MELI MPYA YA MV. MAPINDUZI II YAWASILI BANDARI KUU YA ZANZIBAR
Meli mpya ya mv.mapinduzi ( ii)
imewasili bandarini Zanzibar kwa ajili ya kuanza safari zake baada ya
kukamilika ujenzi wake huko Korea ya kusini.
Hafla ya kuwasili kwa meli hiyo
imeongozwa na waziri wa fedha Omar Yussuf Mzee ambapo amesema ujenzi wa
meli hiyo ni agizo la raisi wa zanzibar na mwenyekiti wa baraza la
mapinduzi Dk. Ali mohamed shein.
Amesema meli hiyo bado iko katika
mikono ya wajenzi hadi sasa na inatarajiwa kuzinduliwa rasmin wiki ijayo
na rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein ambaye ni mgeni rasmi katika
uzinduzi huo.
Waziri mzee amesema meli hiyo
inavifaa vya kutosha kama vile life jacket, pamoja na boti ndogo ili
kuweka usalama kwa abiria wataosafiri katika meli hiyo.
Hata hivyo amesema meli hiyo
itasafiri Pemba pamoja na Dar es-salaam hivyo amewataka wananchi
kuitunza meli hiyo kwani ni matunda yao.
Naye Katibu Mkuu Wizara ya Miundo
mbinu na mawasiliano zanizar Dk. Juma Malik amesema lengo kulifanya
shirika la meli lifanye kazi kibiashara ili kuongeza pato la taifa.
Amewaomba wananchi kuitunza na
kuitumia vizuri meli hiyo kwani wamefanya kazi kubwa na kutumia gharama
hadi kufikia kukamilika kwa meli hiyo.
Sambamba na hayo amesema meli hiyo ina uwezo wa kupakia abiria wasiopunguwa 1,200 pamoja na tani za mizigo 200.
Meli hiyo mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola Mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18.
Meli hiyo mpya ya Mv.Mapinduzi ( ii) imetengenezwa Korea kusini na kugharimu jumla ya dola Mil.30.4 za Marekani ambapo ujenzi wake hadi kukamilika umechukua jumla ya miezi 18.
No comments:
Post a Comment