Kwa Kiriwe.
Taarifa hizo zimesema katika Msikiti wa Masjid Bilal uliopo Mtaa wa Kibaoni wilayani hapa, walikutwa watoto wa kiume 70 wanaotoka katika mikoa mbalimbali nchini.
Watoto wengine 50 wa kiume walikutwa katika Msikiti wa Masjid Othiman uliopo Mtaa wa Uzunguni ambao nao inasemekana wamekusanywa kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Taarifa hizo zinasema watoto wengine 27 walikutwa katika Msikiti wa Kwa Kiriwe ambako pia walikuwa wakifundishwa mafunzo ya dini ya kiislam na walimu Watanzania.
Mkuu wa Wilaya ya Hai, Anthoy Mtaka, alikiri kuwapo watoto hao wilayani kwake.
“Tukio hilo lipo na wanaohusika ni watu wanaotumia mwamvuli wa dini fulani kufanya mambo yasiyofaa katika jamii.
“Kwa hiyo naziomba mamlaka husika likiwamo Baraza Kuu la Waisalam Tanzania (BAKWATA) kutambua miskiti na shughuli zinazoendelea katika nyumba hizo za ibada.
Hili lazima walifanyie kazi kwa sababu hao vijana inasemekana wanafundishwa mazoezi makali ya kareti na judo katika nyumba hizo za ibada,” Mtaka.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Geofrey Kamwela, alisema atazungumzia tukio hilo leo.
Kupatikana kwa watoto hao ni mwendelezo wa matukio ya watoto wanaolelewa kinyume cha sheria mkoani Kilimanjaro baada ya matukio mawili ya aina hiyo kuripotiwa hivi karibuni.
La kwanza lilihusisha watoto 18 na la pili lilihusisha watoto 11 waliokutwa katika maeneo ya Lyamungo wilayani Hai.
MTANZANIA
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda amemwandikia barua Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima akimtaka afike mbele ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya kwa mahojiano.
Inaelezwa kuwa Makonda alimtumia Askofu Gwajima barua hiyo Machi 30 mwaka huu, akiwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ.
Hata hivyo, kiongozi huyo wa kiroho amegoma akisema hawezikwenda ofisini kwa mkuu huyo wa wilaya kwa mahojiano. Mmoja wa wasaidizi wa Askofu Gwajima alisema jana kuwa hatua ya Makonda kumtumia barua haikumpendeza kiongozi huyo wa kanisa.
Makonda alikuja katika Hospitali ya TMJ na kudai amekuja kumwona Askofu Gwajima huku akiwa amebeba barua yake. Baada ya kumwuliza hali ya maendeleo ya afya yake alitoa barua na kumkabidhi jambo ambalo halikuwa jema.
“Baada ya muda Askofu Gwajima alituita wasaidizi wake na kutueleza kuwa amepewa barua ya wito kwa DC, sasa tukajiuliza askofu anaumwa. Je, inakuaje aende tena katika mahojiano na mkuu wa wilaya? “Na kama ni hivyo nini kazi ya polisi maana wamemuhoji tangu siku ya kwanza baada ya kumkamata.
Mtu anahojiwa na polisi sasa inakuaje tena aitwe na DC ahojiwe na kamati ya ulinzi? Amesema hatokwenda,” alisema msaidizi huyo wa Gwajima ambaye hakutaka jina lake litajwe gazetini.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda alitoa ufafanuzi wa barua yake hiyo, ambapo alijibu kwa kifupi kuwa ni kweli amemwandikia barua ya wito kiongozi huyo. Alipoulizwa ni hatua zipi Askofu Gwajima atachukuliwa kwa kutaa kutii wito huo, Makonda alisema. “Kuhusu hatua subirini mtaziona wenyewe” alisema mkuu huyo wa wilaya.
Gwajima kuripoti polisi Wakati hohuo, Askofu Gwajima leo anatarajiwa kuripoti katika Kituo Kuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kuendelea kuhojiwa kuhusiana na tuhuma zinazomkabili.
Gwajima aliachiwa kwa dhamana juzi baada ya kutoka katika Hospitali ya TMJ ambako alikuwa amelazwa kwa matibabu baada ya kuanguka ghafla wakati akihojiwa na polisi.
Mwanasheria wa Gwajima, John Mallya alisema baada ya kuruhusiwa juzi, leo anatakiwa kuripoti tena katika kituo hicho kuendelea na mahojiano. “Polisi walituambia twende kesho (leo) kwa mahojiano kwa sababu yalikuwa hayajakamilika… lakini tunaamini polisi wanaweza kumruhusu kurudi nyumbani kupumzika au kuendelea na mahojiano mengine, Mallya.
Alisema mpaka sasa anaendelea vizuri na matibabu na afya yake inaendelea kuimarika siku hadi siku tofauti na alivyokuwa awali. Gwajima alifikishwa polisi kwa madai ya kumtukana na kumkashifu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Wakati anahojiwa alianguka na kuzimia hali iliyosababisha akimbizwe katika hospitali ya polisi Kurasini kabla ya kuhamishiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) na baadaye Hospitali ya TMJ kwa matibabu zaidi.
Juzi Askofu Gwajima alikwenda polisi akiwa amepandishwa kwenye baiskeli maalumu ya wagonjwa.
HABARILEO
Siku chache baada ya Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta kutaka uangaliwe uwezekano wa kushusha nauli za vyombo vya usafiri nchini, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) imesema inatekeleza agizo hilo na kwamba nauli za daladala na mabasi ya mikoani zitashuka wakati wowote kuanzia sasa.
Imeongeza kuwa, licha ya bei ya mafuta kupanda kidogo jana, hakutaathiri kushuka kwa nauli, kwani ukokotoaji utafanyika kwa wastani wa bei ya mafuta ilivyoshuka kwani haitapanda kwa kiasi kikubwa kwa mara moja.
Hayo yalisemwa jana na Meneja Mawasiliano wa Mamlaka hiyo, David Mziray aliyesema wanatekeleza agizo la Waziri Sitta aliyetaka nauli zishuke kufikia kesho, lakini wamechelewa kutokana na muda wa kuwasilisha maoni kwa wadau waliopewa siku 14 kufikia ukomo leo.
Tunawahakikishia wananchi kuwa baada ya kumaliza siku za kupokea maoni ya wadau hususan wamiliki wa mabasi ya daladala waliopewa siku 14, mchakato huu utakwenda haraka na mapema iwezekanavyo tutatangaza nauli hizo mpya,” alisema.
Mziray alisisitiza kuwa hakuna sababu ya kutoshusha nauli, bali wanafuata taratibu na kanuni hivyo kuwataka wananchi kuwa na subira kwa siku chache zijazo.
Wiki hii, Waziri Sitta aliwataka Sumatra kuharakisha mchakato huo wa kushusha nauli ufanyike haraka iwezekanavyo na ifikapo kesho wawe wametangaza nauli hizo mpya, kwani kwa muda mrefu bei za mafuta zimeshuka kutoka zaidi ya sh 2,200 hadi chini ya Sh 1,800.
Wadau wa usafiri walipendekeza kupunguzwa kwa nauli za mabasi yaendayo mikoani kwa viwango vya kati ya asilimia 15 na 25 huku wakitaka nauli za daladala zipungue kutoka Sh 400 hadi Sh 300 kwa njia ya umbali wa kilometa 10.
Walitaka kwa mabasi ya kawaida kwa Moshi na Arusha (Sh 17,000 badala ya Sh 22,700), Mwanza (Sh 32,369 badala ya Sh 42,000), Mbeya (Sh 23,365) badala ya Sh 30,700), Bukoba (Sh 40,756 badala ya Sh 55,000) na Dodoma (Sh 12,678 badala ya Sh 16,700). Kwa usafiri wa daladala wamesema wanataka iwe
HABARILEO
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu imependekeza kwa Serikali iongeze adhabu ya faini kutoka Sh milioni tatu na kifungo kisichopungua miezi sita na kuwa faini ya Sh milioni tano na kifungo kisichopungua miezi sita kwa wale wote watakaotuma katika mtandao taarifa za uongo.
Aidha, kamati hiyo imependekeza katika adhabu kwa watu wanaonyanyasa wenzao kupitia mtandaoni, adhabu yao iongezwe kutoka kifungo cha mwaka mmoja na kuwa kifungo cha miaka mitano.
Akiwasilisha maoni ya Kamati hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Uhalifu wa Mtando wa mwaka 2015, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Peter Serukamba alisema adhabu zilizowekwa katika sheria hiyo hazitoshelezi kulingana na athari za makosa hayo.
“Kamati imeona umuhimu wa kuongeza adhabu hizi katika maeneo haya, kutokana na ukweli kuwa kumekuwa na wimbi kubwa la watu wanaodhalilisha utu wa watu wengine katika mitandao ya kompyuta jambo lililoathiri watu wengi, familia, jamii na nchi kwa ujumla,” alisema Serukamba.
Alisema kamati hiyo, pia inashauri uwekwe utaratibu wa Serikali kuchukua hatua za ufuatiliaji kabla ya mtu aliyenyanyaswa kuripoti. “Hii ihusishe mfumo wa kuweza kumtambua mtu aliyesambaza picha ama taarifa hizo.
” Awali akiwasilisha maelezo ya muswada huo, Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, alisema kutokana na kukua kwa matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), kumesababisha kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo kuibuka kwa makosa ya mtandao.
Alitaja makosa ya mtandao yaliyokithiri kwa sasa kuwa ni makosa dhidi ya faragha, usalama na upatikanaji wa taarifa za kompyuta na mifumo ya kompyutam makosa yanayohusu maudhui, makosa dhidi ya mifumo ya kompyuta na makosa ya kawaida yanayofanywa kwa kutumia mitandao.
Alisema waathirika na waathirika wa makosa hayo ni pamoja na Serikali, sekta binafsi, watu binafsi na jamii kwa ujumla na takwimu kutoka jeshi la polisi zinaonesha kuwa makosa ya uhalifu wa mtandao yaliyoripotiwa na kuchunguzwa kati ya mwaka 2012 hadi Agosti mwaka jana ni 400.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

Wednesday, April 1, 2015

AMKA NA MAGAZETI NA KUMEKUCHA BLOG

Magazeti yanaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha  Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita kwa wale ambao wanaorisiti. Pia kituo kinatoa kozi za Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Kila siku asubuhi na mapema  uamkapo hakikisha unaperuzi www.tangakumekucha.blogspot.com kwa kupata kusarasa mwanzio mwisho na kujua kila kilichojiri ndani na nje ya nchi

AJIFUNGUA MAPACHA WATATU KWA MPIGO KIGOMA

AJIFUNGUA WATOTO WANNE KWA MKUPUO-KIGOMA


MKAZI wa Kijiji cha Buzebazeba  Manispaa ya Kigoma Ujiji, Zuwena Abdu (29)  amejifungua watoto mapacha wanne kwa mkupuo katika Hospital ya Mkoa wa Kigoma (Maweni).
Zuwena alisema  watoto aliojifungua wenye jinsia ya kiume ni watatu na mmoja ambaye ni wa mwisho ana jinsia ya kike ,wa kwanza akiwa na uzito wa kilo 1.8,pili 2.5 wa tatu 1.7 na wanne 1.7.
Alisema watoto hao alijifungua jana majira ya saa kumi na mbili jioni salama kwa njia ya kawaida 
Hutopitwa na habari yoyote inayonifikia na niko tayari kukutumia kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

HOJA YA MNYIKA YAZUA TAFRANI BUNGENI

Katika zile zilizoingia kwenye Headline leo Bungeni ipo hii ya John Mnyika …

mnyika2Wakati kikao cha Bunge kikiendelea leo Dodoma, Mbunge wa Ubungo John Mnyika alitaka kujadiliwe jambo la dharura kuhusu zoezi la uandikishwaji la wapiga kura.
Mpaka sasa tunavyozungumza zoezi la uandikishaji halijakamilika hata kwa mkoa mmoja tu wa Njombe na Watanzania nchi nzima wako kwenye sintofahamu, lini hasa wataandikishwa kabla ya kura ya maoni ya katiba mpya, jambo hili ni la dharura kwasababu ilikwisha tolewa hoja ya dahraura juu ya jambo hili kwenye mkutano uliopita wa Bunge, ukaagiza kamati ya Bunge ishughulikie na majibu yatolewe kwenye mkutano huu wa Bunge sasa leo mkutano unafungwa bila majibu kutolewa tusitishe shughuli zote tuhakikishe majibu yanatolewa leo
Katika mkutano huu nimeomba muongozo juu ya jambo hili mara mbili na mara zote Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu naamini umeipa maelekezo ya kutoa majibu lakini inakwepa kutoa majibu.
Katika mazingira kama haya hakuna sababu yoyote ya kuendelea na mjadala wowote mwingine kwenye kikao hiki cha Bunge, wala  kusubiria chochote tupate majibu kwenye mkutano huu wa Bunge ili tuweze kufanya kazi ya kuishauri na kuisimamia Serikali, Waziri Mkuu yuko hapa anaweza kutoa majibu hapa na tukajadili hapa“–Mbunge John Mnyika.
Lakini Spika Makinda akasema hoja hiyo inafanana na hoja ambayo ilitangulia hivyo haiwezi kujadiliwa, kitu ambacho kilisababisha mvutano wa Wabunge.

MWENYEKITI WA WAFANYABIASHARA ACHIWA KWA DHAMANA

MWENYEKITI JUMUIYA YA WAFABIASHARA AACHIWA KWA DHAMANA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania, Johnson Minja, (mwenye koti la kahawia), akisindikizwa na mawakili na wafanyabiashara wenzake.MWENYEKITI  huyo wa Jumuiya ya Wafanyabiashara nchini,  ameachiwa kwa dhamana leo jijini Dodoma baada ya kushikiliwa kwa siku sita kufuatia kuondolewa dhamana ya awali kwa madai ya kukiuka masharti ya dhamana. 
  Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Dodoma ikiwa ni siku moja baada ya suala lake kuibuliwa bungeni mjini Dodoma kwa baadhi ya wabunge kuitaka serikali kukaa na kuangalia namna ya kuweza kumaliza mgogoro uliopo kwa kupatiwa dhamana kwa mwenyekiti huyo.
Kushikiliwa kwa Minja kumesababisha kuwepo migomo ya wafanyabiashara wenye maduka  katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo Tanga waliokuwa wamefunga maduka yao kushinikiza kuachiwa kwa mwenyekiti wao huyo.

TEKE LA BEKI WA SLOVAKIA LAZUA UTATA

Teke la Beki wa Slovakia kwa Daniel Kolar wa Czech kwenye headlines…

tekeMatukio ya ajali za uwanjani yamekuwa yakiripotiwa kila wakati na tayari kuna rekodi ya matukio makubwa yaliyowahi kutokea viwanjani na kuleta madhara makubwa kwa wachezaji husika.
Jana kulikuwa na ratiba ya mechi za kirafiki kwa nchi mbalimbali duniani ikiwemo ile ya England kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Italy ikiwa ugenini pamoja na ile ya Slovakia kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Czech.
juuWakati Slovakia jana ikiibuka na ushindi huo katika mchezo wa kirafiki beki wa timu hiyo Martin Skartel alimpiga teke la uso  Daniel Kolar wa Czeck na kumsababishia maumivu makali.
chafuNi halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

VIMBWANGA VYA WALIMWENGU

Baba mdogo wa marehemu apigwa, kisa ni kuzuia mwili wa Marehemu usiingie kwenye nyumba yake

rip_logo_farbig_rotMzee mmoja amepigwa huko Kimara Dar, baada ya kijana aliyekuwa anaishi nae ambae ni mtoto wa kaka yake alipata ajali na kufariki, wakati wa mazishi mzee huyo akakataa maiti isipelekwe nyumbani kwake kwa madai kuwa anamdai marehemu.
Kijana ambae ni rafiki wa marehemu amesema Mzee huyo alikataa maiti isiingie nyumbani kwake kwa madai kuwa ni uchuro na anamdai marehemu shilingi laki tatu, wakavunja geti na kuingia ndani lakini bado aliwakatalia, wakaamua kwenda kwenye uwanja wa mpira ili watu wapate nafasi ya kuaga mwili wa Marehemu.
Mwenyekiti wa eneo hilo alifika akamshauri mzee huyo aende uwanjani kuaga, alipofika vijana hao walianza kumpiga na kumzuia kusafiri na mwili wa marehemu kwenda Moshi kwa ajili ya mazishi.
Mzee huyo alipoulizwa sababu ya kukataa maiti isiingie ndani kwake alikataa kuzungumza.

SENETA KENYA AJIUZULU KUPISHA UCHUNGUZI

Senator wa Nairobi Mike SONKO leo kwenye HEADLINES nyingi za Kenya..

MIKE-SONKO-e1420670792211Senator wa Nairobi Mike Sonko huenda watu wengi wakamfahamu zaidi yeye kuliko viongozi wengine walio kwenye ngazi za juu Kenya, mavazi yake.. maisha yake.. viko tofauti sana na jinsi viongozi wengine walivyo.
Hii ni story kubwa ambayo nimekutana nayo leo imeandikwa zaidi kwenye mitandao ya Kenya, inahusu Senator huyo kujiuzulu kutokana na kutajwa kwenye Ripoti ya kashfa ya Rushwa, ambapo jana March 31 2015 Taasisi ya Kupambana na Rushwa na Ufisadi Kenya ilitaja majina zaidi ya 100 ya watu ambao wako kwenye kashfa za rushwa.
Baada ya jina lake kutajwa alikuwa kiongozi wa kwanza kutangaza kujiuzulu huku akisema kwamba anahitaji kazi ya uchunguzi juu ya kashfa hizo ifanyike kwa uhuru kabisa huku yeye akiwa nje ya ofisi yake.
Sonko amesema anatii sheria za nchi yake, anamheshimu Rais Kenyatta kwa hiyo anachokifanya ni kupisha uchunguzi kama ambavyo Rais Kenyatta ameagiza kwamba kila aliyetajwa anatakiwa aachie ofisi ili ufanyike uchunguzi juu ya tuhuma hizo.
Headlines zenye story za Senator huyu ni nyingi, lakini moja ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara ni ishu ya wapi anatoa pesa za kutolea huduma kama za magari ya Ambulance, Breakdown, Zimamoto, bure kabisa kwa watu wake wa Nairobi?
Story ambayo imeripotiwa na Radio Jambo Kenya..

MESSI AMNYANYASA RONALDO

Orodha nyingine jinsi Lionel Messi alivyompoteza Cristiano Ronaldo

doooo imetoa orodha ya wachezaji bora katika vipengele vitano tofauti  ambapo mastaa mbalimbali wameweza kuonekana.
Katika chati hiyo Gael Clichy wa Manchester City amefanikiwa kuwa beki bora wa kulia huku Mesut Ozil wa Arsenal akichaguliwa kama kiungo bora mshambuliaji sambamba na Eden Hazard wa Chelsea.
mesiKwa upande wa washambuliaji Lionel Messi mwenye mabao 19 amefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwa kupata pointi 100 akifatiwa na Arjen Robben mwenye 92 huku nafasi ya tatu ikishikwa na Bas Dost Wolfsburg mwenye pointi 72.
Cristiano Ronaldo ambaye amefunga mabao sita tangu ashinde tuzo ya Ballon d’Or iliyotolewa mwezi January anakamata nafasi ya 29.
Orodha ya washambuliaji 10 bora Ulaya
1. Lionel Messi, Barcelona (100)
2. Arjen Robben, Bayern Munich (92)
3. Bas Dost, Wolfsburg (77)
4. Luis Suarez, Barcelona (71)
5. Diego Costa, Chelsea (61)
=6. Harry Kane, Tottenham Hotspur (57)
=6. Marco Reus, Borussia Dortmund (57)
8. Lucas Barrios, Montpellier (56)
9. Pierre-Emerick Aubameyang, Borussia Dortmund (55) 
10. Christophe Mandanne, Guingamp (54)
Viungo 10 bora washambuliaji
1. Eden Hazard, Chelsea (100)
=1. Mesut Ozil, Arsenal (100) 
3. Jesus Navas, Man City (86)
4. Kevin de Bruyne, Wolfsburg (85)
5. Shinji Kagawa, Borussia Dortmund (84)
6. Marek Hamsik, Napoli (79) 
7. David Silva, Man City (77) 
8. Maximilian Meyer, Schalke (73)
=9. Roberto Pereyra, Juventus (72)
=9. Javier Pastore, PSG (72) 
Mabeki 10 bora wa kati
1. Emir Spahic, Bayer Leverkusen (100)
2. Martin Demichelis, Man City (89)
3. Mats Hummels, Borussia Dortmund (79)
4. Chris Smalling, Man Utd (76)
5. Thiago Silva, PSG (71)
=6. David Luiz, PSG (69)
=6. Stefan de Vrij, Lazio (69)
8. Marcos Rojo, Man Utd (68)
=9. Konstantinos Manolas, Roma (64)
=9. Neven Subotic, Borussia Dortmund (64)
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia , niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

BIBI MWENYE UMRI MKUBWA ZAIDI DUNIANI, ANA HIKI CHA KUSEMA

Bibi aliyekuwa kwenye rekodi ya mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani, kingine kuhusu yeye leo kiko hapa

Misao-Okawa_2840965b
Kuna wakati niliwahi kuhisi kwamba huenda huku kwetu Afrika tunavunja rekodi nyingi sana ila hazipati nafasi kusikika duniani kote kwa sababu nyingi, moja ni ishu ya kutokuwa na utaratibu mzuri wa kuhifadhi kumbukumbu.
Jamii zetu zamani hazikuwa na utaratibu mzuri wa utaratibu huo kwa vile vitu kama vyeti vya kuzaliwa havikuwepo, wenzetu walikuwa na utaratibu mzuri miaka mingi iliyopita hivyo waliweza hata kuitambua siku, tarehe na mwaka aliozaliwa Misao Okawa, ambaye alikuwa kwenye kumbukumbu za Kitabu cha Guiness.
oldest28n-1-webRekodi zilizomuingiza Misao Okawa kwenye kitabu hicho mwaka 2013 ni ile ya mtu mwenye umri mkubwa zaidi duniani pamoja na rekodi ya mwanamke mwenye umri mkubwa zaidi duniani.
Misao Okawa amefariki akiwa na umri wa miaka 117, kumbukumbu zinaonesha alizaliwa March 5 1898, ameacha watoto watatu na wajukuu wanne.
Wakati wa birthday yake mwaka huu alisema siri ya kuishi muda mrefu ni ratiba yake ya kulala kwa saa nane kila siku na kula sushi, chakula alichokipenda zaidi.

STEVEN GERRARD NA MJENGO WAKE MPYA ATAKAPOTUA GALAXY

Mazingira mapya ya Steven Gerrard baada ya kuondoka Liverpool…(Pichaz)

mansion3Mwishoni mwa msimu huu kiungo wa Liverpool Steven Gerrard atakuwa akiiaga timu yake hiyo baada ya kuitumikia kwa miaka 17 na kuhamia katika klabu mpya ya Galaxy ya Marekani ambapo ametengewa dau kubwa kwa ajili ya kwenda kuitumikia.
mansionGalaxy imemwandali kiungo huyo hatari na kipenzi cha mashabiki wengi maisha mazuri akiwa na timu hiyo ikiwa ni pamoja na mshahara mzuri na jumba la kifahari ambalo unaambiwa thamani yake ni pauni milioni 16.8.
mansion2
Steven Gerrard akiwa na familia yake
Gerrard atahama Liverpool akiwa tayari amedumu kwa miaka 17 sambamba na mkewe Alex na mabinti zake watatu katika jumba hilo lililopo kwenye ufukwe wa Malibu Magharibi mwa Marekani.
mansion3
mansion4
mansion5
mansion6Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu  tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com

SOMA MAKUBWA YALIYOANDIKWA MAGAZETI YA LEO, APRIL 01 TZ

Uchambuzi huu wa magazeti unaletwa kwenu kwa hisani kubwa ya kituo cha Elimu Cha Candle Education Centre Tanga, kituo kinaongoza kufaulisha wanafunzi kidato cha pili hadi cha sita kwa wale ambao wanarisiti Kituo pia kinatoa kozi ya Kiingereza na Computer. Wapo Tanga mkabala na Bank ya CRDB simu 0715 772746

LATENIPASHE
Muswada wa Mahakama ya Kadhi umeondolewa bungeni na sasa hautajadiliwa katika Mkutano wa 19 wa Bunge unaohitimishwa leo mjini hapa.
Huu ni muswada wa tatu kuondolewa Bungeni baada ya ile miwili ya sekta ya habari ambayo ni muswada wa Sheria ya kupata Taarifa wa mwaka 2015 na ule wa sheria ya huduma wa Vyombo vya Habari iliyoondelewa mwishoni mwa wiki iliyopita.
Muswada huo ulipangwa kuwasilishwa Bungeni leo, lakini serikali imeamua kuuondoa kutokana na hofu ya kutokea mpasuko nchini.
Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, akizungumza jana ofisini kwake alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi hautakuwapo tena katika mkutano huo.
Dk. Kashilila alisema haijulikani ni lini utawasilishwa bungeni kwa sababu Mkutano wa Bunge ujao unaotarajia kufanyika Mei, utakuwa mahsusi kwa ajili ya bajeti.
“Waziri Mkuu alivyosema wataangalia na kushauriana kimsingi, alitoa maneno ya busara tu au ilikuwa kauli ya mtu mzima, lakini huu muswada hautakuwapo,” alisema.
Dk. Kashilila alisema hali iliyojitokeza Jumapili iliyopita wakati wa semina ya wabunge haikuwa nzuri kutokana na mvutano mkali miongoni mwa wabunge.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alipoulizwa kuhusu kama muswada huo utawasilishwa bungeni, alisema hakuwa na majibu badala yake alitaka suala hilo iulizwe ofisi ya Spika.
“Suala hili usiniulize, nenda Ofisi ya Spika au muulize huyu (Magati) ambaye yupo sekretarieti,” alisema huku akiwa na haraka kuelekea ofisini kwake.
Naibu Spika, Job Ndugai, akizungumza nje ya ukumbi wa Bunge muda mfupi baada ya kuahirisha Bunge, alisema muswada wa Mahakama ya Kadhi hautawasilishwa bungeni leo.
“Huo muswada hauwezi kuletwa bungeni kutokana na hali ilivyo,” alisema Ndugai bila kufafanua zaidi.
Naye Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Asha-Rose Migiro, alipoulizwa kama muswada huo utawasilishwa bungeni alimtaka mwandishi asimuulize maswali yanayohusiana na muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Sitaki kabisa kuulizwa suala la Muswada wa Mahakama ya Kadhi, kwanza wewe unatoka gazeti gani, “alijibu Dk. Migiro kwa hasira huku akiingia kantini.
Katika hatua nyingine, juzi jioni maaskofu zaidi ya 40 kutoka mikoa yote nchini, walikutana na wabunge katika ukumbi wa Kanisa La Kiinjili la Kilutheli (KKKT) mjini Dodoma kujadiliana suala la muswada wa Mahakama ya Kadhi.
Baadhi ya wabunge waliohudhuria mkutano huo walisema kuwa katika mkutano, maaskofu walitoa azimio kuwa muswada huo usiwasilishwe bungeni kwa kuwa hatua hiyo inaweza kuhatarisha amani iliyoko nchini.
NIPASHE
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kagera linawashikilia watu wawili kwa tuhuma za kukutwa na viungo vya mtu mwenye ulemavu wa ngozi (albino).
Watu hao wanatuhumiwa kufukua kaburi la mtu huyo na kuchukua kila kiungo cha mwili wa mtu huyo aliyejulikana kwa jina la Bartazar John, aliyefariki mwaka 1991.
Hatua hiyo imechukuliwa na jeshi hilo zikiwa zimepita siku saba tangu watu wengine wawili kutiwa nguvuni kwa tuhuma za kuhusika  kuuza viungo vya marehemu Wilaya ya Muleba, mkoani humo.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Henry Mwaibambe, alisema watu hao walikamatwa Machi 27, mwaka huu, katika nyumba moja ya kulala wageni, iliyoko eneo la Kyaka, Wilaya ya Missenyi baada ya kukutwa wakiwa na baadhi ya viungo hivyo, ambavyo walikuwa wanakwenda kuviuza.
Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Laston Faustine (41), ambaye ni mkazi wa Lukulaijo aliyekutwa na mfuko uliokuwa umehifadhi mifupa mitatu ya binadamu na mwingine ni January Korongo (43), mkazi wa Kadengesho, wiyani Karagwe.
Kamanda Mwaibambe alisema baada ya kumbana, mtuhumiwa wa kwanza, Laston aliliambia Jeshi la Polisi kuwa aliyempa viungo hivyo ni mwenzake, January, kwa ajili ya kuviuza kwa Sh. milioni 20.
Baada ya kuhojiwa, January alikiri kufukua kaburi la mjomba wake, aitwaye Baltazari aliyekuwa na ulemavu wa ngozi albino pia mlemavu wa viungo, ambaye alifariki dunia mwaka 1991 na walifukua kaburi lake mwaka 2009.
Mwaibambe alisema baada ya kumhoji zaidi mtuhumiwa huyo, alikubali kuongozana na polisi hadi nyumbani kwake, ambako alionyesha fuvu la kichwa, mifupa mitatu ya miguu pamoja na mifupa ya sehemu mbalimbali, ambayo ilikuwa imefungwa kwenye mfuko nje ya nyumba yake.
Polisi waliomba kibali cha Mahakama Wilaya ya Karagwe kuruhusiwa kufukua kaburi hilo ili kuhakikisha kama kweli kuna mabaki ya mwili huo, lakini hakuna kilichopatikana.
NIPASHE
Jukwaa la Wakristo Tanzania, limesema linashangazwa na tabia ya baadhi ya viongozi wa serikali wenye tabia ya kuitisha mikutano wanayoiita ni ya viongozi wa dini huku ikiwa siyo rasmi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Jukwaa hilo, imeeleza kuwa viongozi hao wamekuwa chanzo cha mvutano uliopo baina ya dini mbili na kwamba watakuwa chanzo cha kuvurugika kwa amani nchini.
Taarifa hiyo ambayo imesainiwa na Mkuu Habari na Mawasiliano wa Baraza la Kikiristo Tanzania (CCT), Mchungaji John Kamoyo, ilisema jopo la Maaskofu kutoka TEC, CPT lilikutana Machi 30, mwaka huu, mjini Dodoma, kuondoa dhana kuwa linaongozwa na hasira na mihemko katika kufikia maamuzi linavyoyafanya kama wengine wanavyotafsiri bali linasukumwa kwa upendo wa wananchi ili kujenga taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano.
Kamoyo alisema Machi 03, 2015 Waziri Mkuu aliitisha mkutano kupitia Mchungaji mmoja ambapo hakuna kiongozi wa taasisi au Kanisa aliyeshiriki, na kwamba Machi 28, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, alikutana na kikundi ambacho sio rasmi yaani Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam.
“Maaskofu tuliokutana Dodoma hatuongozwi na hasaira wala mihemko katika kufanya uamuzi kama wengine wananavyotafsiri, tunafikia uamuzi baada ya maombi kwa upendo wa wananchi na kujenga taifa lenye umoja na amani,” alisema Mchungaji Kamoyo.
Kamoyo alisema walikewenda Dodoma kufuatilia kwa kina Muswada wa Sheria mbalimabali za mwaka 2014 pamoja na mrekebisho mengine ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964.
MWANANCHI
Siku tano baada ya Rais Jakaya Kikwete kusema kuwa tamko la Jukwaa la Wakristo (TCF) kuwataka waumini wao kupigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa lilikuwa la hasira, viongozi hao wamejitokeza tena na kusisitiza kwamba msimamo wao huo utabaki kama ulivyo.
Katika tamko pamoja walilolitoa jana baada ya kukutana juzi mjini Dodoma, viongozi hao wamemtahadharisha Rais Kikwete kuwa kuendelea kupigia debe Katiba Inayopendekezwa na kuruhusu Mahakama ya Kadhi, kunaweza kulitumbukiza Taifa katika machafuko na hali ikiwa hivyo Serikali ndiyo itakayolaumiwa.
Tamko hilo limesainiwa na viongozi walewale waliosaini lile la awali la Machi 12, mwaka huu ambao ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT), Askofu Dk Alex Malasusa, Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Tarcisius Ngalalekumtwa na Mwenyekiti wa Kanisa la Pentekoste Tanzania (CPCT), Askofu Daniel Awet.
Tamko hilo la maneno 921, limeendelea kuwataka waumini wao kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura, kuisoma Katiba Inayopendekezwa na kujitokeza kuikataa kwa kupiga kura ya ‘hapana,’ msimamo ambao tayari umeibua msuguano baina yao na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo aliyesema viongozi wa dini hawana mamlaka ya kuwaamulia waumini wao aina ya kura wanayostahili kupiga.
Pia, Jukwaa hilo limewataka viongozi wakuu wa Serikali –Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais Kikwete wasifurahi kwamba ujumbe wao umewafikia viongozi wa dini waliozungumza nao hivi karibuni, kwa kuwa watu waliokutana nao si wawakilishi rasmi na hawana uwezo wa kutoa uamuzi au kukubaliana juu ya jambo la kitaifa.
“Maaskofu tuliokutana hapa (mjini Dodoma) hatuna hasira na wala hatuongozwi na hasira wala mihemko katika kufikia maamuzi tunayofanya kama ambavyo wengine wanavyotutafsiri, tunafikia maamuzi yetu baada ya maombi na sala na tunasukumwa na upendo kwa wananchi ili kujenga Taifa lenye umoja, amani, utulivu na maelewano,” lilisema tamko hilo likihitimishwa kwa maneno ya Biblia kutoka Mithali 29: 1, “Aonywaye mara nyingi akishupaza shingo, atavunjika ghafla, wala hapati dawa.”
Jumamosi iliyopita, Rais Kikwete akifungua mkutano wa Kamati ya Amani ya Mkoa wa Dar es Salaam iliyoshirikisha wajumbe kutoka mikoa mbalimbali ikijumuisha viongozi wa dini za Kiislamu na Kikristo, alisema msimamo wa TCF kuhusu kuipigia kura ya ‘hapana’ Katiba Inayopendekezwa ni wa hasira na usiokuwa na tija kwa maendeleo ya Taifa.
Nimeyasoma matamko hayo yote kwa umakini, imenishangaza, imenisikitisha na kunihuzunisha. Siamini kwa nini wamefikia huko kwa kuunga au kutokuunga mkono,” Rais Kikwete.
Rais Kikwete alisema: “Waacheni waumini waamue Katiba wanayoitaka wao… hayo matamko niliyoyasoma yamejaa hasira kwa Serikali kupeleka bungeni Muswada wa Mahakama ya Kadhi.”
Maaskofu hao walikuwa Dodoma kufuatilia kwa kina Muswada wa Marekebisho ya Sheria mbalimbali ya mwaka 2014 unaopendekeza, pamoja na mambo mengine, marekebisho ya Sheria ya Tamko la Sheria za Kiislamu la mwaka 1964 unaotambua Mahakama ya Kadhi.
“Muswada huu unapendekeza kuanzishwa Mahakama ya Kadhi ambao utawasilishwa bungeni leo kwa hati ya dharura na hivyo kuufanya umma wa Watanzania kutokujua maudhui yaliyomo katika muswada huo wakati bado hoja zetu za msingi tulizopeleka kwenye Kamati ya Katiba na Sheria ya Bunge na kwa Waziri Mkuu hazijajibiwa,” Ilieleza taarifa hiyo.
MWANANCHI
Askari polisi wawili wameuawa na mmoja kujeruhiwa baada ya kuvamiwa na watu wanaodhaniwa kuwa na viashiria vya ama ugaidi au ujambazi katika kizuizi cha barabara ya Kilwa, Kipara Mpakani, Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani.
Tukio hilo ambalo tayari limelaaniwa na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe na Tume ya Utawala Bora na Haki za Binadamu, limekuja katika kipindi ambacho Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Ernest Mangu amepangua makamanda na maofisa wa polisi 160 nchini kote.
Wakati Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ikisema inachunguza chanzo cha vifo vya askari hao ambao ni wa kanda hiyo, Chikawe alisema tukio hilo linawezekana kuwa la kigaidi au ujambazi lenye lengo la kuchukua silaha kwenda kufanyia matuko mbalimbali.
Askari waliouawa ni D.2865 SGT Francis na  E.177 CPL Michael wakati aliyejeruhiwa ni D 5573 D/SGT Ally.
Walioshuhudia tukio hilo walisema lilitokea juzi saa mbili usiku na kudumu kwa dakika 10 na kufanya eneo hilo kuwa kama uwanja wa vita kutokana na milio ya risasi.
Mkazi wa eneo hilo, Mohamed Ali alisema aliwaona watu watano wakitokea katika Pori la Kipara Mpakani, mmoja akiwa ameshika bunduki na mwingine panga.
“Niliwaona wakiwafuata askari karibu na kizuizi, mmoja alimpiga polisi risasi kifuani na mwingine akamkata polisi kwa panga shingoni,” alisema na kuongeza kuwa aliwaona askari hao wakiwa wamelala chini baada ya kuuawa… “Baada ya tukio hilo, watu wote waliokuwa karibu na eneo hili walikimbia kujificha wakihofia usalama wao.”
Shuhuda mwingine, Shiraz Abdul alisema alimwona mmoja wa askari mwingine akikimbia pamoja na wananchi baada ya tafrani hiyo… “Niliwaona askari watatu wakiwa wamelala chini, mmoja akiwa analia kuomba msaada,” aliongeza.
Shuhuda, Rehema Yusuph ambaye anaishi karibu na barabara kilipo kizuizi hicho alisema, walianza kusikia watu wakipiga kelele na kuhisi kwamba ilikuwa ajali.
“Mara nyingi huwa ajali zinatokea hapo barabarani, kwa hiyo sisi tulidhani kwamba ilikuwa ajali. Lakini baada ya sekunde chache tulianza kusikia milio ya risasi. Mara nikaona watu wanakimbilia  kwenye veranda yangu, baada ya kuuliza wakasema kuna watu wamevamia hicho kituo na wameua na kujeruhi askari.”
MTANZANIA
Ni maumivu. Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima kutoka Hospitali ya TMJ alikokuwa amelazwa kwa siku tano kwa kutumia baiskeli ya wagonjwa (wheelchair) kwenda Kituo cha Polisi Oysterbay kuhojiwa kwa mara ya pili.
Askofu Gwajima, alipandishwa kwenye baiskeli hiyo, baada ya kupelekewa na mmoja wa wafuasi ambaye alikuwa amevalia mavazi ya kichungaji.
Wakati akipelekwa katika gari Askofu Gwajima, alionekana akigugumia kutokana na maumivu makali ambayo haikujulikana mara moja chanzo chake.
Baada ya wafuasi wake kukamilisha taratibu zote, ilipofika saa 6:15 mchana, gari la polisi aina ya Land Cruiser lenye namba za usajili KX 06 EFY liliwasili hospitalini hapo.
Gari hilo, lilikuwa na askari wanne, mmoja akiwa ni ofisa wa polisi aliyekuwa amevalia sare za askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) na wengine wakiwa wamevalia kiraia.
Askari hao ambao walikuwa wamebeba bunduki walikwenda moja kwa moja wodini na baadae kutoka pamoja na kiongozi huyo wa kiroho.
Baada ya muda kidogo, askari hao walishuka chini na ilipofika saa 06:34 chana, gari nyingine ndogo aina ya Yutong MG 6 Turbo yenye namba STL 110 iliwasili eneo hilo ikiwa na askari mmoja.
Ilipofika saa 6:45, Askofu Gwajima alishushwa katika lifti ya hospitali hiyo, akiwa anasindikizwa na zaidi ya watu wane, huku yeye akiwa amekaa kwenye baiskeli hiyo na kupandishwa moja kwa moja kwenye gari la polisi.
Akiwa anainuliwa kwenye kiti na kupandishwa katika gari, Askofu Gwajima alionekana akikunja uso na kufungua mdomo kama mtu anayegugumia kutokana na maumivu makali.
Baada ya kutoka hospitalini, msafara huo ulielekea moja kwa moja Kituo cha Polisi cha Oysterbay.
Alifikishwa kituoni hapo saa 6:55 na kupelekwa chumba kilichokuwa kimeandikwa ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Kinondoni.
Alipofika mlangoni alikutana na ofisa mmoja, ambaye jina lake halikutambuliwa mara moja, alimuaru asubiri ili wakili wake afanye taratibu za dhamana.
Subiri hapa mfanye taratibu za dhamana mkishamaliza hakikisha Alhamisi (kesho) unaripoti Central Polisi (kituo kikuu cha polisi Dar es Salaam),”alisikika ofisa huyo akisema.
Wakati taratibu za dhamana zikiendelea, wafuasi wa Askofu Gwajima waliendelea kukusanyika eneo hilo kwa madai kuwa wanamsubiri kiongozi wao.
Wakiwa wamekusanyika makundi makundi, huku wengine wakiwa wameshikilia makaratasi yenye maandishi na picha ndogo kwa ajili ya kusaidia udhamini kama ukihitajika.
MTANZANIA
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umelaani na kusikitishwa na kauli za viongozi wa Chama cha Wananchi (CUF) kuitupia lawama CCM kwa kudai imehusika katika kushambuliwa wafuasi wao.
Wakati CCM wakitoa kauli hiyo, CUF kimemtupia lawama Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), Balozi Seif Ali Idd kuwa ndiye amekuwa akitoa kauli za kuchochea vurugu visiwani humo.
Taarifa ya UVCCM Zanzibar kulaani matamshi hayo ilitolewa jana kwa vyombo vya habari na Naibu Katibu Mkuu wake, Shaka Hamdu Shaka.
Wafuasi wa CUF walivamiwa na kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wanachama wa CCM, ambapo katika vurugu hizo watu 25 waliokuwa wakitokea katika mkutano uliokuwa unafanyika Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja walijeruhiwa.
Shaka alisema katika taarifa yake kwamba baadhi ya viongozi wa CUF wakiwamo wawakilishi wa chama hicho, kwa nyakati tofauti wamesikika na kunukuliwa na vyombo vya habari wakidai shambulio hilo la kudhuru limepangwa na kufanywa na vijana wa CCM jambo alilosema si kweli na halina ushahidi.
“Shutuma za CUF kwa namna moja au nyingine zimejiegemeza katika kuficha ukweli wa chanzo halisi kwani itakumbukwa hivi karibuni Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad katika moja ya mikutano yake ya hadhara alioufanya Kiembesamaki, sehemu kubwa ya hotuba yake ililenga kuwahamasisha na kuwachochea vijana wa chama chake kujiandaa kwa vurugu na kutotii sheria za nchi.
“UVCCM tunaamini vitendo hivyo viovu na vya kikatili vilivyofanyika ni matokeo ya matamshi ya uchochezi yaliyotolewa na katibu mkuu huyo na kuonyesha ni chimbuko la kuanza kushamiri matukio ya uvunjaji wa sheria kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba mwaka huu,” alisema.
Alisema mara kadhaa UVCCM imekuwa ikihimiza na kuwataka viongozi wa juu wa kisiasa kuchunga ndimi zao ili kuendesha siasa za kuvumiliana, kushindana kwa nguvu ya hoja, pia kuyaenzi na kuyalinda maridhiano ya kisasa yaliyofikiwa kati ya vyama vya CCM na CUF hadi kuundwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa mwaka 2010.
“Inashangaza hivi leo kumuona mmoja kati ya viongozi wanaojinasibu ni muumini na waasisi wa maridhiano akipanda majukwaani na kuanza kurejesha siasa za “mti kwa macho” na kushupaliana huku akitoa semi za uvunjaji wa sheria, akisema yuko tayari hata kupigwa mabomu na kuwa wa kwanza kuuawa hali inayoonyesha anakumbatia uvunjaji wa sheria,” alisema Shaka katika taarifa yake.
Chama cha CUF kimesema kutokea kwa vurugu kisiwani Unguja juzi, kumesababishwa na kauli iliyotolewa na Makamu wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Idd.
Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa chama hicho, Salum Bimani, alisema dalili za kutokea kwa vurugu na watu kujeruhiwa zilianza muda mrefu.
HABARILEO
Polisi mkoani Katavi inamshikilia mkazi wa kitongoji cha Ntumba, kijiji cha Mnyengele wilayani Mpanda, Deogratius Pastory (30) kwa kumjeruhi vibaya mkewe kwa kumkata mkono wake wa kushoto na kupasua tumbo la mpenzi wa mkewe kwa panga.
Mtu huyo aliwatendea unyama huo baada ya kuwafumania mkewe aitwae Tabu Nestory (20) na mpenzi wake wa kiume aitwaye Masaga Elias (28) wakifanya mapenzi katika jiko la nyumbani kwake kijijini humo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari alithibitisha mkasa huo.
Alisema tukio hilo ni la Machi 23, mwaka huu saa tano usiku katika kitongoji cha Ntumba katika kijiji cha Mnyengele. Akielezea mkasa huo, Kidavashari alidai kuwa jioni ya siku hiyo ya tukio, mtuhumiwa alimuaga mkewe Tabu kuwa anakwenda kijiji ambacho kiko umbali mrefu kutoka kijijini hapo kwa ajili ya kuangalia shamba lao.
Inadaiwa mtuhumiwa huyo alitumia baiskeli yake katika safari yake hiyo. Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakati mtuhumiwa huyo akiendelea na safari yake ghafla baiskeli yake aliyokuwa akiitumia katika safari yake hiyo iliharibika, wakati huo ilikuwa tayari imetimu saa tatu usiku .
“Kwa sababu alikuwa bado amebakiza mwendo mrefu kufika alikokuwa akienda aliamua kugeuza na kuanza kurejea nyumbani kwake, ambako alifika saa tano usiku …na alipofika kwake alimkuta mkewe na mpenzi wake wakifanya mapenzi katika jiko nyumbani kwake,” alieleza.
Inadaiwa kuwa kitendo hicho kilimkasirisha mtuhumiwa, ambaye alimwamuru mkewe na mgoni wake kuingia ndani, ambapo alimkamata mwanamume huyo na kumfunga kamba mikononi, kisha akachukua panga na kumchana tumbo chini ya kitovu hadi utumbo wake ‘ukamwagika’ nje .
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, mtu huyo alitumia panga hilo alilotumia kuchana tumbo la mgoni wake, kukata mkono wa kushoto wa mke wake.
HABARILEO
Wazazi 19 wa wanafunzi walioshindwa kuripoti kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo wa 2014/2015 wamehukumiwa kifungo cha nje cha miezi mitatu kila mmoja kutokana na kosa la kushindwa kuwapeleka watoto wao shuleni.
Wazazi waliohukumiwa kifungo hiki ni wale wa kata za Mpindimbi na Lukuledi zilizopo katika Halmashauri ya wilaya ya Masasi, Mtwara Aidha, wametakiwa kuripoti kwenye Mahakama ya Mwanzo ya Lisekese wilayani hapa kila baada ya wiki mbili wakati wote watakapokuwa wanatumikia adhabu yao.
Mbele ya Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Lisekese wilayani Masasi, Gloria Mkwera karani wa mahakama hiyo, Agnes Hanga alidai washitakiwa hao walitenda kosa hilo mwanzoni mwa mwaka huu kwa waliposhindwa kutimiza wajibu wao wa kuwapeleka watoto wao shuleni huku wakijua ni wajibu wao.
Ni halali yako kupata kila stori inayonifikia mtu wangu, niko tayari kukutumia wakati wowote kupitia www.tangakumekucha.blogspot.com