Tuesday, December 1, 2015

MBUNGE WA JIMBO LA MLALO, RASHID SHANGAZI TUMAINI JIPYA MLALO



Tangakumekuchablog
Mlalo, MBUNGE wa jimbo la Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, amewataka wakulima wa matunda na mbogamboga jimboni humo kuongeza nguvu ya kilimo kwa madai kuwa pembejeo za kilimo  na masoko ya uhakika yanapatikana.
Akizungumza katika hafla fupi ya kuwashukuru wananchi wa jimbo hilo kwa kumchagua kuwa Mbunge wao jana na kuwashirikisha Madiwani, Wenyeviti wa vijijini na wa Chama pamoja na maofisa kilimo na biashara, Shangazi alisema anataka kulirejesha jimbo hilo katika hadhi yake ya kuzalisha matunda na mbogamboga.
Alisema wakulima wengi wa matunda na mbogamboga wamepunguza kasi ya kulima kutokana na kukata tamaa ya upatikanaji wa soko la uhakika na pembejeo za kilimo  hivyo kulima kilimo cha mazoea.
“Kwa heshima na taadhima ndugu zangu wazee wangu mashangazi na wajomba nawashukuru kwa kuniunga mkono kwenu na leo hii kusimama hapa kama mbunge---nawaahidi sitakuwa mbunge wa kutafutwa kwa tochi” alisema Shangazi na kuongeza
“Mimi ni mbunge wenu na niko tayari kushirikiana na kila mmoja ili kulienua jimbo letu kiuchumi hasa kukiendeleza kilimo chetu cha mbogamboga na matunda na masoko niwambie kuwa yapo” alisema
Akizungumzia fursa za mikopo kwa vijana na vikundi vya ushirika, Shangazi alisema pesa hizo zipo ila hitolewa kwa utaratibu na hivyo kuwataka wananchi kuchangamkia ili kujikomboa na umasikini.
Aliwataka wananchi wanawake na wanaume na vijana kuunda vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kupata vursa za mikopo katika taasisi za fedha pamoja na asilimia kumi na asilimia 5 za halmashauri zilizotengwa kwa wanawake na vijana.
“Ndugu zangu ziko njia nyingi za kupata pesa na kujikwamua na umasikini----undeni  vikundi vitakavyotuwezesha kupata mikopo katika taasisi za fedha na ziko tuchangamke” alisema Mbunge huyo
Alisema ili kulifanikisha hilo amedai kuleta wataalamu ambao watatoa elimu kwa vikundi vya ujasiriamali ikiwa lengo ni kuhakikisha maisha ya watu yanabadilika na kufanya kazi kwa ustadi  na yenye tija.
                                                 Mwisho





 Wananchi wa jimbo la Mlalo Wilayani Lushoto Mkoani Tanga, wakimsikiliza Mbunge wa jimbo hilo, Rashid Shangazi katika kikao kilichoitishwa na Mbunge huyo kuwashukuru kwa kumchagua kuwa Mbunge wa jimbo hilo.
 Mbunge wa jimbo la Mlalo (CCM) Rashid Shangazi, akizungumza katika hafla ya kuwashukuru wananchi kwa kuwamchangua kuwa Mbunge wao hafla hiyo iliyofanyika juzi.













  Mbunge wa jimbo la Mlalo (CCM) Rshid Shangazi akiwaonyesha wanaNchi cheti cha pongezi ailichopewa na Umoja wa Wakazi wa Mlalo waishio Dar es Salaam (MLAWA)  wakati wa hafla fupi ya kupongezwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo juzi.


No comments:

Post a Comment