Katika zile zilizoingia kwenye Headline leo Bungeni ipo hii ya John Mnyika …
“Mpaka
sasa tunavyozungumza zoezi la uandikishaji halijakamilika hata kwa mkoa
mmoja tu wa Njombe na Watanzania nchi nzima wako kwenye sintofahamu,
lini hasa wataandikishwa kabla ya kura ya maoni ya katiba mpya, jambo
hili ni la dharura kwasababu ilikwisha tolewa hoja ya dahraura juu ya
jambo hili kwenye mkutano uliopita wa Bunge, ukaagiza kamati ya Bunge
ishughulikie na majibu yatolewe kwenye mkutano huu wa Bunge sasa leo
mkutano unafungwa bila majibu kutolewa tusitishe shughuli zote
tuhakikishe majibu yanatolewa leo“
“Katika
mkutano huu nimeomba muongozo juu ya jambo hili mara mbili na mara zote
Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu naamini umeipa maelekezo ya kutoa
majibu lakini inakwepa kutoa majibu.
Katika
mazingira kama haya hakuna sababu yoyote ya kuendelea na mjadala wowote
mwingine kwenye kikao hiki cha Bunge, wala kusubiria chochote tupate
majibu kwenye mkutano huu wa Bunge ili tuweze kufanya kazi ya kuishauri
na kuisimamia Serikali, Waziri Mkuu yuko hapa anaweza kutoa majibu hapa
na tukajadili hapa“–Mbunge John Mnyika.
Lakini Spika Makinda akasema hoja hiyo inafanana na hoja ambayo ilitangulia hivyo haiwezi kujadiliwa, kitu ambacho kilisababisha mvutano wa Wabunge.
No comments:
Post a Comment