Unaambiwa lock hii ndio komesha ya wizi wa Baiskeli…
Kama uliwahi kukerwa na ishu ya wizi wa Baiskeli, basi wataalamu watatu wamekuja na majibu yote mtu wangu..!!
Cristóbal Cabello, Andrés Roi Eggers na Juan José Monsalve
waliachana na masomo ya Chuo wanaweka nguvu yao wote kwa pamoja kwenye
project ya kutafuta Ufumbuzi wa tatizo la wizi wa Baiskeli… wote watatu
ni raia wa Chile.
Hasira yao ilitokana pia na mmoja wao
kuibiwa baiskeli yake!! Wakaona isiwe tabu, project yao ilipata
ufadhili wa kama dola laki moja hivi (sawa na Tshs. 210,000,000/=),
nguvu yao ikazaa matunda ya kutokea hii baiskeli ambayo unaweza kucheki
kwenye picha hapa pamoja na kipande cha video kinachoonesha unavyoweza
kuifunga na ikabaki salama kabisa.
No comments:
Post a Comment