Baba mdogo wa marehemu apigwa, kisa ni kuzuia mwili wa Marehemu usiingie kwenye nyumba yake
Kijana ambae ni rafiki wa marehemu
amesema Mzee huyo alikataa maiti isiingie nyumbani kwake kwa madai kuwa
ni uchuro na anamdai marehemu shilingi laki tatu, wakavunja geti na
kuingia ndani lakini bado aliwakatalia, wakaamua kwenda kwenye uwanja wa
mpira ili watu wapate nafasi ya kuaga mwili wa Marehemu.
Mwenyekiti wa eneo hilo alifika
akamshauri mzee huyo aende uwanjani kuaga, alipofika vijana hao walianza
kumpiga na kumzuia kusafiri na mwili wa marehemu kwenda Moshi kwa ajili
ya mazishi.
Mzee huyo alipoulizwa sababu ya kukataa maiti isiingie ndani kwake alikataa kuzungumza.
No comments:
Post a Comment